Sorry,nilishindwa kuweka mwendelezo na pia kujibu maswali kadhaa kutokana na kubanwa na shughuli nyingine,wa South wanasema ni bora bester afungwe hukohuko tanzania kwani hawaiamini SAPS kabisa,wana mashaka kuwa anaweza kutoroshwa tena kutoka gerezani huko SA, kuna jambo nililiona tokea habari za bester kuonekana akiwa na Dr Nandipha kwenye supermarket,huku ikiaminika kuwa alishafariki kwa kujichoma moto akiwa gerezani na baadaye akafanyiwa cremation rasmi, thabo bester na Nandipha walikuwa ni wapenzi zamani,lakini waliachana muda mrefu kabla ya bester kuhukumiwa,inasemekana Dr Nandipha alikuwa akimpenda sana jambazi bester, hivyo aliposikia kuwa bester amehukumiwa altona ndiyo gap la kurudisha penzi Lao kwa gharama yoyote,ndipo alipoanza kusuka mipango ya kumtoa bester gerezani,so plan yote ya kumchomoa bester gerezani aliisuka Nandipha,hadi kuwahonga askari wa G4s waliokuwa wanaendesha gereza hilo,kununua maiti waliyoichoma moto wakidai ni ya bester, akagharimia kila kitu ikiwemo nyumba,gari,na expenses zote zitakazomfanya bester kuufurahia uhuru huo bandia,na hata baada ya picha za bester kusambaa akiwa kwenye Mall na nyingine ikimuonyesha akiwa nje ya duka jingine kubwa kusambaa,Nandipha alimhamishia bester kwenye nyumba ya kifahari aliyoipanga kwenye eneo la brooklyn huko Pretoria,baadaye tetesi zikachomoza kuhusu uwepo wa bester kwenye eneo hilo,mwandishi wa habari za kiuchunguzi aitwaye Barry roux ndiye aliyetoa hint kuhusu besters whereabouts, hivyo Dr Nandipha akalazimika kumhamisha tena bester na kumpeleka sehemu isiyojulikana!! Hadi walipokamatwa huko arusha usiku wa jana wakiwa na mtu mwingine ambaye ametambulika kama raia wa Mozambique, pia polisi wa arusha wanasema kuna mtuhumiwa mwingine mmoja ambaye alikuwa pamoja na bester ila bado hajakamatwa, hayo ndiyo mapenzi! Kuna mtu hapo juu aliuliza jinsi ambavyo bester alifanikisha uhalifu wake,bester anajulikana kama Facebook rapist!! Sababu ni hii,bester alikuwa akitumia mtandao wa Facebook kuweka matangazo ya nafasi za ajira nzuri nzuri,alikuwa akiweka na address za kuweza kuwasiliana naye ikiwa utavutiwa na ajira alizotangaza,sasa ukiwasiliana naye anakupa location ya kwenda kwa ajili ya interview na mengineyo,huku akiahidi kuwa gharama za usafiri na malazi utarudishiwa ukishafika kituoni,hapo ndipo watu walijichomeka bila kujua! Kwani baada ya kufika ulikoelekezwa ungepokelewa na bester mwenyewe,atakuonyesha sehemu ya kufikia na kula na kila kitu,sasa hapo ndipo atakuja kukupa interview, atakubaka,atakupora kila kitu,na kama Huna bahati anakuua kabisa!! Umeelewa sasa? Swali ni kuwa Dr Nandipha aliipata wapi maiti aliyoichoma kwa jina la bester? Maskini Dr Nandipha ndiyo ameshaharibu career yake kwa ajili ya mapenzi ya jambazi,muuaji na mbakaji bester, umeona kitu hapo?