The Best FIFA Football Awards 2019: Messi atwaa tuzo ya Mchezaji bora, Klopp awa Kocha bora

Halafu ndugu yangu vigezo vyote alivyoshindia Messi kwa mujibu wako ni hivyo hivyo walitumia UEFA. Messi anacheza mpira europe vipi kule ashindwe kabla ya miezi miezi miwili leo awe mshindi. utasema UEFA wamekosea na mimi nitasema FIFA wamekosea.
Sio kweli vigezo vya UEFA sio sawa na vigezo vya FIFA.
UEFA wanaangalia mashindano ya UEFA tu lakini FIFA wanaangalia mashindano yote.
Pia hawaangalii umechukua nini kama timu wanaangalia umefanya individually
 
Ahahahaha we jamaa Modric na Salah msimu uliyopita alikua bora sana Salah kweli?
Angalia performance ya modric UEFA msimu uliyopita na kombe la dunia afu uje hapa na hizo statistics zako
 
Ningeomba unijibu swali langu
Hivi Modric mwaka jana ilikua ni individual au Team performance?

Kwangu thats was a big mistake kumpa uchezaji bora Modrid, he ddnt deserve kubeba ile tuzo mwaka jana, hakuwa na kiwango bora cha kubeba ile tuzo

kwa last year ile tuzo Mohamed Salah alistahili na sio Modric, nadhani nitakuwa nimekujibu vizuri.

Note: sijataka kuzungumzia kama ni team perfomance au individual perfomance kuz sikuafiki matokeo yale japo wapiga kura ndio wenye maamuzi.

Kuna muda yatupasa kukubali kuwa saa nyingine wapigaji wa hizi kura nao wana mapenzi yao.

Kama umeona zile graph ambazo fifa wametoa Messi kawapita kwa mbali sana Virgil na Ronaldo.
 
Modric alikua bora kuliko CR7 na Messi. Mpira alioupiga ndani ya World Cup ni waheshima kabisa. Wakati alipokua akilitawala duara Messi alikua mtalii uwanjani anazunguka tu.

Mpira mchezo wa takwimu mzee baba, Je modric ni kiungo mkabaji au mshambuliaji?

Kama ni kiungo mshambuliaji, Je alikuwa na assist ngapi kwenye UCL, La liga na World Cup last season?

Kama ni kiungo mkabaji, Je alipokonya mipira mara ngapi kwenye hizo competition zote?

Je alipiga accurate pass ngapi? Unaposema alikuwa anatawala dimba la kati uwe na takwimu pia, kama huna takwimu utakuwa mbabaishaji, Kwa Worldcup kwangu Pogba alicheza vizuri sana than Modric na bila kupepesa macho kabisa nakiri kwa kusema Kylian Mbappe ndio alikuwa mchezaji bora wa mashindano.
 

Naungana na wewe kabisa na hata post yangu kabla ya hii nimekubali kabisa kuwa last season Mohamed Salah alistahili kupewa ile tuzo na sijui walitumia kigezo gani kumpa Modric, wapiga kura ndio wanajua hilo.

Tukija kwenye perfomance ya mchezaji kwa mtazamo wangu ni kwamba pamoja na mchezaji kutobeba makombe doesnt mean hakuperfom vizuri, kuna muda wachezaji wanakuwa kwenye ubora sana ila timu wanazochezea zinakuwa kwenye viwango vibovu ndio maana nikasema PFL msimu uliopita waliopiga kura walifanya sahihi kabisa, pamoja na liverpool kutobeba uefa ila Virgil alikuwa bora ndio maana akapewa ile tuzo na hata msimu ule mwingine pamoja na De Bruyne kuwa kwenye ubora ila ubora wake haukumfikia Mohamed Salah na ndio maana alipewa tuzo ya uchezaji bora wa EPL
 
Hizi nondo kama kuna mpinzani atakayetaka akupinge hakika anapenda ubishi.
 
Nashindwa kuelewa, kwa maelezo yote haya wao hawaelewi sehemu ganiiii????
 
Hivi kuna watu bado mnazitilia maanani kabisa kiasi hizi tuzo mpaka mnamwagana mapovu hapa?

Hizi tuzo zilishapoteza maana siku nyingi sana... Binafsi niliacha kuzichukulia serious hizi tangu mwaka 2012.

Kabla ya hapo ndio tulikuwa tunaona mshindi akiapatikana kwa uhalali ambapo kilichokuwa kinaamua ni vigezo vya kimpira na hata malalamiko yalikuwa sio mengi.

Siku hizi tuzo hizi zinatolewa kwa misingi ya kisiasa na kibiashara na wala sio mpira tena. Vigezo vya kimpira vinachukuliwa kwa juu juu tu na havina uzito kama jinsi ambavyo vigezo vya kibiashara vinapewa uzito kwenye maamuzi.

Sasa ya nini mtu ukae unatunisha misuli ya shingo kwa jambo ambalo linaendeshwa kisiasa,kibiashara na utashi wa watu binafsi!?

Kama kweli hizi tuzo zingekuwa haziendeshwi kibiashara zaidi wala kisiasa, yaani kama kinachozingatiwa ni football facts mtu kama Bernardo Silva alikuwa sio wa kukosa kwenye shortlist. Lakini cha ajabu hata kwenye 5 bora tu hayumo, sasa si ni upuuzi huo?

Hao mabwana wawili tunaendelea kuwaona wakipokezana hii tuzo mpaka wanauacha huu mpira haijalishi wameshinda goli moja,wameshinda kombe la mbuzi,wamecheza mbili au wametoa assist pekee tu. Sababu tuzo hiyo ipo kwa ajili yao, wengine wataendelea kuwa escorts tu.
 
CR7 kabaniwa...
Vikombe kashinda n juve na timu ya taifa kaisaidia kutwaa kombe.
 
Mkuu, mimi kazi yangu kukupa LIKE tu.
 
Umevuruga hapo kwenye team peromance haipo bali ni ndividual.....
 
Pogba mtoe kwa waliokiwasha WC iliyopita.
Modric
Mbappe
Hazard
Hawa wajomba saluti sana kwao aisee..!!
 
Mane anacheza namba ngapi na salah anacheza Namba ngapi ???
Ngoja kidogo niweke sawa. ikiwa majina ya Mane na Salah wamekuwa voted juu ya wote kasoro wale watatu bora basi kwa nafasi zao ni lazima wawepo top 11. Mane na Salah ni kama wingers kushoto na kulia sasa iweje mbappe ambaye hakupata vote kabisa awe top 11. Hazard alikuwa number 9 katika list lakini kapachikwa kama kiungo wa kati ili Adidas wafurahi. huwezi kuwa shule high score number 4 halafu akaja mwingine number 12 shuleni akachaguliwa kimkoa wewe 4 usiwepo.
 
Nimesoma katika site zao kwa kuangalia criteria zote zinafanana tofauti ni 2 tu kubwa. UEFA wanaocheza ndani ya Europe iwe club au team ya taifa uzuri wa UEFA kura zinapigwa na waandishi wa habari na makocha team zilizoshiriki UEFA champions league. Sasa FIFA wanasema wachezaji wanaocheza kokote tatizo la FIFA kura zinapigwa na makocha na captain wa team zote za Taifa sio club. Hapa ndio inakuja shida kwa mfano ni rahisi mtu kama captain wa team ya Tanzania kupiga kura kwa mapenzi na huu ni mfano tu ila UEFA wanaopiga kura niwale wanaoshiriki katika mechi za champions league makocha na waandishi wa habari kwa hapa nawapa uzito UEFA. tatizo la FIFA hawana mashindano mengi kuwapa makocha na captain wa taifa kupiga kura sio sawa labda baada ya mashindano ya world cup maana wanakuwa washiriki ndio maana siku zote nominees wanakuwa walewale tatizo nani anapiga kura? UEFA washiriki na FIFA sio washiriki kwa maana makocha na captains. unategemea nini kocha na captain wa South Sudan atachaguwa.....
 
Kwa kutazama kwako stats za Ronaldo na Messi zinalingana na hao uliowataja hapo juu?
 
Taraaatibu umeanza kuelewa, YES atastahili Messi.

Kwasababu ameonesha uwezo wake binafsi haswa, kama pia akatokea Mane au Salah ktk hayo mataji waliyoshinda, juhudi kubwa zaidi imetokea kwake, mfano labda uweze binafsi wa Mane ni 80% au Contribution ya Salah ni 80% ya kuchukua hizo tuzo basi atastahili badala ya Messi.

Mchango wa Liverpool kuchukua ubingwa ulijawa na watu wengi pale Liver na sio uwezo wa huyo jamaa.

Hivi ndivyo nilivyowaelewa wadau walivyozungumza humu ndani.
 
Mtu kapeleka UEFA 3 Bernabeu, tena kwa misimu kufuatana, sio mtu wa kawaida huyu.

Hao wote aliowataja si wacheza Bernabeu, kuna mtu anayefika rekodi ya Ronaldo hapo? Mbona kuna mambo tunazungumza utafkiri hatuyajui?

Messi na Ronaldo wapo level nyingine, walau tuseme Maradnona angeweza kuchuana nao.
 
nilichogundua brother unamchukia sana van virgil,
akifanya vizuri messi na ronaldo ni individual perforamance ila anachokifanya van virgil na wachezaji wengineo nje ya messi na ronaldo ni team performance.
Mimi nilifikiria pia hii tuzo alipaswa kuibeba virgil ila baada ya kumsoma huyo jamaa hii tuzo anapaswa kuipokea mtu aliyefanya nini basi naunga mkono hoja yake kuwa ni kweli kwa msimu ulopita Messi alistahili.

Nilikuwa nafatilia huu uzi post kwa post, ukishaelewa tu juhudi za mtu binafsi na juhudi ya timu ktk kuleta mafanikio basi utaweza kumwelewa jamaa kiundani.
 
Hivyo hivyo Mkuu, wataelewa tuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…