Ndugu Mtanzania tufikie mahali tuangalie Tanzania na si vyama vyetu.Naona michango inavyo changanya nia nk.Umewavaa sana Chadema CCM
Chifu,
Ungesaidia kama ungeeleza ni michango gani inachanganya ili nifafanue na pia kwanini unadhani ninawavaa CHADEMA? Kwanini husemi ninawavaa CCM?
Kwa uzoefu wangu hapa mambo yanayoongelewa kwasehemu kubwa yanahusu CHADEMA na CCM, kuna mengine pia lakini sehemu kubwa ni juu ya hivyo vyama viwili.
Siko hapa kuwafundisha CHADEMA wafanye nini, kwanza uwezo huo sina na CHADEMA wana wetu wengi wenye uwezo kuliko mimi juu ya siasa. Ninachofanya ni kutoa maoni yangu juu ya ninavyoona mimi
kama mwana JF na Mtanzania.
Binafsi sioni kama matatizo ni CCM au CHADEMA au TLP. Ninaamini matatizo ni watu, ni viongozi wa hivi vyama. Aidha ninaamini
viongozi wengi wa CCM ya leo wanatuwakilisha sisi Watanzania tulio wengi, yaani matendo yao ni reflection ya mawazo, fikra na matendo ya Watanzania walio wengi wa leo.
Ni rahisi kuiondoa CCM madarakani kuliko kuondoa hii culture ya ubinafsi, uwizi,uroho, uvivu na uongozi wa mabavu ambayo imetukumba watanzania.
Sasa kama hatusemi haya mambo leo kwasababu CHADEMA ni chama chetu, au hawako madarakani, basi tujiandae kupata akina Mwai Kibaki wengine, akina Muluzi na kale kajamaa ka Zambia nk.
Sasa kama kuyasema hayo ni kuwavaa CHADEMA? basi ni jambo zuri kuwavaa kama tunavyowavaa CCM. Maneno ya Mzee ES yana maana sana hasa "kumkoma Nyani giladi"
Wengine tunaamini hapa hatuogopi mtu wala chama, tutaendelea kuwavaa tu. CCM wakikosea tutasema, CHADEMA wakikosea tutasema lakini pia CCM wakifanya mema tutasema na hivyo hivyo CHADEMA wakifanya mema tutasema.