The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London



Afadhali useme wewe! Wengine tukisema tunaambiwa "tutajuta"!
 

Acha vitisho vya kijinga. Wewe mtu mzima na akili yako unadiriki kutishia watu eti watajuta kisa they don't share your views and beliefs! Hapa ndio mnapochemsha nyie watu wa CHADEMA kwasababu mnajionyesha your true colours as undemocratic and intolerant to different views. Mbona hapa niko gia namba moja tu. Sasa nataka nikuahidi kwamba nitaendelea kukejeli pumba mnazotoa humu ikiwa ni pamoja na zile za Mwenyekiti wenu ambaye sasa hivi anatumia jina tofauti licha ya kuingia hapa JF kwa mbwembwe na kudai watu watumie majina yao ya kweli. That is the height of hypocrisy.
 
Nafikiri waheshimiwa walijisahau kuwa mjadala unaendeshwa live na watanzania wote wanaangalia kinacho endelea na hasa spika alivyo endeleza mapambano ya kuhakikisha mhe.Zito kuadhibiwa kwani alikuwa akimkumbusha mhe. mdhihiri asisahau hoja yake mara kadha baada ya hoja ya zitto.

Tulisikitishwa jinsi spika alivyoendesha hicho kikao kwani hata alipofikia kuuliza wabunge wanaoafiki hoja ya zitto waseme ndio na wasio afiki waseme sio na sauti za wale walio sema ndio na sio zilikuwa kama zinalingana na pengine sauti ya wale waliounga mkono hoja ya zitto ni kama ndio ilikuwa kubwa zaidi lakini spika akasema harakaharaka kuwa hoja imepingwa.

Adhabu inatolewa bila ya kuchunguza ukweli wa mkataba na anayeuliza baadala ya kujibiwa anaadhibiwa.

Naomba mhe.JK afanye kazi yake na kama waziri amechemsha basi ampige stop na wabunge ndio hawatarudia kosa hilo na sijui kama spika ataenda kumwomba msamaha Rais pamoja na Mhe. Zitto kwani kilichofanyika bungeni ni aibu kubwa ambayo Rais tu ndio anaweza kusafisha serekali na kumbukeni hakuna siri isiyotoka hatakidogo tusubiri kidogo mambo yatakuwa wazi na spika ajiandae kuomba umma msamaha kwani mambo yata mwendea vibaya kwani nguvu ya umma hakuna yeyote anayeweza kuzuia na umma wa watanzania umeshuhudia dhana ya utawala bora ikitupwa mbali na kuendelezwa dhana ya utawala wa kibabe na hasa ndani ya bunge.
 


Kwa hilo Nampa Heshima yake; ukiondoa chuki yake (aliyoionyesha dhahiri) dhidi ya Chadema, napenda kuongeza kuwa mawazo tofauti ndio hufanya maamuzi kuwa ya busara zaidi. Hatuko hapa kudanganyana kwamba wote tunachukia kilichoendelea bungeni; wapo wanaona ni sahihi kilichofanyika kama mugongo na wengine niliopata kuwasikia, wapo pia wanaona sio sahihi (kama wengi wana Jambo) lakini vyovyote vile tunavyotofautina ni lazima tuwe makini kuweka hoja mbele na ubinafsi nyuma. Hongera Mugongo kwa kutokuwa mwepesi wa kujibu tuhuma binafsi; natumai utaendeleza na hoja.

Sijasoma hoja za Field Marshall ES juu ya hili...yupo vacation nini?
 
CHADEMA hivi mnajua kwamba huko vijijini hakuna TV? Si ajabu wapiga kura wa Zitto wengi hawajui hata kwamba kasimamishwa bungeni.

Hakuna haja ya kupoteza muda mjini ambako sasa kila mtu anajua nini kimetokea, kufanya hivyo ni sawa na kutumia muda mwingi kumtongoza mkewe, tayari huyo anajua uzuri na ubaya wako.

Nendeni vijijini na huko through a word of a mouth, jumbe zenu zitawafikia watu wengi. Hata mkifanya mkutano mmoja wilayani ukawa mkubwa basi, habari zitaanza kuenea taratibu.

Mtikila itakuwa ngumu kushinda case ya Zitto kwasababu naamini bunge limetumia wajibu wake. Sheria hiyo ni mbaya lakini kwasababu ipo naamini ni halali hata kama wengi wetu hatuipendi.

Badala ya kuwahukumu CCM mahakamani, wahukumuni kwa wananchi na tumieni nafasi hii kuwavuta vijana wengi wasomi ili mwaka 2010 wasisumbuke kwenda CCM na wajiunge na vyama vya upinzani.

Laiti vyama vya upinzani vingechunguza kwanini Mrema alishindwa 1995, naamini majibu hayo yangeliwasaidia sana sasa. Ninacheka ninapoona makosa yale yale ya 1995, wanayarudia mpaka leo, hakuna lessons learned hapo.

Ni ushindi gani ambao Zitto amepata ambao unastahili party? Kilichotokea ni kwamba Zitto kaonewa, toka lini mtu aliyeonewa anafanya party? Wakati nyie mnafanya party, CCM wanawawahi huko vijijini.
 
Hongera Mugongo kwa kutokuwa mwepesi wa kujibu tuhuma binafsi; natumai utaendeleza na hoja.

Sijasoma hoja za Field Marshall ES juu ya hili...yupo vacation nini?

Mwendo mdundo tu hapa...wako wengi lakini wanachoishia sasa ni kutukana na kutishia eti utajuta na unachoandika hapa. Ingekuwa mwenzangu mmoja hapa angeshachapisha petition kwamba anatishiwa maisha, but my mission hapa ni kudhihirisha unafki wa wana-CHADEMA hapa na kuonyesha kwamba their messiah is phony.
 
Mtanzania,

Napenda postings zako, hauko upande wowote!! gud job keep it up!!

FD
 

Kwi kwi kwiiiiiiiiii mwaga mavitu mwanangu, usiwatukane tu!!!

Kweli party za nini wakati wameonewa?? wangetumia hizo hela kuwatembelea wananchi na kuwaelimisha jinsi Zitto alivyoonewa bungeni!!!!

Safiiiii????? Saffiiiiii sannaaaaaa!!

FD
 
Jamani Majibu Ya Waziri Karamagi Kwa Hoja Ya Zitto Yako Wapi?
Kama Hamtuwekei Majibu Ya Waziri "how Can We Say That The Beam Of Justice Is Evenly Balanced?"
 
Jamani Majibu Ya Waziri Karamagi Kwa Hoja Ya Zitto Yako Wapi?
Kama Hamtuwekei Majibu Ya Waziri "how Can We Say That The Beam Of Justice Is Evenly Balanced?"

Jana niliahidi kuya-post hapa ni 24-hours time. Still working on it. Bongo internet mzozo wakati mwingine. Lakini what is interesting ni kwamba kuna majority ya wana-CHADEMA hapa and surely one of them must have majibu ya Karamagi. Why are they not posting them? You guessed it.
 
Jamani Majibu Ya Waziri Karamagi Kwa Hoja Ya Zitto Yako Wapi?
Kama Hamtuwekei Majibu Ya Waziri "how Can We Say That The Beam Of Justice Is Evenly Balanced?"

That is what I said. Tuliletewa hoja za Zitto bila majibu ya Karamagi. Hii imenifanya nishindwe kujua kama kweli Zitto alionewa au kweli alidanya. Ingawa nimesoma magazetini watu mbalimbali wakionyesha kutoridhika na majibu ya Karamagi, ninataka niyasome mwenyewe kusudi nifanye uchambuzi wangu.
 

Yaani wewe mwafrika wa kike 🙂 🙂
 
Mtanzania,

Napenda postings zako, hauko upande wowote!! gud job keep it up!!

FD

Hahaha! So, is it a good thing or bad thing? Lakini, Dante, that genious Italian, alipata kuandika kwamba "the hottest places in hell are reserved for those who, in times of moral crisis, preserved their neutrality"

Lakini, at the same time, "feng shui" or "balance" is "in" these days. Hahaha!
 

Ninadhani kuwa hayo mashirika 60 yasiyokuwa ya kiserikali hayashabikii chama chochote.
 
Ninadhani kuwa hayo mashirika 60 yasiyokuwa ya kiserikali hayashabikii chama chochote.

Kichuguu, hujui kwamba CHADEMA ni NGO? Kwahiyo, usishangazwe na NGO nyenzake kujitokeza kumpokea shujaa...anayepokewa kwa kutimiza wajibu wake wa kuipinga Serikali. Wabongo kweli tumelemaa...yaaani tunafanya maandamano kisa Mbunge wa Upinzani kaleta hoja Bungeni ya kuipinga Serikali. What did we expect him to do?
 
Wakubwa heshima yenu.... Mh kwa kweli swali sio kuwa alikurupuka, panapofuka pana moshi. Sasa kama wakubwa wanasema hana ushahidi, ameenda kinyume na maadili ya bunge, hakuna ukweli na sababu za kujikosha nyingine nyiingi basi watupe ukweli wa mambo roho zetu zitulie!!! Tulianza na IPTL, then Richmonds, tukaenda Dowans, wakaja wa radar uingereza, sijui BOT Twin Towers, Kiwira coal mines na nyingine nyiingi.... Sasa kama hao wakubwa wanakaa Dodoma na kuacha kuhoji haya mambo eti ni hoja ya mpinzani, ina maana nchi iende jalalani sababu ni wapinzani ndio wameanzisha hoja??! Hao wabunge wa chama tawala, PCB, Mambo ya Ndani na wengine wengi ina maana hawayaoni haya?? au kwa vile ni chama tawala we say "mali inakula mali??".... na huko tunapoenda kutakuwa hata na mali ya kuliwa na mali???

inasikitisha sana kwa kweli kuona haya mambo yanavyoenda lakini tatizo la wakubwa wetu hapa nyumbani hawana UKWELI, UWAZI, DIRA, UCHUNGU WA NCHI, URAIA WEMA bali wengi (kama sio wote) wamezidiwa na UBINAFSI, ULAFI, RUSHWA, NJAA, FIKRA FUPI NA POTOFU.... kwa vile wahenga walisema penye kutakiwa sifa tuweke sifa zake, sikatai naunga mkono kwa kweli ARI NI MPYA, NA NGUVU NI NYINGI SANA NA MPYAAA SANA - swali ni "ARI NA NGUVU YA KUFANYA NINI, KUJENGA AU KUBOMOA/KULA??"

Naomba kuwakilisha....
 

Upewe kazi ya kufundisha kidhungu huku JF, that suits you i think.
 
well, mambo mazito sana mtaani. Kila kijiwe sasa maongezi ni Zitto na bunge letu. Kuna kila dalili kuwa watu sasa wanahitaji bunge makini.

Hata hivyo katika kupitapita kwangu na kusikiliza sikiliza maoni mbali kwenye vyombo vya habari na vijiweni, kuna point moja ambayo hatujaielewa. Ni hivi, si sahihi kulaumu bunge hili la sasa kama lilivyo. We are not hitting the iron. Mzizi wa tatizo ni kuchagua wabunge wengi kutoka chama kimoja katika mfumo wa vyama vingi. Kwa hiyo hii sakata ya Zitto na bunge itufundishe kuwa wakati uchaguzi mwingine ukija tusifanye ujinga wa kuchagua wabunge wengi kutoka chama kimoja tu. Yaani tukiendelea na ujinga wetu wa kuchagua wawakilishi kutoka chama kimoja wakati tupo katika mfumo wa vingi haya yanayotokea katika bunge la Sitta yataendelea kutokea milele.

Tuna options mbili tu. Ama tubadilike kwa kuchagua wabunge wengi kutoka katika vyama vya upinzani ili kusiwe rahisi kupitisha maamuzi ya kijinga kwa kura, au tuendelee kuwa na mfumo wa chama kimoja huku tukijifanya kufanya uchaguzi wa vyama vingi.

Kwa hivyo kwa maoni yangu tumelibebesha bunge letu la sasa lawama nyingi bila sisi wananchi kuchukua sehemu ya lawama hizo kwa kuipenda mno CCM na hata tukarundika wabunge kutoka chama hicho pekee, ambao kwa asili ya chama hiki hawawezi kamwe kuweka mbele maslahi ya nchi a wananchi dhidi ya chama chao.Na hii yote ni kwa sababu wabunge wengi wa CCM hawakuchaguliwa kwa sababu wana sifa, bali kwa sababu waligombea kupitia CCM, kwa hivyo boss wao sio wananchi, bali ni CCM. It is that simple. Hali hii pia ndiyo tunayoweza kuielezea hata katika mabaraza ya madiwani.
 
Upewe kazi ya kufundisha kidhungu huku JF, that suits you i think.

Judy, nimefanya yale masahihisho with context. Nilikuwa namrekebisha Bwana Philemon Mikael, kiongozi mwenye dhamana kubwa katika jamii yetu, na ambaye watu wanadai he is extremely intelligent lakini anadai kuandika "rainball" badala ya "rainbow" ni kuteleza vidole. Caught him on stupidity. Caught him on a lie. Nilikuwa natoa "ushahidi". Kwikwikwi!
 
Wanamfungia Zitto kwa kosa gani? Tatizo letu ni sisi wananchi
ambao hatuwawajibishi wabunge wajinga na wanaotetea ujinga huko bungeni.

Hivi suala la madini, kweli Zitto ndio anatakiwa kufungiwa?

Kama elimu inamsaidia mbunge kutofautisha propaganda na reality pamoja na uwezo wa kunyumbulisha na kuunganisha mambo mbalimbali, basi Tanzania tuna tatizo hili kwani wengi wa wabunge wetu wana wingi wa pesa na umaarufu na ulegevu wa cv hasa kwenye suala la elimu.

Natumaini NGO zenye maslai kisiasa ziandae workshop ili angalau kuwanoa hawa wabunge wajue kilichowapeleka bungeni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…