Thamani (Value) ya Kombe la CAF Champion v/s CAF Confederation

Umetumia akili kuandika, sio ushabiki wa yanga vs simba.
Simba tumefanya makosa
Mechi ya Dsm tulitakiwa kuimaliza mapema, kocha akawaelekeza wachezaji wacheleweshe mipira ikitoka.
Mpira unatoka unaona Kapombe anatembea kama hataki, sekunde zinakatika...

Kocha akachelewa fanya sub, alipofanya akaweka mabeki

Tumeenda Moroco mchezo ukawa huo huo
Wachezaji hawajitumi kushambulia wao wanazuia tu huku wakijua fika ni wabovu kwenye penati.

Afu eti tumetoka kiume, huo ni upumbavu na wenda wazimu
 
Uko sahihi,
Lakini na Ugumu wa Michuano nao unachangia Mkuu.
Jaribu kufikiri Leo angekua ndio Yanga anacheza na Bingwa Mtetezi Wydad Casablanca angemtoa kirahisi kama alivyomtoa Rivers?

Labda next year tujitoleshe Championship ili tuangukie Confederation tujaribu bahati yetu huko. Sababu huko timu zake sio ngumu sana kama za Championship.
 
Yaani Horoya aliekua wa 3 kwenye kundi la Simba ana value kubwa. (US$550,000) kuliko yoyote yule katika Michuano ya kina Yanga atakaeishia nusu fainali (US$ 450,000)
 
Wamesogea kwenda wapi?
Kwani hawakushiriki CL, kwanini hawakuingia makundi?
 
Akili ndogo na wivu wa kijinga, kwani last season ulikuwa wapi? Mbona haukufika alikofika Young Africans kama team za huko ni mbovu ..?
 
Akili ndogo na wivu wa kijinga, kwani last season ulikuwa wapi? Mbona haukufika alikofika Young Africans kama team za huko ni mbovu ..?
Sawa,
Kwa hiyo akili kubwa yako inakuambia timu za huko zinazidi viwango timu za Championship?

Yaani tuweke top 4 ya viwango vya Semi-finalist wa Championship vs wa Confederation tuone wapi wako juu?
 
Hujaelewa, je Man city Atakubali kutolewa champions league ili akashiriki Europa?

Je Man city Akishinda Europa atajitapa?
 
mwaka jana ulikuwa huko ulifika wapi
 
Naomba niwakumbushe ndugu zangu Yanga imeingia nusu fainali

Haya mjadala uendelee
 
Mtajifariji kwa Kila namna

Ili msijinyonge,basi nawaunga mkono

Ili mpate hata faraja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…