The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

Sijui definition yako ya neno defeat lakini unahitaji kusoma zaidi matumizi na maana ya neno hilo kisha ukalihusisha na kesi ya zito hapa.....

Naona kuomba "definitions" ndio kitu mnachokipenda sana... Defeated on FACTS - Alishindwa kwa HOJA.
 
c5rt6.jpg

c6ge6.jpg

c7xu9.jpg

c2xd5.jpg

c4hl2.jpg

c3kl6.jpg

Picha zote kwa hisani ya Michuzi Blog.
 
Akinukuliwa na Hansard ya tarehe 16/07/2007, Mheshimiwa Kabwe Zitto alisema nanukuu " kutokana na majibu ya Mheshimiwa Waziri kuhusiana na Mkataba mpya wa Mgodi Buzwagi ambao Mheshimiwa Waziri ameeleza maelezo ambayo siyo sahihi, amedanganya na ameeleza vitu ambavyo kwa kweli sivyo ambavyo vipo katika Mkataba ambao ameusaini" mwisho wa kunukuu.

Sasa kama mheshimiwa ZITTO alimuita Karamagi muongo,lakini Zitto akashindwa kuprove kuwa KAramagi kweli ni Muongo hapo ni nani Muongo? Zitto au Karamagi? nani kalidanganya Bunge hapo?

Kama Zitto ametoa maelezo katika Bunge ambapo ikaja kudhihirika kwamba kumbe Zitto anachanganya mambo,sasa ni nani atakuwa ameeleza maelezo ambayo siyo sahihi? Zitto au Karamagi? ni nani muongo hapo?

Na kama sasa imedhihiri kuwa Zitto ndiye muongo na si karamagi,kwa nini ZITTO ASICHUKULIWE HATUA ZA KINIDHAMU ZA KULIDANGANYA BUNGE?
__________________
Ni haki yangu kuukataa uwongo kama ilivyo wajibu wangu kuukubali ukweli ,itakuwa ni makosa makubwa kuukataa ukweli eti kwa vile siupendi-gamba la nyoka.

Gamba la Nyoka, hivi Mudhihir aliwasilisha mkataba bungeni ulioonyesha kwamba maneno hayo ni uongo? Hivi Kwa hiyo hotuba waliyoandika wataalamu wote wa serikali kutoka ofisi zote na kwa kutumia nyaraka zote na kupitiwa na wasanii wote ndani na nje ya serikali na kusomwa na Karamagi, ndio MKATABA ambao Zitto kauzungumzia? Kama Karamagi na wenzake wa CCM wameshindwa kuuwasilisha mkataba bungeni na hata bila kujibu barua ya kuombwa mkataba waliyoandikiwa, unawezaje kuhukumu mtu kwa kitu ambacho unacho mwenyewe? Mkataba wamekataa usichunguzwe, maana hata wangeuwasilisha bungeni bado ingebidi kamati ichunguze na kubaini undani wa mkataba husika. Tatizo hapo ni MOB JUSTICE imetumika na sasa inawatokea puani... Kikao cha ndani cha CCM wamemshambulia MUDHIHIR na wamemruka.. Kazi kweli kweli
 
Nimesoma Nyaraka alizopost Zitto kutoka Hansard. Zinaonyesha mwanzo hadi mwisho kila aliyezungumza. Zinahitaji muda kusipitia zote, lakini ni muhimu kwa mtu anayetaka kujadili suala hili.

Tafuteni muda zisome kabla ya kuhukumiana hapa. Tangu alipotoa hoja, hadi alipohukumiwa. Zipo.
 
Zitto,
Pole ndugu yangu pole sana!...
Nimeupitia mjadala mzima na hakika CCM wamekujengea kile walichokitaka - FITNA!..
Kila niliposoma nimegundua tu kwamba wewe ulikuwa ukinukuu sheria tofauti ya ile ya Mh. Waziri jambo ambalo wewe umewakilisha hoja yako ili kutaka kufahamu..Ni kawaida kabisa kwa bunge lolote lile.

Sikuona hata sehemu MOJA uliyosema kuwa waziri wetu Ni MUONGO! analidanganya taifa ila ni Karamage mwenyewe aliyeanzisha hili neno Kudangabya!
Ni pale alipotanguliza maneno haya ktk hotuba yake:-
Mheshimiwa spika, mtoa hoja amejielekeza ktk masuala makuu mawili ambayo anadai wakati nayaelezea, aidha sikuwa sahihi au nilidanganya.

Haya ni maneno yake mwenyewe waziri ambaye kwa kujibu hoja yako na alichukua moja Kudanganya kisha akalijengea hema kuwatia chunvi wabunge hadi wafikie kuamini kwamba wewe hukuwa na hoja ila kutafuta muongo nani kati yenu!.Na walivyokuwa Wadanganyika wakanunua mtego wa waziri kiasi kwamba ikabadilishwa hoja na kuwa swala la uongo!.
Hivi kweli, ulitakiwa uulize vipi?...lugha gani ilitakiwa uitumie ili wao waone kama umewakilisha hoja yakokutafuta usahihi wa swala zima.
Kuna vipengele fulani ambavyo sikubalini na Waziri. mathlan hilo la kuweka mkataba Uingereza haiwezekani mkataba ukafungwa nje ya makazi ya watu wote wawili. Barricks makao yao yapo Toronto na sio Uingereza na hata kama mikataba ingetumwa sehemu mbili isingeliikuwa Uingereza. Why UK? ndio swali ulouliza! kwa kuzingatia kuwa hakuna uhusiano wowote wa Uingereza na mkataba huu, na umeuliza vizuri kama kuna sababu hasa ya Mkataba huo kuwekwa Uingereza.
Ningeshauri sana hizo nakala za Mkataba zitazamwe vizuri maanake siwezi kuelewa kwa nini Waziri wetu awe na mihuli ya serikali kwenda itumia London ktk Mkataba ambao alifahamu unaweza sainiwa hapa nchini...February haikuwa shida kwani Barricks wana Ofisi zao nchini sio kampuni ambayo haiwezi kuapatikana kirahisi. Something fishy! bob.... mtakuja nambia.

Pili swala la kigezo cha gharama za ujenzi wa mradi huo kachukua cheap shot sana baada ya kuitumia Bulyanhulu ambao ulijengwa miaka ya tisini badala ya North Mara!..Hata hiyo Bulyanhulu ilijengwa wakati dhahabu ikiuzwa kwa dollar 200 na kitu kwa aunzi moja tofauti kabisa na hali iliyopo leo. Mbona hawakusema hawataweza kuweka mkataba hadi hapo dhahabu itakapo panda bei?.. North Mara imeweka mkataba lini, ama Tualawake mbona asichukue hiyo mifano kufafanua hoja yako!
Huyu waziri ndiye aliyetufunga kamba ktk Richomond kwa maneno mazito na yenye uhakika lakini mwisho wa yote tumekuja gundua kuwa ni Kanyaboya!.. sijamwona akisimama na kutuambia kwamba kweli alitudanganya!..... lakini leo imekuwa rahisi kwake kujijengea daraja la dhana zake kuwa ndio ukweli. Muda wote amekutaja wewe kwa jina lako bila kukupa heshima ya Ubunge na sijui kakutaja mara ngapi ktk hotuba yote kisha anasema ati anakuheshimu kwa kutanguliza mheshimiwa halafu mawe na dharau za kihuni ambazo nashangaa kuna wabunge wameziona kama vile ndio sifa!..
Pole ndugu yangu bunge letu ni lao na wanatumia maneno mazito sana kwa wapinzani ambayo sidhani kama yangetoka upande huu wangeweza hata kunywa maji.
Lugha hiyo ipo kwa wapinzani tu, nina hakika kuna kila hila zimetumika ktk mkataba huu kwani haukufahamika kwa wananchi wala Wabunge hadi ulipowasilisha wewe hoja yako bungeni. Uwazi uko wapi?...
Sasa tuwaulize wao wananchi wakazi wa sehemu hiyo wameandaliwa vipi na serikali! ama pia tunasubiri hao wa Mazingira!
Je, Ikiwa hawa Barricks watakataliwa toka upande wa mazingira ina maana mkataba umekufa?.
 
Akinukuliwa na Hansard ya tarehe 16/07/2007, Mheshimiwa Kabwe Zitto alisema nanukuu “ kutokana na majibu ya Mheshimiwa Waziri kuhusiana na Mkataba mpya wa Mgodi Buzwagi ambao Mheshimiwa Waziri ameeleza maelezo ambayo siyo sahihi, amedanganya na ameeleza vitu ambavyo kwa kweli sivyo ambavyo vipo katika Mkataba ambao ameusaini” mwisho wa kunukuu. ...

Gamba,

Hiyo nukuu hapo juu, imekaa kiaina hivi....................kwa namna fulani....ukiangalia toka Zitto aianzishe hoja inawezekana kabisa aliuona huo Mkataba wenyewe.......ukweli anaujua yeye Zitto....
 
Halafu kuna key issues za kisheria, kwa mfano inapo tokea migogoro ktk mikataba, je ni Sheria za Wapi zitatumika ktk arbitration, za Uingereza kuliko sainiwa mkataba au za Bongo au zakimataifa. Sasa Ka-damage akitueleza, kama kusaini uingereza au Dar au kokote hakuta kuwa na efffect, kwa sababu incase of dispute wamekubaliana sheria zitakazo tumika.
Ndio hapa ina kuja Hoja za Kina Mkono ktk kuwa waangalifu ktk ku-saini mikataba kama hii.
Halafu hiyo haraka ya kusaini ilitokana na nini? kwamba muwekezaji alikuwa anakimbia na sisi tuna muhitaji au? au hayo madini yataoza?
last but not the least ikiwa sisi tu-dance according to the tune of investor, then interest za nchi zina lindwa vipi, maana kila kukicha tuna badili sheria iwe ya kodi au ya investment au ya madini. Kuna kiswahili kirahisi kina sema kizuri kinajiuza kibaya kinajitembeza, sasa sijui taifa la tanzania tumefikia hatua hiyo ya kujitembeza badala ya kufuatwa. Basi ujue tuna tatizo hapo, labda tu wagumba/tasa

yap yap august, well said
 
Katika majibu ya Kramagi tarehe 16/7 kwa Zitto alisema mgodi wa Buzwagi ni mdogo sana,

Katika majibu yake anaonyesha huo mgodi ulikuwa wa mhimu sana, utaongeza pesa lukuki na ajira zaidi ya 600!

Huu ndio mgodi mdogo? na kama huu ndo mdogo mikubwa ni ipi na imezalisha ajira na kuingizia Taifa pesa kiasi gani?

Mbona majibu yake haya mawili yana gongana? kuna nini hapo kati kati?

.....pamoja na kwamba its a relative simple analysis within migodi ya barrick.........lakini bado...Why kuukimbilia?
 
Zitto,
Pole ndugu yangu pole sana!........

Sikuona hata sehemu MOJA uliyosema kuwa waziri wetu Ni MUONGO! analidanganya taifa ila ni Karamage mwenyewe aliyeanzisha hili neno Kudangabya!
Ni pale alipotanguliza maneno haya ktk hotuba yake:-
Mheshimiwa spika, mtoa hoja amejielekeza ktk masuala makuu mawili ambayo anadai wakati nayaelezea, aidha sikuwa sahihi au nilidanganya.........

Haya ni maneno yake mwenyewe waziri ambaye kwa kujibu hoja yako na alichukua moja Kudanganya kisha akalijengea hema kuwatia chunvi wabunge hadi wafikie kuamini kwamba wewe hukuwa na hoja ila kutafuta muongo nani kati yenu!.Na walivyokuwa Wadanganyika wakanunua mtego wa waziri kiasi kwamba ikabadilishwa hoja na kuwa swala la uongo!. ........
Hivi kweli, ulitakiwa uulize vipi?...lugha gani ilitakiwa uitumie ili wao waone kama umewakilisha hoja yakokutafuta usahihi wa swala zima........

Mkandara,

Uchambuzi mzuri sana...... Karamagi anadai kuwa Zito katumia maneno kudanganya au kutokuwa sahihi....ambayo so far hayamo kwenye hoja ya zito. Asante kwa kuonyesha hilo.....

Nimesoma pia jinsi Chacha Wangwe alivyokuwa anasimamishwa evry now and then wakati akijenga hoja kwa mifano.

Kuna solution moja tu kwa mambo kama haya wanayofanya wenye meno ya kutafuna mali zetu................
 
Haiwezekani majibu ya Karamang kuwa sahihi kwani hakuna mkataba.Yeye anatetea alichokifanya lakini hakuna mbunge ambaye anajua nini kipo kwenye mkataba sasa hukumu itakawa vipi ya haki?
Naona sasa watanzania wanaanza kuchanganyikiwa.

Hoja ya msingi ya kabwe ni kwamba mkataba unamapungufu, sasa hayo mapungufu yangejulikana iwapo tu mkataba ungetolewa kwa pande zote mbili na bunge ili waujadili halafu tujue je ni kipi si cha kweli.

Halafu wasiwasi mwingine ambao nauona ni pale bunge lilipomfungia mbunge kwasababu tu ameonyesha wasiwasi wake kwa utendaji wa waziri na wizara. Kama kila anachosema waziri ni sahihi tunahitaji bunge la nini? nini kinawapeleka bungeni kama mawaziri hawkosei wala hawakosolewi. Je kuhoji kama anachokifanya waziri ni kwa maslahi ya taifa au la ni kosa gani.

Inatia kichefuchefu kuona bunge limegubikwa na watu
waliokatatamaa.
Lazima tukubali bila kuwa na wabunge wawajibikaji bila kujali vyama vyao nchi imekufa.

Majibu ya waziri ni ya kihuni kwani haielezi nini kipo ndani ya mkataba wa buzwagi, hajibu hoja bali anatumia kivuli cha siasa akijua wapambe ni wakutosha.
Wakati umefika wa mtanzania kujua kila kosa la serikali ni msalaba kwa mwananchi, inashangaza kuona hakuna maji,barara safi na hospitali bora kwa sababu ya ndio mzee.

Wanashindwa kuwajibika na kuikuta nchi inakufa, wameuwa hospitali wakizani watatibiwa wote ulaya, sasa uone ujinga wao wakizidiwa wanapelekwa muhimbili kwanza kabla hawajaenda kufa nje, ila wakiwa juu ya viti vya bunge wanajibu utumbo kama wao malaika.

wanachokijua ni kula rushwa basi. Kulikuwa hakuna haraka yeyote ile zaidi ya rushwa kusaini ule mkataba uingireza kwani kizuri chajiuza kibaya.......

Ukweli hauko mbali na historia itasema, dhabmi za iptl, richmond,bulyanhulu, bado inatutafuna, sasa tungoje tuone...

you can support either way, result is ours

ujinga ni ugonjwa mkali kuliko ukimwi------------
 
waziri Karamagi alisema.........

Mheshimiwa Spika, maana ya mabadiliko hayo ni kwamba 15% additional capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure ilirudishwa kwa makampuni ya madini yaliyoingia mkataba na Serikali kabla ya tarehe 1 Julai 2001. Ndio sababu migodi iliyokuwa na mkataba na Serikali kabla ya tarehe 1 Julai, 2001 ilieendelea kuwa na kivutio 15% additional capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure hata baada ya kuondolewa kwa fungu hilo.

something very fishy ktk hiyo paragraph hapo juu, hichi ndicho kilichowakimbiza kusainia UK
 
Nimeshagundua, hawana hoja, kweli Kitila namkubali ingawa sio Chadema mimi.

FD

Anakuwa tishio kwa Mbowe na soon wataanza kumfanyia fitna kama walivyomtoa Shaibu Akwilombe na Amani Walid Kaburu.

No wonder kuna siku hapa JF mtu mmoja alipo-suggest kuwa yeye ndio awe kiongozi wa CHADEMA huyu bwana aliomba kauli ifutwe mara moja kwasababu anajua madhara yake. Kwikwikwi!

Yaani mnachokifanya hapa ni kama ni kama Bush na Blair kumpigia debe Morgan Tsvangirai....ama Netanyahu kumkubali Mahmoud Abbas

Tanzanianjema
 
waziri karamagi anasema............

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la Mkataba kusainiwa Uingereza, kama nilivyolielezea Bunge lako Tukufu wakati nahitimisha hoja ya Makadirio ya Matumizi ya Wizara yangu kwa mwaka wa fedha 2007/08, mkataba huo uliandaliwa Tanzania na wataalamu wetu na ukapitia taratibu zote zinazopaswa kufuatwa ikiwa ni pamoja na kuidhinishwa na Kamati ya Ushauri ya Madini (Mining Advisory Committee) na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Mhe. Spika naomba kuwasilisha kwako vielelezo vya ushahidi wa kauli yangu hii. Vile vile uamuzi wa kuingiza mradi wa Buzwagi kwenye miradi ya Barrick Gold Corporation ambayo ni kampuni mama ulihitajika kufanyika kabla ya Machi, 2007, vinginevyo fursa ya uwekezaji katika mradi huu ingepotea.

Ukiskia.......UMAFIA ndio huo hapo juu!!
 
Kilichonishangaza ni kuwa wabunge wamesikiliza majibu yale wakafurahishwa na mtiririko ule wakasahahu kuchambua facts....

Pole sana kaka, unadhani kuna waliokuwa wakisubiri fact mle ndani? Kama waliokuwepo hawazidi kumi mle ndani na wengine waliamua kujiondokea kuliko kushuhudia ule msumari wa mwisho

Tanzanianjema
 
Haiwezekani majibu ya Karamang kuwa sahihi kwani hakuna mkataba.Yeye anatetea alichokifanya lakini hakuna mbunge ambaye anajua nini kipo kwenye mkataba sasa hukumu itakawa vipi ya haki?
Naona sasa watanzania wanaanza kuchanganyikiwa.

Hoja ya msingi ya kabwe ni kwamba mkataba unamapungufu, sasa hayo mapungufu yangejulikana iwapo tu mkataba ungetolewa kwa pande zote mbili na bunge ili waujadili halafu tujue je ni kipi si cha kweli.

Halafu wasiwasi mwingine ambao nauona ni pale bunge lilipomfungia mbunge kwasababu tu ameonyesha wasiwasi wake kwa utendaji wa waziri na wizara. Kama kila anachosema waziri ni sahihi tunahitaji bunge la nini? nini kinawapeleka bungeni kama mawaziri hawkosei wala hawakosolewi. Je kuhoji kama anachokifanya waziri ni kwa maslahi ya taifa au la ni kosa gani.

Inatia kichefuchefu kuona bunge limegubikwa na watu
waliokatatamaa.
Lazima tukubali bila kuwa na wabunge wawajibikaji bila kujali vyama vyao nchi imekufa.

Majibu ya waziri ni ya kihuni kwani haielezi nini kipo ndani ya mkataba wa buzwagi, hajibu hoja bali anatumia kivuli cha siasa akijua wapambe ni wakutosha.
Wakati umefika wa mtanzania kujua kila kosa la serikali ni msalaba kwa mwananchi, inashangaza kuona hakuna maji,barara safi na hospitali bora kwa sababu ya ndio mzee.

Wanashindwa kuwajibika na kuikuta nchi inakufa, wameuwa hospitali wakizani watatibiwa wote ulaya, sasa uone ujinga wao wakizidiwa wanapelekwa muhimbili kwanza kabla hawajaenda kufa nje, ila wakiwa juu ya viti vya bunge wanajibu utumbo kama wao malaika.

wanachokijua ni kula rushwa basi. Kulikuwa hakuna haraka yeyote ile zaidi ya rushwa kusaini ule mkataba uingireza kwani kizuri chajiuza kibaya.......

Ukweli hauko mbali na historia itasema, dhabmi za iptl, richmond,bulyanhulu, bado inatutafuna, sasa tungoje tuone...

you can support either way, result is ours

ujinga ni ugonjwa mkali kuliko ukimwi------------
Kinepi,
1. Hii mpya- ukiwa Mbunge ukihoji Waziri na kama una wasiwasi2 na jambo- hata kama unataka ufafanuzi! Lazima uadhibiwe na usimamishwe????

2. Hii mpya- kwa hiyo Serikali isihojiwe na Wabunge- na wasikae waonyeshe wasi2 laa sivyo- utafuangiwa???

3. Waungwana- mko hapo? Logic na hekima ya Bunge la Tanzania liko wapi? Sasa serikali linaanza udictata na kuwafunga Wabunge midomo?

4. Isije ikatokea sasa Mbunge usipopiga makofi- ukaangaliwa na jicho mbaya ukafungiwa! Mimi siko CHADEMA wala CCM ila kama Mtanzania- fairness iko wapi?

5. CCM yenye wabunge wengi kiasi hicho haina haja kuwaonea wapinzania walio wachache! Otherwise haina haja kuwa na Upinzani kwa sasa! Kumsimamisha Zitto siyo fair!
 
mwanakijiji,

swali lako la gharama ya jengo.............ni very interesting and especially ukilinganisha na majibu ya Karamagi kuhusu migodi
 
Lazima tukubali kwamba katika rhetoric, Karamagi alimzidi Zitto. Kwa wanaotazama rhetoric wanaishia kwenye utetezi mzuri wa Karamagi kusema Zitto ni mwongo.

Ukweli hapa ni kwamba hoja za Karamagi zimesimama kwa sababu serikali ilipata muda wa kuziweka sawa kwa kutumia document za Zitto. Hata mimie ningeweza kumshushua Zitto kama ningekuwa upande mwingine na akanipa hoja zake mapema.

Zitto mwenyewe alipoomba apewe mkataba wenyewe auone na baadhi ya documents alinyimwa. Hapa ndipo alipopigwa bao. Hivyo, ilitarajiwa kwamba serikali ingejibu mapigo kwani ilishajiandaa. Lakini kujibu mapigo siyo kusema ukweli.

Zitto, kwa kujua hili, ndiyo maana aliomba iundwe kamati ichunguze hata majibu haya ya Karamagi. Ingekuwa fursa pia ya kujua uchafu ulio katika mkataba huu na mingine ambayo serikali imekuwa inawanyima wabunge.

Kinachompa ushujaa Zitto ni unpopularity ya serikali kwa sababu sasa wananchi wameshajua kwamba ni corrupt government by corrupt leaders! Hata hivyo, bila KAMATI majibu ya Karamagi yanabaki kuwa rhetoric tu.

Hivi kumbe kuna political analysts humu...

Tanzanianjema
 
(1) Barricks makao yao yapo Toronto na sio Uingereza na hata kama mikataba ingetumwa sehemu mbili isingeliikuwa Uingereza. Why UK? ndio swali ulouliza! kwa kuzingatia kuwa hakuna uhusiano wowote wa Uingereza na mkataba huu, na umeuliza vizuri kama kuna sababu hasa ya Mkataba huo kuwekwa Uingereza.
Ningeshauri sana hizo nakala za Mkataba zitazamwe vizuri maanake siwezi kuelewa kwa nini Waziri wetu awe na mihuli ya serikali kwenda itumia London ktk Mkataba ambao alifahamu unaweza sainiwa hapa nchini...February haikuwa shida kwani Barricks wana Ofisi zao nchini sio kampuni ambayo haiwezi kuapatikana kirahisi. Something fishy! bob.... mtakuja nambia.

Pili swala la kigezo cha gharama za ujenzi wa mradi huo kachukua cheap shot sana baada ya kuitumia Bulyanhulu ambao ulijengwa miaka ya tisini badala ya North Mara!..Hata hiyo Bulyanhulu ilijengwa wakati dhahabu ikiuzwa kwa dollar 200 na kitu kwa aunzi moja tofauti kabisa na hali iliyopo leo. Mbona hawakusema hawataweza kuweka mkataba hadi hapo dhahabu itakapo panda bei?.. North Mara imeweka mkataba lini, ama Tualawake mbona asichukue hiyo mifano kufafanua hoja yako!

Kaka Mkandara, naona umeyaangalia majibu yale kwa makini. Soma reports za Barrick kuhusu mradi huo na mingine ya Tanzania hapa.
 
Back
Top Bottom