Mkuu Zakumi, with due respect this is anachronism. Usiniwekee ''maneno mdomoni'' ndiyo maana hufanyi 'quote' ili iwe rahisi kumchanganya mtu anayesoma bila kujua nini kilisemwa (dishonest)
Nilichokieleza kuhusu Mohamed kimetoka katika kitabu chake nikionyesha 'contradiction'
"Zakumi, post: 30038204, member: 12016"]Ngoja nionyeshe mapungufu ya uchambuzi wako. Nyerere kazaliwa 1922. Hivyo mwaka 1948 alikuwa na miaka 26 tu. Hivyo bado alikuwa kijana sana kusema kwamba alikuwa na mchango mkubwa kwa TAA.
Sijasema, nimekariri maneno ya kitabu na mijadala tuliyokuwa nayo na Mohamed. Nilimuuliza swali, ilikuwaje Nyerere akiwa katibu wa TAA Tabora alifika katika mkutano mkuu Dar, halafu Nyerere huyo huyo akaandikwa kufika Dar kwa mara ya kwanza 1953? wewe unajibu?
Nikauliza alipokuja katika mkutano mkuu ambao viongozi walikuwa akina Abdul hakukutana nao akiwa katibu wa Tawi kuu la Tabora? angalia kuna alama ya kuuliza, si kauli.
Haya yapo katika kitabu chake na mijadala, sikutafiti, sijaandika. Mohamed hakuwa na jibu!
Pili Nyerere alikuwa masomoni Makerere mwaka 1943 - 1947. Hivyo aliondoka akiwa na miaka 21 na kurudi akiwa na miaka 25. Hivyo katika kipindi ambacho alikuwa masomoni, alikuwa nje ya TAA. Hivyo huwezi kusema alikuwa anajulikana vizuri ndani ya TAA.
Sijaandika anajulikana TAA.
Nilichosema ni kuwa akiwa katibu mkuu wa Tawi la Tabora, definite alijulikana. Kulikuwa na matawi mangapi? Tabora ilikuwa na nafasi gani? Again nilimuuliza mwanahistoria hakujibu. Hayo unayoandika na maneno yako
Tatu, wakoloni walifuatilia wanafunzi walioanza kuwa radicalized na kuwanyima nafasi za kuendelea.
Kwa mfano Odinga Oginga naye alisoma Makerere na alionyesha u-radical wake na matokeo yake hakupewa nafasi za kuendelea. Hakuna sehemu zinazoonyesha Nyerere was radicalize akiwa mwanafunzi. Na kama angekuwa radical, nafasi ya kusoma Scotland asingepewa.
The same thing! Hakuna mahali nimeandika kuhusu unayosema hapo!
Nilichofanya ni nukuu ya kitabu ndiyo maana nimetumia neno ''critic' kwa kuonyesha kuna kitu kinahojiwa
Nne, Nyerere alikuwa Masomo Scotland kuanzia 1949-1952. Hivyo ukiondoa kipindi alichokuwa Masomoni Makerere, utaona kuwa Nyerere alijitokeza sana kwenye siasa akiwa na zaidi ya miaka 30. Alianza shule akiwa na miaka 12. Alimaliza O level akiwa na miak 20 (1942). Baada ya hapo alikuwa Makerere mpaka 1947. Hivyo katika kipindi cha miaka yake 30 ya mwanzo ni mwaka 1948 alikuwa mfanyakazi anayejitegemea na ambaye angeweza kushiriki kwenye masuala ya kisiasa. Zaidi ya hapo alikuwa ni mwanafunzi.
Well, unamueleza Mwanahistoria si mimi. Mimi natumia kitabu kilichoandikwa
Pengine nikusaidie hoja, Mwl alizaliwa 1922, kwa miaka 30 unayosema ilikuwa mwaka 1952, mwaka mmoja kabla ya kupewa uongozi. Hii ni tafakuri tu na ndipo ninapoweza kuonyesha matundu ya hoja (between the lines)
Tano, Nyerere aliporudi kutoka masomoni (Scotland) alitaka kuanzisha chama chake. Kama yeye alikuwa anajulika ndani ya TAA kwanini alikuwa na nia ya kuanzisha chama chake? Ni wakina Kambona walioshawishi ajiunge na TAA na watu wakamwachia nafasi.
Kitabu kinasema alikuwa katibu wa TAA Tabora. Na kitabu kinawataja akima Mwapachu ndio waliomshawishi kuingia siasa za TAA.
Sasa kama kuna Kambona hiyo ni sehemu ya historia unayotueleza pengine tusioijua.
Narudi kule kule maelezo yangu yanatokana na mijadala na kitabu cha MS
Sita, kwa mujibu wa Kambona. Na maneno haya aliyesema aliporudi 1992 na hakuna mtu aliyekataa. Kambona alisema kuwa baada wakoloni kumwambia Nyerere achague kazi ya kufundisha au kuwa mwanasiasa, Nyerere alitaka kurudi kufundisha na kuacha TANU. Ni baada ya wazee kumwambia kuwa watamlipa posho na kumwakikishia maslahi yake ndipo aliondelea na shughuli.
Ahsante kwa maelezo, lakini haijawa hoja yangu popote pale
Naheshimu sana mawazo yako, hata hivyo ni vema ukifanya 'quote' kila unapojibu hoja badala ya kutunga maneno na kisha kusema ni yangu.
Udhaifu wangu ni ule ule kwamba, huwa siongozwi na grudge, naheshimu kazi ya mtu bila kujali dini, kabila au rangi. Kwangu ''intellect'' ni muhimu sana na hilo linanisaidia kutosoma vitu kama noval, kujenga hoja kwa mantiki na kubwa zaidi kutumia vizuri kaubongo kangu kadogooo
Mjadala na MS unajulikana hapa JF, tumekuwa naye miaka mingi. Vitabu vyake vimesaidia sana kufungua sehemu ya historia ambayo haikuwa wazi hasa kwa watu wa Pwani.
Lakini pia kupitia mijadala na MS, tuliweza kuonyesha uimara na udhaifu wa alichoandika, hasa kuonyesha matundu kwa nia njema ya kumsaidia na kusaidia wasomaji ambao wengi walibebwa na udini zaidi ya historia, wakashindwa kusoma between the lines, wakajenga chuki bila kujua
Nitakupa mfano. MS anasema baada ya Uhuru Nyerere aliwatupa wenzake wote aliokuwa nao katika harakati na aliowakuta katika harakati hasa Waislam.
Ni kweli kabisa, kwasababu hakuna mahali Abdul Sykes alionekana tena katika siasa baada ya Uhuru na wengine wengi. Apparently Nyerere ni mtu mbaya kwa wanaosoma tu bila kujua
Tulimuuliza MS, baada ya Uhuru, 98% ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya TANU walikuwa Waislam, nini ilikuwa role yao katika kukabiliana na mwenendo wa Mwalimu? MS hakuwa na jibu hata moja
Je, kwanini AMNUT na Abdul hawakufanikiwa? Kwanini hakuungwa mkono na Waislam katika hilo?
Akahamia kwenye EAMWS ilivyo uawa na Mwl. Tukamuuliza hayo yakitokea 98% ya halmashauri kuu ya TANU ilikuwa waislam, walifanya nini? Hakuwa na jibu.
Maswali haya si kupinga au kumkomoa MS, ilikuwa kumuonyesha matundu, kwamba, kuna chuki dhidi ya Nyerere, could be right or wrong, hata hivyo kuna matundu katika historia kwa kushindwa kuonyesha Halmashauri kuu na udhaifu uliopelekea Mwl kuwa na nguvu zaidi ya 98% ya wajumbe. Usaliti miongoni mwa wazee wake!!!
Mtu akiongozwa na prejudice ,reservations etc, anapunguza intellectual capacity, hawezi kuona tofauti
Mapungufu hayo yanakuwa compensated na fabrications and hyperbole.
Wazungu wanasema '' the devil is in the detail'' you will never see it if you don't read between the lines with sober mind