Thabit Abdul kuipeleka taarabu kanisani

Thabit Abdul kuipeleka taarabu kanisani

brigedia mafia

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2016
Posts
2,260
Reaction score
2,279
Thabit Abdul amefunguka kuwa ana mpango wa kuipeleka taarabu kanisani kwa kuimba kwaya yenye mahadhi ya taarabu

Thabit amedai kuwa waimba kwaya wengi wenye majina makubwa nchini wamemfuata ili wafanye nae kolabo ingawa mwanzoni alisita ila kwa sasa kaamua kukubali na kutoa ahadi ya kutoa nyimbo za kutosha za kwaya zenye mahadhi ya taarabu

1475253824846.jpg

Haya sasa kazi kwenu wapenda kwaya anachotaka kukifanya huyu kijana kipo sawa? Kwa upande wangu naona hayuko sawa maana mziki wanaouimba hauko sawa hata kidogo na umejaa ufirauni sasa suala la kuamishia kanisani naona ukakasi kidogo au mnasemaje waungwana?
 
Mungu alimpa mwanadamu utashi na miongozo ya mambo ya kufanya na mamlaka ya kuhukumu anayo mwenyewe tofauti na mungu wa upande wa pili yule aliyeagiza watu wake wahukumu. Sasa hao wa taarabu gospel nadhani watajua wenyewe kama waki sahihi au lau
 
Hold on.....huyu ni Thabit Abdul mtoto wa Ilala aliekuwa akiimbia TOT au mwengine?ile case yake ya ubakaji alichomokaga kweli,isijekuwa ilimdatisha maana kitambo sana sijamsikia.
 
kuimba nyimbo za injili kwa miondoko ya taarabu hatakuwa wa kwanza, miaka ya 2004,2005 hapo kuna jackson bent aliwahi kuimba...,

wenye kumbukumbu nzuri kipindi hiko watakumbuka
 
Nitawashangaa sana BASATA kama wataruhusu hiki kituko. Na ikiwezekana hatua kali za zichukuliwe dhidi ya muhusika. Yaani ule mselebuko wa kishangingi uingie kanisani!!? Isifike mahala watu wakaanza kudhihaki dini za wengine kwa tamaa ya pesa.
Huyu anachokifanya hakikubaliki kwa waungwana na watu wanaotakia mema utashi wa kidini. Au mwenzetu amefilisika kiusanii sasa anatafuta kiki ya kutokea?
Kwa hili kama kuna watu "eti" wamemshauri anajiandalia kaburi lake kisanii. Mimi ni mpenzi wa Taarabu lakini kwa hili analotaka kulifanya huyu Bwana ni kutafuta jinsi ya kuuzika muziki wa Taarabu na kuuweka mahala ambapo ni vigumu kuukwamua.
 
Thabit Abdul amefunguka kuwa ana mpango wa kuipeleka taarabu kanisani kwa kuimba kwaya yenye mahadhi ya taarabu

Thabit amedai kuwa waimba kwaya wengi wenye majina makubwa nchini wamemfuata ili wafanye nae kolabo ingawa mwanzoni alisita ila kwa sasa kaamua kukubali na kutoa ahadi ya kutoa nyimbo za kutosha za kwaya zenye mahadhi ya taarabu

View attachment 409858

Haya sasa kazi kwenu wapenda kwaya anachotaka kukifanya huyu kijana kipo sawa? Kwa upande wangu naona hayuko sawa maana mziki wanaouimba hauko sawa hata kidogo na umejaa ufirauni sasa suala la kuamishia kanisani naona ukakasi kidogo au mnasemaje waungwana?
" Haloooooooo haloooow njoo kwa yesu babu wee" hiyo haikubaliki hata kidogo..he need to sit down and shut his mouth or someone shut it up for him
 
Back
Top Bottom