The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

Mwafrika wa kike,
Ninakubaliana na wewe kwa 100%.

Na ukweli huu ndio unaofanya moyo wangu mdogo kuvunjika kabisa, na kukusudia kufumba macho na masikio yangu ili nisione wala kusikia haya mauzauza.

Im very proud of my country TZ. Nimejaribu kuwa mzalendo kwa nchi yangu mara zote ninapokuwa nimezungukwa na marafiki wa kigeni, non-colored & colored. Lakini sasa, nahisi wenzangu hawa watakuwa wananicheka kwamba mapenzi kwa nchi yangu yamenitia upofu wa kushindwa kuona mauzauza yanayoendelea huko.

Sijui hata niseme nini, I'm just terribly hurt. That's all I can say!

.
Zinduka,

Mabalozi (wengi wao) hapo nchini wanafurahia kinachoendelea sasa hivi dhidi ya Zito kwa sababu mambo kama haya ndio hupelekea civil unrest katika nchi. wauza silaha wengi wamekuwa wakisubiri kwa hamu siku nchi yenye utajiri kama Tz itakapotumbukia kwenye civil war ili wajiuzie silaha kama hawana akili nzuri.

Kwa sasa usitegemee reaction kubwa toka kwao...

It's very sad but true.
 
wapi hizo hoja 11 za Mh Zitto na majibu yake Karamagi tuyachambue hapa......eti wanasema nini? EIA imefanya nini??

Ogah,

kichuguu aliiweka tangia jana, see below as reported by Mwananchi Newspaper:-

Hoja kuchunguza mkataba Buzwagi yatibua Bunge


*Waziri, Mbunge watunishiana misuli
*Hoja yageuzwa ya kisiasa
*Wabunge wengine wavutana
*Baadhi watishiana, wengine walalama

Na Ndyesumbilai Florian, Dodoma

HOJA binafsi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema) kuhusu utaratibu uliotumiwa na Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, kusaini haraka mkataba wa mradi wa madini wa Buzwagi, Wilayani Kahama, umeligeuza Bunge kuwa kikao cha mapambano ya kiitikadi na kupunguza uzito wa hoja na mjadala wenyewe.
Kinyume na ilivyotarajiwa na wengi, hatma ya hoja hiyo ilionyesha zaidi kufuatiwa na kurushiana vijembe na kejeli kutoka miongoni mwa wabunge wa chama tawala, CCM dhidi ya wale wa upinzani ambao kwa kiasi kikubwa walionekana dhaifu, kushindwa kuhimili vishindo, hususan katika kujibu mapigo ya Waziri Karamagi dhidi ya hoja ya msingi ya Kabwe.

Matokeo yake, karibu kila mchangiaji aliyesimama, alikuwa akionyesha kuegemea zaidi kwenye itikadi au fungamano la kambi yake kisiasa, kuliko uzito wa hoja hiyo iliyoibuliwa na kujengwa na mwanasiasa huyo kijana, hasa ile inayohusu matatizo kuhusu mikataba katika sekta ya madini na sheria zinazosimamia sekta hiyo.

Akiwasilisha hoja hiyo, Kabwe alilitaka Bunge likubali kuunda kamati hiyo teule ili kuchunguza mwenendo mzima wa kusainiwa kwa mradi huo kulikofanyika jijini London, Uingereza Februari mwaka huu. Alidai kuwapo kwa ukiukwaji katika baadhi ya taratibu zinazosimamia, kuongoza sekta ya madini nchini.

Miongoni mwake ilikuwa ni haraka iliyomfanya Waziri Karamagi ausaini mkataba huo akiwa nje ya nchi bila kusubiri kwanza ripoti ya tathmini ya athari kwa mazingira (EIA) kuhusiana na mradi huo ambazo kwa kawaida hutolewa na Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (Nemc).

Katika hoja yake yenye vipengele 11, Kabwe alitaka kamati hiyo iundwe kwa lengo la kujiridhisha na kuondoa utata huo ambao alidai umejitokeza zaidi na kugubika mchakato mzima wa kusainiwa kwa mkataba huo, akidai kuwa ilikuwa kinyume na Sheria ya Madini ya mwaka 1998.

Pia, alihoji sababu za kuendelea kuiita miradi wakati Kampuni ya Barrick imewekeza mtaji mkubwa katika mradi huo, kiasi cha dola za Kimarekani milioni 400, ikiwa ndio mradi mkubwa wa pili baada ya ule wa Bulyankhulu, pia ulioko Kahama, ambao umewekezwa dola milioni 600 na kampuni hiyo.

Hata hivyo, aliposimama, Waziri Karamagi alianza kuzipangua hoja hizo moja baada ya nyingine, huku akishangiliwa kwa makofi na wabunge wa CCM.

Kama vile hiyo haitoshi, Karamagi alionyesha dhahiri kukejeli hoja za Kabwe kuwa hazikuwa na msingi na zaidi zilitokana na ukosefu wa uelewa wa masuala yanayosimamia sekta ya madini na kuongeza kuwa hakukuwa na uvunjaji wowote wa sheria za nchi.

Badala yake, alisema alichokifanya akiwa katika ziara ya kikazi ya muda mrefu nje ya nchi, ni kupata habari kuhusu kuwapo kwa nafasi ya uwekezaji katika mradi huo wa madini na hivyo kuichangamkia.

Alisema alichoshindwa kuelewa Kabwe ni kushindwa kutofautisha na kisha kuchanganya sheria zinazohusu utafutaji na uwekezaji katika madini na uchimbaji halisi.

Aliongeza kuwa hilo ndilo limemfanya afikirie suala la EIA kwa mradi wa Buzwagi, ambalo kwa kawaida huwagusa zaidi wachimbaji ambao tayari wamepewa leseni za uchimbaji katika migodi ya madini na siyo wale wanaoendelea na uwekezaji kama ilivyo kwa kampuni ya Barrick kupitia mradi wa Buzwagi.

Kwa maana hiyo, Karamagi alieleza kuwa hakukuwa na sababu ya kuhitaji kwanza ripoti hiyo ambayo itafikiwa wakati wawekezaji hao watakapoanza shughuli rasmi za uchimbaji wa dhahabu katika mgodi huo.

Kuhusu manufaa ambayo Watanzania wataweza kupata kutokana na mradi huo, Karamagi alieleza kuwa ni kupatikana kwa ajira zaidi ya 600 kwa Watanzania, zikiwamo zile za maafisa wa vyeo vya juu.

Aliongeza kuwa mradi huo utaweza kuwekeza kiasi cha zaidi ya dola milioni 800 baada ya kukamilisha uwekezaji wake na kuongeza kuwa kamwe serikali isingeweza kuacha nafasi hiyo ipotee bure na ndiyo maana ikasaini mkataba huo mapema Februari kabla ya tarehe ya mwisho ya Machi mwaka huu.

Karamagi ambaye alizipangua hoja za Kabwe kwa umakini mkubwa, hatimaye alionyesha kuteleza na kutumbukia katika mtego wa kiitikadi alipodai kuwa hoja hiyo iliibuliwa na Kabwe na sasa imechukuliwa kama ajenda na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, anayeipigia debe majukwaani huku akivishambulia vyombo vya habari kuwa vimetumika kumchafua na kumpaka matope.

Wakichangia hoja hiyo, wabunge wa kambi ya upinzani, Khalifa Suleiman Khalifa (Gando-CUF), Mhonga Ruhwanya (Viti Maalum-Chadema), Chacha Wangwe (Tarime-Chadema), Maulida Anna Kome (Viti Maalum-Chadema) na Margareth Sakaya (Viti Maalum- CUF), wao waliunga mkono hoja ya kuundwa kwa kamati hiyo.

Hata hivyo, alikuwa Komu aliyewaacha hoi wabunge kwa kudai kuwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere pekee, ndiye anayeweza kukemea mambo yanayoendeshwa na serikali ya CCM ikiwamo wizi na ubadhirifu wa rasilmali za umma, yakiwamo madini.

Waliochangia kwa upande wa CCM, walikuwa Ruth Msafiri (Muleba Kaskazini-CCM), Suleiman Kumchaya (Lulindi), Adam Malima (Mkuranga), ambao walionyesha dhahiri kuungana na msimamo wa serikali na hata kuwabeza wapinzani.
 
Jamani mi ndo namaliza kuugulia hili la Zitto. Katika kuugulia kwangu hata hivyo nimejifunza mambo kadhaa.
1.Kwamba Zitto kwa muda mrefu amekuwa mwiba kwa wabunge wa CCM hasa wazee..wamekuwa wakimuangalia kwa jicho la kusema 'iko siku' sasa hapa ndo wamepata nafasi.

2. Kwamba Spika kwa muda mrefu amekuwa akikosa usingizi kwa huyu 'mtoto' kuleta kimbunga bungeni...kila akilala alikuwa anajiuliza 'haka katoto kesho katakuja na nini tena Mungu wangu..'hapa kapumua kwa ahueni, atapata usingizi
nina hakika hata wezi na walafi wakuu serikalini hapa wamapumua

3. CCM hawajui kushindana kwa hoja..wanatumia mabavu..na hawajifunzi kutokana na makosa. Hii mambo ya kujifanya wanafunza watu adabu ilimpatia Mrema umaarufu kiasi kwamba pamoja na mapungufu yake isingekuwa wizi wao angejipatia uraisi...

4. wabunge wengi ni wabunge bubu..sijui kanuni za bunge lakini najiuliza, hivi ina maana woote wamekubaliana na hoj ya kumsimamisha Zitto, au kila mmoja anachunga mkate wake?

5. CHADEMA inabidi watulie wajipange vizuri namna ya kutumia tukio hili kwa manufaa yao..if they play their cards right, this could be a golden opportunity to them

Duh, nadhani huu ni muda muafaka wa kujiunga na CHADEMA....jamani naomba kujiunga...
 
Japo na mimi niseme juu ya hili, sina information nyingi sana kama alichokisema zitto ni ukweli au uongo bali nachokiona mimi bunge letu haliko serious kabisa, kilichopo ni ushadadiajji tu wa itikadi za kichama na sio masilahi ya nchi, matokeo yake hata kama jambo lina ukweli na limetoka kwa mpinzani utaona tu linavyopindishwa ili mradi tu ccm wabaki salama, i find this very disturbing. Ukewli sioni busara ya kumtoa zitto bungeni. Hivi sio meghji aliyesema pamoja na kupanda kodi ya mafuta wananchi hawataathirika sana na mfumuko wa bei hasa kwenye usafiri? na ikawa vingine na wameshindwa ku control? au huu si uongo? yeye Mudhihir anayesema zitto atoke bungeni amewadanganya wananchi wake mara ngapi kwenye kampeni? kwa ufupi most of the places jimboni kwake hazifikiki, nilifanya research huko hali ni mbaya, kulala porini ni kawaida. yeye kapewa adhabu gni kwa kudanganya wananchi? Na mugongo mugongo una chuki za binafsi katika hoja zako? Sikuelewi.
 
Mzee Malecela naye eti anaongea kwa uchungu, hawa wazee kweli wana uchungu wowote? Ndio maana Nyerere aliwaita wahuni.

Mimi hili bunge nitaacha kulisikiliza maana unaweza kuchukia
na kufanya mambo ya ajabu.

Mimi imeniudhi sana maana nilitegemea watu kama akina Malecela angalau wangelikuwa na busara ya kuwashauri wabunge wao lakini yeye ndio anaongoza kumfungia mtu ambaye mchango wake ni mkubwa kuliko wengi wao?

Malecela anapewa heshima sana ndani ya CCM katika kuendesha mambo kihuni.Angalia hata katika kuchangia hoja za kumfungia Zito,yeye kapangwa kuwa msemaji wa mwisho na kabla hajazungumza eti anaitwa Zito azungumze kama ana lolote la ziada(kuomba radhi) kabla HAKIMU mkuu Malecela hajapitisha hukumu.
Hii ni aibu sana. Hata hivyo kama ilivyotegemewa na wengi SHUJAA KIJANA WA KITANZANIA ZITO KABWE hakubembeleza wanafiki na wasaliti wa nchi hii bali aliwaambia wafanye vile watakavyo na kuwa fikra za kimapinduzi zitadumu.Wazee kama hao wasubiri aibu mwisho wa safari kisiasa.
 
Zitto,

Hongera, Ama kwa hakika tumechemsha (CCM) adhabu ilikuwa nzito saana ukilinganisha na kosa lenyewe.

Imenishangaza mzee JSM kutetea wewe kusimamishwa, hawa ndio watu waliobakia wenye busara ambao tunawategemea. Angalau ange tumia busara kuwasaidia vijana wanaokua kisiasa kama Zitto na wengine na sio kukandamiza!!!.

Anyway, ndio siasa at its best. Hongera kijana unafanya kazi nzuri sana.

Mungu atakubariki na kukusaidia.

FD
 
Waungwana,

Haitoshi kulalamika hapa, mimi nafikiri tuchukue hatua zilizoko kwenye uwezo wetu.

Mimi sina mapenzi na hivyi vyama ila ni mwumini wa demokrasia na kile kilichofanyika pale kisipozuiwa mapema, bunge letu litakufa.

1.Baadhi ya mambo ambayo tunaweza kufanya ni kuandika makala nyingi magazetini kupinga kitendo hicho.
2. Kununua ukurasa mzima au hata mbili kwenye gazeti linalosomwa na Watanzania wengi na kuandika barua kali pamoja na kuweka majina yetu. Hizo pesa zinaweza kuchangwa.
3. Kuwaandikia barua wabunge zetu.
4. Kuchanga pesa japo kidogo na kumkabidhi Zitto lakini zoezi hilo kuongozana na publicity ya hali ya juu, inaweza kuwa organized na kuhusisha mkutano na waandishi wa habari ambapo watu toka sehemu mbalimbali wanaweza kupiga simu na kuonyesha walivyochukishwa na kitendo hicho na hata wengine kutishia kupambana na hao wabunge waliochukua hatua hiyo.

Na mambo mengine mengi.
Tusilalamike tu hapa, wacha tuchukue hatua.
 
kazi ipo, nnaona ndugu yetu Kabwe tokea yale ayliomkuta hajui ni nini anafanya, bora apumzike kwanza na katika kupumzika akae na kutafakari, kisha ajisawazishe na kuanaglia wapi alipokosea.


huyu jamaa tokea kutokea msiba ambaop yeye anahusika amekuwa hajielewi, mara ooh rais kanizalilisha, mara ooo EAC kuwa EAF bomba, mara ooo karamagi hivi, kwa nini umekuwa kiromo romo?

umekuwa mtu wa kukurupuka tu, au ile halbadiri na ww imekupata?


sasa turudi kwenye mada ukiangalia kwa umakini utagundua kuwa zitto hajajipanga, kakurupuka, na haya ndio matatizo ya upinzani, kunahitajika mashambulizi ya uhakika na ya maana kabla ya kushambulia sio tetesi tu, au hisia maana sasa mnaotukanisha upinzani, kila siku nyie mnasema maneno halafu mnamalizia kushindwa kutetea hoja zenu.

demekrasia imefata mkondo wake kwa mujibu wa katiba tulio nayo, Kabwe kawakilisha hoja, waziri kajibu mapigo, wachangiaji wa pande zote mbili wamepata fursa za kuchangia.

michango ya wapinzani ilionekana wazi kuwa dhaifu, sasa tumlaumu nani? jamani yaani kwa kuwa wapinzani hata wakija na hoja dhaifu tuseme wameonewa na CCM hata wakija na hoja za msingi tuseme wameonea kwa kuwa wao wengi? nmo tuwe fair and balanced.


hili ni somo zuri, siasa ni mapambano kwa hiyo panga mashambulizi na pima uwezo wa unaepambana nae ili ujue ni nguvu gani ujtumie.

Afadhali useme wewe. Manake hawa jamaa wa CHADEMA wao kila kitu anachosema Zitto kina maana. Eti sasa wanataka afanye a victory tour...I suspected this all along....kumbe yote hii habari ni kutaka kutafuta umaarufu. Wanasiasa wote are of the same colour...kazi yao kutuchezea shere.

Mimi nadhani dogo inabidi atulie ajipange, hapa tena sio siasa za pale UDSM. Lazime azinduke kwenye scandal ya AC, na aache kunywa konyagi nyingi anapopata sakata kama hizi. This is major league. Lakini mtu mwenyewe kama mlezi wake wa kisiasa ni Mbowe, ambaye sasa anatoa ushauri Bunge livunjwe, what do you expect?

By the way, mimi nina hard copies tu, mwenye electronic copies za hoja ya Zitto na Karamagi azi-post...na sisi tuzichambue kama walivyozichambua Wabunge, watu waache longolongo wakati hata hoja zenyewe hawajaziona.
 
Hawa wabunge wa ccm wana tofauti gani na wachekeshaji wa kipindi cha "ze comedy" wanamdebwedo?
 
Waungwana,

Haitoshi kulalamika hapa, mimi nafikiri tuchukue hatua zilizoko kwenye uwezo wetu.

Na mambo mengine mengi.
Tusilalamike tu hapa, wacha tuchukue hatua.

Wewe ndio umenena jambo la maana miongoni mwa wana-CHADEMA tangu thread hii ianze. Do something. Steve Biko once said: Ask nothing, blame nobody, do something!

(ingawa kuandika makala is really useless, Mbowe has been doing that, Mwanakijiji is doing that, and nobody notices these days)
 
Mugongo Mugongo,

Mimi kwa mara ya kwanza jana nimeangalia kila kitu.

Hakukuwa na kitu cha maana pale, kama ni kujieleza Zitto aliwazidi kabisa.

CCM kosa wanalofanya ni kuwanyamazisha wabunge wao na hivyo kumpa Zitto uwanja mkubwa wa kutamba. Wabunge wa CCM hawawezi kupinga jambo hata lile ambalo ni wazi kama la BOT. Matokeo yake wataonekana wazuzuzu tu.

Kuna haja ya kupata video zote za mwenendo wa bunge na kuzitumia hizo hizo mwaka 2010.

Hivi kule kwa Malima hakuna kijana anayetaka kupambana naye? Inabidi kuanza kufikiria njia za kuwaondoa wale wanaojiweka mbele kukwamisha demokrasi bungeni.
 
Malecela anapewa heshima sana ndani ya CCM katika kuendesha mambo kihuni.Angalia hata katika kuchangia hoja za kumfungia Zito,yeye kapangwa kuwa msemaji wa mwisho na kabla hajazungumza eti anaitwa Zito azungumze kama ana lolote la ziada(kuomba radhi) kabla HAKIMU mkuu Malecela hajapitisha hukumu.
Hii ni aibu sana. Hata hivyo kama ilivyotegemewa na wengi SHUJAA KIJANA WA KITANZANIA ZITO KABWE hakubembeleza wanafiki na wasaliti wa nchi hii bali aliwaambia wafanye vile watakavyo na kuwa fikra za kimapinduzi zitadumu.Wazee kama hao wasubiri aibu mwisho wa safari kisiasa.

Big Up CHAKAZA, ni wabunge wachache sana wenye moyo wa namna hiyo kama Zitto!!! Na safari ya aibu yao imewadia, yetu macho na masikio kwani kila zama na kitabu chake.
 
Mugongo Mugongo,

Mimi kwa mara ya kwanza jana nimeangalia kila kitu.

Hakukuwa na kitu cha maana pale, kama ni kujieleza Zitto aliwazidi kabisa.

Pole. Mimi sikuwa natazama kujieleza. Kushabikia watu kwa kujieleza ndio kumetufikisha hapa tulipo. Nilisoma hoja kumi na moja za Zitto, nikasoma majibu ya Karamagi kwa kipengele kimoja kimoja cha hoja za Zitto, nikaangalia na viambatanisho vya Karamagi. Nika-conclude kwamba Zitto alikuwa anatuhadaa na alikurupuka kutafuta umaarufu.

Sasa, kwenye kumfungia Ubunge, nilisema toka jana kwamba I thought it was a bad idea. The fact that ameonekana muongo ingetosha. Lakini, well, Bunge lina kanuni nyingi kuliko kanisa.
 
Wewe nani kakwambia Zito anasema uongo.... unatumia authority ipi ya kudai kuwa Zito ameongopa..... Mjadala unaendelea na kwa mujibu wa aliyeanzisha hoja TV zimeskip kuonyesha live

Asante binti wa Kiafrika,

Nachoona hapa ni fitina za kisiasa tu na ushabiki. Nimeshawahi kusema na ninasema tena na nitasema tena- CCM WANAJALI MASLAHI YA CHAMA CHAO KWANZA, MASLAHI YA TAIFA YANAKUJA MWISHO!

Kama kweli Zitto kaongopa kwa nini basi TV zetu zote zilikata mjadala huo pale ambapo Zitto alikuwa anataka kwenda kutetea hoja zake?

Pamoja na fitina hizo za CCM ni vema wakumbuke Tanzania ni yetu wote- hii itapelekea class struggle muda si mrefu baini ya watawala na watawaliwa.

Hongera Zitto! Usivunjike moyo, endelea na mapambano. Ni vema tukumbuke kuwa hoja hiyo imeibuliwa na Mbunge na si CHADEMA!
 
....(ingawa huyu bwana hana uso wa haya hata anapogundulika kasema uongo)....

(ingawa shida yake ni kujifanya mjuaji).

Mzee Mugong,

Hapo naona umeiruka hoja na kumvamia Zitto kibinafsi, kama ulivyofanya kwenye kuwa unadhani alitumia mpira!
 
Hoja ya mheshimiwa Zitto, nitaiweka hapa.

MAELEZO YANGU KUHUSU HOJA YA KUUNDWA KAMATI TEULE YA BUNGE KUCHUNGUZA MAPITIO YA MIKATABA YA MADINI NA MAZINGIRA YA KUSAINIWA KWA MKATABA (MDA) MPYA WA MADINI WA BUZWAGI KULIKOFANYWA NA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MHESHIMIWA NAZIR KARAMAGI (MB) HUKO UINGEREZA MWEZI FEBRUARI 2007.
{Kanuni 104(2)}

1. Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kunipatia fursa ya kuleta hoja hii hapa kwenye Bunge lako Tukufu kwa mujibu wa kanuni zetu za Bunge. Kuletwa kwa hoja hii, bila kujali maamuzi ya kuhusu hoja yenyewe, ni ishara tosha ya ukomavu wa demokrasia yetu ambayo inakuzwa na mijadala ya Bunge lako Tukufu. Nakupongeza kwa dhati kabisa kwa juhudi zako za kuliimarisha Bunge letu na kujenga muhimili imara wa ulinzi wa demokrasia ya vyama vingi nchini kwetu.

2. Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 16/7/2007 mara baada ya hoja ya Waziri wa Nishati na Madini kuamuliwa na Bunge lako Tukufu nilisimama mahala pangu na kutoa taarifa ya kukusudia kuleta hoja ya kuunda kamati teule ya Bunge. Nilisema kama ifuatavyo (kwa mujibu wa kumbukumbu sahihi za Mijadala ya Bunge), ninanukuu ‘…… naomba kutoa taarifa rasmi …… kwamba nakusudia kuleta hoja ya kuunda Kamati Teule kuchunguza mkataba mpya wa Madini ambao Waziri wa Nishati na Madini ameusaini bila kuzingatia maagizo ya Rais (wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) ya kupitia mikataba ya Madini aliyoyatoa mbele ya Bunge lako tukufu tarehe 30 Desemba, 2005. Mwisho wa kunukuu.

3. Mheshimiwa Spika, nimeshawasilisha hoja yangu hii kwa maandishi kwa Katibu wa Bunge na sasa nawasilisha rasmi katika kikao hiki cha Bunge kwa uamuzi. Nimezingatia kanuni 104 (2) katika kuwasilisha hoja yangu.

4. Mheshimiwa Spika, katika maelezo yangu niliyowasilisha Bungeni wakati wa mjadala wa Hotuba ya Waziri wa Nishati na Madini siku ya tarehe 16/7/2007 nilihitaji maelezo kutoka serikalini katika masuala makuu mawili yafuatayo:

i. Kusainiwa kwa Mkataba mpya wa wa Madini wa mgodi (mradi) wa Buzwagi kati ya serikali na Kampuni ya Barrick na sababu za mkataba huo kusainiwa nje ya nchi, London Uingereza na vilevile kwa nini mkataba huo umesainiwa wakati bado serikali inafanya durusu (review) ya mikataba kufuatana na maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Jakaya Mrisho Kikwete.
ii. Kuondolewa kwa kipengele katika sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 1973 kuhusiana na asilimia 15% ya ‘capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure’ bila ya kibali cha Bunge lako Tukufu.

5. Mheshimiwa Spika, wakati akijibu hoja zangu Waziri wa Nishati na Madini alijenga hoja zake kama ifuatavyo,

a. Kusainiwa kwa Mkataba wa Mgodi (Mradi) wa Buzwagi.

6. Mheshimiwa Spika, Wakati akijibu hoja yangu kuhusiana na suala la Mkataba mpya wa mgodi wa Buzwagi, Waziri wa Nishati na Madini amenukuliwa na kumbukumbu za majadiliano ya Bunge akisema kama ifuatavyo, nanukuu,

“Mheshimiwa Spika, katika tathmini ya Migodi, Mgodi wa Buzwagi ni marginal mine ambao uhai wake si wa muda mrefu. Bila ya kutumia fursa ya sasa ya bei ya Dhahabu uwekezaji wake usingeweza kuwa wa faida. Hata hivyo, Mkataba wa Buzwagi hauna mapungufu yaliyokuwamo kwenye mikataba ya zamani”. Mwisho wa kunukuu.

7. Mheshimiwa Spika, Kwanza kabisa napenda nilikumbushe Bunge lako Tukufu kuwa Rais alikwishapiga marufuku kusainiwa kwa mikataba mipya ya Madini mpaka hapo sheria za madini zitakarekebishwa. Akisoma hotuba ya Wizara ya Nishati na Madini mnamo tarehe 17/7/2006, Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Ibrahim Msabaha alilitaarifu Bunge kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amezuia kusainiwa kwa Mikataba mipya ya Madini. Nimeambatanisha Hansard ya siku hiyo kama uthibitisho wa kauli hiyo. Sasa inakuwaje Waziri wa Nishati na Madini kwenda kinyume na maagizo ya Rais? Tena nje ya Nchi?

7. Mheshimiwa Spika, Licha ya Marufuku hiyo ya Rais, mapitio ya mikataba ya madini ni mchakato ambao mwisho wake ni kuletwa kwa sheria ya madini hapa Bungeni na kuifanyia marekebisho ili kuiboresha na kuondoa mapungufu. Hivyo, mpaka hapo sheria itakaporekebishwa ndipo tutasema tumemaliza zoezi la kupitia mikataba ya madini na hivyo kusaini mikataba mipya na makampuni yote ya madini yaliyopo nchini na yatakayokuja kuwekeza.

8. Mheshimiwa Spika, suala ambalo linanipelekea kuomba kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza mkataba huu mpya ni kuhusu uharaka uliopelekea Waziri wa Nishati na Madini kusaini Mkataba huu. Sheria ya Madini bado haijarekebishwa, je Waziri anatumia vigezo gani kusema mkataba mpya wa Buzwagi aliousaini London hauna mapungufu?

9. Mheshimiwa Spika, Waziri wa Nishati na Madini aliliambia Bunge lako Tukufu kuwa Buzwagi ni marginal mine. Vile vile Waziri anasema kuwa Kampuni ya Barrick inamiliki migodi mitatu tu kupitia kampuni zake tanzu ambazo ni Bulyanhulu Gold Mine, North Mara Gold Mine na Pangea Minerals Limited Tulawaka. Kwa maelezo haya ya Waziri Karamagi, Buzwagi sio Mgodi.

10. Mheshimiwa Spika, hoja hii ya kuwa Buzwagi sio mgodi inashabihiana kabisa na hoja ya Kampuni ya Barrick kwamba Buzwagi ni Project. Taarifa ya kampuni hii ya ‘Barrick Gold Corporation-Global operations-Africa- Buzwagi, inaonesha kuwa Buzwagi ni mradi. Taarifa hii ninaiambatanisha katika hoja hii.

11. Mheshimiwa Spika, taarifa ya Barrick Annual Review 2006 inasema ifuatavyo katika ukurasa wa 23, ninanukuu. “A major milestone was reached in February 2007 when we signed a mineral Development Agreement (MDA) with the Tanzanian government. In 2007, we expect to complete a detailed construction design and receive EIA approval”.

12. Mheshimiwa Spika, suala ambalo vile vile linanisukuma kuomba Bunge lako Tukufu kuunda Kamati Teule ni kwamba, iwapo Buzwagi sio mgodi bali ni mradi, ni kwa nini tumesaini Mineral Development Agreement (MDA) mpya? Kwa kuwa Pangea Minerals Tulawaka ndio inaonekana kumiliki mradi huu, Je serikali imefanya marekebisho tu ya MDA na kampuni ya Barrick?. Naomba Kamati Teule ichunguze ni nini kilichosainiwa, marekebisho ya mkataba wa Tulawaka au MDA mpya ya Buzwagi?

13. Mheshimiwa Spika, Buzwagi inashika nafasi ya pili kwa uwekezaji wa Barrick katika migodi hapa nchini. Wakati kampuni hii inawekeza dola za kimarekani 400 milioni katika Buzwagi, imewekeza dola za kimarekani 600 katika Bulyanhulu. Je ni kwa vipi Buzwagi iwe marginal mine wakati uwekezaji wake unashinda uwekezaji wa Tulawaka na North Mara?

14. Mheshimiwa Spika, chini ya kifungu cha 47 cha Sheria ya Madini ya Mwaka 1998 (Na.5/98), pamoja na mambo mengine kinataka leseni yeyote isitolewe mpaka taarifa ya mazingira iwe imetolewa na kuruhusu mgodi kuendelea na kazi.

15. Mheshimiwa Spika, wakati Waziri wa Nishati na Madini ameweka saini Mkataba wa Buzwagi juma la mwisho la mwezi Februari 2007, Baraza la Mazingira nchini limetoa kibali (Environmental Impact Assessment- EIA approval) tarehe 11 mwezi Mei 2007. Ni kwa nini Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Nazir Karamagi alisaini MDA ya Buzwagi na Kampuni ya Barrick kabla Baraza la Mazingira la Taifa (NEMC) halijatoa ruhusa? Kulikuwa na haraka gani? Maslahi ya Taifa yalizingatiwa?

16. Mheshimiwa Spika, Sheria ya Madini, niliyoitaja hapo awali, imeunda Kamati ya Ushauri ya Madini (Mining advisory Committee). Kabla ya Waziri kusaini mkataba wowote ni lazima apate ushauri kutoka kamati hii. Kwa taratibu za Kiserikali, kama kamati ikimshauri Waziri na Waziri akakataa ushauri huo, inampasa Waziri atoe sababu ni kwa nini anakataa ushauri. Je Waziri alifuata ushauri wa kamati ya Ushauri ya Madini kuhusiana na wakati mwafaka wa kusaini Mkataba huu?

17. Mheshimiwa Spika, inawezekana kabisa MDA ya Buzwagi kusainiwa Uingereza sio tatizo. Kwa mfano, Mwaka 2006 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilisaini mikataba kadhaa. Ni mingapi kati ya Mikataba hii imesainiwa nje ya nchi? Nini madhara ya kisheria kwa Mkataba kusaniwa Uingereza? Je Mkataba umeandikwa “signed in London ……..” au “signed in Dar es Salaam …..? Kamati Teule ya Bunge ndio chombo pekee kitakachoweza kutoa majibu ya maswali haya.

18. Mheshimiwa Spika, suala hili ni suala la Kitaifa. Halina hata chembe ya itikadi za kivyama. Ninaamini wabunge wataamua kwa maslahi ya Taifa letu. Uundwaji wa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza mapitio ya mikataba ya madini na mazingira ya kusainiwa kwa mkataba mpya wa Buzwagi yatatoa msaada mkubwa kwa azma ya Rais wetu ndugu Jakaya Mrisho Kikwete ya kuona rasilimali za madini zinafaidisha nchi yetu.


b. Kuhusiana na asilimia 15% ya ‘capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure’

19. Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini amenukuliwa na kumbukumbu za majadiliano ya Bunge akisema, ninanukuu “..….kwa hiyo pamoja na kwamba ninamheshimu sana Mheshimiwa Kabwe Zitto na sote tunamheshimu ni msomaji mzuri, lakini wakati mwingine lazima kuangalia vitu gani unasoma. Ni kwamba kipengele hiki cha sheria kililetwa hapa Bungeni mwaka 2001 kwenye Bajeti kikabadilishwa…..” Mwisho wa kunukuu.

20. Mheshimiwa Spika, katika kuandaa hoja yangu hii, ilinibidi kupitia upya kumbukumbu za majadiliano ya Bunge ili kujiridhisha na maelezo ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini, maelezo ambayo mimi nililitaarifu Bunge lako tukufu tarehe 16/7/2007 kuwa sio sahihi.

21. Mheshimiwa Spika, Kumbukumbu hizo zinaonesha kwamba, sheria ya fedha ya mwaka 2001 (Finance Act. No.14 ya 2001) ilifanyiwa marekebisho kadhaa ikiwemo marekebisho ya sheria ya madini kifungu cha 87 ambapo kifungu kidogo cha (3) cha kifungu cha 87 kiliongezwa. Kifungu kidogo hicho kinasema, ninanukuu

‘(3) The provisions of subsections (1) and (2) shall not apply to any person who, immediately before the first day of July, 2001 was not the holder of a mineral right granted under this Act’

22. Mheshimiwa Spika, kifungu cha 87 cha Sheria ya Madini ya mwaka 1998 (No.5/1998) kinazungumzia Mrahaba wa Madini (Remission and deferment of royalties). Hivyo, kama sheria ya fedha ya mwaka 2001 haikubadili kipenge hiki, Mheshimiwa Waziri ametoa wapi jibu aliloliambia Bunge?

23. Mheshimiwa Spika, suala hili linahusu haki, kinga na madaraka ya Bunge kwa mujibu wa sheria namba 3 ya 1988.

24. Mheshimiwa Spika, hata hivyo katika hotuba ya Waziri wa Fedha Mheshimiwa Basil Mramba, akiwasilisha Hotuba ya Bajeti mwaka 2002, tarehe 13 mwezi Juni, alizungumzia kipengele hiki. Ninaomba kunukuu sehemu ya hotuba ya Waziri wa Fedha Mhe. Basili Mramba

“Amendment to the Income Tax structure, (44) Mr. Speaker, in this area I propose to take the following measures:
(v) I propose to reinstate the additional 15 percent capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure as set out in the Mining Act. No. 5 of 1998”….. Mwisho wa kunukuu.

25. Mheshimiwa Spika, nilipopitia sheria ya fedha ya mwaka 2002 nimekuta sehemu ya 8 inazungumzia mabadiliko katika kodi ya mapato ya 1973. Na hata katika ukurasa wa kwanza wa sheria hii (Arrangement of Contents), sheria ya Madini haitajwi.

26. Mheshimiwa Spika, maelezo haya ya Waziri wa Fedha ya mwaka 2002 yanaonesha dhahiri utata wa kipengele hiki. Ni kwa vipi kifungu cha sheria ambacho hakijafutwa kirejeshwe?

27. Mheshimiwa Spika, tuchukulie kuwa maneno ya Waziri ni ya kweli. Je kwa nini makampuni ya Madini ambayo yameingia Mkataba na serikali kuanzia Julai mosi 2001 hayajaanza kulipa kodi ya mapato?

28. Mheshimiwa Spika, utata huu ambao umegubika sekta hii ya madini unaweza kufafanuliwa na Bunge lako tukufu kupitia Kamati Teule. Kamati teule ya Bunge ichunguze upitiaji wa mikataba hii na kuona kama kuna vitendo vyovyote vya uvunjifu wa sheria za nchi na kupotea kwa mapato ya Serikali na ufisadi.

Mheshimiwa Spika, ninaomba kutoa hoja.



…………………………….
KABWE ZUBERI ZITTO (MB)
JIMBO LA KIGOMA KASKAZINI



Nampongeza sana huyu kijana kwa ujasiri wa hali ya juu.
Nitaweka ya kagamagi baadae ili tuweze kuchambua moja baada ya nyingine ,tumalize kwanza hii ya zitto the great to me.
 
Hivi jamani? kuna tofauti ipi kati ya wabunge wa CCM na mawaziri ? mbona kwenye hili la Zitto wabunga wa ccm
walijimuvuzisha kuwa mawaziri ,hee!!
walijibu hoja badala ya kuchambua hoja, hawakuonyesha kuwa wawakilishi wa waliowatuma bungeni
 
kazi kwenu ,nadhani ingekuwa busara tuchambue kwanza hii then baadae ndio ntaweka ya karamagi nayo tuitolee uchambuzi wa kina .

Zitto, huu ni wakati wa kufanya kazi zako kaqma naibu katibu mkuu wa CHADEMA hivyo wamekupa fursa za kujenga chama chako zaidi ya wakati mwingine wowote ule
 
Wazee huko bungeni bila kujali vyama venu au nani mshindi na nani mshindwa pokeeni ujumbe wa Huyu mzee aliyewahi kuishi pale white house alitamka haya ktk maisha yake,

"It is to be regretted that the rich and powerful too often bend the acts of government to their selfish purposes." - Jackson

Na mwingine aliondoka pale na maneno haya
"I did not have sexual relations with that woman." - Clinton
 
Back
Top Bottom