The 60 meter exclusion zone rule is outdated and impractical for our cities

The 60 meter exclusion zone rule is outdated and impractical for our cities

Na anapoandika kwa lugha ya "yai"anafikiri yule jamaa wa "elimu ya hapa na pale" ataambulia kitu?
Wewe na wanaokuzunguka mmeambulia kitu? Issue ya maana unaleta ujinga
 
Ali Mafuruki ni mnafiki anapiga yowe coz anajua amejenga viwanja vya wazi na kwenye mkondo wa mto,infotech japo kiwanja kimepimwa lakini ni magumashi kipo sehemu ya maji...Avunjiwe ye si alikuwa Ana support ccm? Avunjiwe tu.
Mhhh "Kimepimwa" halafu ni "Magumashi" haviendi pamoja kwa uelewa wangu kupimwa ndiko kunakouondoa huo umagumashi
 
Huu ni Ubinafsi mkubwa sana wa Ali Mafuruki na sababu kubwa ya yeye kuandika hivi ni kwamba ni mfaidika wa land grabbing anamiliki jengo la Infotech pale Kawe Mlalakuwa karibu na roundabout ambalo kwa hali ya kawaida halikupaswa kuwepo pale, hivyo siyo kwamba ana machungu na WatanZania wa Mabondeni bali ana machungu na mali yake!

Ningewaomba sana WatanZania mtenganishe watu waliokweli Wazalendo na wanaofanya fanya mambo kwa kusukumwa na utu dhidi ya wale ambao kama Ali Mfuruki ambaye ni muathirika na anafanya mambo kwa ajili ya maslahi yake binafsi, laiti kama asingekuwa muathirika angekuwa wa kwanza kushabikia hii bomoa bomoa!

Nasema BOMOA!
Mkuu unahangaika sana
 
Wewe na wanaokuzunguka mmeambulia kitu? Issue ya maana unaleta ujinga
Sio ujinga,ila kwa akili za hapa na pale ndio unaweza kuona ujinga.sasa tusipoambulia kitu tutawezaje kuchangia issue na hii ni open and free forum?na pia tuna wabunge viongozi wetu kama wabunge sio wote wanaoielewa fluently(na sio lazima kuielewa sana kwa kuwa sio lugha ya taifa)na iwapo makala husika hawajaielewa wanawezaji kunyonya humo vitu vya maana ili wakajenge hoja huko?Usipanick mkuu,mwiba ukikuchoma uchomoe songa mbele.
 
Hawa jamaa hawatumii brain zao ku-tame nature bali wanatumia zaidi brain zao kuua upinzani kwa faida yao.

Wanapoenda kwenye nchi za wenzetu wanapaswa kujifunza na kuiga yale yaliyo mazuri na kuyaleta hapa nchini.

Nini faida ya viongozi wetu kupata exposure za kila siku kama zinakuwa hazina tija?
Kwa kweli maamuzi ya bomoabomoa ni doa kubwa kwa Serikali ya Magu. Wanataka kumwaribia!!. Katika Jiji la New Delhi kuna malazi yasiyo rasmi (slams) yapo karibu kabisa na Ubalozi wa marekani, yaani pua na mdomo lakini serikali ya India imewaacha hapo wakiendelea na maisha yao, walichofanya ni kuboresha slam hiyo na wananchi ambao ni maskini kabisa wanaishi hapo. Kuna documentary moja nilioona nadhani aljazeera au BBC jinsi serikali ya Colombia inavyoboresha slams zilizopo milimani na mabondeni katika Jiji la Bogota. Wameboresha slams kwa kujenga barabara za kisasa za juu na chini za magari na treni (metro) pia wameweka escalators pamoja na lift ambazo zinasaidia slam dwellers. Nikipata hiyo documentary nitaweka hapa. Aidha, jirani zetu Kenya tumeona walivyofund project kubwa ya kuboresha kibera slam ata UHURU kenyata alikwenda kufungua project hizo huko kibera, ambazo ziliboresha kibera kwa kujenga miundo mbinu. Serikali Makini duniani azidemolish makazi ya watu maskini waliojenga holela (slams) lakini uboresha na kuyafanya kuwa makazi salama na ya kisasa na rasmi. Watu zaidi ya 200,000 ni wengi mno!, huu ni mtaji tosha wa kura! We have to use common sense sio nguvu nyingi!
 
Akili ndogo plus chuki dhidi ya wenye nacho ndo inakusumbua. Walioziba njia ni matajiri au masikini ambao ndo wamejenga kwenye maeneo yasiyo pimwa? Hakuna anayepinga kubomoa baadhi ya structures ili kupisha shughuli za maendeleo. Hoja ya Mafuruki ni kujaribu kuangalia sababu hasa ya bomoa bomoa inayo endelea .Anasema solution siyo kukimbia maji bali kuyatengenezea njia nzuri ya kipita. Soma vizuri uelewe hoja ya msingi.

Wewe na Mfuruki wote ndiyo hamna akili! Ila nina wasi wasa Mfuruki amekuzidi akili kidogo kwa maana unashindwa kuelewa anachotetea nini, Mfuruki anateteta Mali zake, Jengo lake ambalo amelijenga sehemu isiyo ruhusiwa sasa sijui wewe unateteta nini?!

Uliona wapi Dunia hii watu wanajenga kwenye njia asili za maji halafu wanasema suluhisho ni kuyatafutia Maji njia nyingine? Hiyo ni akili au matope? Hata wanyama wanaelewa kwamba huwezi kucheza na nature!
Hivi unaelewa kwanza hata geografia ya Mji wa Dar ilivyo? Unafahamu Maji huwa yanatoka wapi na yanakwenda wapi? Na Wazungu ambao wana uzoefu na mafuriko nchini mwao waliku ni wajinga walivyoweka Mito yote kwenye ramani? Na unafikiri msemo wa maji hufwata mkondo wake hauna maana yoyote?
 
DSC_1437.JPG
We ni muongo hufai angalia hiyo picha ya Norway hapo ni meter ngapi toka mtoni huo mji unaitwa troneharm pale karibu na kanisani kama ulishafika Norway ni sehemu maarufu hapo kanisani.Mafuruki yuko sahihi asilimia 70
 
kuna watu wanaponda andiko la mafuruki ila ukisoma kitaalamu haya ni moja ya mawazo bora kabisa kwa hili tatizo, big up mafuruki yani nimesoma nikarudia tena kusoma taifa linahitaji vichwa kuendelea sio kazi mtindo ule ule
 
Wewe na Mfuruki wote ndiyo hamna akili! Ila nina wasi wasa Mfuruki amekuzidi akili kidogo kwa maana unashindwa kuelewa anachotetea nini, Mfuruki anateteta Mali zake, Jengo lake ambalo amelijenga sehemu isiyo ruhusiwa sasa sijui wewe unateteta nini?!

Uliona wapi Dunia hii watu wanajenga kwenye njia asili za maji halafu wanasema suluhisho ni kuyatafutia Maji njia nyingine? Hiyo ni akili au matope? Hata wanyama wanaelewa kwamba huwezi kucheza na nature!
Hivi unaelewa kwanza hata geografia ya Mji wa Dar ilivyo? Unafahamu Maji huwa yanatoka wapi na yanakwenda wapi? Na Wazungu ambao wana uzoefu na mafuriko nchini mwao waliku ni wajinga walivyoweka Mito yote kwenye ramani? Na unafikiri msemo wa maji hufwata mkondo wake hauna maana yoyote?

Mkuu..
Kwa hii hoja yako nakuunga mkono 100/100..

Hata siku moja huwezi kujenga kwenye mkondo wa maji ili badae uje hushauri serkali itafute njia mbadala kupitisha maji..
Mimi napenda kushauri wale wote waliopora maeneo ya wazi,majenzi kwenye vyanzo na mikondo ya maji Lisiwe ombi bali wavunjiwe bila mazungumzo..Hawa wakina "Mafuruki and alike" wamatabia zakishenzi sana..
Huku mbezi beach wapo wanaofanana na huyu jamaa wamepora maeneo ya wazi na kuziba baranara za mitaa,
Mh Lukuvi tunaomba hili zoezi lifanywe kitaalamu sababu wapo wengi wenye hatia..
 
kama nchi tunaenda kuingia kwenye chumi mkubwa wa gesi na mafuta mtwara na lindi, pamoja na majiji na miji yote bila kuandaa master plan na kudesign miji kwa viwango vya treni za umeme, underground tunels flyovers, skyscropers,8lanes highways, basi hiyo gasi na mafuta si mali yetu. tunawatunzia wenye nayo. nilitaraji lukuvi aje na mkakati wa kureview master plan za miji, kudesign masatelite city, badala ya kuhangaika na bomoabomoa ambayo haina manufaa wala mkakati wa uendelazaji sehemu zilizobomolewa,
Ile ni komoakomoa sio bomoabomoa nyie hamjaelewa somo
 
Mhhh "Kimepimwa" halafu ni "Magumashi" haviendi pamoja kwa uelewa wangu kupimwa ndiko kunakouondoa huo umagumashi
Kimepimishwa kimagumashi kwa kupindisha sheria,ukiwa na pesa kwa serikali iliyopita unakuwa juu ya sheria ona mwanasheria wa NEMC alivyolambishwa mchanga kwa kupindisha sheria.
 
Kw
View attachment 315932 We ni muongo hufai angalia hiyo picha ya Norway hapo ni meter ngapi toka mtoni huo mji unaitwa troneharm pale karibu na kanisani kama ulishafika Norway ni sehemu maarufu hapo kanisani.Mafuruki yuko sahihi asilimia 70
Kwa hiyo hata wazungu wote wakiamua kuwa mashoga na sisi tutaiga kwasababu inafanyika ulaya?Kabla ya kuiga lazima tutafakari mazingira na uchumi wetu unaruhusu hilo jambo?kwa mfano wa hiyo picha uliyoweka kwa Tz ikitokea janga hapo kwa ufinyu wa mbinu,vifaa na bajeti ya kukabiliana na majanga atapona mtu?
 
Pole mkuu Mfuruki !

Kwanza barua yako ndefu ! Lukuvi hawezi kuisoma
 
M
Kw

Kwa hiyo hata wazungu wote wakiamua kuwa mashoga na sisi tutaiga kwasababu inafanyika ulaya?Kabla ya kuiga lazima tutafakari mazingira na uchumi wetu unaruhusu hilo jambo?kwa mfano wa hiyo picha uliyoweka kwa Tz ikitokea janga hapo kwa ufinyu wa mbinu,vifaa na bajeti ya kukabiliana na majanga atapona mtu?

Mafuruki anachosema technology ipo ya kufanya hivyo tukiwa na better plan, Dar ina master plan? budget ni issue nyingine assume una pesa now utatekeleza master plan ipi? Tusikwepe hoja zake za msingi. Tungekuwa na dar master plan then hatuna budget ya kutekeleza ni sawa but haipo una budget for what? Unataka pesa ya kutekeleza kitu ambacho hakipo au kiwe kama kitengo cha maafa kila mwaka wanapewa budget hata kama maafa hayakutokea zinatumika tu na ya kitokea tunaomba msaada toka red Cross na international organizations
 
Last edited:
Kw

Kwa hiyo hata wazungu wote wakiamua kuwa mashoga na sisi tutaiga kwasababu inafanyika ulaya?Kabla ya kuiga lazima tutafakari mazingira na uchumi wetu unaruhusu hilo jambo?kwa mfano wa hiyo picha uliyoweka kwa Tz ikitokea janga hapo kwa ufinyu wa mbinu,vifaa na bajeti ya kukabiliana na majanga atapona mtu?
Angalia mipango ya miji mkuu katika hii link , , natumaini utajifunza kitu
 
Last edited:
Uzi mzuri, mada nzuri, ila lugha!. Mkuu Kibanga Ampiga Mkoloni, kama wewe umeelewa anazungumzia nini, ukitutafasiria sisi wa kina St. Kayumba, tutakushukuru na kuchangia!.

Pasco
Kaka mimi mwenyewe ni Copy and Paste sijaelewa, na ndio maana naona wachangiaji wamekuwa wachache sana.
 
Huu ni Ubinafsi mkubwa sana wa Ali Mafuruki na sababu kubwa ya yeye kuandika hivi ni kwamba ni mfaidika wa land grabbing anamiliki jengo la Infotech pale Kawe Mlalakuwa karibu na roundabout ambalo kwa hali ya kawaida halikupaswa kuwepo pale, hivyo siyo kwamba ana machungu na WatanZania wa Mabondeni bali ana machungu na mali yake!

Ningewaomba sana WatanZania mtenganishe watu waliokweli Wazalendo na wanaofanya fanya mambo kwa kusukumwa na utu dhidi ya wale ambao kama Ali Mfuruki ambaye ni muathirika na anafanya mambo kwa ajili ya maslahi yake binafsi, laiti kama asingekuwa muathirika angekuwa wa kwanza kushabikia hii bomoa bomoa!

Nasema BOMOA!
Kama lugha ya yai inapanda, utamuelewa Ali Mfuruki, mimi nimemsoma huku nimetulia nimemuelewa sana. Kwanza ameunga mkono bomoa bomoa zote katika road reserve, open spaces, unplanned areas na risky buildings.

Amesema anatatizwa ule umbali wa mita 60 toka kwenye njia za maji, tangu DSM City Master Plan ya mwaka 1968-1979 haijatekelezwa, na Master plan mpya ya 2012-2032 ambayo mpaka sasa haijapitishwa na huu ni mwaka wa 6!, hakuna popote ufafanuzi hizi mita 60 ni kwenye njia zipi za maji?. Amesema kama sheria hiyo ingekuwepo, tusingekuwa na beach hotel hata moja!, amesisitiza anatatizo na tishio la kuwabomolea watu mahekali yao kule beach na kuuliza, kwa kuyabomoa, serikali inataka kupata nini?, ametolea mfano mji wa Amsterdam, usingekuwepo, akatolea mfano jiji la London na majijini mengine, mto unapita katikati ya mji na hakuna tatizo. Hoja yake ni waliojenga beach, wapewe jukumu la kujenga miundo mbunu rafiki ya kuhifadhi mazingira ya maeneo yao na kutolea mfano Kunduchi Beach, Bahari Beach na Africana hotels, au kitu kinachofanyika barabara ya Ocean Road.

Mimi sina nyumba beach area lakini naungana kabisa na logic ya Ali Mfuruki. unawabomea watu mahekalu yao ili uhifadhi nini, wakati hayo mahekalu yanaweza kuwepo na mazingira kulindwa!.

Paskali
 
Back
Top Bottom