Thamani ya Uhai wa Mtu yaweza linganishwa na Nafasi ya Udiwani?

Thamani ya Uhai wa Mtu yaweza linganishwa na Nafasi ya Udiwani?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
761
Reaction score
6,985
Tunapoteza kijana wetu, bila kujali chama anachotoka tunapaswa kumlilia na kulia na wauaji. Kama anavyoumia mzazi wa kijana huyu ndivyo utakavyoumia kiongozi wa Jeshi la Polisi au kiongozi wa kisiasa pale utakapompoteza mpendo wako.

Namna nafsi ya kiumbe flani itakavyokuelekeza kupindisha haki katika uchunguzi wako na kukuelekeza kamati yule na yule kwa sababu yakutaka ushindi wakisiasa ndivyo pia mshahara wa dhambi unavyokunyemelea.

Mshahara wa milioni mbili ni mdogo sana kukuweka katika jaribu la kutotenda haki, damu inapomwagika uendelea kulia juu ya ardhi maisha yote.

Epuka kikombe hiki ewe Mwanadamu uliyekabidhiwa madaraka, usijioni shujaa kwa kufumbia macho uovu maana uovu utaambana nawewe ndotoni ukiwa umelewa au upo soba. Naamini wenye dhamana mmeelewa ninalomaanusha, hakuna boss wakudumu-asipopita yeye utapita wewe nakuwaachia wengine. Usimtegemee Bali simamia haki.

Natama mnielewe, natamani familia zenu ziwaweke kwenye maombi mweze kuelewa umuhimu wa UHAI wa Mwanadamu.

R.I.P wote mliotangulizwa na wenye uchu wa madaraka huku wenye dhamana wakipindisha ukweli na kutangaza uongo wakiamini mmelala milele.
 
CCM na viongozi wake wamekosa uhalali wa kuongoza Tanzania na Watanzania. Hiki chama kimekuwa ni chama cha kishetani kabisa.
Ni ushetani tu unaoweza kufanya hayo yafanyikayo huko Tanzania.

Mustakabali mwema wa mimi, wewe, yule, hao na wale ni kuhakikisha CCM inatoweka katika medani za siasa.
 
Back
Top Bottom