Haiwezekani majibu ya Karamang kuwa sahihi kwani hakuna mkataba.Yeye anatetea alichokifanya lakini hakuna mbunge ambaye anajua nini kipo kwenye mkataba sasa hukumu itakawa vipi ya haki?
Naona sasa watanzania wanaanza kuchanganyikiwa.
Hoja ya msingi ya kabwe ni kwamba mkataba unamapungufu, sasa hayo mapungufu yangejulikana iwapo tu mkataba ungetolewa kwa pande zote mbili na bunge ili waujadili halafu tujue je ni kipi si cha kweli.
Halafu wasiwasi mwingine ambao nauona ni pale bunge lilipomfungia mbunge kwasababu tu ameonyesha wasiwasi wake kwa utendaji wa waziri na wizara. Kama kila anachosema waziri ni sahihi tunahitaji bunge la nini? nini kinawapeleka bungeni kama mawaziri hawkosei wala hawakosolewi. Je kuhoji kama anachokifanya waziri ni kwa maslahi ya taifa au la ni kosa gani.
Inatia kichefuchefu kuona bunge limegubikwa na watu
waliokatatamaa.
Lazima tukubali bila kuwa na wabunge wawajibikaji bila kujali vyama vyao nchi imekufa.
Majibu ya waziri ni ya kihuni kwani haielezi nini kipo ndani ya mkataba wa buzwagi, hajibu hoja bali anatumia kivuli cha siasa akijua wapambe ni wakutosha.
Wakati umefika wa mtanzania kujua kila kosa la serikali ni msalaba kwa mwananchi, inashangaza kuona hakuna maji,barara safi na hospitali bora kwa sababu ya ndio mzee.
Wanashindwa kuwajibika na kuikuta nchi inakufa, wameuwa hospitali wakizani watatibiwa wote ulaya, sasa uone ujinga wao wakizidiwa wanapelekwa muhimbili kwanza kabla hawajaenda kufa nje, ila wakiwa juu ya viti vya bunge wanajibu utumbo kama wao malaika.
wanachokijua ni kula rushwa basi. Kulikuwa hakuna haraka yeyote ile zaidi ya rushwa kusaini ule mkataba uingireza kwani kizuri chajiuza kibaya.......
Ukweli hauko mbali na historia itasema, dhabmi za iptl, richmond,bulyanhulu, bado inatutafuna, sasa tungoje tuone...
you can support either way, result is ours
ujinga ni ugonjwa mkali kuliko ukimwi------------