Thabo Bester maarufu 'Mbakaji wa Facebook' na Dkt. Nandipha Magudumana wakamatiwa Arusha Tanzania. Wafahamu kwa undani wapenzi hawa

Thabo Bester maarufu 'Mbakaji wa Facebook' na Dkt. Nandipha Magudumana wakamatiwa Arusha Tanzania. Wafahamu kwa undani wapenzi hawa

mbona hamjafafanua vizur inaonekana mwamba ana profile ya hatari na ya kutuletea hapa jukwaani namna alivyokuwa akitekeleza huo ubakaji na uuaji na picha zake pia ila hapa naona mnatangaza kikawaida sana
Mimi hata siwaelewi maana wanaongea ongea vitu vya kusadikika hawatoi profile kamili ya huyu jamaa ipoje, ana matukio mangapi, ameua watu wangapi na amebaka wangapi, history yake ni ipi.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
MBIO ZA UTORO ZA THABO BESTER ZAISHIA SAKAFUNI TANZANIA

Waziri Ronald Ozzy Lamola wa wizara ya katiba na vyuo vya mafunzo Afrika ya Kusini athiibithisha kukamatwa Thabo Bester nchini Tanzania na tayari mipango ya mchakato wa kisheria ili Thabo Bester awe deported kurudishwa Tanzania imeanza.

Thabo Bester akiwa na mpenzi wake wa kike Dr Nandipha Magudumana pamoja na raia mwingine wa Mozambique wamekamatwa mkoani Arusha wakiwa na hati kadhaa za kusafiria amesema Mh. Bheki Cele waziri wa Polisi wa Afrika ya Kusini.

Mbali ya kutoroka toka jela moja yenye ulinzi mkali Afrika ya Kusini alikokuwa akitumikia kesi za mauaji na ubakaji Thabo Bester pia alikuwa anaendesha biashara za kitapeli za udalali wa majumba na magari ya kifahari kwa kushirikiana girlfriend wake Dr Nandipha Magudumana.

Dr. Nandipha Magudumana aliweza wakati mmoja kufanikisha Thabo Bester kuongea kupitia mtandao wa Zoom akiwa ktk chumba cha ulinzi wa juu jela na mkurugenzi wa kampuni moja iliyopo jijini New York Marekani inayomilikiwa na bilionea Tom Motsepe.

Mkurugezi huyo alichukua hatua za tahadhari na kuomba huduma za makachero binafsi / private detective kuweza kumchunguza mtu aliyeongea naye ni nani ktk zoom ndipo alipobaini anaongea na mhalifu aliye jela nchini Afrika ya Kusini akitumikia kifungo kirefu hivyo mkurugenzi huyo kuachana naye mazungumzo ya biashara alizokuwa akizinadi pengine kwa uhakika zingekuwa haramu na za kitapeli....

Dr. Nandipha Magudumana ni msichana msomi wa elimu ya juu, ana digrii mbili za fani ya utabibu na sayansi ya Afya ambazo ni Bachelor of Health Sciences (BHSc) in Biomedical Sciences na Bachelor of Medicine and Bachelor of Surgery (MBChB), toka chuo kikuu tajwa cha University of the Witwatersrand, Johannesburg almaaruf Wits cha nchini Afrika ya Kusini.

Baada ya unaosemekana mwili wa Thabo Bester kugundulika ukiwa umeungua vibaya kiasi cha kutotambulika kati selo ya jela maarufu yenye ulinzi mkali huko Bloemfontein nchini Afrika ya Kusini, Dr. Nandipha Magudumana alitayarisha ombi la affidavit la kupewa mwili wa aliyekuwa mpenzi wake ili ukafanyiwe maziko Soweto.

Lakini katika hali ya kushangaza baadaye Thabo Bester alionekana akiwa ameongozana na Dr. Nandipha Magudumana wakifanya shopping ktk supermarket moja karibu na walipopana jumba la kifahari la kodi mbaya lililopo Sandton mitaa ya matajiri kilometa moja toka makazi ya Rais Cyril Ramaphosa, na ndipo uchunguzi kuhusu 'kifo' cha Thabo Bester ulipoanza tena.

Uchunguzi huo kwa kutumia picha za CCTV zilizowachukua wapenzi hao supermarket na pia kutaka kufahamu kwa kina vinasaba DNA vya mwili ulio uliungua vibaya jela ulikuwa ni wa nani, ulifikaje vipi ktk selo ya jela na kuzua taharuki kuwa jambazi sugu Thabo Bester ametoroka jela akiwa hai .. hatimaye wapenzi hao wawili katika uhalifu na wakiongozana na jamaa mmoja Zakaria Alberto raia wa Mozambique kunaswa nchini Tanzania.

Thabo Bester | Lamola says Bester and Magudumana were arrested in Tanzania on Friday night

Ila wanawake wa kizazi hiki hawanaga akili hata wasome. Tena waliosoma ndio changamoto mara mbili. Huyu Dada anajua kabisa jamaa ni convicted felonist hata kama ni mwanaume ambaye alishawahi date nae before ila kwasasa ana rekodi mbaya ya uhalifu.

Hii hali inaitwa Hybristophilia ukisoma utaelewa ni ujinga ujinga wanawake wanapenda kufanya ili wajisikie vizuri.


Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Sorry,nilishindwa kuweka mwendelezo na pia kujibu maswali kadhaa kutokana na kubanwa na shughuli nyingine,wa South wanasema ni bora bester afungwe hukohuko tanzania kwani hawaiamini SAPS kabisa,wana mashaka kuwa anaweza kutoroshwa tena kutoka gerezani huko SA, kuna jambo nililiona tokea habari za bester kuonekana akiwa na Dr Nandipha kwenye supermarket,huku ikiaminika kuwa alishafariki kwa kujichoma moto akiwa gerezani na baadaye akafanyiwa cremation rasmi, thabo bester na Nandipha walikuwa ni wapenzi zamani,lakini waliachana muda mrefu kabla ya bester kuhukumiwa,inasemekana Dr Nandipha alikuwa akimpenda sana jambazi bester, hivyo aliposikia kuwa bester amehukumiwa altona ndiyo gap la kurudisha penzi Lao kwa gharama yoyote,ndipo alipoanza kusuka mipango ya kumtoa bester gerezani,so plan yote ya kumchomoa bester gerezani aliisuka Nandipha,hadi kuwahonga askari wa G4s waliokuwa wanaendesha gereza hilo,kununua maiti waliyoichoma moto wakidai ni ya bester, akagharimia kila kitu ikiwemo nyumba,gari,na expenses zote zitakazomfanya bester kuufurahia uhuru huo bandia,na hata baada ya picha za bester kusambaa akiwa kwenye Mall na nyingine ikimuonyesha akiwa nje ya duka jingine kubwa kusambaa,Nandipha alimhamishia bester kwenye nyumba ya kifahari aliyoipanga kwenye eneo la brooklyn huko Pretoria,baadaye tetesi zikachomoza kuhusu uwepo wa bester kwenye eneo hilo,mwandishi wa habari za kiuchunguzi aitwaye Barry roux ndiye aliyetoa hint kuhusu besters whereabouts, hivyo Dr Nandipha akalazimika kumhamisha tena bester na kumpeleka sehemu isiyojulikana!! Hadi walipokamatwa huko arusha usiku wa jana wakiwa na mtu mwingine ambaye ametambulika kama raia wa Mozambique, pia polisi wa arusha wanasema kuna mtuhumiwa mwingine mmoja ambaye alikuwa pamoja na bester ila bado hajakamatwa, hayo ndiyo mapenzi! Kuna mtu hapo juu aliuliza jinsi ambavyo bester alifanikisha uhalifu wake,bester anajulikana kama Facebook rapist!! Sababu ni hii,bester alikuwa akitumia mtandao wa Facebook kuweka matangazo ya nafasi za ajira nzuri nzuri,alikuwa akiweka na address za kuweza kuwasiliana naye ikiwa utavutiwa na ajira alizotangaza,sasa ukiwasiliana naye anakupa location ya kwenda kwa ajili ya interview na mengineyo,huku akiahidi kuwa gharama za usafiri na malazi utarudishiwa ukishafika kituoni,hapo ndipo watu walijichomeka bila kujua! Kwani baada ya kufika ulikoelekezwa ungepokelewa na bester mwenyewe,atakuonyesha sehemu ya kufikia na kula na kila kitu,sasa hapo ndipo atakuja kukupa interview, atakubaka,atakupora kila kitu,na kama Huna bahati anakuua kabisa!! Umeelewa sasa? Swali ni kuwa Dr Nandipha aliipata wapi maiti aliyoichoma kwa jina la bester? Maskini Dr Nandipha ndiyo ameshaharibu career yake kwa ajili ya mapenzi ya jambazi,muuaji na mbakaji bester, umeona kitu hapo?
Please weka Aya maana kusoma reply ndefu bila aya inachosha macho.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
VIPI WALIOMPIGA RISASI TUNDU LISSU na KUMTEKA MO wamewapata au mpaka zamu ya Makachero wa South afrika?
[emoji23][emoji23][emoji23]wewe unaongelea waliomchapa risasi tundulissu, je wale walimfanyia ukatili dokta ulimboka nusu ya kumuua akavimba mwili mzima, kisa kutetea masilahi ya madaktari. Ulisikia popote wameongelewa tena. [emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Pamoja na hawa fugitives kukamatiwa hapa nchini, ni muhimu mno sheria zetu zikafuatwa, tusi just roll over ili kuwafurahisha SA, kwanza wajibu ilikuaje waukesha mpaka wao bila wahusika kujua, Mr.Bester ndiye pekee aliyehukumiwa, Dr.Nandipa na Mozambique citizen hawa ni illegal immigrants, wapelekwe mahakama na sheria ichukue mkondo wake, kuwa deport SA straight haitakua sawa
Najiuliza huyu hamlifu amepitaje katika borders zetu inamaana hatuna ukaguzi wa kutosha. Hatuna facial recognition system ambazo zinaweza mtambua mhalifu hata kama si wakwetu.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Why mkuu ?,huyu raia wa Mozambique na Dr. Nandipa kosa lao hapa ni kuingia nchini kwa njia za panya, kama wasomali/Ethiopians wanavyofanya, sasa why hawa wawe tofauti?,SA lazima waheshimu sheria zetu na elewa hawa wawili hawana cases kule SA, but Mr. Bester ni tofauti maana yupo convicted kwa rapes na murder
Wewe unaongea vitu gani wewe?!

1. Wameshiriki kumtorosha mhalifu hatari jela.

2. Huyo dada ametumia profession yake ya udaktari kufoji taarifa muhimu za vipimo juu ya mwili ambao anajua wazi si wa muhusika.

3. Huyu dada kwasasa anakuwa ni mhalifu sababu ya kushirikiana na mhalifu ambaye anajua wazi kuwa jamaa ni hatari na ana matukio hatari.

4. Amekuja kwenye mipaka ya taifa jingine yaani Tanzania na kumvusha huyu mhalifu huo ni uhalifu pia sababu mbali na kwamba anasafirisha mtu hatari ila anadanganya mamlaka zetu za mipaka juu ya identity ya muhusika.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Yes amekamatwa hapo Arusha, welldone kwa police wote wa Arusha, hasa interpol na undercovers wote,u make our country proud, kudos RPC wa Arusha na askari wako wote, Tanzania 🇹🇿 yeeeee!,huyu jamaa anasitahili kuwa jela not to roam outside there, mpigeni pingu mwili mzima maana yupo very clever, na msiogope maana ameshakua convicted with a court of law, ingekuwa ni mimi ningemrudisha pale Bloemfontein na mijeledi ya nguvu, ni jitu katili lenye baby face
Unawasifu bure. Huyu walisham-trace aliko na wakapewa tu taarifa. Hawakufanya lolote special
 
Huyu watabadilishana na askari wa B4 aliywtorokea south

Wasauzi wanamtaka Thabo na sisi tunamtaka soja wetu aliyepo kwao

Ngoja tuone mifumo ya haki jinai (criminal justice system) ya nchi hizi mbili zipo huru kiasi gani kuachiwa kufanya kazi zake .

Mfumo huru wa haki jinai unataka mamlaka zinazotuhumu watuhumiwa kufikishwa ktk vyombo husika uhamiaji, polisi kisha kupelekwa mbele ya mahakama na sheria kufuata mkondo wake.

Ndiyo maana mawaziri wa Afrika ya Kusini jenerali Bheki Cele waziri wa polisi na Bw. Ronald Lamola waziri wa sheria pamoja na vyuo vya mafunzo (magereza) wanesema serikali ya Afrika ya Kusini imetuma ujumbe mzito wa maafisa kuja Tanzania kuona namna gani wanaweza kuwapata wapenzi hawa wawili ktk uhalifu huku wakisema kuwa ushiriki wa raia wa Mozambique Zakaria Alberto ni suala lingine mtambuka pengine hana uhusiano wa kiuhalifu na Thabo Bester au Dr. Nandhipha Magudumana.

Kuhusu suala la askari polisi wa Tanzania anayetuhumiwa kuhusika na kufuja bilioni 4 za mfuko wa maziko wa jeshi la Polisi la Tanzania bado kama kawaida ya mfumo wa haki jamii wa Tanzania.

Upande wa serikali yetu Tanzania 'ukikamatwa' mtuhumiwa hupotea ndani ya mfumo wa haki jinai bila vyombo vya habari au jamii na jamaa kupata mrejesho vyombo vinafanya kazi kesi husika kwa namna ipi, uchunguzi umefika hatua gani wala yepi wanayafahamu baada ya mahojiano n.k .

Kwa maneno mengine mfumo wa haki jinai Tanzania wanafanya kazi zao kwa usiri na kufunikafunika bila kutoa taarifa za kina kwa umma wa Tanzania hata wa kimataifa siyo tu kuhusu Thabo Bester au askari polisi wa Tanzania aliyeko Afrika ya Kusini wana mpango gani mkono mrefu wa sheria kumfikia.


 
Ngoja tuone mifumo ya haki jinai (criminal justice system) ya nchi hizi mbili zipo huru kiasi gani kuachiwa kufanya kazi zake .

Mfumo huru wa haki jinai unataka mamlaka zinazotuhumu watuhumiwa kufikishwa ktk vyombo husika uhamiaji, polisi kisha kupelekwa mbele ya mahakama na sheria kufuata mkondo wake.

Ndiyo maana mawaziri wa Afrika ya Kusini jenerali. Bheki Cele waziri wa polisi na Bw. Ronald Lamola waziri wa sheria pamoja na vyuo vya mafunzo (magereza) wanesema serikali ya Afrika ya Kusini imetuma ujumbe mzito wa maafisa kuja Tanzania kuona namna gani wanaweza kuwapata wapenzi hawa wawili ktk uhalifu huku wakisema kuwa ushiriki wa raia wa Mozambique Zakaria Alberto ni suala lingine mtambuka pengine hana uhusiano wa kiuhalifu na Thabo Bester au Dr. Nandhipha Magudumana.

Kuhusu suala la askari polisi wa Tanzania anayetuhumiwa kuhusika na kufuja bilioni 4 za mfuko wa maziko wa jeshi la Polisi la Tanzania bado kama kawaida ya mfumo wa haki jamii wa Tanzania.

Upande wa serikali yetu Tanzania 'ukikamatwa' mtuhumiwa hupotea ndani ya mfumo wa haki jinai bila vyombo vya habari au jamii na jamaa kupata mrejesho vyombo vinafanya kazi kesi husika kwa namna ipi, uchunguzi umefika hatua gani wala yepi wanayafahamu baada ya mahojiano n.k .

Kwa maneno mengine mfumo wa haki jinai Tanzania wanafanya kazi zao kwa usiri na kufunikafunika bila kutoa taarifa za kina kwa umma wa Tanzania hata wa kimataifa siyo tu kuhusu Thabo Bester au askari polisi wa Tanzania aliyeko Afrika ya Kusini wana mpango gani mkono mrefu wa sheria kumfikia.
Nimeweza kuelewa hapa kwamba inabidi extradiction ifanyike kwa mfumo wa sheria bila kuwepo na veto za maamuzi nje ya mfumo wa mahakama

Lakini kwa namna dola yetu ilivyojimilikisha haki ya kuishi na kufanya maamuzi kwa niaba ya maisha utasikia jamaa kassfirishwa huko
 
Hii ni mbaya sana yaani unaratibu mauji ya mtu asiye na Hatia Kwa kuchoma gereza Ili tuu wewe utoroke gerezani.

Kuna mashaka sana na security appatus za Afrika Kusini.

Reference: Thabo Bester and Spouse Dr Nandipha Magadugula.

=======

Tanzania Police have confirmed the arrest of South African prison escapee Thabo Bester and his accomplice Dr. Nandipa Magudumana and one other person by the name of Zakaria Alberto.

In a short statement released by the Police Spokesperson David A Misime, Tanzania Police said they are finalizing, “other international and national procedures” for the case.

Thabo Bester, a serial rapist, scammer, and murderer was confirmed to have escaped Mangaung Prison in South Africa in March 2023 after a viral Twitter picture that showed him shopping. It was later learned that Bester had escaped prison in May 2022 in a ploy that involved fake suicide.

Prison cell where Bester was kept had caught fire only for his corpse to be found burnt beyond recognition. Bester was pronounced dead, only for the news to resurface on social media that he was living large with South African celebrity Doctor, Nandipa Magundumana.

Reports show it was a complex scheme that involved Dr Nandipa Magundumana who collected the burnt corpse from prison, claiming she was the wife of Thabo Bester.

Confirming the arrest of Thabo Bester, South Africa Minister of Justice and Correctional Services Ronald Lamola, says he is expecting to be in Tanzania on Sunday, April 09, 2023, to follow up on the case.

“We have confirmed with all relevant authorities in Tanzania which include the national Police in Tanzania and Interpol that fugitives have been processed in the Tanzania criminal justice system,” said Lamola in a press statement.
 
Hao ni majasusi wa dunia.

Mbaya kuua mtu ili wewe uokoke, mbaya zaidi mbele za Mungu pia.

All in all polisi wa tz wako vizuri, naogopa kusema CONGRATULATIONS.

Angesogea hapo kwa Uhuru asingekamatwa mpaka afe kweli kweli.
 
... SA walifuta adhabu ya kunyonga adhabu pekee aliyostahili Bester! Angekatiwa hiyo adhabu na ikatekelezwa inavyopaswa bila figisu shida zote hizi za kuhangaika naye zingeshasahaulika zamani. Adhabu ya kunyonga bado ina umuhimu mkubwa duniani.
 
Hao ni majasusi wa dunia.

Mbaya kuua mtu ili wewe uokoke, mbaya zaidi mbele za Mungu pia.

All in all polisi wa tz wako vizuri, naogopa kusema CONGRATULATIONS.

Angesogea hapo kwa Uhuru asingekamatwa mpaka afe kweli kweli.
Hiyo ni kazi ya Interpol, ndiyo wanaotoa descriptions na ndiyo wanao ongoza msako lakini arresting hufanywa na askari wa nchi husika (aliyokamatiwa) hata taarifa hutolewa na nchi ambapo mharifu amekamatiwa.
Wakati mwingine inaweza isiwe interpol lakini ikawa ni joint mission
 
Back
Top Bottom