The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

Na kwa sheria ya PCB ina maana mwisho wa mjadala kwa sasa. Kazi kwelikweli....

Tanzanianjema
 
Michezo ya kuigiza inaendelea....kwa kasi mpya, ari mpya na nguvu mpya. Tutafika tu.
 
Mjadala wa kitaifa wa madini watakiwa

2007-08-24 09:17:58
Na Mwandishi Wetu

Shirika lisilo la kiserikali la Mtandao wa Madeni na Maendeleo (TCDD), limetaka Mjadala juu ya mustakabali wa uwekezaji katika sekta ya madini ufanyike kwa nchi nzima na uwashirikishe Watanzania wote.

Katika tamko lililotolewa baada ya Mkutano Mkuu uliofanyika chini ya Mwenyekiti wake, Mchungaji Christopher Mbuga na Mratibu, Bw. Chamba Kajege, shirika hilo limependekeza kuwepo kwa uwazi na ushirikishwaji wa umma katika masuala ya mikataba ya madini.

Shirika hilo lilishauri kuwa kwa vile Rais katika hotuba yake ya Desemba 2005 alipozindua Bunge alitangaza kuwa mikataba ya madini itapitiwa upya, ni vyema taarifa ya kamati iliyoteuliwa kuchunguza mikataba ikawekwa hadharani ili wananchi wajue kilichoibuliwa katika kupitia nyaraka hizo.

`Agizo la Rais Jakaya Kikwete juu ya kupitia upya mikataba ya madini litekelezwe na taarifa ya kamati iliyoteuliwa kuidurusu itoe ilichoona kwa umma ili wananchi wajue nini kimejiri na kujadili,` alisema Mchungaji Mbuga.

Tamko hilo lilisema kwamba kazi ya kurekebisha sheria ya madini kutokana na mapungufu yaliyobainishwa na kamati ya Rais iwashirikishe wadau wote.

Kwa upande wa mradi wa madini wa Buzwagi mkoani Mwanza uliozua gumzo na mashaka, TCDD ilimtaka Rais kuunda kamati huru kwa ajili ya kuchunguza suala zima la mradi huo.

`Ili kurahisisha uchunguzi, kamati huru itakapoundwa na Rais, basi Waziri wa Nishati na Madini , Bw. Nazir Karamagi ajiuzulu au asimame kazi mpaka uchunguzi huru utakapokamilika.

TCDD imesema kuwa mkutano wao mkuu ulitafakari na kugundua kwamba maendeleo ya demokrasia nchini, hususan mgawanyo wa madaraka baina ya mihimili ya uongozi, watawala, Bunge na Mahakama bado umezorota.

* SOURCE: Nipashe

Jamani mimi nadhani tukipata wa akina zito 10 wajitoe sadaka kwa mambo makubwa kumi ilikuibua mijadala ya kitaifa tunaweza tukapiga hatua na kuondoa ukiritimba wa watu wachache kufanya maamuzi makubwa kwa faida binafsi bila kushirikisha wananchi ambao wisho wa siku ndio wanaotaabika kutokana na maamuzi haya. MEMBERS MNASEMAJE?
 
kama huitumii elimu yako inachujuka na kukosa maana. Haya ndiyo ambayo yanamkuta dr shoo kwani elimu yake haifai hata kwa wauza vitumbua, anajikomba ili apate madaraka, sasa wakiongezeka kina shoo kumi ndani ya ccm kazi tunayo.
Dr shoo ushauri wa bure tumia elimu yako kuelimisha jamii bila woga, kwani umri ulionao hunaulichobakiza. Umaskini wa akili usiuonyeshe adharani. Heri ukae kimya kuliko kujiumbua.
Angalia wana zuoni waliotukuka na makala zao: kama shivji, baregu, mvungi, mabere. hawa na wengine wengi sio kwamba hawana maswahiba ndani ya system bali wameona system haibebeki, wewe utaweza kuibeba? Ungelikuwa na akili ungejua umaskini wako ambao unapelekea kujikomba kwa vihiyo wa ccm na kudhalilisha elimu yako ni maamuzi mabovu ya viongozi unaowatetea. baada ya kununuliwa na rostoma rai imekosa dira.

BILA JASHO LA DAMU, MAENDELEO TANZANIA NI NDOTO.
 


Mzee Masanja, kwa sababu siwezi kumjibu "Dr" Shoo, basi nikuuunge mkono tu, maana huyu doktar, ndio kina Dokta Mzindakaya hawa!

Keep it up mkuu!
 
Huyu Hosea mbona hakusema wanashughulikia madai ya Dr Slaa? hii taasisi naona inataka kufanya watu hawana akili, basi si bora wangeingia kimya kimya wakaja kutoa hayo majibu baadaye.
 
NAOMBA UTABIRI HUU UTUNZWE VIZURI MAANA KAMA PCB WAKICHUNGUZA MAJIBU YATAKUWA NI HAYO AU MENGINE YA KUSAFISHA UCHAFU WA WAHUSIKA. PCB ni ka laundy/au bafu la kuoshea rushwa. haiwezi kudhubutu. tusubiri unabii wa mkjj utimie.
 
Mwanakijiji,
Hivi ni wapi Zitto alisema kuna rushwa?

Nakwambia watazua kila aina ya uongo kujaribu kupindisha ukweli...labda wao wenyewe wameisha gundua kuwa kuna kiharufu cha rushwa! unajua tena guilty conscious!
 
Hosea hana credibility tena na watu wenye akili zao timamu hivyo ameamua na yeye kama chichiemu kujikita kwa wajinga ambao ndiyo wengi. unapoamua kufanya kitu cha kipumbavu hadharani moja kwa moja inaonesha kuwa umeshafanya tathmini na kugundua kuwa wengi wa watakao pata hiyo taarifa ni wajinga
 
Nadhani Dr.Shoo ametoa maelezo yake akiwa chooni uchi wa nyama, yaani kesha vua hizo digree zake zote.
Nimesoma maelezo yake hayakwenda shule kabisa, anaongea sawa na mtu wa mtaani ambaye anatumia dhana na hadithi za simulizi. Ebu amtazame prof Shivji alivyovunja vitu hapo kwa kunukuu vipande na sheria zake.. Hii ndio elimu sio kuja na habari ambazo hata mimi hapa Mkandara nilosema chini ya mwembe siwezi andika.
Mawazo yake na ya yule Mudhihir hayana tofauti kabisa kwani wanachoona wao ni Mungu Karamagi ametukanwa!.. huyu ni binadamu na kweli amefanya makosa mengi makubwa ambayo sasa yanadhihirika wazi zaidi ya hoja za Zitto bungeni. Ushahidi gani unaotakiwa ikiwa maiti kunayo na Kisu kipo mezani hii sii kazi yenu wataalam wengine kuchunguza!.. maneno mengi kortini sio ushahidi hata kidogo na hakuna hoja inayoweza tolewa kwa kubembelezana.
Rais hakujulishwa, Wabunge hawakujulishwa, Wananchi wote Tanzania hatukufahamu, mbunge wa Kahama na wakazi wa Buzwagi walikuwa kizani...kuna ushahidi gani zaidi hali mkataba ulisainiwa hotelini tena akiondoka na mihuli (seal) ya nchi yetu mfukoni.

Ushahidi gani tena mnauhitaji wajinga nyie... huu udaktari mlopata ni ule wa visiwa vya Virgin Island ama?
 
kukurupuka
kukurukukuru
kupurukuta
kupukutika
kukurukakara

Kutumia maneno mahali pasipo takiwa kunaleta unyafuzi wa lugha
 

TOOO BIG, AINT GONNA READ ALL THIS DAWG
 

Source: HabariLEO Agosti 25, 2007
 
Gideon Shoo ni mwandishi wa siku nyingi sana. Nadhani safari hii aliombwa na "RAI" aandike "riwaya ya kufikirika inayoonyesha kuwa Zitto alikosea."
 
JApo Scotland Yard walikuja na kufanya uchunguzi juu ya moto wa Shule ya ShauriTanga.
MH Malecela alitoa taarifa ya utafiti kwa niaba ya Scotland Yard na kusema ulikuwa ni Mshumaa.

Jamani Mshumaa???

Hizi nyumba za Marekani na mshumaa sawa! Lakini zile nyumba zetu Bongo hapana mshumaa utaunguzaje ghafla.
Malecela alipika majibu ya SY.

Kwa hiyo hata nani afanye uchunguzi CCM watayakorofisha hayo majibu au watakaa na Taarifa mpka ujuo wa Yesu.
 
Hili bomu jingine kama kweli lisha sainiwa basi tumewaibua kabla mapemaaa!
Maneno ama maombi ya Adam Malima kwa waziri Mh. Karamagi yamedhihirisha wazi kuwa tunaibiwa.
Adam Malima kwa kujisifu kamuomba waziri Karamagi kutafuta mwekeshaji ktk jimbo lake kuwekesha bila kujua kama Mwekeshaji tayari kisha patikana na mgawanyo umesha fanyika. Hivyo dhahiri hata yeye mwenyewe mbunge wa Nkuranga alikuwa kizani wakati akitoa hoja yake Bungeni.
Kwa kumtaarifu tu - Karamagi sio mtaalam, hivyo asitumie wataalam kusaini mikataba kuwa ndio somo hapa. Uganda kwa taarifa yake walipeleka vijana wao nje kusomea Utaalam wa mikataba ktk sectors za energy na mineral (wizara) na walisimamisha kabisa mikataba yote hadi hapo vijana wao watakapo kuwa tayari. Na ktk hiyo list ya wataalam M 7 wala Bibie ( Ms.) Syda Bbumba sii mmmoja wao. Wamevumbua tayari mafuta na wameisha anza kujikusanya kesho Uganda itakuwa moja ya nchi zinazotoa mafuta! vijana wameisha anza kazi zao, M7 anacheka tu.
Ndugu Adam inabidi afahamu kuwa Waziri sio Mtaalam wala mtendakazi hatupo jeshini hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…