TFF yaufungia uwanja wa Mkwakwani kwa kukosa vigezo

TFF yaufungia uwanja wa Mkwakwani kwa kukosa vigezo

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,040
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Leo Novemba 26 limeufungia Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga kutumika kwenye michezo ya Ligi kutokana na kukosa vigezo vya kikanuni na kisheria vinavyohitajika kwa matumizi ya viwanja vya mpira. Kwa mujibu wa TFF, miundombinu ya uwanja huo haikidhi matakwa ya Kanuni na masharti ya Leseni za Klabu.

1764168452257.png


Kutokana na uamuzi huo, timu zinazotumia uwanja huo kama uwanja wa nyumbani zitatakiwa kutumia uwanja mwingine unaokidhi viwango hadi pale marekebisho yatakapokamilika na kuhakikiwa rasmi na TFF.

Shirikisho pia limezikumbusha klabu zote kuendelea kuboresha na kutunza miundombinu ya viwanja vyao ili kufuata kanuni za ligi.
 
Uwanja wa Mkwakwakani uliporwa na CCM Kinyemela wakati haikushiriku kuujenga. Uwanja huo umekuwapo hata kabla ya CCM kuzaliwa. Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana viwanja vyote vilicvyoporwa na CCM vinakosa matuzo, na kukosa vigezo. Utashangaa kuwa Uwanja wa Kirumba nao ni kama hauna vigezo tenna; Ali Hassani Mwinyi kule Tabora ni wa kulazimisha tu. Viwanja hivyo vinatakiwa virudi serikalini vihudumia na serikali za mitaa kama ule wa KMC.
 
Back
Top Bottom