Thanks God for Giving us Kikwete

Thanks God for Giving us Kikwete

Jamani mumemuelwewa vibaya,sio kama anamsifie Kikwete,someni upya mutafahamu nini anamaanisha.
Ni tungo tata mno inayohitaji uyakinifu kuipembua,hicho ni kiswhili cha mafumbo.
Mungu wabariki wazaramo.
Is this another crusade??? Huyu mchungaji nina wasiwasi na kondoo anaowachunga... leave us alone rev!! mchungaji siku zote huchunga kauli zake na hana lugha ya matusi.Ila kishoka... labada anawachunga wafuasi wa shetani
 
Is this another crusade??? Huyu mchungaji nina wasiwasi na kondoo anaowachunga... leave us alone rev!! mchungaji siku zote huchunga kauli zake na hana lugha ya matusi.Ila kishoka... labada anawachunga wafuasi wa shetani

Hata wafuasi wa Shetani ni watoto wa Mungu waliopotea kama wewe...
 
Rev,

Mimi ningeenda mbali zaidi nikasema tumshukuru Mungu kwa viongozi wote hata wale waliopita.

Kila awamu ilikua na fursa zake na changamoto zake kutujenga sisi kama Watanzania.
 
Wakati mwingine kiongozi anaweza kuchaguliwa na mungu halafu asiongoze kwa kusudi la mungu. Hapo ndipo yanapomkuta mamyo yanayofanana na matukio ya sasa.

Wakati mwingine kiongozi kama kikwete huchaguliwa na mungu(mzembe mzembe kama wengi wanavyosema), namungu anacha iwe hivyo ili mabo fulani yatokee kama vile richmond,kagoda, halafu watu wafunguke macho na kuona what is going on, na kulalama kama tunavyolalama. Na kwa vyovyote viongozi wakishajua wananchi wamestukia dili wataacha ufisadi. So huenda kikwete ni chaguo la mungu.

Mungu bariki Tanzania, wabariki viongozi wake. Amen!
 
Watanzania hatuna budi kumshukuru Muumba kwa kuruhusu JK akawa madarakani maana ni kioo halisi chenye kuonesha dira yanchi yetu!mambo ya kupuuzia, na kuwa na visasi visivyo na maana kwa wanaodai haki zao mf.madakitari na walimu.

Kwa ufupi wanamapinduzi tunatakiwa kumtumia sana huyu mheshimiwa ni kiungo muhimu sana kwa ukombozi wa nchi hii,maana kamba hukatikia pembamba, na kwa huyu muheshimiwa ndipo tunapopata point nyingi, anapojiachia na kufanya mambo too personal hapo ndipo ulipo ukombozi.

Huyu bwana ni sawa na beki anayejifunga, beki ambaye akibanwa anajifunga mwenyewe,maamuzi mengi anayoyafanya yakitumiwa vizuri kwa wanamapinduzi ni hakika magamba tamati yao ni hapo 2015, hivyo inawezekana ni mpango wa Mola kumuweka JK madarakani ili tujikomboe wenywe, hivi forward ukipata beki uchochoro si unafurahi?

Basi tuache kutukana giza, na tuwashe mshumaa, mwenye masikio na asikie
 
Duh! sugi, umechakurachakura weee! mpaka hii post ya Rev.Kishoka umeipata. Na Rev. walahataki ku"edit" post yake ya kwanza ya uzi huu.
 
Last edited by a moderator:
Asante Mungu kwa kutupa JK! ndo mchango wangu mfupi kuunga hoja! imetusaidia kujua madhara ya kuweka viongozi na uongozi mbovu kwenye nchi. somo letu ni kutokurudia tena makosa haya yaliyopelekea mpaka mtu kama JK kuwa rais wa nchi
 
Katika hiki Kitab Alf Layla wa Layla, napenda kutoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu, Subhana Wataala kwa kutupa Jakaya Mirisho Kikwete kuwa Raisi wetu.

We need to thank God for so much blessings to have Kikwete as man in charge.

Yes I have been critical of his leadership, I have mocked him, I have challenged him for his in-activeness and forgot that it was blessings in disguise from our Lord God!

Mungu ni wa ajabu sana, na nafikiri ni mapenzi yake tumepewa Kikwete awe kiongozi wetu. Ni mapenzi ya Mungu leo hii tupo hapa tukipiga kelele na baragumu tukitumia vinubi, zumari na tarumbeta kufukuta hasira zetu, vilio vyetu, aibu yetu na umoja wetu.

Si kwa mapenzi yake Jakaya Kikwete, bali ni mapenzi ya Mungu, kuwa yanayotokea sasa hivi, yalipangwa mapema na Mola.

Nasi tumkubali Jakaya Mrisho Kikwete kwa mapungufu yake yote, ukimya, uzembe, uvivu, uzubaaji, kutokuchangamka, kutokuwajibika na dhana kuwa analinda wale wahujumu. Mapungufu yake, ndiyo ngao na silaha yetu tuliyopewa na Mungu dhidi ya wale wenye kutaka kutufanyia dhuluma na kutuumiza.

Kuporomoka kwa Mawaziri wakubwa na mashuhuri wanne si mapenzi yake Kikwete, maana alitoa machozi. Lakini ni mapenzi ya Mungu leo hii nchi nzima si vilio kuhusu ufisadi tuu, bali mazungumzo ya kutaka uwajibikaji, mazungumzo ya kuimarisha ufanisi, na kulitakia Taifa letu maisha mema na Baraka za Mungu ndiyo yaliyotawala.

Tunataka mshikamano, tunataka uongozi madhubuti, tunataka tufaidi matunda ya utajiri wetu wa asili, uhuru wetu na matunda ya jasho letu bila kunyonywa, kudhulumiwa, kuonewa au kudhihakiwa.

Haya yote yasingetokea kama Kikwete wetu, mtalii, Vasco Da Gama, Sinbad, Chekacheka, Kisura asingekuwa madarakani.

Najiuliza je tungekuwa na mwamko mkubwa namna hii wa kutetea haki zetu kama tungekuwa chini ya Nyerere? Labda ungekuwako, lakini tungekuwa na woga.

Najiuliza je tungekuwa na ukali namna hii wakati wa Mwinyi, yawezekana, lakini bado tungekuwa na woga.

Najiuliza tena tungekuwa na uwezo wa kuchambua mambo muhimu kwa Taifa letu, kuishupalia Serikali, kutafuta ushahidi na hata kuimbua Serikali yetu wakati wa Mkapa? tungeweza, lakini angetupuuza na angetumia ujeuri na dharau zake kutokutusikiliza.

Sidhani kama Kikwete ni msikilizaji mzuri, ila ni baraka za Mungu kuwa kujivuta vuta kwake ambao wengine wamekuita Uyakhe yakhe, Ukwerekwere na Usaigon, ndio umetusaidia sana.

Yeye mwenyewe sijui kama analijua hili, lakini tafadhali sana wewe uliye mwakilishi wa Mheshimiwa Kikwete unayepita kuchungulia JF wamesema nini, mnapoamka Ijumaa hii na kujiandaa na Gwaride la Muungano, mwambie Mheshimiwa Raisi, tunamshukuru Mungu kwa kuwa yeye ni Raisi wetu.

Mapambano yetu bado hayajaisha. Tuendelee kutumia kudra, rehema na baraka hizi za Mwenyezi Mungu, kuendeleza Libeneke la kutaka uwajibikaji, ufanisi, umahiri kupiga vita Uhujumu, Uzembe, Dhuluma, Umasikini, Ujinga na Maradhi.

Kila jamii ina njia yake ambayo Mungu kawatengenezea. Njia yetu ya Ukombozi ni wakati huu wa ndugu yetu Muungwana akiwa Raisi!

Tutumie fursa hii kupigana na wale mahasidi wasiotutakia mema, tuendeleze shinikizo letu kwa viongozi wetu wawe watii wa sheria, walinzi wa katiba, wafuata haki na wanaothamini utu.

Through Jesus Christ our Lord, Amen, Amen, Amen
Through Muhamed our Lord, Amen, Amen Amen
By the Grace of Allmighty Lord, Amen, Amen, Amen

Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania, Tubariki watoto wa Tanzania.

1) What has Alf lela u lela got anything to do with "shukrani kwa Mwenyezi Mungu"?

Or is it a mockery?

2) Muhammad is no one's lord. He is simply a prophet of Allah and we never worship him.

Instead of trying to be smart and making wrong instigations on Muslims, knowingly or unknowingly, you had better stick to what you believe, we will understand you better rather than trying to act smart with Muslims by making unwarranted mockery.
 
nadhani kuna aliyotegemea lakini yamekuwa kinyume
ha ha ........unaona mwenyewe post ilikuwa ya mwaka 2008..
2012 napenda kujua kama bado anaendelea kushukuru ?

Hajui bongo inaendelea kwa misemo na nahau kuliko kazi na matukio? Mpe habari! I did not expect anything therefore am not disappointed. Ingawa kwenye katiba ntasema....
 
Asante Mungu kwa kutupa JK! ndo mchango wangu mfupi kuunga hoja! imetusaidia kujua madhara ya kuweka viongozi na uongozi mbovu kwenye nchi. somo letu ni kutokurudia tena makosa haya yaliyopelekea mpaka mtu kama JK kuwa rais wa nchi

Na ameanza kutayarisha dynasty kwa kumweka mkewe na mwanaye kwenye NEC ya chama chake. Asante Mungu!
 
Hajui bongo inaendelea kwa misemo na nahau kuliko kazi na matukio? Mpe habari! I did not expect anything therefore am not disappointed. Ingawa kwenye katiba ntasema....


Ukienda kusema kwenye katiba naomba nipitie na mimi
Nina mengi ya kusema
 
1) What has Alf lela u lela got anything to do with "shukrani kwa Mwenyezi Mungu"?

Or is it a mockery?

2) Muhammad is no one's lord. He is simply a prophet of Allah and we never worship him.

Instead of trying to be smart and making wrong instigations on Muslims, knowingly or unknowingly, you had better stick to what you believe, we will understand you better rather than trying to act smart with Muslims by making unwarranted mockery.

The unfortunate of your accusation s that you were not even here when I wrote this, so you would not have understand anything or even my reference of Kitab!

For your information and those who may be curios to know about Kitab Alf, when I wrote this, it was my 1000 post and hence reference of Kitab Alf! now since you are angling into Udini, your focus has been simply relating the stories of the Kitab Alf and you do not see any relationship. Everyone has a style and unique way even perspective to write, so until when you can learn to understand the writer and his or her styling, then you can be in a position to admire the literature work of a writer.

As far as the Lord goes, again artistic reference and it has been used (charge me with plagarizing I will accept lifting someone else work)!
 
hee mchungaji bado unaendelea kushukuru tu....???

Kwa nini tusiendelee kushukuru? Maana hata katika udhaifu wake kama mtendaji na kiongozi, mengi yanafunuka hata kuhusu sisi kama Taifa na wananchi! Tujiulize kwa nini tulimpa dhamana tena 2010? Je tulikuwa tumelewa au ni upofu uliokomaa?

Yote haya yanayotokea, ni lazima yatokee na ni kutokana na namna ya uongozi wake, tunaweza kujipima kama Taifa na jamii kuona kama tuko kwenye mstari sahihi au tuanze upya.

Ni Fasihi dada yangu na ukweli ni kuwa jamii ni lazima ijitazame hata kutumia fasihi na kujitambua ala, kumbe nasi twachangia na si Kikwete pekee.

Nilipoandika Screw Muungwana, ilikuwa miezi michache baada ya yeye kuchaguliwa, na hata kabla hajaapishwa niliandika mada nyingine "Hercules..." nayo ikionyesha wazi maoni yangu kuhusu uwezo wake wa kufanya kazi na kuwa kiongozi.

Sasa ukirudi kuvisoma, utafikiri ulikuwa ni unajimu!

So bado namshukuru, maana si Kikwete pekee, bali hata wengine twaanza kuwatambua na tunaanza kujitambua kama jamii!
 
Back
Top Bottom