Thamani ya pesa yetu inazidi kuporomoka. Shida ni nini?

Thamani ya pesa yetu inazidi kuporomoka. Shida ni nini?

Leo dola moja ni Tsh 2350 mtandaoni. Gharama za vitu tunavyoagiza itazidi kupanda. Shida nini pesa yetu kuporomoka namna hii? Hivi kuna namna tunaweza kuachana na kuagiza vitu kwa dola?
Si mnachekelea Mwigulu anavyokopa,hadi maji mtaiita Mmmma! na bado Dola itazidi kupanda kwa kasi sana!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Hamjui kusoma alama za nyakati.

Kuanzia 2023 imetabiriwa Uchumi wa Dunia kuporomoka, Mungu aliumba Dunia, akatukabidhi, Badala ya kumwabudu Mungu, tunatumia pesa zetu kumtenda dhambi.

Kila kitu kitavurugwa, ni tuanze moja, tukumbuke tulipojikwaa.

Kuanzia 2023 na kuendelea, hayupo atakayetegemea pesa ktk mabenki alikotunza akiba maana vyote vitapukutika.

Imeandikwa, mwenye HAKI ataishi Kwa Imani, huu ni mwanzo wa Ishara tu, mziki wenyewe unaanza 2024 na kuendelea.

Tutarudi tu shambani, Ili mtu ale ni lazima afanye KAZI na atoke JASHO, mifumo yote ya ajira itavurugika.

Ingia kwenye safina kama utapenda kustahimili mkwamo unaokuja .

Ameen
 
Tuzalishe ndani bidhaa tunazonunua nje. Vinginevyo shilingi itazidi kuporomoka.

Bidhaa ambazo hata hapa ndani twaweza kutengeneza ya nini tuagize nje?

Hizo tusizoweza kuzizalisha lakini tunaagiza kwa wingi, tupange mikakati ya kuzalisha hapa. Hata kama ni kwa developmental state approach ilimradi tujitegemee.

Miongo ijayo ndio hali itakuwa mbaya zaidi kama hatutakuwa na viongozi wenye uzalendo wa kweli kwa taifa lao.
 
Leo dola moja ni Tsh 2350 mtandaoni. Gharama za vitu tunavyoagiza itazidi kupanda. Shida nini pesa yetu kuporomoka namna hii? Hivi kuna namna tunaweza kuachana na kuagiza vitu kwa dola?
Kwanza imejitahudi,Hali ya uchumi wa Dunia sio nzuri,currency crunch sio Tanzania tuu ni karibu Nchi nzote Kwa sasa
 
Tuigeuze na kuipa majukumu mapya BOT, ondoa politics pale na wafanye kazi including kuilinda sarafu yetu na rates zake,tuchukue ths.yetu na kuipandikiza kwenye BWP,futa zeros zote tubakiwe na noti ya she.100tu kwenye mzunguko wetu, tudhibiti matumizi makubwa ya serikali including to have serikali ndogo iliyo smart, tusiagize zaidi kuliko tunavyouza nje
 
Leo dola moja ni Tsh 2350 mtandaoni. Gharama za vitu tunavyoagiza itazidi kupanda. Shida nini pesa yetu kuporomoka namna hii? Hivi kuna namna tunaweza kuachana na kuagiza vitu kwa dola?
Labda tunauza sana bidhaa nje, ili kurahisisha na kuboresha Uchumi!!! Lakini, kama hatuuzi sana bidhaa nje basi hilo letu!!!
 
Hamjui kusoma alama za nyakati.

Kuanzia 2023 imetabiriwa Uchumi wa Dunia kuporomoka, Mungu aliumba Dunia, akatukabidhi, Badala ya kumwabudu Mungu, tunatumia pesa zetu kumtenda dhambi.

Kila kitu kitavurugwa, ni tuanze moja, tukumbuke tulipojikwaa.

Kuanzia 2023 na kuendelea, hayupo atakayetegemea pesa ktk mabenki alikotunza akiba maana vyote vitapukutika.

Imeandikwa, mwenye HAKI ataishi Kwa Imani, huu ni mwanzo wa Ishara tu, mziki wenyewe unaanza 2024 na kuendelea.

Tutarudi tu shambani, Ili mtu ale ni lazima afanye KAZI na atoke JASHO, mifumo yote ya ajira itavurugika.

Ingia kwenye safina kama utapenda kustahimili mkwamo unaokuja .

Ameen
Tunatumia pia pesa kumpa huyo mungu wako uchumi ukiharibika sijui atapata nin huyo mungu wako
 
Kuna kisiwa kinadaiwa trilioni 91 huko, ukiuliza nini, unaambiwa, walikopa MCHELE.

Kweli? Unakopa mchele? 945,000km square of mass land!

Wengine wakaenda kununua mchele nje, kweli?

Wageni wananunua mazai shambani!

Pesa za mikopo zinanunua mabasi na malori, V8 za kuwahonga kina barabara.

Shilingi ikae wapi sasa? Haina pa kujishika, itaporomoka mpaka maka!
 
Back
Top Bottom