TFF yawafungulia mashtaka Haji Manara, Hersi, wote waitwa Kamati ya Maadili

Nilikuwa namuona Engineer Hersi anafanya mambo yake kisomi, kumbe nae hamna kitu, ameiharibu sana title yake ya "Rais wa klabu".

Mtu unajua kabisa, Manara amefungiwa kujihusisha na shughuli za mpira ndani ya Tanzania, halafu eti unadai "kumualika" kwenye shughuli yako akawe MC!.

Kwani ile haikuwa shughuli ya mpira? Kama walitaka kumualika wangemualika kwenye harusi, lakini sio kumpeleka pale uwanjani, lile lilikuwa kosa la makusudi linalostahili adhabu kali kwa wote wawili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…