Binafsi nilijua ngoma itakuwa nzito kwa sababu kuu moja:
Wakati Ndugu Zitto anatoa hoja/swali kabla ya kuwasilisha hoja hii iliripotiwa kuwa huyo waziri wakati anasaini huo mkataba huko Uingereza, alikuwa safarini na mkuu wa kaya. Kwa hali hiyo, niliamini kuwa bosi mwenyewe alitoa baraka zake. Isingekuwa rahisi waziri asaini, akiwa ziarani na rais, pasi na rais kujua au kubariki, ilhali ni yeye aliyesema mikataba mipya sasa basi mpaka kieleweke!
Hata hivyo, kwa upande mwingine, ikiwa ni kweli mkataba huu una masharti mazuri KIDOGO kuliko ile mingine ya awali, basi ni afadhali.
Taarifa nilizonazo ni kwamba hawa jamaa walitaka kusainisha mkataba huu mwishoni mwishoni mwa utawala wa MJASIRIAMALI, somehow, ikashindikana. Alipokuja Muungwana wakataka kusaini chapchap, lakini jamaa somehow akachelewesha kubariki zoezi hilo. Binafsi nilipata habari hizi za mzee "kuwakwepa" hao wawekezaji kuhusu mradi huo tangu mwaka jana kwani walitaka akazindue mradi huo tangu mwaka jana. Najua vyombo vya habari (magazeti ya BONGO) vimekuwa vikiandika siku nyingi kwa kurudia rudia habari ya mradi huo (hata pale kulipokuwa hamna kitu kipya) kwa nia ya kuweka msukumo fulani kwa serikali (mtazamo wangu).
Kuchelewa kusainiwa kulikuwa kukinipa faraja kuwa serikali kwa ujumla na Muungwana in particular, wameamua kusimamia kidete mikataba safi katika sekta hiyo. Sasa hili la kusaini katika mazingira ambayo kidogo (kama si sana!) yameleta maswali kumenichanganya. NDIYO MAANA NAAMINI KUWA MZEE ALIBARIKI ZOEZI HILO!