TFF yatoa tamko baada ya Shaffih Dauda kutangaza Ndondo Cup

TFF yatoa tamko baada ya Shaffih Dauda kutangaza Ndondo Cup

Ukipitia baadhi ya comment za wadau humu ndio unapata picha kuwa tunaishi kwenye jamii ya namna Gani.

Kufanya jambo kwa kutofuata utaratibu wa jambo hakumaanishi uhalali wa jambo....na kutosimamia jambo ambalo linatakiwa kusimamiwa hakuondoi hakubatilishi jambo.

Kama huo utaratibu upo basi wahusika wanapaswa kufuata utaratibu.

Tusipime uhalali wa jambo kwa mazoea au kwa kumtazama anayefanya au kufanyiwa bali kwa uhalali wake.

Watanzania tuache tabi za kulia lia badala tutumie vyema kilichomo ndani ya mafuvu yetu.
 
Roho mbaya tu TFF wanachojua n majungu tu huku arusha na sehem nyingi tu ndondo inapigwa Kama kawaida IPO siku watasema ata kununua mipira n kibali
 
Tanzania Vituko Haviishi, Miaka Tele Walipokuwa Wanacheza Ilikuwa Vp

Ama Ndiyo Leo Wameyaona Hayo Mashindano
 
Sio mbaya kupata kibali ila hii maana yake nikua kuna percent inatakiwa hapo.fedhwa!!
 
Mpira wa migui unaweza kufanyika nje ya TFF? Au TFF wana hakimiliki ya mpira wa miguu TZ.

IMG_20230323_101024.jpg
 
Fifa wanataka mpira uchezwe Hadi mapolini.

TFF hawataki.

Tena wanaingilia majukumu ya DRFA.
ya ndondo cup.

AIBU NAONA MIMI.
 
Ndondo cup ni mpira wa mtaani TFF ahahusika vipi na ligi zisizo rasimi? hayo mamlaka wanatoa wapi?
 
Punguzeni mihemko hamjui kitu ila mnaropoka tu, chama cha mkoa husika ndo hupeleka maombi TFF kuhusu kuanzishwa kwa mashindano, na siku zote Ndondo Cup hupeleka barua kwa chama cha soka cha mkoa husika kisha TFF wanaidhinisha mashindano kuendelea.

Kupitia Sports Extra jana Shaffih Dauda alizungumza kua TFF imeawakumbusha tu kua wanatakiwa kutuma maombi TFF kwaajili ya ridhaa ya Ndondo Cup na kwakua Ndondo cup muda wa kuanza bado upo wa kutosha basi chama cha soka kitapelea maombi na utaratibu utaendelea kama kawaida.

Sasa unakuta mtu hana taarifa yoyote kasoma tu anakuja huku kueneza chuki niwakumbushe tu TFF ni taasisi inayoongoza kwa sheria na taratibu zilizoweka hivyo kumshutumu karia ni matatizo ya akili ya mtu bibafsi.

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Lilikuwa ni suala la muda tu. Mashindano tayari yana maslahi, wadhamini wanapatikana na washiriki wanatoa ushirikiano katika michango. Katika hatua hii kutokufuata taratibu lazima kuonekane.
 
Back
Top Bottom