Pole. Mimi sikuwa natazama kujieleza. Kushabikia watu kwa kujieleza ndio kumetufikisha hapa tulipo. Nilisoma hoja kumi na moja za Zitto, nikasoma majibu ya Karamagi kwa kipengele kimoja kimoja cha hoja za Zitto, nikaangalia na viambatanisho vya Karamagi. Nika-conclude kwamba Zitto alikuwa anatuhadaa na alikurupuka kutafuta umaarufu.
Sasa, kwenye kumfungia Ubunge, nilisema toka jana kwamba I thought it was a bad idea. The fact that ameonekana muongo ingetosha. Lakini, well, Bunge lina kanuni nyingi kuliko kanisa.
MAREKEBISHO KICHWA CHA HABARI
Hoja ya Zitto yatupwa; asimamishwa KUHUDHURIA VIKAO VYA BUNGE
TUWE WAZALENDO KIDOGO TUSIANDIKE NA KUCHANGIA HOJA KWA ITIKADI TANZANIA YOTE NI YETU NA ZITTO TUNAOMBA UNAPOJIBU HOJA USITUMIE MICHANGO YA MITANDAO KAMA FORUMS AU CHATROOMS FANYIA TAFITI MAJIBU YAKO AU ULIZA KABDA HUJAKURUPUKA
AHSANTE
Mimi nilivyoona ni kuwa majibu ya Karamagi kweli yalikuwa yamenyooka kiasi kuwa hoja za Zitto zilionekana kuwa hazikufanyiwa maandalizi ya kutosha. Inaelekea aliyaandaa majibu yale kwa muda wa kutosha.Hata hivyo ninapoyapitia kwa makini majibu yale dhidi ya hoja Zitto na kuchambua facts said:Sasa Kichuguu kama bado hujazipitia hizo sheria za madini na za fedha,ni vipi umeweza kuzichambua facts kama unavyodai? ni kipi usichokubaliana nacho katika majibu ya waziri?
waziri karamagi anasema............
Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la Mkataba kusainiwa Uingereza, kama nilivyolielezea Bunge lako Tukufu wakati nahitimisha hoja ya Makadirio ya Matumizi ya Wizara yangu kwa mwaka wa fedha 2007/08, mkataba huo uliandaliwa Tanzania na wataalamu wetu na ukapitia taratibu zote zinazopaswa kufuatwa ikiwa ni pamoja na kuidhinishwa na Kamati ya Ushauri ya Madini (Mining Advisory Committee) na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Mhe. Spika naomba kuwasilisha kwako vielelezo vya ushahidi wa kauli yangu hii. Vile vile uamuzi wa kuingiza mradi wa Buzwagi kwenye miradi ya Barrick Gold Corporation ambayo ni kampuni mama ulihitajika kufanyika kabla ya Machi, 2007, vinginevyo fursa ya uwekezaji katika mradi huu ingepotea.
Ukiskia.......UMAFIA ndio huo hapo juu!!
Yaani Wbunge wetu wamepoteza opportunity ya ajabu- Kuunda tume kuchunguza nani muongo katia ya Waziri Karamagi na Mhe. Zitto.
Kumbe hawa Wabunge wa CCM wanaunga mkono hizi siri za mikataba ya madini. Nimekunguwazwa sana, kama wangekuwa wakweli na wanaitakia nchi hii mustakabali mwema hiyo ilikuwa ni good opportunity ya kuungalia huo mkataba vizuri, kumbe wanapiga kelel bure kutudanganya Watanzania. Wamelishwa yamini, wako tayari ku-support uozo kwa kulishwa carrot na Serikali.
Kwang mimi kama tume ingeundwa, whatever the judgement after matokeo ya uchunguzi wa tume ya Bunge ningefurahi sana; lakini kwa kukwepa kuunda tume basi kuna jambo linafichwa na linajulikana. Bado naamini Zitto amesema ukweli vinginevyo tume ingeundwa na matoke ya uchunguzi wa Tume hiyo nadhani yangebadili mustakablai mzima wa nchi hii, kitu ambacho Wakubwa wetu wanakijua na ndiyo maana wamembania Zitto!
Wana JF, serikali imeshituka ndiyo maana wameizima hoja ya Zitto, tungeona mengi na pengine mwisho wa Walanchi hawa ungefika.
Tanzania Njema,
Umeona mjadala ulivyonoga??? Ndio tunavyopenda.
Zitto kakosea, Karamagi naye hakupatia ktk majibu yake ila alikuwa mjanja sana kujibu na kuwanunua wabunge kwenye majibu yake, halafu inaelekea ulikuwa ni mkakati uliopangwa.
Kwa kifupi kwa maoni yangu, Zitto alikosea ila adhabu ni kubwa mnoooo!!
Asante
FD
1. Hii mpya- ukiwa Mbunge ukihoji Waziri na kama una wasiwasi2 na jambo- hata kama unataka ufafanuzi! Lazima uadhibiwe na usimamishwe????
2. Hii mpya- kwa hiyo Serikali isihojiwe na Wabunge- na wasikae waonyeshe wasi2 laa sivyo- utafuangiwa???
3. Waungwana- mko hapo? Logic na hekima ya Bunge la Tanzania liko wapi? Sasa serikali linaanza udictata na kuwafunga Wabunge midomo?
4. Isije ikatokea sasa Mbunge usipopiga makofi- ukaangaliwa na jicho mbaya ukafungiwa! Mimi siko CHADEMA wala CCM ila kama Mtanzania- fairness iko wapi?
5. CCM yenye wabunge wengi kiasi hicho haina haja kuwaonea wapinzania walio wachache! Otherwise haina haja kuwa na Upinzani kwa sasa! Kumsimamisha Zitto siyo fair!
Pedro,Mzalendo halisi hapo nakuunga mkona moja kwa moja, hivi mbona zamani hata enzi za chama kimoja, ilikuwa kama hatumsikii mbunge wetu redioni akiihoji serikali basi tunaona kama ni anazembea? Sasa leo hii inakuwaje kukaa kimya na kupiga makofi ndio chati?
Na nchi itaendeleaje kama hamna debate za aina yoyote mahojiano n.k? sasa kama mawaziri hawawezi kuulizwa watetee shughuli zao si watafanya watakalo? na kuipeleka nchi wanavyotaka?
Imagine Malecela ndie angekuwa raisi wetu pale ingekuwaje? hivi mzee wa umri ule si ndio kwanza alitakiwa atumie busara? maana mimi sijawahi kusikia Babu akichapa viboko wajukuu, yeye huwa ni mtu mtulivu wa kugawa busara na kusolve mambo ki-style, sasa yeye na ubabe-ubabe wake na kutoa maonyo ya vitisho kama vile mbeba zege? wakati alishatuhakikishia kuwa yeye sio mbeba zege?
And that is very annoying for those of us that are not party supporters and are above the "Yanga/Simba syndrome "
waziri karamagi anasema............
Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la Mkataba kusainiwa Uingereza, kama nilivyolielezea Bunge lako Tukufu wakati nahitimisha hoja ya Makadirio ya Matumizi ya Wizara yangu kwa mwaka wa fedha 2007/08, mkataba huo uliandaliwa Tanzania na wataalamu wetu na ukapitia taratibu zote zinazopaswa kufuatwa ikiwa ni pamoja na kuidhinishwa na Kamati ya Ushauri ya Madini (Mining Advisory Committee) na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Mhe. Spika naomba kuwasilisha kwako vielelezo vya ushahidi wa kauli yangu hii. Vile vile uamuzi wa kuingiza mradi wa Buzwagi kwenye miradi ya Barrick Gold Corporation ambayo ni kampuni mama ulihitajika kufanyika kabla ya Machi, 2007, vinginevyo fursa ya uwekezaji katika mradi huu ingepotea.
Ukiskia.......UMAFIA ndio huo hapo juu!!
Bunge wanakosea,Nimesikia ofisi ya bunge imetoa onyo kwa vikundi vya kupigania haki za binadamu kuwa makini kutowapotosha wananchi juu ya sakata la kusimamishwa kwa Zitto. Kulikoni bwana katibu wa bunge?