Mnaongelea ilani za chadema, cha kushangaza ni kuwa kwa nini chadema wasiwekeze kwenye umeme? wanangoja nini? nani aliyewazuia na wao ni chama chenye wafuasi wengi na bajeti nzuri tu wanayo? ya kupewa hapa na serikali na ya kuletewa na chama cha demokrasia cha kikristo cha ujerumani.
Haiingii akilini chama hakina kutekeleza japo kimoja ya wanayoyalalamikia siku zote. Mngeanza kuonesha japo kwenye majimbo yenu ya uchaguzi tu, mkawapa umeme usiokatika saa zote, maji safi kaya zote, shule zilizosheheni waalimu, madawati, vyoo vya kisasa, maabara, mngeweka hospitali za kisasa kwenye jimbo lenu hata moja tu.
Mnabaki kulalama, kususa, kuandamana. Tuonesheni vitu hai ili tujuwe kweli nyinyi ni zaidi ya serikali ya sasa ili tuwape kura zetu haraka haraka. Nani asiyetaka maendeleo? mnatuchosha na mulalama kwenu kusiko kwisha bila kuonesha mfano hata mdogo tu. Bora hata mrema alikwenda kuileta kuileta kampuni ya umeme poa, ingawa haijafanikisha lakini tuliona kawaleta, alionesha jitihada za vitendo na si kulalamika tu saa zote.
Kama uongozi rahisi si tungeona ile hospitali anaeongoza katibu mkuu wenu ikiwa kama mfano wa kuigwa? kiko wapi? ukienda pale ni foleni kuanzia asubuhi mpaka saa kumi jioni lakini ukitoa kitu kidogo unapelelkwa kumuona dokta mbio mbio, au hamlijui hilo? Na ndio katibu mkuu wenu kiongozi wa pale, au kaacha kwa kugombea urais alioukosa?
Zomba ijapokuwa hii posti umeiweka kisiasa lakini mie naomba nikujibu kitaaluma zaidi.
Umesema watu wamebakia kulalama lakini hawatoi njia za kufanya kufikia malengo mie nakupa mfano mmoja wa solution ya hili tatizo nao ni ukata wa fedha.
Stiegler Gorge project yenye kuzalisha 2100 MW inakisiwa kugharimu si chini ya $2 Billion (Reuters, Dec 2010). Tunaambiwa Brazil watashiriki ujenz by 2015 tutaanza kuenjoy (statement iliyotolewa na Mh Bernard Membe na Somebody Aloyce Masanja (mwaka jana)).
Kabla serikali haijaenda kukopa huko inaweza kuzipata hizo $2 Billion kwa kubana matumizi yake ya uendeshaji wa serikali na bunge. Sehemu moja ni posho za wabunge na viti maalum.
Inakisiwa mbunge anapata 70,000 akiwa kwenye vikao vya bunge= Bunge la Budget hukaa vikao 73 na hivyo kila kikao Jumla ya gharama za Bunge na Serikali ni Tshs 1.788 Billion per year = 1.788 x 5 = 8.9425 billion / $1=Tshs 1608 = Final figure after 5 years assuming exchange rate is constant is $ 5.561 Million serikali will save.
Viti maalum kuna wabunge 102 ambao kila mbunge hulipwa stahiki ya Tshs 7.3 Million kila mwezi. Wakiamua kufuta viti hivi maalumu (jambo lililo ndani ya uwezo wao itakuwa kama ifuatavyo:-
102 x 7, 300,000 = 744,600,000 kila mwezi.
Mwaka = 8,935,200,000
Miaka 5 = 44,676,000,000
Sawa na USD =44,676,000,000/1,608 = $27,783,582 + $5, 561, 000 = $33, 344,582 mpaka hapa
Matumizi magari ya mawaziri pia yatasaidiwa kupunguza gharama za serikali . Landcruiser V8 linakisiwa kugharimu milioni 250. Kuna wizara zaidi ya 29 ambazo zina mawaziri , manaibu waziri wawili hadi watatu, na makatibu wakuu. Tuchukulie a standard ratio ya naibu waziri mmoja .
250,000,000 x 87 (29 x 3 (waziri, naibu na katibu wake))= 21,750,000,000 (mawaziri hawa wanaweza kukopeshwa hela wanunue magari yao binafsi au watumie usafiri wa jamii au madaladala au mabasi kama nchi za ulaya wanavyofanya) mfano Waziri wa biashara na viwanda Uingereza Vince Cable anaendesha baiskeli kwenda kazini)). Hivyo tunasave:-
21,750,000,000 /1608 = $13,526,119 =13, 526, 119 + $33,344, 582 =$46,870,701
Pia Ukimuisha na usimamizi mbovu wa matumizi ya serikali kwa mwaka unaokisiwa kufikia 2,415,670,026,437/ 1608 = $1.5 Billion
Total saving tunazipata ni $1.5 Billion + $0.046 = $1.55 Billion - $2 Billion (gharama za ujenzi) = tunabakia na $450,000,000 (kiasi kinachoweza kupatikana kwa kubana matumizi kwenye kila wizara na idara ya serikali.
Hivyo Zomba mradi huu tunaweza kuulipia wenyewe pasina msaada wa Brazil wala World Bank. Serikali inaendesha shughuli zake , kodi itakusanywa na pesa za kujenga Dam ya Rufiji zitapatikana kwenye kusimamia pesa za serikali na kubana matumizi. Labda nikuulize je serikali hii iko tayari kwa hilo. Tatizo la umeme linaweza kusababisha serikali hii ifilisike kama hawatakuwa waangalifu. Hatulalamiki ila tunajaribu kutahadharisha mwenye akili atatafakari asie nazo hatajali ila siku janga likifika tutakaoumia ni sote.