Je, Mdahalo huu utakuwa kwa manufaa ya wananchi wa kawaida wa Kenya waelewe wagombea urais wanataka kuifanyia Kenya nini ili wafanye uamuzi wa busara yupi wampe kura au mdahalo (debate)ni maalum kuwaridhisha wafadhili wa nchi za Magharibi (Google, CNN, Reuters etc)?
Je wagombea wataweza kujieleza vizuri kwa Kiswahili ili wananchi walio wengi waelewe mipango, sera na ahadi za wagombea urais au wagombea watafanya mdahalo kwa lugha ya Kiingereza kwa ajili ya elite class ya Kenya ambao ni wachache?
Nashauri NTV managing editor Linus Kaikai na Julie Gichuru wa the Royal Media Services wafanye safari ya haraka kuja Tanzania tuwapatie uzoefu tulionao wa midahalo (debate) toka mwaka 1995 ili umma wa Kenya unufaike na zoezi hilo muhimu.