Na mimi naona ni comedy tu. Na tena mwakani tutaanza kuwapa mamilioni ya Constituency Development Fund! Bunge livunjwe?
MugongoMungongo, kama kweli yanatoka moyoni mwako, naona umenena maana hawa wabunge wengi ambao wanatoka CCM wameshindwa kutetea wananachi wao na badala yake wanaangalia matumbo yao... Wanaogopa yasiwakute ya kina Tom Nyimbo, Njelu Kasaka, Simpasa, Derefa na kadhalika ambao walikua wakiishambulia serikali ya chama chao kwa yale waliyoyaamini... Hebu angalia ni aibu iliyoje kwa watu wote waliochangia kuchangia wakielemea kusema tu, "Waziri Karamagi kajibu vizuri sana" bila kuwa na angalau maneno ya kuonyesha wanafikiri kwa vichwa vyao... Hivi mbona wakati wa Bunge la chama kimoja mambo yalikua magumu kwa mawaziri? Hivi hawa wabunge wanamuwakilisha nani? Hivi Karamagi anawasilisha maslahi ya nani? Lakini naamini kwa hili kuna mambo mazito kuliko Zito alivyoyawasilisha na ndio maana VITA DHIDI YA ZITTO ilikua kubwa kupita kiasi na CCM ilijipanga hadi kumfanya Spika Sitta, kumeza WEMBE bila kupenda,, hata Mbunge Stela Manyanya (CCM), yeye alitaka Zitto asiadhibiwe, hata Adam Malima (CCM) pamoja na kumshambulia ZItto alijiuma uma katika kujenga hoja kutaka kuonyesha naye anamheshimu Zitto, hata Mbunge MAnju Msambya (CCM), alionekana kumsaidia Zitto bila kujijua aliposema Zitto angepewa mkataba auone ili ajiridhishe, lakini akazungumzia kwamba eti ingekua hoja kama mkataba ule ungesainiwa na NAibu Waziri, Ngeleja lakini Karamagi ilikua ni sawa. Kwa ujumla hakuna mbunge wa CCM aliyechangia kwa dhati ya moyo wake na ndio maana hata Chacha Wangwe, alisema MUNGU ANAWAONA WANAVYOZISALITI NAFSI ZAO.. Hata hivyo Chacha aliifanya hoja iwe nzito kwa Zitto alipotaka mikataba yote ichunguzwe ikiwamo ile ya miaka ya 80, kipindi ambacho aliyekua waziri kwa sasa ana madaraka ya juu.. hapo kuna waliomuona kuwa alimlenga JK alipokuwa Waziri wa Nishati na Madini ambako alitoa leseni kadhaa za madini katika migodi mikubwa... Hapo alizidisha maadui ndani ya CCM na kuwapa nguvu Karamagi na kundi lake dogo linaloongozwa na UTATU MTAKATIFU... (EL, Karamagi, Rostam).
Hoja ya MSINGI ilikua ni kwanini Waziri alisaini mkataba wa Buzwagi London, na kwamba Waziri alidanganya Bunge kwa kusema kwamba alikwenda huko kwa kuwa alikua anatoka sekta binafsi na kuonyesha kwamba ilikua ni suala la haraka na ghafla wakati mchakato wa mkataba huo ulianza mapema na Waziri alifahamu kuwa atasafiri kwenda nje ya nchi na kwamba ni lazima angerudi.. lakini pia Waziri alisema mgodi wa Buzwagi ni kamgodi kadogo, leo anasema ni mgodi utakoliingizia Taifa fedha nyingi na kwamba utatoa ajira.. Sasa hapo aliyedanganya Bunge ni nani?
Lakini mapema habari za UHAKIKA zilisema kwamba Baraza la Mawaziri na Rais hawakua na taarifa, kabla ya Zitto kuzungumzia mkataba huo bungeni na waziri kukiri...Lakini leo tunaona watu wanakurupuka na kutetea kwa misingi ya U-CCM...
JAMANI HII NI HATARI SANA, TUNAKOELEKEA NI KUBAYA KUPITA KIASI.. SIJAPATA USINGIZI NA SAA HIZI NAANDIKA NI SAA 10 ALFAJIRI ZA TANZANIA (04.05) NAONA UCHUNGU SIASA ZINAVYOTUMIKA KUTUMALIZA. SIASA ZIMEJAA MATAPELI NA WANAFIKI WA AJABU.. NASEMA NINA USHAHIDI NITAUTOA SIKU SI NYINGI JINSI MADIWANI NA WABUNGE AMBAO WANA HISTORIA YA UHALIFU.. WAKO AMBAO WAMEKWISHAKAMATWA NA KULALA GEREZANI MARA NYINGI, BAADHI HUMU NCHINI NA NJE YA NCHI, BAADHI NI WEZI WANAOJULIKANA WAZIWAZI, LEO NI VIONGOZI NDANI YA CCM NA WANATETEA WAOVU WENZAO. HAO NI WALE NINAOWAJUA KWA USHAHIDI WA WAZI, JE, NI WANGAPI NISIOKUA NA USHAHIDI NAO?