TFF yatoa tamko baada ya Shaffih Dauda kutangaza Ndondo Cup

TFF yatoa tamko baada ya Shaffih Dauda kutangaza Ndondo Cup

Wanaugomvi binafsi na mwajiriwa wa taasisi ambayo ni clouds ,ni ujinga yale siyo mashindano ya Shafii ila alikuwa mmoja wa waratibu na saizi anaratibu Mkazuzu

Ikiwa wataomba kibali kwa TFF, ni athari gani ambazo zitaikumba hiyo taasisi?
 
Tangu TFF chini ya Malinzi pengine hata kabla ya hapo hawataki kabisa Dauda ajihusishe na mpira wa miguu.

MwanaFA angesaidia kuondoa huu urasimu,yeye ni mtu wa soka kiasi hapa hawamkomoi Shaffih.

Vibali vitolewe hata na associations/vyama vya mpira ngazi ya wilaya.
 
Kwamba muda wa kuomba kibali umeisha kwakua tangazo limetoka leo?

Wao waombe kibali mashindano yaendelee, hizi habari za kila mtu kutaka huruma za wananchi ili sheria zipindishwe kwa masilahi yake binafsi ni ushamba. Alianza Manara kutafuta huruma sasa ni DAUDA, mwisho wa siku sheria ni lazima zifuatwe.
Mshauri vizuri huyo rais wako wa TFF, kuna mtifuano wa chini chini toka walipompiga chini uongozi wa DRFA acheni kuua vipaji vya vijana wanaochipukia kumbuka.

FB_IMG_1679072944605.jpg
 
TFF kama inataka vibali waje vingunguti faru wadai vibali na tufuate sheria maaana kuna ligi inaendelea
Mnadai kuwa Ndondo Cup ni mashindano yabayoibua vipaji kwaajili ya Taifa letu ila hamtaki Shirikisho linasimamia mpira wa Taifa letu lihusike kwenye hayo mashindano, hizo ni akili?

Kaombeni kibali, mkinyimwa ndio mje kulalamika hapa.
 
Ila TFF


 
Nashangaa watu humu wanalalamikia TFF. Tuambie kivipi pamoja na Dauda kufuata taratibu ila bado anahujumiwa. Tuambie jinsi alivyoomba kibali. Au kama sio hivyo sema basi hatakiwi kuomba kibali.

Usiseme sijui mbona kuna Diwani Cup. Aliyekuambia Diwani Cup hakupewa kibali nani?

Mwambieni akaombe kibali afuate taratibu
 
Ninachojua hayo mashindano huwa yanaratibiwa na DRFA ,Kutakuwa na Jambo nyuma ya pazia tusubili tuone .
 
Unajua haya mambo usipoyaelewa kiundani zaid utaishia kulaum upande mmoja.

Niwe mkweli ndondo cup ni michuano ambayo imekuwepo Muda mrefu na kama hawakua na kibali ni vyema wafuaye taratib zilizowekwa.

Japo Hawa TFF wamekua wakikandmiza sna watu hasa wakereketwa wa mpira Kwa maslahi Yao binafsi.

Je kuomba kibali Kuna gharama yoyote?

Je kama gharama ipo inaumiza au la?

Je wameshindwa kumwambia mhusika (Shaffi)mpaka waweke Tangazo waziwazi??
 
Mashindano yote ambayo yapo chini ya TFF kwenye malato kuna percentage wanachukua.kinachotafutwa ni hiyo percentage tu hapo.
 
Back
Top Bottom