Thabo Bester maarufu 'Mbakaji wa Facebook' na Dkt. Nandipha Magudumana wakamatiwa Arusha Tanzania. Wafahamu kwa undani wapenzi hawa

Thabo Bester maarufu 'Mbakaji wa Facebook' na Dkt. Nandipha Magudumana wakamatiwa Arusha Tanzania. Wafahamu kwa undani wapenzi hawa

Thabo bester aliyekuwa akitafutwa kwa udi na uvumba na mamlaka za afrika ya kusini amekamatwa leo asubuhi huko mkoani arusha,bester maarufu kama Facebook rapist anatuhumiwa kwa makosa kadhaa yakiwemo ubakaji,utapeli na mauaji,

Kabla ya kukamatiwa tanzania bester alikuwa akitumikia kifungo jela ya Mangaung huko nchini afrika ya kusini ambapo iliripotiwa kuwa bester alifariki akiwa gerezani,na ndipo dada mmoja daktari aitwaye Nandipha Magudumana alijitokeza kuomba kupewa mwili wa bester ili akauzike akidai kuwa ni mke wa thabo bester,ambapo alikubaliwa na kuuchukua mwili kutoka kwenye hospitali ya mangaung na kwenda kuuchoma siku hiyo hiyo,

Lakini siku kadhaa baadae camera za usalama kwenye mall moja hukohuko SAzilimwonyesha mtu anayefanana na bester akiwa na ndevu nyingi na kujitanda kiajemi,ndipo tetesi za kuwa bester you had zilipozagaa na kuishtua polisi ya SA (SAPS)na kuanzisha msako mkali,

Who is real Thabo Bester?
His CV and whareabouts?

Nani alimhost Arusha?
 
Why mkuu ?,huyu raia wa Mozambique na Dr. Nandipa kosa lao hapa ni kuingia nchini kwa njia za panya, kama wasomali/Ethiopians wanavyofanya, sasa why hawa wawe tofauti?,SA lazima waheshimu sheria zetu na elewa hawa wawili hawana cases kule SA, but Mr. Bester ni tofauti maana yupo convicted kwa rapes na murder
Ndugu, hata washitakiwe, nchi husika itawachukua .... Yaani Tanzania itakua imeisaidia S. A kuwakamata watuhumiwa wao, kumbuka habari za huko kwao zinasema Kuna maafisa wa huko walikua wakiwafatilia, na situ wamekamatwa na TZ pekee hapana, na walikua wanaelekea Kenya, yaani wako chini ya ulinzi kwa sababu ni nchi husika walio kamatiwa, lakini maafisa wa nchi yao wapo hapa pia, kwa hivyo lazima warejee nao kwao
 
MBIO ZA UTORO ZA THABO BESTER ZAISHIA SAKAFUNI TANZANIA

Waziri Ronald Ozzy Lamola wa wizara ya katiba na vyuo vya mafunzo Afrika ya Kusini athiibithisha kukamatwa Thabo Bester nchini Tanzania na tayari mipango ya mchakato wa kisheria ili Thabo Bester awe deported kurudishwa Tanzania imeanza.

Thabo Bester akiwa na mpenzi wake wa kike Dr Nandipha Magudumana pamoja na raia mwingine wa Mozambique wamekamatwa mkoani Arusha wakiwa na hati kadhaa za kusafiria amesema Mh. Bheki Cele waziri wa Polisi wa Afrika ya Kusini.

Mbali ya kutoroka toka jela moja yenye ulinzi mkali Afrika ya Kusini alikokuwa akitumikia kesi za mauaji na ubakaji Thabo Bester pia alikuwa anaendesha biashara za kitapeli za udalali wa majumba na magari ya kifahari kwa kushirikiana girlfriend wake Dr Nandipha Magudumana.

Dr. Nandipha Magudumana aliweza wakati mmoja kufanikisha Thabo Bester kuongea kupitia mtandao wa Zoom akiwa ktk chumba cha ulinzi wa juu jela na mkurugenzi wa kampuni moja iliyopo jijini New York Marekani inayomilikiwa na bilionea Tom Motsepe.

Mkurugezi huyo alichukua hatua za tahadhari na kuomba huduma za makachero binafsi / private detective kuweza kumchunguza mtu aliyeongea naye ni nani ktk zoom ndipo alipobaini anaongea na mhalifu aliye jela nchini Afrika ya Kusini akitumikia kifungo kirefu hivyo mkurugenzi huyo kuachana naye mazungumzo ya biashara alizokuwa akizinadi pengine kwa uhakika zingekuwa haramu na za kitapeli....

Dr. Nandipha Magudumana ni msichana msomi wa elimu ya juu, ana digrii mbili za fani ya utabibu na sayansi ya Afya ambazo ni Bachelor of Health Sciences (BHSc) in Biomedical Sciences na Bachelor of Medicine and Bachelor of Surgery (MBChB), toka chuo kikuu tajwa cha University of the Witwatersrand, Johannesburg almaaruf Wits cha nchini Afrika ya Kusini.

Baada ya unaosemekana mwili wa Thabo Bester kugundulika ukiwa umeungua vibaya kiasi cha kutotambulika kati selo ya jela maarufu yenye ulinzi mkali huko Bloemfontein nchini Afrika ya Kusini, Dr. Nandipha Magudumana alitayarisha ombi la affidavit la kupewa mwili wa aliyekuwa mpenzi wake ili ukafanyiwe maziko Soweto.

Lakini katika hali ya kushangaza baadaye Thabo Bester alionekana akiwa ameongozana na Dr. Nandipha Magudumana wakifanya shopping ktk supermarket moja karibu na walipopana jumba la kifahari la kodi mbaya lililopo Sandton mitaa ya matajiri kilometa moja toka makazi ya Rais Cyril Ramaphosa, na ndipo uchunguzi kuhusu 'kifo' cha Thabo Bester ulipoanza tena.

Uchunguzi huo kwa kutumia picha za CCTV zilizowachukua wapenzi hao supermarket na pia kutaka kufahamu kwa kina vinasaba DNA vya mwili ulio uliungua vibaya jela ulikuwa ni wa nani, ulifikaje vipi ktk selo ya jela na kuzua taharuki kuwa jambazi sugu Thabo Bester ametoroka jela akiwa hai .. hatimaye wapenzi hao wawili katika uhalifu na wakiongozana na jamaa mmoja Zakaria Alberto raia wa Mozambique kunaswa nchini Tanzania.

Thabo Bester | Lamola says Bester and Magudumana were arrested in Tanzania on Friday night


Huyu watabadilishana na askari wa B4 aliywtorokea south

Wasauzi wanamtaka Thabo na sisi tunamtaka soja wetu aliyepo kwao
 
Ndugu, hata washitakiwe, nchi husika itawachukua .... Yaani Tanzania itakua imeisaidia S. A kuwakamata watuhumiwa wao, kumbuka habari za huko kwao zinasema Kuna maafisa wa huko walikua wakiwafatilia, na situ wamekamatwa na TZ pekee hapana, na walikua wanaelekea Kenya, yaani wako chini ya ulinzi kwa sababu ni nchi husika walio kamatiwa, lakini maafisa wa nchi yao wapi hapa pia, kwa hivyo lazima warejee nao kwao
Kumbe unaongea kisiasa,elewa Mr.Bester case yake ipo tofauti na hao wengine ambao kosa lao ni kuwa illegals hapa Tanzania, Mr Bester hawezi kurudishwa tu SA bila kufuata sheria zetu zinasemaje kuhusu issue kama hii,we can't roll over kisa kuwafurahisha SA, elewa Malawi hadi leo almost more than 2yrs hawajamrudisha tapering bushiri SA,maana ana case ya raping na money laundering
 
Acha upumbavu mkuu, udaku gani hapa nimeuandika?,source gani unaitaka?,let's me assume wewe ni mjinga ,ngoja nikutafunie maana middle class ninyi mmezoea kutafuniwa, mtu wa kwanza to escape from SA maximum prison ni raia wa Mozambique, Mase na kwa sasa ni marehemu, huyu alitoroka kwa kutokea dirishani baada ya kutengeneza kamba ya matambala na Bester amemfuatia huyu ametumia uchawi wa kizungu pesa, hope's umefahamu na next time try kushirikisha ubongo wako wenye elimu ya UPE
Toa source mbwiga wewe
 
Kwa sinema aliyo fanya huyu ndugu hakutakiwa kukamatwa milele, uzembe ndio umewaponza, angeondoka south africa mapema alivyomaliza mchezo ange ishi mda mrefu sana, pia asinge jihusisha na mawasiliano yoyote ya watu wanaomfahamu kwa sababu kwao alikua amesha kufa na wamemzika

Sent from my TECNO LB6 using JamiiForums mobile app
 
Why mkuu ?,huyu raia wa Mozambique na Dr. Nandipa kosa lao hapa ni kuingia nchini kwa njia za panya, kama wasomali/Ethiopians wanavyofanya, sasa why hawa wawe tofauti?,SA lazima waheshimu sheria zetu na elewa hawa wawili hawana cases kule SA, but Mr. Bester ni tofauti maana yupo convicted kwa rapes na murder
Huyo Dr. anakesi ya kumtorosha huyo Bester toka Gerezani huko SA labda huyo raia wa Msumbiji lakini hatuwezi jua labda alishiriki pia katika kumtorosha huyo mfugwa Bester toka Gerezani SA. Nafikiri SA wana data za kutosha na utaratibu wa kisheria ni kwamba watafikishwa mahakamani hapa TZ ili mahakama itoe idhini ya kurudishwa SA kujibu mashitaka yao huko kwa kuwa nafikiri TZ na SA wanautaratibu wa kurudishiana watuhumiwa.
 
Nilkua nawaza Bester ni mzembe kwa kukamatwa tena baada ya kufanikiwa kutoroka gerezani ila nmekumbuka kuna kitu hakiepukiki kinaitwa "DESTINY"
 
Huyo Dr. anakesi ya kumtorosha huyo Bester toka Gerezani huko SA labda huyo raia wa Msumbiji lakini hatuwezi jua labda alishiriki pia katika kumtorosha huyo mfugwa Bester toka Gerezani SA. Nafikiri SA wana data za kutosha na utaratibu wa kisheria ni kwamba watafikishwa mahakamani hapa TZ ili mahakama itoe idhini ya kurudishwa SA kujibu mashitaka yao huko kwa kuwa nafikiri TZ na SA wanautaratibu wa kurudishiana watuhumiwa.
Nakubaliana nawe kipengele cha hawa suspects (isipokua Mr. Bester)kuwa mahakama zetu ziwahukumu kama illegals wanavyofanyiwa sio kuwapigia magoti SA na kuwarudisha, nchi yetu ni huru na sheria zake LAZIMA ziheshimiwe, kwenye magereza yetu kuna wahamiaji haramu wengi tu, na hawa wawili ni sehemu yao no favour, na pia Dr.Nandipa hana kesi kule SA,hajafunguliwa mashitaka yeyote na hii ni fact mkuu
 
Malawi hadi leo haijawarudisha tapeli bushiri na mke wake ambayo wamekimbia kesi baada ya kupewa dhamana sasa why us to roll over kwa SA?
 
Huyo ni kumtundika shaba. Nachukia mtu mbakaji.

Halafu anayesema Polisi wa SA ni afadhali kuliko wa kwetu naona hawajui hao polisi wa SA. Polisi wa SA ni majambazi bora elfu wa kwetu.
 
Nakubaliana nawe kipengele cha hawa suspects (isipokua Mr. Bester)kuwa mahakama zetu ziwahukumu kama illegals wanavyofanyiwa sio kuwapigia magoti SA na kuwarudisha, nchi yetu ni huru na sheria zake LAZIMA ziheshimiwe, kwenye magereza yetu kuna wahamiaji haramu wengi tu, na hawa wawili ni sehemu yao no favour, na pia Dr.Nandipa hana kesi kule SA,hajafunguliwa mashitaka yeyote na hii ni fact mkuu
Mkuu unauhakika Dr. Nandipa hajafunguliwa kesi huko SA? Wakati alikuwa anatafutwa na ndio kisa cha kukimbia SA. Naona huna taarifa kamili ya issue hii.
 
Yes amekamatwa hapo Arusha, welldone kwa police wote wa Arusha, hasa interpol na undercovers wote,u make our country proud, kudos RPC wa Arusha na askari wako wote, Tanzania [emoji1241] yeeeee!,huyu jamaa anasitahili kuwa jela not to roam outside there, mpigeni pingu mwili mzima maana yupo very clever, na msiogope maana ameshakua convicted with a court of law, ingekuwa ni mimi ningemrudisha pale Bloemfontein na mijeledi ya nguvu, ni jitu katili lenye baby face
Wangemalizana nae tu. Chapa risasi za kichwa hadi ubongo umwagike kisha anafukiwa kama mzoga mwingine tu story imeisha. Watu wa hovyo kama hao ambao imeshathibitika ni hatari kuwa loose kwann aendelee kupumua.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom