DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), imewataka wadau wa uchaguzi wakiwemo viongozi wa dini na vyama vya siasa kujiepusha na lugha za matusi, kejeli, ubaguzi na uchochezi, hasa wakati wa kampeni huku akiwasisitiza kutanguliza mbele masilahi ya taifa.
Wito huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa THBUB Mohamed Khamis Hamad Alhamisi Agosti 7, 2025 katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea Nzuguni Jijini Dodoma.
Amesema “Kampeni zifanyike kwa staha, hoja na maadili, tujiepushe na lugha za kashfa, matusi au zile zinazodhalilisha watu wengine, tukumbuke kuwa tuna wajibu wa kulinda taswira njema ya taifa letu na ya uchaguzi wetu," amesisitiza.
Aidha, Hamad amewakumbusha wananchi kuwa amani ni tunu ya taifa, hivyo kila mmoja anao wajibu wa kuilinda na kusisitiza kuwa wananchi wasikubali kuingizwa kwenye mihemko isiyo ya lazima, bali wazingatie sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa ili kuepusha machafuko na migogoro kwenye jamii.
Chanzo: Jambo Tv