The Bachelor's Kitchen a.k.a Jiko la msela


Thanks a lot sister, but kuna kifaa sikijui jina nilikiona uganda nahisi hata bongo kitakuwepo, yaan nilifika sehem mtu akaandaa supu ikaletwa ipo kwenye kitu kama rice cooker na ilikuwa imetoka nzuri kweli, now ndo nimekikumbuka but sikijui jina nashindwa nikakitafute vipi. Kama unafaham jina ya hiyo kitu msaada please. Shuran sana hizo non sticky sufuria hopin kuosha ni rahisi sana, what about kuunga mboga kwa urahisi kifaa gani muhim?
 
Last edited by a moderator:
nunua jiko la gesi la auto ignation hili husaidia sana kuandaa chakula fasta sana..

Nalo halina mambo ya mitungi? Sipendi majiko ya gesi especially muda wa kubeba mtungi ukaujaze gas.. Hilo jiko lipo vipi?
 
kupika supu si ni kuchemsha tu, unahitaji jiko na ingredients
mboga unamaanisha salad au cha kulia wali au ugali?
usisahau na microwave, zipo zinazopika mazagazaga yote mpaka huo wali unaoununulia rice cooker

Yap yap hata salads tu muhimu, ni kifaa gani kinatengeneza fasta
 
Hahahaha, ukiwa na hii inabodi uwe na mke wa kijijini kwa ajili ya kuokota kuni. Ni vifaa muhimu kwa kweli,lol
hata hii kitu ni muhimu kuwa navyo kwa vyakulaa mbavyo ni vibishi kuiva . lol
 
Kuna vifaa vya aina nyingi, unakata different shapes. Ukienda supermarket angalia maboksi. Ama sabasaba. Japo best salad ni ya lettuce, parachichi na mayonaisse kiduchu.

Labda tunahitazi thread ya bachelors' foods?
Yap yap hata salads tu muhimu, ni kifaa gani kinatengeneza fasta
 
Wewe naye umefanya haraka kama unaandika huku umepanda baiskeli.............Hebu nenda polepole mdogo wako nielewe!! niachane na chukuchuku.......Tahadhari: usitoe twisheni ya mapishi yanayozidi dakika 15, nataka ya fastafasta

sasa hujaelewa nini? non sticky pot ni zile ambazo hazishiki uchau ni easy to wash, salad maker ni mashine ya kutengenezea salad hii itakusaidia usijikate na visu ama mikono kunuka vitunguu lol! plastic tins ma conytainers hizi hata njian huuzwa ni nzuri kwa kuhifanndhia vitu kwenye friji yaani friji haitakiwi kuwekwa vitu vikazagaa humo ndani vinaharibika. huwa vitu vinahifadhiwa kwenye hizi tins ama containers na hata vikae mwez haviharibiki manake viko salama. mfano mkate ukiuweka kwenye jokofu bila kuueka kwenye container iliyofungwa basi unakuwa mgumu na hupoteza ladha yake ila ukiuweka ukiwa ndani ya mfuko na ukaudumbukiza kwenye container kila siku utakula mkate fresh. hata nyanya na karoti ni hivyo hivyo. pia hivi vitapunguza frii yako kunuka.
 
atakuwa alitumia presha cooker, zipo za dizaini tofauti na ukubwa tofauti tofauti. mboga za kuunga hazina chombo zaid ya sufuria na mwiko na ndo mana nakushari utumie non sticky
 

Ni bora lakini ukajihadhari na matumizi ya visahani/vyombo vya plastic ndani ya microwave - kuna uwezekano wa kupata shida za kiafya huko mbele. Tumia vyombo vya melamine au glasi.
 
Nimesahau, non stick sufuria. Very easy to wash.

Hizi sufuria ndio muhimu kuliko vyote.
Hizi unaweza kuzitumia kama rice cooker n.k.
Kwenye kupika ni makini sana, na kwenye kuosha ni makini sana. Hupotezi muda, ladha ya chakula wala maji ndani ya chakula.

Pia usisahau miiko ya mbao ndio bora na salama kutumia kuliko aina nyingine za miiko au upawa. Ni salama kwa afya yako na kwa sufuria zako za non-stick.
 
Nalo halina mambo ya mitungi? Sipendi majiko ya gesi especially muda wa kubeba mtungi ukaujaze gas.. Hilo jiko lipo vipi?

Unaelekea wewe ni mteja mzuri wa TAA-NESI-KO; Ongeza water heater (Kenwood is my favorite brand), Na jiko la umeme lenye oven.
 
Hahahaha, ukiwa na hii inabodi uwe na mke wa kijijini kwa ajili ya kuokota kuni. Ni vifaa muhimu kwa kweli,lol

CHUNGU KINAFANYA KAZI KWENYE JIKO LOLOTE LIWE LA UMEME, GAS, KUNI HATA MKAA.
Chungu ni moja ya vifaa vya kupikia salama zaidi kuliko vingine vingi.
 
naomba na mimi nichangie,vitu muhimu kwa bachelor ziko in two categories,vyombo na ingredients
for a start tafuta microwave(inayoweza ku-grill),microwave safe containers(vikombe,sahani,na vibakuli),rice cooker,na gas cooker.fridge/freezer nayo ni muhimu kama utapenda,japo si muhimu sana,nitaelezea zaidi hapo chini.
katika upande wa ingredients,hapo ndani usikose oat meal,chumvi,nyama ya kusaga,spices,spaghetti,na tray moja la mayai.kwisha habari.rice cooker unaweza kuitumia kupikia hata mboga,unafungua mfuniko na unashusha kile ki-button kwenye cook.ila hakikisha ile sufuria ya rice cooker ina kitu ndani,kwa sababu ina-detect weight ndo ianze kupata moto.mimi nilikuwa natumia rice cooker kupikia hadi mboga.
hapo juu nilielezea kwamba freezer sio muhimu sana(hasa kama ndio unaanza maisha),unaweza ukawa unanunua vyakula in small amounts,na unafunga kwenye mifuko midogo ya plastic,unaweza ukatumia foil kwa mkate.vitu kama nyanya,vitunguu,unaweza kutandika gazeti,au karatasi safi kwenye sakafu(ya cement,nyingine sijui) na havitaharibika,kwa carrots,uwe unazifunga kwenye plastic bags,hakikisha haziingii hewa kwa maana zitajikunja na kuharibika haraka.
pia usisahau dust-bin na container za kupangia vyombo,they are the most important things in every kitchen japo huvitumii kupikia.
 
Nimesahau, non stick sufuria. Very easy to wash.
He heh umenivunja mbavu maake zingine zinatoa ''volcano'' kwa kukaa muda mrefu bila kuoshwa,ila Rice cooker nayo poa sana unatupia tu mchele wewe unaendelea kuangalia Merlin
 
King'asti ingawa mi si muanzisha thread ila nakupa bonge la THANKS...umenifunza mambo.
Btw mi sina rice cooker maana sipikag maharage aisee nkitaka kuyala naenda mgahawani tu.
Ndio maana inaitwa Rice cooker,kupikia maharage rice cooker haitaweza ,bali unaweza kupikia vitu vya fasta pia kama unapenda vitu vya kuivia mvuke kama mboga mboga,samaki rice cooker pia ni mwake,usije unguza nyumba kwa kupikia maharage kwenye rice cooker,nunua pressure cooker ufaidi mandondo na makande
 
Kama ulikuwa moyoni kwangu hiyo kitu kwenye red naweza nunua wapi hapa Dar nataka ya matumizi ya nyumbani, chezea chapati wewe
 
hata hii kitu ni muhimu kuwa navyo kwa vyakulaa mbavyo ni vibishi kuiva . lol
Tunaita indeko inafaa sana kuwekea maji kwa wasio na fiiji,ukiwa na mtungi kama huo ni kama una friji ya kuwekea maji,maji yanakuwa bariiidi ,
 
Aisee, kuna mdada mmoja black america alikuwa anafuta sufuria na napkins mara baada ya kupakua. Alikuwa ananiudhi huyo! Ila mchafu wa asili tu, tunaenda gym for an hour, tukirudia kwake anakaa sakafuni hadi anakauka na atalala na gym cloths!. Siku hatuendi gym akitoka job analala na nguo akiamka nazo anaingia nazo ofisini. Ingekuwa huku uswazi kwetu nahisi mende wangemtafuna wakammaliza!
He heh umenivunja mbavu maake zingine zinatoa ''volcano'' kwa kukaa muda mrefu bila kuoshwa,ila Rice cooker nayo poa sana unatupia tu mchele wewe unaendelea kuangalia Merlin
 
Chungu kwenye jiko la umeme? Even shape yake tu is not economically supported na jiko la umeme. Unalazimishia banaa, haya chukua kombe baba.
CHUNGU KINAFANYA KAZI KWENYE JIKO LOLOTE LIWE LA UMEME, GAS, KUNI HATA MKAA.
Chungu ni moja ya vifaa vya kupikia salama zaidi kuliko vingine vingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…