The Bold Interview: Maisha, Intelijensia na mengi usiyoyajua

The Bold Interview: Maisha, Intelijensia na mengi usiyoyajua

Status
Not open for further replies.
Bold ashalala au yupo na baby yake niffah ohoo nyie endleeni kuulza maswali @m
 
The bold naomba unijibu
ni kweli story ya mbasha ilikuletea matatizo..
kusema ukweli wengi tulikujulia pale..namna ulivyofafanua ile skendo kwa namna yakipekee..hakika una kipaji sana.. Binafsi umenipa heshima sana kazini kwangu kwa story zako..
 
The Bold kuna maswali umeyaruka kwa kutokuyaona au kupitiwa kwa sababu ya kuyaweka kiporo naomba nikukumbushe kidogo maana yana umuhumu mkubwa sana hapa jamvini bila kusahau na mimi nitakuswalika yangu humo humo so itakua ni jaza ujazwe

1.Ulijuaje kua kuna watu wanakudukua na ukatumia njia gani kuweza kudhibiti hali hilo?

2.Kitu gani kimekuvutia hadi unataka uweze kumiliki Appache Helicopter coz ile ni military grade Gear/Tool

3.Unadhani ni kwanini Millitary ,Police & Intelligence opps za Tanzania hua haziwekwi wazi??Huoni kama hili linawavunja watu mioyo na morali kwa nchi yao ??

4.Naomba majina matano ya waandishi wa vitabu ambao unazikubali kazi zao bila kusahau na majina ya vitabu vyao au riwaya zao au maandishi yao.

5.Je kwa utafiti wako wa kusoma maandiko mengi wakati unaandaa Makala zako, umewahi ona sehemu ambako wamesema Rais wa USA kuna baadhi ya files ziko classified kiasi kwamba hata yeye(Rais) hana madaraka ya kuziaccess????

6. Je nchi yetu hua inafanya covert opps kwa nchi za Ng`ambo???

7. Ukiachana na vita ya kagera na ile ya kuwapiga waasi wa M23 Operation gani ambazo zimewahi fanywa na nchi yetu zimekuvutia sana hadi ukatamani siku moja kuweza kuiandikia Makala???

8. Ikitokea Rais akakuteua kua DG wa TISS (Huu ni mfano ) ndani ya siku 100 utafanya mambo yapi???

9. Je umeona kuna fursa zipi za kuweza kumuongezea kipato Mtanzania yeyote ambae atataka kuwekeza kwenye sekra ya Intelligence hapa nchini???

10.Una ushauri gani kwa wanajukwaa la Intellegensia ambalo siku hizi limekua kama limepoteza mvuto hivi ili kuweza kulipa heshima yake ya kuwa jukwaa nambari moja hapa jf???

kwa sasa naishia hapa maswali mengine yatakuta tuuu anza kujibu haya kwanza??
 
Salute mkuu the bold, kiukweli simulizi zako ni matata sana. Swali langu simple tu.

Kabla ya Kuwa na niffah ushawahi Kuwa na mahusiano na mtu mwingine serious kama sasa? Kama Ndio nini kilifanya mkaachana?
 
Pamoja mkuu...

Ingawa nahisi kuna maswali watu walikuwa na kiu nayo haujayauliza...

Tusubiri wadau labda watauliza...
Dah nilihisi nitakuwa mchoyo endapo nitayamaliza maswali yote pekeyangu, alafu wakati ule tunafanya mahojiano mimi nilikuwa ndani ya bus safarini, kwahiyo nilikuwa katika kipindi kigumu pia... All in all shukrani za dhati zikufikie kwa kujitolea muda wako.
 
I love you.....kijana jasiri

Nifah upoo? Hongereni ila siku ukizingua tu kwa mchumba ako natambaa nae kweupeee (joke)

The bold
kwakuwa una fahamiana na watu wengi/kampuni nyingi pia, naomba niione fursa ya kukuomba nikutumie Cv yangu. Kisha naweza fanya kazi na ww hata kwa kujitolea tu kwanza!
Nahitaji kufika nikutakako ila bado sijapata fursa hiyo!

Tafadhali The bold.
 
Nasoma sana vitabu... Sana sana!

Sio kwa sababu ya kujielimisha tu, la hasha... Ni hobby pia

Yani mfano ukienda mbele alafu ukaniletea kitabu ambacho labda siwezi kukipata kwenye bookshops hapa Bongo nitakushukuru kuliko ukiniletea 'raba Kali'

Pia napenda sana kuangalia sinema
hongera sana mkuu The bold ....umesema unapenda kuangalia cinema hebu tuambie kati ya wakali hawa wawili wa hollywood rambo vs anord yupi unamkubali zaidi na kwa sababu zipi hasa
 
Naomba kujibiwa hili swali kwann ulichukua maamuz ya kushabikia timu moja na dogo joseverest yaan Madrid?
 
Ninja naomba zawadi yangu
Yani bora ungekuja kinamna nyengine ningekupatia ila nishakujua hahahahah
wewe haustahili hata jero, tena unafaa wewe ndo unipe mimi hiyo zawadi manake data zote unazo
 
We need to modernise our intelligence machinery... Bado kwa asilimia kubwa haiendani na kasi ya karne ya 21...

Wanausalama wetu they have to work twice as hard kufikia lengo...

Pia majukumu ya TISS yapunguzwe kwa kuundwa Idara dada za Usalama ambazo zinajitegemea...

Kwa sasa Tiss na polisi wanamajukumu mengi mno... Mfano masuala ya counterterrorism hayako sawia ni nani hasa anapaswa kuyatekeleza... Matokea yake Tiss wanabebeshwa mzigo mkubwa ambao muda mwingi unavuka mpaka malengo ya kuanzishwa kwake...

Kuwe na Idara nyingine mahususi za masuala ya Intelijensia...


Kwenye jeshi... Kitengo MI (Military Intelligence) ipewe mikono zaidi ya kufanya mambo bila urasimu wa kiprotokali... Ikiwezekana iwe-rebranded hata ijitegemee na kubadilishwa jina na jeshini wabaki na MI ya kwao (ambayo haitakuwa hii mpya)

Pia ni vyema ikaanzishwa ofisi ya National Director of Intelligence... Simuongelei mkurugenzi wa Tiss... Mkurugenzi wa Tiss abakie vile vile kama DG wa TISS... Huyu ni National Director of Intelligence (Au tunaweza kuita vingine) hii ofisi ndio ambapo masuala yote ya Intelijensia watakuwa wanayachakata na kuyawasilisha mahala husika... (Mfano kwa rais)

Hii itasaidia kuwa na flow na coordination nzuri ya Intelijensia kutoka vyombo vyote... Tiss, polisi, jeshi na vingine ambavyo nahisi ni vyema vianzishwe...

Lakini pia itaondoa hii kasumba ya Rais kuwa Sponsor wa mashushushu wote... Rais ni mwanasiasa na binadamu... Kufanya yeye kuwa Sponsor wa Tiss inaweza kuleta mgongano wa kimaslahi ya taifa na maslahi yake...

Ni vyema huyu National Director of Intelligence ndio awe anatoa briefing zote za Intelijensia kwa Rais kutoka Idara na vitengo vyoye vya ushushu...


Kuna changamoto kubwa sana ya coordination ya taarifa za Intelijensia kwenye vyombo vyetu! Kila mtu yuko na Lwake... We need a center point... Sehemu mahususi ambayo itachakata hizi Intelijensia na kutoa miongozi mahususi kwa serikali ma vyombo husika... Nadhani tukianzisha ofisi ya National Director of Intelligence inaweza kutupeleka mahala...


(Kumbuka siongelea director wa Tiss)
Hakika nimeelewa
Nimekuelewa pia
All in all tunafurahia sana uwepo wako siyo humu Jf pekee but hata Tanzania kwa ujumla, wanaofahamu mchango wako kwenye jamii,taifa na bongo za watu hawatopingana na hili, if not you haya tungeyafahamu wapi? Pengine tungeyafahamu but too late
Mungu akubariki na kukutangulia katika kile ukipangacho yawe mema lakini, Hongera sana mama kwa kukuzaa, Hongera pia kwa niffah kwa kukupata make (wakina fulani wanakunyemelea sana hili wampokonye)
Blees up bro The bold na msalimie cheupe
 
Nijibu moja moja...


MAKALA

Ugumu upo kwenye research... Unajua hakuna tukio ambalo utaandika watu hawalijui... Kwa hiyo unatakiwa ufanye tafiti ili uje na facts mpya au hata kama ni zile zile basi uingie deep zaidi... Muda mwingine unanunua kitabu kabisa ili ujue kidetail fulani kidogo tu...

Ni kazi nzito kiasi... Kukusanya taarifa


RIWAYA/FICTION

Hii kila kitu ni kigumu...
Kuanzia namna ya kutengeneza Plot ya stori... Wahusika... Matukio... Visa... Hakuna kilicho chepesi

Unaumba kitu ambacho hakipo na unatakiwa ukifanye kiwepo na kiaminike... Si suala dogo
Nakuelewa the bold
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom