The Bold Interview: Maisha, Intelijensia na mengi usiyoyajua

Status
Not open for further replies.
Naomba kupitia uzi huu nijibu seriously kuondoa doubts au wanaodhani tunachangamsha genge...

Mimi na Nifah sio kwamba tu ni wapenzi bali ni wachumba... Soon mtakula pilau la harusi

Mengine nitaeleza kadiri mahojiano yatakavyoendelea
Ooh Hongera sana boss,
na Je, kati yenu nani wakwanza kumtumia picha (au kumuona) mwenzake?
Pia haukuwa na hofu yoyote ile pale siku ya kwanza ambayo ulikwenda kuonana na nifah ana kwa ana?
 
Hapana sijao bado...

Nina mchumba (si sawa nikisema mpenzi maana tumevuka hapo)

Ni mwanafamilia mwenzetu wa JF.! Bibie Nifah (naamini ataniruhusu leo niseme japo jina lake la kwanza... Hanifah)
We jishaue tu wakati bado hujamalizia mahari??

Nifah unamuona jamaa amegeuka makubaliano ? Si nlimwambia atakuita mchumba akimaliza mahari??

Hapana... not to zis eksitent

Wanaukoo lazima tuiweke hii font fent.

Samahani kwa kuvamia intavyuu... ila mimi sijaribiwi.
 
-Je, ni nini ambacho kilikushawishi mpaka ukamuamini member wa jf(nifah) kwa kiasi hiko mpaka ikapelekea ukaanzisha nae mahusiano...
Na kwanini awe Nifah na asiwe binti yoyote humu jf?
Unajua mapenzi kwa maana ya mapenzi ya kweli huwa hayapangwi... Yaani namaanisha ni kwamba ni kitu ambacho kinatokea automatic

Niliwahi kueleza kuhusu mwanzo wetu Mimi na Nifah... Tulikuwa maadui wakubwa sana! Tulikuwa tunakwaruzana sana tukikutana kwenye nyuzi mbali mbali... Ilifikia kipindi mpaka wote hakuna aliyekuwa anaweza kulike, au kuquote au kummetion mwenzake

Lakini mwisho wa siku tuko hapa... Tumebakiza siku chache kuhalalisha ndoa

Kilichonivutia kwa Nifah kabla hata ya kuonana naye ni haiba yake (peesonality)... Binafsi naangalia zaidi 'the inner' person kuliko 'mtu wa nje'... Namshukuru tu Mungu na uzuri nao kajaliwa haswaaaa...

Lakini ninapenda zaidi haiba yake... Yule Nifah halisi wa ndani ya nafsi
 
Ulikuwa unajisikia vipi ulipokuwa njiani kwenda kukutana na mtu ambae humjui zaidi ya kuona I'd fake tu hapa Jukwanani!?
 
Vile vile unahisi upo salama kiasi hiko unapokuwa mitandaoni?
Alafu watu wengi kiu yetu kubwa ni kukufahamu, unatuahidi nini kuhusu kuweka real identinty,
au utaendelea kujificha nyuma ya keybord milele?
 
Ooh Hongera sana boss,
na Je, kati yenu nani wakwanza kumtumia picha (au kumuona) mwenzake?
Pia haukuwa na hofu yoyote ile pale siku ya kwanza ambayo ulikwenda kuonana na nifah ana kwa ana?
Hii natamani nijibu kwa kirefu sana...

Baada ya ugomvi wetu kuisha (sijui hata uliishaje) na kuanza 'kudalizana dalizana' kwenye threads tukaamia PM...

Daaaahh ndugu yangu nilitupa mawe mwezi mzima mtoto anachomoa... Baadae nikawa namuona anaanza kuelekea kabisa lakini wapi haniambii live ile

Kumbe bhana kuna uzi fulani huko wa 2013 jukwaa la matangazo kuna mtu tulikuwa tunafanya biashara nikaweka namba ya simu, bibie alifukunyua akaipata namba...

So mwezi mzima ananisoma nyendo zangu WhatsApp... Yani DP ninazoweka, status etc...

So sikuwenyewe namtumia Picha zangu PM kwa mbwembwe kabisa ndio ananichana kuwa "acha mbwembwe nakujua bold" [emoji23] [emoji23]


So na yeye akanitumia za kwake mambo yakawa muswani kabisa...


Siku ya kwanza kuonana ofcoz ile nervousness lazima iwepo kiasi fulani... But uzuri tulikuwa tunaongea sana sana... Zile kama watoto wa sekondari... Naweza kumpigia simu saa tano usiku tukamaliza kuongea saa saba usiku [emoji23] [emoji23]


So siku ya kukutana I was nervous for like 20 or 30 minutes baada ya hapo I manned up... Mambo yakaenda poa kabisa!
Its one of the most memorable days kwenye maisha
 
Dah hongera sana na ningependa mahusiano yenu yadumu mpaka babu na bibi
 
Hongereni sana Nifah na The bold na kwa hakika msinisahau kwenye mualiko..
Sasa chief
na je, unatoa ushauri gani kwa watu ambao wanatafuta wapenzi humu JF?

Ninachowaambia ni kwamba usikae humu unatafuta mpenzi kama unatafuta sindano umedondosha uvunguni...

Acha mambo yaitike yenyewe... Mimi na Nifah pia hakuna ambaye kati yetu alikuwa anatafuta mpenzi humu! Kitu kilitokea chenyewe naturally... Na hivyo ndivyo inavyotakiwa!! Ndio maana bond yetu imekuwa strong

Acha mioyo isemezane yenyewe
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…