Thamani tena hakuna, yameachwa nje,

Thamani tena hakuna, yameachwa nje,

mabuba

Senior Member
Joined
Dec 5, 2006
Posts
133
Reaction score
90
Thamani tena hakuna, yameachwa nje,
Usiri tena hakuna, yameachwa nje,
Aibu tena hakuna, yameachwa nje,
Ustaarabu tena hakuna, yameachwa nje.

Balehe ilipofika, yalitunzwa hakika,
Binti aliyefiki, elimishwa pasi taabika,
Kuyatunza bila kukimbilia, aibu akaja sononeka,
Aibu tena hakuna, yameachwa nje.

Umri ukifika, chakula mtoto chake,
Baba naye afaidika akiwa mahala pake,
Madodo yanapukutika, mengi kwa makeke,
Thamani tena hakuna, yameachwa nje.

Wadada na wamama, sasa wameyaachia,
Wajidai yamesimama, winchi wameyapigia,
Hata yaliyo mraba, pembe tatu yajiitia,
Usiri tena hakuna, yameachwa nje.

Uchina wameyaendea, kuyatia hamirani,
Ukubwa wameyatakia, ilikuleta tafrani,
Madodo twakimbilia, hata yaliyokuzimuni.
Ustaarabu tena hakuna, yameachwa nje.


Yameachwa nje, wenyewe waita usasa
Wazi wayaanike, hata mbele ya ibada
Waenda kifua mbele, pasi kuona karaha
Yameachwa nje, wenyewe waita usasa

Na mengine mistari, mingi imeshamiri
Wapo wanaodiriki, kuyaanika ukweni
Maradhi yametamaraki, usia nawapeni
Na usasa jihadhari, kubaya utawapelekeni
Yameachwa nje, wenyewe waita usasa
 
Thamani tena hakuna, yameachwa nje,
Usiri tena hakuna, yameachwa nje,
Aibu tena hakuna, yameachwa nje,
Ustaarabu tena hakuna, yameachwa nje.

Balehe ilipofika, yalitunzwa hakika,
Binti aliyefiki, elimishwa pasi taabika,
Kuyatunza bila kukimbilia, aibu akaja sononeka,
Aibu tena hakuna, yameachwa nje.

Umri ukifika, chakula mtoto chake,
Baba naye afaidika akiwa mahala pake,
Madodo yanapukutika, mengi kwa makeke,
Thamani tena hakuna, yameachwa nje.

Wadada na wamama, sasa wameyaachia,
Wajidai yamesimama, winchi wameyapigia,
Hata yaliyo mraba, pembe tatu yajiitia,
Usiri tena hakuna, yameachwa nje.

Uchina wameyaendea, kuyatia hamirani,
Ukubwa wameyatakia, ilikuleta tafrani,
Madodo twakimbilia, hata yaliyokuzimuni.
Ustaarabu tena hakuna, yameachwa nje.


Yameachwa nje, wenyewe waita usasa
Wazi wayaanike, hata mbele ya ibada
Waenda kifua mbele, pasi kuona karaha
Yameachwa nje, wenyewe waita usasa

Na mengine mistari, mingi imeshamiri
Wapo wanaodiriki, kuyaanika ukweni
Maradhi yametamaraki, usia nawapeni
Na usasa jihadhari, kubaya utawapelekeni
Yameachwa nje, wenyewe waita usasa

Jukwaa la Siasa?Mods? I believe huwa mnahamisha post mnazoamini haziko mahali sahihi, let me see you handle this!!
 
Haya ni maadili na sio lugha Mod
 
Ila zamani wakati najifunza mashairi shule ya msingi, nakumbuka kulikuwa na kitu kinaitwa vina na mizani. Sijui kama mkuu umelizingatia hili.
 
"Thamani tena hakuna?", thamani aweka nani?
Ndevu anaezipuna, na bakora mkononi?
Suruali amebana, na shati la darizini?
Mali ya kwangu mwenyewe, matumizi nipangiwe?!

Ya wazi akiyaona, roho yamtapa tapa
Macho humtoka pima, pumzi huja kwa pupa
Njiani humwandama, na kijasho cha kikwapa
Mali ya kwangu mwenyewe, matumizi nipangiwe?!

Kisha hujibarauza, 'bingiri' kusema mengi
Eti mila ana kuza, kwa kukalia vigengi
Utukufu kujitunza, wa mema yaliyo mengi
Mali ya kwangu mwenyewe, matumizi nipangiwe?!
 
thamani ya kitu ni mtu,pasi yeye kujielewa
thamani ya mali ni mtu,pasi yeye kuitumia
hawekewi mipaka tele,kutwa kuwaza ya watu
ujuwapo thamani ya kitu,mwachie yeye mhusika.

Mengi yameongelewa,na mengine yamekatazwa,
ila moja twasumbukia,na kusahau yalipangwa
ni nani ayatambuaye,kama sio wa pembeni
ujuwapo thamani ya kitu,mwachie yeye mhusika.

hapa nasemeya kipendwa,kile dume alitakalo
na usasa wa dunia ya sasa,nalo pia lachangia
kusukumwa na uhalisia,japo kuwa wa kuibia
ujuwapo thamani ya kitu,mwachie yeye mhusika.

wamama na mabinti hawa,husukumwa na nini pia?
kwanini mizigo kuachia,hadharani wakianika?
uliza sukumo latoka wapi,hasa na huu uchina?
ujuwapo thamani ya kitu,mwachie yeye mhusika.

tuwache kuwapalamia,na lazima kuwatakia
tuwache usasa wa bandia,ili wapate tulia
tulidhike na ya wahenga wa kale,uhalisia kuukumbati
ujuwapo thamani ya kitu,mwachie yeye mhusika.

tulidhike asili yetu,uafrika wa kale thamani
tukumbatie tamaduni zetu,na ndani yatahifadhiwa
tuwache kupenda uzungu,kwa matendo na tutekeleze
thamani itahifadhiwa,wakina baba tunahusika.

😛ray2:
 
Mkuu kuna aina mbili za ushairi, usasa na umapokeo. huu ni usasa
 
Back
Top Bottom