Ni mengi ya kutafakarisha yametokea tangu Magufuli awe Rais, na kila siku wengi wetu tunajifunza mapya na kukumbuka mengi.
Nasema ni shukrani maana katufungulia na kutufunulia mengi kuhusu Tanzania na zaidi kuhusu sisi kama Taifa na wananchi wake.
!
Nimerejea kauli yako nikabaini ilikuwa na maana pana kuliko ufupi wa mistari yake
Tunajifunza mapya. Kwa walioishi kipindi cha Mwalimu na waliofuata kuna mengi wanapaswa kujifunza kuliko waliyojifunza
Nimekumbuka hili la mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa(RC)
Kiuhalisia kamati ni utaratibu wa kiutawala katika ulinzi na usalama (admin)
RC ni mjumbe kama alivyo kamanda wa mkoa au kanda na wanakamati wengine
Kamati ni chombo cha kiutawala siutendaji. Watendaji ni pamoja na vyombo vya dola kama Polisi
Polisi wana utaratibu wa mamlaka zao na zimeanishwa kuanzia ngazi ya chini hadi ya Juu
RC anapoingia ''barracks' na kuchukua majukumu ni jambo jipya la kujifunza
RC kama m/kiti angeweza kupeleka salam kwa kutumia wajumbe kutoka vyombo vya dola ndani ya kamati yake. Hao wangeweza kuwasiliana na 'timu' zao kupokea salaam
Polisi ni sehemu ya wizara ya mambo ya ndani. Taratibu za maeneo hayo zipo
Tunaposikia kuna msemaji wa wizara, katibu mkuu, waziri, IGP,Msemaji wa Polisi, RPC, OC n.k. si jambo la bahati mbaya. Viongozi hao wapo kwasababu maalumu za kisheria na kiungozi
Leo askari wanaposerebuka kambini na RC, viongozi wa wizara na jeshi wanakuwa katika hali gani! Pengine ndiyo maana hawazungumzii au hawaoni umuhimu wa tukio au wamekwazika
Hata hivyo, busara ingetumika zaidi kuliko ilivyotokea. Kupongeza si jambo baya, lakini je, linafanyika kwa wakati gani?Je, kitendo kile kilifanyika sehemu, wakati na watu muafaka?
Je, ni busara kuipongeza Simba kwa kuwafunga Bacelona wakati Askofu anasoma misa ya mazishi? Wakati sheikh anafanya hitma ya msiba?
Sherehe wakati wa matokeo kutangazwa Ukonga na Monduli zinatoa picha mpya ya zama hizi
Kuna hisia hisia katika jamii kuhusu mahusiano ya Polisi, wananchi, wanasiasa na jamii.
Ni hisia tu zinazoweza kutokuwa na ukweli au kuwa na ukweli
Aliyewahi kuwa IGP kabla, alikemea tabia ya wananchi kusherehekea maafa kama yale ya mkoa wa Pwani. Zile hisia za mahusiano ya jeshi na wananchi zikaanza kuonekana na ufa wake
Kuna hisia kuhusu Tume ya uchaguzi na uendeshaji wa chaguzi nchini
Ukikusanya mazonge zonge yoote hayo utabaini RC amesaidia kuondoa shaka dhidi ya hisia(doubts). Kwanza, ameikwaza serikali na kutoa picha isiyopendeza.
Pili, ameikwaza wizara na kuleta mkanganyiko wa madaraka. Tatu, amelikwaza jeshi kwa ''ushahidi' dhidi ya hisia, na Mwisho ameikwaza tume ya uchaguzi kwa kuijengea taswira tofauti
Haya yote tunajifunza, kwa miaka 23 ya Mwl pengine yalifanyika, lakini sasa yanafanyika hadharani mchana bila hofu tena kwa kugonga glass bila kusoma hisia au uso wa jamii.
Ni jambo la kujifunza, kwamba, tunadhani tunaelewa kumbe yapo mengi tusiyoyaelewa.
Tunajifunza kuwa, tunaweza kuwa na amani na utulivu, tukaamua kufikia maendeleo yetu haraka kwa njia za mkato bila kuwa na ukiritimba wa nidhamu (discipline)
Namshukuru
Rev. Kishoka kwa mada yake, tunajifunza