Sijui definition yako ya neno defeat lakini unahitaji kusoma zaidi matumizi na maana ya neno hilo kisha ukalihusisha na kesi ya zito hapa.....
Vichekesho...
So asingejibu? Then ingekuwa HOJA?
Akinukuliwa na Hansard ya tarehe 16/07/2007, Mheshimiwa Kabwe Zitto alisema nanukuu " kutokana na majibu ya Mheshimiwa Waziri kuhusiana na Mkataba mpya wa Mgodi Buzwagi ambao Mheshimiwa Waziri ameeleza maelezo ambayo siyo sahihi, amedanganya na ameeleza vitu ambavyo kwa kweli sivyo ambavyo vipo katika Mkataba ambao ameusaini" mwisho wa kunukuu.
Sasa kama mheshimiwa ZITTO alimuita Karamagi muongo,lakini Zitto akashindwa kuprove kuwa KAramagi kweli ni Muongo hapo ni nani Muongo? Zitto au Karamagi? nani kalidanganya Bunge hapo?
Kama Zitto ametoa maelezo katika Bunge ambapo ikaja kudhihirika kwamba kumbe Zitto anachanganya mambo,sasa ni nani atakuwa ameeleza maelezo ambayo siyo sahihi? Zitto au Karamagi? ni nani muongo hapo?
Na kama sasa imedhihiri kuwa Zitto ndiye muongo na si karamagi,kwa nini ZITTO ASICHUKULIWE HATUA ZA KINIDHAMU ZA KULIDANGANYA BUNGE?
__________________
Ni haki yangu kuukataa uwongo kama ilivyo wajibu wangu kuukubali ukweli ,itakuwa ni makosa makubwa kuukataa ukweli eti kwa vile siupendi-gamba la nyoka.
Akinukuliwa na Hansard ya tarehe 16/07/2007, Mheshimiwa Kabwe Zitto alisema nanukuu kutokana na majibu ya Mheshimiwa Waziri kuhusiana na Mkataba mpya wa Mgodi Buzwagi ambao Mheshimiwa Waziri ameeleza maelezo ambayo siyo sahihi, amedanganya na ameeleza vitu ambavyo kwa kweli sivyo ambavyo vipo katika Mkataba ambao ameusaini mwisho wa kunukuu. ...
Halafu kuna key issues za kisheria, kwa mfano inapo tokea migogoro ktk mikataba, je ni Sheria za Wapi zitatumika ktk arbitration, za Uingereza kuliko sainiwa mkataba au za Bongo au zakimataifa. Sasa Ka-damage akitueleza, kama kusaini uingereza au Dar au kokote hakuta kuwa na efffect, kwa sababu incase of dispute wamekubaliana sheria zitakazo tumika.
Ndio hapa ina kuja Hoja za Kina Mkono ktk kuwa waangalifu ktk ku-saini mikataba kama hii.
Halafu hiyo haraka ya kusaini ilitokana na nini? kwamba muwekezaji alikuwa anakimbia na sisi tuna muhitaji au? au hayo madini yataoza?
last but not the least ikiwa sisi tu-dance according to the tune of investor, then interest za nchi zina lindwa vipi, maana kila kukicha tuna badili sheria iwe ya kodi au ya investment au ya madini. Kuna kiswahili kirahisi kina sema kizuri kinajiuza kibaya kinajitembeza, sasa sijui taifa la tanzania tumefikia hatua hiyo ya kujitembeza badala ya kufuatwa. Basi ujue tuna tatizo hapo, labda tu wagumba/tasa
Katika majibu ya Kramagi tarehe 16/7 kwa Zitto alisema mgodi wa Buzwagi ni mdogo sana,
Katika majibu yake anaonyesha huo mgodi ulikuwa wa mhimu sana, utaongeza pesa lukuki na ajira zaidi ya 600!
Huu ndio mgodi mdogo? na kama huu ndo mdogo mikubwa ni ipi na imezalisha ajira na kuingizia Taifa pesa kiasi gani?
Mbona majibu yake haya mawili yana gongana? kuna nini hapo kati kati?
Zitto,
Pole ndugu yangu pole sana!........
Sikuona hata sehemu MOJA uliyosema kuwa waziri wetu Ni MUONGO! analidanganya taifa ila ni Karamage mwenyewe aliyeanzisha hili neno Kudangabya!
Ni pale alipotanguliza maneno haya ktk hotuba yake:-
Mheshimiwa spika, mtoa hoja amejielekeza ktk masuala makuu mawili ambayo anadai wakati nayaelezea, aidha sikuwa sahihi au nilidanganya.........
Haya ni maneno yake mwenyewe waziri ambaye kwa kujibu hoja yako na alichukua moja Kudanganya kisha akalijengea hema kuwatia chunvi wabunge hadi wafikie kuamini kwamba wewe hukuwa na hoja ila kutafuta muongo nani kati yenu!.Na walivyokuwa Wadanganyika wakanunua mtego wa waziri kiasi kwamba ikabadilishwa hoja na kuwa swala la uongo!. ........
Hivi kweli, ulitakiwa uulize vipi?...lugha gani ilitakiwa uitumie ili wao waone kama umewakilisha hoja yakokutafuta usahihi wa swala zima........
Nimeshagundua, hawana hoja, kweli Kitila namkubali ingawa sio Chadema mimi.
FD
Anakuwa tishio kwa Mbowe na soon wataanza kumfanyia fitna kama walivyomtoa Shaibu Akwilombe na Amani Walid Kaburu.
No wonder kuna siku hapa JF mtu mmoja alipo-suggest kuwa yeye ndio awe kiongozi wa CHADEMA huyu bwana aliomba kauli ifutwe mara moja kwasababu anajua madhara yake. Kwikwikwi!
Kilichonishangaza ni kuwa wabunge wamesikiliza majibu yale wakafurahishwa na mtiririko ule wakasahahu kuchambua facts....
Kinepi,Haiwezekani majibu ya Karamang kuwa sahihi kwani hakuna mkataba.Yeye anatetea alichokifanya lakini hakuna mbunge ambaye anajua nini kipo kwenye mkataba sasa hukumu itakawa vipi ya haki?
Naona sasa watanzania wanaanza kuchanganyikiwa.
Hoja ya msingi ya kabwe ni kwamba mkataba unamapungufu, sasa hayo mapungufu yangejulikana iwapo tu mkataba ungetolewa kwa pande zote mbili na bunge ili waujadili halafu tujue je ni kipi si cha kweli.
Halafu wasiwasi mwingine ambao nauona ni pale bunge lilipomfungia mbunge kwasababu tu ameonyesha wasiwasi wake kwa utendaji wa waziri na wizara. Kama kila anachosema waziri ni sahihi tunahitaji bunge la nini? nini kinawapeleka bungeni kama mawaziri hawkosei wala hawakosolewi. Je kuhoji kama anachokifanya waziri ni kwa maslahi ya taifa au la ni kosa gani.
Inatia kichefuchefu kuona bunge limegubikwa na watu
waliokatatamaa.
Lazima tukubali bila kuwa na wabunge wawajibikaji bila kujali vyama vyao nchi imekufa.
Majibu ya waziri ni ya kihuni kwani haielezi nini kipo ndani ya mkataba wa buzwagi, hajibu hoja bali anatumia kivuli cha siasa akijua wapambe ni wakutosha.
Wakati umefika wa mtanzania kujua kila kosa la serikali ni msalaba kwa mwananchi, inashangaza kuona hakuna maji,barara safi na hospitali bora kwa sababu ya ndio mzee.
Wanashindwa kuwajibika na kuikuta nchi inakufa, wameuwa hospitali wakizani watatibiwa wote ulaya, sasa uone ujinga wao wakizidiwa wanapelekwa muhimbili kwanza kabla hawajaenda kufa nje, ila wakiwa juu ya viti vya bunge wanajibu utumbo kama wao malaika.
wanachokijua ni kula rushwa basi. Kulikuwa hakuna haraka yeyote ile zaidi ya rushwa kusaini ule mkataba uingireza kwani kizuri chajiuza kibaya.......
Ukweli hauko mbali na historia itasema, dhabmi za iptl, richmond,bulyanhulu, bado inatutafuna, sasa tungoje tuone...
you can support either way, result is ours
ujinga ni ugonjwa mkali kuliko ukimwi------------
kiharage
Lazima tukubali kwamba katika rhetoric, Karamagi alimzidi Zitto. Kwa wanaotazama rhetoric wanaishia kwenye utetezi mzuri wa Karamagi kusema Zitto ni mwongo.
Ukweli hapa ni kwamba hoja za Karamagi zimesimama kwa sababu serikali ilipata muda wa kuziweka sawa kwa kutumia document za Zitto. Hata mimie ningeweza kumshushua Zitto kama ningekuwa upande mwingine na akanipa hoja zake mapema.
Zitto mwenyewe alipoomba apewe mkataba wenyewe auone na baadhi ya documents alinyimwa. Hapa ndipo alipopigwa bao. Hivyo, ilitarajiwa kwamba serikali ingejibu mapigo kwani ilishajiandaa. Lakini kujibu mapigo siyo kusema ukweli.
Zitto, kwa kujua hili, ndiyo maana aliomba iundwe kamati ichunguze hata majibu haya ya Karamagi. Ingekuwa fursa pia ya kujua uchafu ulio katika mkataba huu na mingine ambayo serikali imekuwa inawanyima wabunge.
Kinachompa ushujaa Zitto ni unpopularity ya serikali kwa sababu sasa wananchi wameshajua kwamba ni corrupt government by corrupt leaders! Hata hivyo, bila KAMATI majibu ya Karamagi yanabaki kuwa rhetoric tu.
(1) Barricks makao yao yapo Toronto na sio Uingereza na hata kama mikataba ingetumwa sehemu mbili isingeliikuwa Uingereza. Why UK? ndio swali ulouliza! kwa kuzingatia kuwa hakuna uhusiano wowote wa Uingereza na mkataba huu, na umeuliza vizuri kama kuna sababu hasa ya Mkataba huo kuwekwa Uingereza.
Ningeshauri sana hizo nakala za Mkataba zitazamwe vizuri maanake siwezi kuelewa kwa nini Waziri wetu awe na mihuli ya serikali kwenda itumia London ktk Mkataba ambao alifahamu unaweza sainiwa hapa nchini...February haikuwa shida kwani Barricks wana Ofisi zao nchini sio kampuni ambayo haiwezi kuapatikana kirahisi. Something fishy! bob.... mtakuja nambia.
Pili swala la kigezo cha gharama za ujenzi wa mradi huo kachukua cheap shot sana baada ya kuitumia Bulyanhulu ambao ulijengwa miaka ya tisini badala ya North Mara!..Hata hiyo Bulyanhulu ilijengwa wakati dhahabu ikiuzwa kwa dollar 200 na kitu kwa aunzi moja tofauti kabisa na hali iliyopo leo. Mbona hawakusema hawataweza kuweka mkataba hadi hapo dhahabu itakapo panda bei?.. North Mara imeweka mkataba lini, ama Tualawake mbona asichukue hiyo mifano kufafanua hoja yako!