The Best League in the world is back...Ligi kuu Uingereza ndiyo ligi bora zaidi kwa sasa duniani.

Kinyonyoke

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2016
Posts
3,498
Reaction score
13,138
Naam timu nne toka Uingereza zilitinga robo fainali UEFA, na hatimaye mbili zinakwenda kucheza fainal baada ya kupindua meza kibabe (Comebacks) huku kule Europa league kuna team mbili toka Uingereza pia zilifika nusu fainali na kuna uwezekano mkubwa wa kukutana fainali baada ya kuongoza michezo yao ya Mwanzo.hii inatokea kama sijasahau baada ya miaka 11 toka timu za England zilipopambana katika kipute cha fainal, hivyo baada ya zaidi ya miaka mitano ndoo ya UEFA inaenda kutua pale Uingereza.
Kwenye ligi pia mambo ni moto mchaka mchaka wa kuukimbiza ubingwa wa EPL unaendelea pamoja na kubakiwa na mechi moja mkononi kwa kila timu bingwa ataamuliwa pale mechi zitakapomalizika rasmi!.jambo ambalo ni tofauti na league nyingine ambazo mshindi hujulikana mapema tena akisaliwa na mechi nyingi mkononi,Pep Guardiola amekiri kuwa hajawahi kukutana na ligi ngumu na yenye ushindani na upinzani mkali kama EPL ,πŸ™Œ bila kusahau kuwa ni league yenye matokeo yasiyotabirika ki urahisi kulinganisha na ligi nyingine, Wazee wa mikeka hili wanalitambua vyema 😁😁 Naam.
 
Je haya matokeo ya msimu huu yatakuwa na muendelezo kwa msimu ijayo ama ni maji kupwa na kujaa? Maana spain wao kwenye michuano ya ulaya wamezoea kufanya vema..
 
Je haya matokeo ya msimu huu yatakuwa na muendelezo kwa msimu ijayo ama ni maji kupwa na kujaa? Maana spain wao kwenye michuano ya ulaya wamezoea kufanya vema..
Swala la muendelezo sina shaka nalo, nadhani hata msimu uliopita moja ya timu iliyokipiga fainali ilitoka uingereza the likes of City...Tottenham zilifika mbali pia, kwa hiyo naweza kusema timu za England zimeamka sasa tazama ubora wa Liverpool,City na hata Tottenham ni timu ambazo zinaonyesha ukomavu na consistency katika michuano ya ulaya hasa katika miaka ya karibuni hivyo naona ni mwanzo mpya wa utawala wa timu za England katika michuano ya Ulaya, naam.
 
Liver msindikizaji yule
 
Spain watabaki kuwa wababe wakutoa ligi bora na ubora wake hauna mfano, kufeli swali moja hakufanyi aliefeli maswali kumi kuwa bora!
 
Liver msindikizaji yule
Msindikizaji? inawezekana lakini si rahisi ki hivyo mkuu mimi nikiwa kama shabiki wa united kindakindaki nisingependa liver ashinde taji hili, lakini hqkuna namna sioni wakumzuia hata hivyo amelisubir kwa mufa mrefu.
 
Msindikizaji? inawezekana lakini si rahisi ki hivyo mkuu mimi nikiwa kama shabiki wa united kindakindaki nisingependa liver ashinde taji hili, lakini hqkuna namna sioni wakumzuia hata hivyo amelisubir kwa mufa mrefu.
Inakuwaje hakuna wa kumzuia na trophy anapishana nazo sema mbovu hana uwezo wa kubeba trophy yoyote ile.
 
Waingereza walikua wanafeli kipind kile.kutokana na ain ya soka lao walilokuwa wanacheza
Mpira umebadilika ikabd nao wabadilike nao, kuruhusu makocha wakigen kuja kuongoza club kubwa zmebadlisha kabisa aina ya soka ambalo linachezwa na team za kingereza sasa hv
Angalia liverpool, Mancity Totenham wote wanacheza soccer maridad kabisa.
Leo hii best coaches asilimia kubwa wapo kwenye league ya Epl
Guardiola, Sarri, Pochetino na wengneo
 
Spain watabaki kuwa wababe wakutoa ligi bora na ubora wake hauna mfano, kufeli swali moja hakufanyi aliefeli maswali kumi kuwa bora!
Sikupingi mkuu lakini pia tambua you can fool people once but not all the time, Spain wamekuwa watawala kwa kipindi chao sasa England nao ni muda wao kutamba, ndivyo mpira ulivyo huwezi kuwa juu siku zote.
 
sarri 😁😁😁😁 ambaye ajawahi chukua kocha wa mwezi mimi ni chelsea damu ila si kwa sarr
 
Inakuwaje hakuna wa kumzuia na trophy anapishana nazo sema mbovu hana uwezo wa kubeba trophy yoyote ile.
Je unadhani Tottenham atamtoa Nishai Liverpool?, japo inawezekana lakini Liverpool anapewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hili akibebwa na uzoefu na fomu aliyonayo ukimlinganisha na Tottenham ambao wanaingia katika fainali hii kama underdogs hivyo Liverpool ana nafasi kubwa ya kunyanyua hii ndoo.
 
Sio nadhani ndivyo ninavyoamini na halipingiki hilo.
 
Naam uko sahihi kabisa mkuu, this is what they call 'Modern Football era', tunaona Total football ambayo imefanyiwa 'manipulation' na Guardiola, Gegenpressing ya Klopp, Sarriball chini ya Sarri.Timu nyng zinacheza Pressing game ki ukweli makocha wageni wamebadili kabisa falsafa ya soka la kiingereza, naam.
 
sarri [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] ambaye ajawahi chukua kocha wa mwezi mimi ni chelsea damu ila si kwa sarr
[emoji16][emoji16][emoji16] naam lakini pia nae ana style yake ya kipekee 'Sarriball'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…