The Bold & Nifah: Happy Six Months "Anniversary"!

The Bold & Nifah: Happy Six Months "Anniversary"!

Ngoja tu niseme ukweli,suala la teams kwa sasa hivi limepoa sana baina yetu.
Kiasi tukiwa pamoja huwa tunaelezana ukweli kabisa na hata kuwakandia wasanii wetu wanapoboronga.

Ila mwanzo ulikuwa mtihani maana Bold aliniwakiaaaaa,hataki anione namsifia Kiba.
Eti anaona wivu sio kwa mahaba yale [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Nini kwenda kwenye tamasha mkuu? Ukitukuta tukiwa tunaserebuka huu wimbo remix alioimba Diamond,Mohombi na nani sijui hutoamini tunavyoyarudi [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Kwahiyo basi...INAWEZEKANA KABISA.

Hapo kwenye red pamesababisha nicheke sana! Ila naona mkuu The bold alikuwa anajaribu kutafuta njia muafaka ya kuku-neutralize. Sina hakika kama hapo awali ulikuwa unaweza kuserebuka nyimbo za mondi.

Ila kiukweli hongereni sana.
 
Mbarikiwe sana Nifah na The bold Mungu awape maisha marefu yenye furaha na mafanikio..nafurahia sana mnavyofurahi na kuishi kwa amani.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Ilikuwa patashika mkuu

Mondi simpendi yeye kama yeye,ila nyimbo zake nazipenda sana tu.

Asante mkuu.
[emoji2] [emoji2] [emoji2] Nafikiri hata kiba unapenda nyimbo zake tu si yeye kama yeye!


Nawaza tu lakini[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kabisa mkuu,hili ndilo nimuambialo Bold kila siku.

Sijawahi kumpenda Kiba kabisa,zaidi mimi ni shabiki wake wa damu pekee.
He he heeee! Huo ushabiki wa damu ndo unampa Bold shida! Na akisikia damu nzito kuliko maji, anaweza fikiri yeye ni maji[emoji2] [emoji2] [emoji2]


Inabidi usiwe shabiki wa damu uwe tu shabiki wa kawaida! Sahamani lakini kama ntakuwa nimevuka msitari![emoji120] [emoji120] [emoji120]
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Itabidi niangalie namna ya kulifuta hili neno 'shabiki wa damu' huenda nalo ni tatizo.

Hujakosea mkuu,dah nimecheka sana.
Akhsante mkuu, once again hongereni sana!
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] I wish ungelisikia jisauti lake [emoji12]
Halafu katoka kuniambia hivyo muda sio mrefu [emoji85]
[emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] Aiseee

[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Hongereni aisee kitoti kikizaliwa kiiteni jamii forum
 
Daahh!! Hongereni.
Nimesisimka sana kwa History ya mapenzi yenu.

Na hiyo post ya niffah hapo juu I inaonesha ni mwanamke wa aina gani, Nakubaliana nawe @TheBold kweli umepata Kichwa kama unavyopenda kumwita.

Hongereni, Sana Sie wengine kila siku tunakosea njia.
 
Nchi za mashariki mwa bara la Asia kuna falsafa ya kale sana wanayoiamini kuhusiana na muunganiko na mahusiano ya binadamu. Falsafa hii inaitwa Red String Of Fate (Yīnyuán hóngxiàn).

Kwamba, kuna 'uzi' usioonekana unawaunganisha watu tangu siku wamezaliwa, watu ambao maishani wanatakiwa kuja kukutana, au kusaidiana au kuwa pamoja.

Uzi huu usioonekana unalindwa na kusimamiwa na aina ya Mungu/roho anayeitwa Yuè Xià Lãorén (au kwa kifupi Yuè Lão).

Tafsiri rahisi ya jina la "mungu/roho" huyu ni "matchmaker god"
Yeye anasimamia uzi huu unaowaunganisha watu hawa usikatike daima mpaka pale watakapokuja kukutana.

Nchini china wanaamini uzi huu unafungwa kwenye viwiko vya mkono, na nchini Japan wao wanaamini uzi huu unafungwa kwenye kidole kidogo cha mwisho na kwamba uzi huu unaowaunganisha watu hawa, unaweza kupinda (tangle) au kunyooka zaidi (stretch) lakini kamwe hauwezi kukatika mpaka watu hawa wakutane.

Kwa kifupi, imani hii ya watu Asia inarandana na imani ya watu wa magharibi kuhusu 'Soulmate'.

Mimi na Nifah: Historia fupi

Nikiwa sekondari nilikuwa naisikia sikia kitu kinaitwa "jambo forums" na 'kasheshe' zake lakini sikuijua sana kwa undani.

Baadae mwaka 2009 nikiwa kidato cha tano nikaichungulia ndani kujua yaliyomo, kipindi hiki ilikuwa imeanza kuitwa "Jamii Forums".

Kipindi hiki kulikuwa na mijadala 'mizito mizito' sana na karibu yote ilihusu siasa.
Japokuwa nilikuwa 'mtoto wa sekondari' nilivutiwa nayo sana, napenda sana mijadala, hasa mijadala mizito (yenye hoja sio matusi).

Mwaka 2011 nikajiunga rasmi (kwa ID nyingine) lakini baadae nikasahau password ya ile ID. Ndipo hapa mwaka 2013 nikafungua ID hii ya The bold.
Mwanzoni nilikuwa nasoma tu, sikuwa mchangiaji sana, lakini kuanzia 2014 nikaanza kuwa active zaidi na hata kuanzisha threads.

Kwa sababu zangu binafsi, nikaepuka mijadala ya jukwaa la siasa, na nikajikuta navutiwa zaidi na Jukwaa la Jamii Intelligence. Na nikitaka kupumzika nikawa naingia Celebrities Forums… na huko ndiko mambo yalikoanzia.

Binafsi nina maslahi fulani fulani na pia ni shabiki mkubwa wa vijana wa WCB. Huko Celebrities Forum nikakutana na bibie Nifah mkosoaji mkubwa wa WCB.
Taratibu tukaanza kukwaruzana kwenye mijadala. Ugomvi huu ukawa mkubwa zaidi na kufikia pabaya mwaka 2015 na mwanzoni kwa 2016. Ulikuwa ni ugomvi mkubwa haswaaa kiasi kwamba tulikuwa tunatoleana lugha Kali za aibu kabisa. Ugomvi huu ukaendelea na kukua siku baada ya siku, kiasi kwamba Nifah akawa adui yangu namba 1 humu JF na mimi nikawa hivyo kwake.

Lakini ukweli ni kwamba rohoni nilikuwa namkubali sana huyu bibie na nilikuwa navutiwa nae sana, IQ yake, ujengaji hoja wake na niliamini ni mtoto mrembo haswaaa!!

Kwahiyo mara kwa mara nilikuwa nafanya ule mchezo wa kutembelea profile yake na kuanza kuangalia replies zake kwenye threads mbalimbali. Nikazidi kuvutiwa naye zaidi na nikajikuta naanza kulike posts za huyu "adui" yangu.

Pasipo mimi kujua, kumbe naye anafanya mchezo huu wa kutembelea profile ya mimi "adui" yake na ghafla nikaanza kuona likes kutoka kwake.
Baadae tension kati yetu ikaanza kupungua na tukawa tukikutana kwenye threads yoyote lazima tuchit chat.
Kipindi cha uchaguzi wa marekani nakumbuka tulibet, yeye akaweka 100K kwa Clinton, mimi nikaweka 100K kwa Trump, [emoji23].. Alijuta [emoji23][emoji23]

Chit chat kwenye threads zikaendelea…

Kisha tukahamia PM. Huko PM kilichoendelea sitaki kuwasimulia… ila kwa ufupi mwana wane sikutaka ujinga, nikajitutumua, nikafanya yangu… and the rest is history.!

Tangu hapo… we have been crazily in love together!

Najivunia kumpata mwanamke wa dizaini yake, ana heshima, mnyenyekevu, big IQ, beautiful, anajua kukalangiza jikoni na mwenye kujua haswa mapenzi ya dhati… bila kusahau usiku tukizima taa huwa najihisi tumeenda kutalii sayari ya Mars!! Mashallaaahh…

Nafurahi pia ndugu zake wanajivunia mimi kuwa na binti yao, na ndugu zangu pia wanajivunia mimi kuwa na huyu binti.!

Mwenyezi Mungu akutunze white masai wangu… na wakuu mtuombee soon tunataka kufanya halal..

Imekuwa six months sasa tuko pamoja… let's make it to six more years, and then 60 years na hatimaye 600 years!! Let's make this forever...

Happy six months anniversary soulmate...
Nakupenda sana Cheupe!

The Bold
-----------
My honesty question to both Nifah and the Bold:

"Are you a serious couple?".

Please assure me before I would tell you what I'm intending to.
 
Naombe hiyo harusi nialikwe kwa garama zangu nitaudhuri uwa natamani siku moja niwaone mubashara the bold na nifah
 
Daahh!! Hongereni.
Nimesisimka sana kwa History ya mapenzi yenu.

Na hiyo post ya niffah hapo juu I inaonesha ni mwanamke wa aina gani, Nakubaliana nawe @TheBold kweli umepata Kichwa kama unavyopenda kumwita.

Hongereni, Sana Sie wengine kila siku tunakosea njia.
Umenichekesa mkuu hongera kwako
 
Hivi hii siku ndo inakuaje sasa!!!

Siku mliotongozana kwa mara ya kwanza!??

Siku Nifah alipokubali ombi lako!?

Siku mlipogegedana kwa mara ya kwanza!?

Nilelewesheni maana sijui kuanzisha mahusiano rasmi ni siku ipi.

HONGERENI SANA.

wakikujibu nitag mkuu 😀😀😀😀
 
Back
Top Bottom