The 2nd 2013 Kenyan Presidential Debate.

Hivi kuna ugumu gani kwa uhuru Kenyata kusema kiasi cha ardhi ambacho familia yake inamiliki

Dida anamning'iniza ishu ya ardhi Kiambuu ambako Uhuru anatoka

Uhuru anazunguka zunguka tu
Hapa kwangu mimi amechemka
Tatizo ku pasta ushahidi ni Ngumu hakuna asijua Kuwa Kenyatta family wanamiliki arhdhi kubwa
 
Dida hana hata ndugu na jamaa wa kuuza sura nao?!?
 
Tatizo ku pasta ushahidi ni Ngumu hakuna asijua Kuwa Kenyatta family wanamiliki arhdhi kubwa

Yeye kasema kwamba mambo yote iko wazi kwa ofisi ya Tume ya Maadili ya kwao. Ambapo utangaza mali zao wanazomiliki.

Kumbuka lakini kasema pia wana ekari elfu 30 pale Taveta!!
 
Yeye kasema kwamba mambo yote iko wazi kwa ofisi ya Tume ya Maadili ya kwao. Ambapo utangaza mali zao wanazomiliki.

Kumbuka lakini kasema pia wana ekari elfu 30 pale Taveta!!

By the way sijaangalia TV hakuna umeme umekatika, Mudavadi amesema nini kuhusu Uhuru any attack? Especially kwenye land issue?
 
Huku kwetu nilianza kunogewa na huo mdahalo mara Tanesco wakachukua umeme wao mpaka sa hii ni giza totoro
 
Kwa mujibu wa michango yenu; inaonekana kuwa mgombea Dida anafanana na yule mgombea wa UPDP 2010 Fahmi Dovutwa.
Huku kwetu Tanesco na mgao wao usio haya wala rasmi, wamerudisha umeme karibia saa nne!
 
Ana wake 3 kidume

Ana watoto 11 wa kwanza ana umri wa miaka16 . Dida mwenyewe ana aka 39 hadi kufika aka 50 si ajabu atakuwa na watoto 30 iwapo atakuwa na wake hao hao watatu,chezea somali wewe,nyota ya kijani kwake ni kama mbwa na paka
 
Lol...kila mtu naona analalamikia umeme wa TANESCO.

Kwani mnaishi wapi nyinyi?
 
???TBC, duh mbona huwa wanaacha kuonesha yanayotuhusu kwa nini kukimbilia ya Kenya?
............si ndio akili zinakuja, Jk mwiteni majina yote Vasco, Dhaifu etc, lakini kuhusu uhuru wa vyombo vya habari, tutamkumbuka.
 
Kwa nini yeye tu aseme? Kwa nini wote wasiseme ili iwe fair kwa wote. Na wanavyoifanya iwe ni kama vile ni jinai kumiliki ardhi.
...........ndugu yangu Nyani, nini kigeni kwako ama ni ushabiki tu? hujui nini kuhusu Kenyata (baba) alivyotaifisha ardhi ya wakoloni by then na kujimilikisha? hiyo ndiyo Kenyata (mtoto) anayosema amerithi, ekari zaidi ya laki tano, wengine hawana hata plot, halafu wewe unataka uwaongoze hawa, sijui ni busara gani inayomuongoza huyu tajiri wa 23 Africa (Kenyata-mtoto)...
 
Kheee...hujawaona wale wamama wawili waliovaa ushungi mweupe? Nadhani ni wake zake wale...

Nilikuwa sijawaona wakati naandika. Nilimwona akizubaazubaa, nikadhani hana ndugu aliyekuwepo ukumbini.

Ila jamaa ni mkali, yaani miaka 38, halafu wake watatu au wanne!!

Cc: Balantanda
 
Last edited by a moderator:
By the way sijaangalia TV hakuna umeme umekatika, Mudavadi amesema nini kuhusu Uhuru any attack? Especially kwenye land issue?

Mdahalo ulitumia muda mwingi kiasi katika suala la ardhi na rushwa.

Katika ardhi hoja ilikuwa ni umiliki wa kufuru wa vipande vya ardhi kwa ukoo wa Kenyatta. Uhuru alishindwa kusema kwa uwazi yeye na familia ua Kenyatta wanamiliki ardhi kiasi gani? Alisema hizo ekari elfu 30 tu wakati akijibu swali la Martha.

Mudavadi yeye alisema anamiliki kama ekari 150, zinazojumuisha na vipande vya ardhi vya urithi.

Raila alimng'ata huku akimpuliza Uhuru pale aliposema kwamba watu wasimnyooshee kidole Uhuru kwa ardhi ya kurithi. Lakini akamkandamiza na hoja ya kwamba, tatizo siyo umiliki na urithi huo, tatizo ni kwamba Kenyatta's waliwatenda wapigania uhuru, waliokuwa na ahadi na ndoto kemkem za kupata vipande vya ardhi baada ya kupigania uhuru. Cha kushangaza the Kenyatta's wakiwageuka wapigania uhuru hao na kujichukulia vipande vingi na vikubwa vya ardhi.

Katika hilo la ardhi, Uhuru alikuwa mdogo kama piriton.

Ni hayo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…