The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

Na kwa sheria ya PCB ina maana mwisho wa mjadala kwa sasa. Kazi kwelikweli....

Tanzanianjema
 
Michezo ya kuigiza inaendelea....kwa kasi mpya, ari mpya na nguvu mpya. Tutafika tu.
 
Mjadala wa kitaifa wa madini watakiwa

2007-08-24 09:17:58
Na Mwandishi Wetu

Shirika lisilo la kiserikali la Mtandao wa Madeni na Maendeleo (TCDD), limetaka Mjadala juu ya mustakabali wa uwekezaji katika sekta ya madini ufanyike kwa nchi nzima na uwashirikishe Watanzania wote.

Katika tamko lililotolewa baada ya Mkutano Mkuu uliofanyika chini ya Mwenyekiti wake, Mchungaji Christopher Mbuga na Mratibu, Bw. Chamba Kajege, shirika hilo limependekeza kuwepo kwa uwazi na ushirikishwaji wa umma katika masuala ya mikataba ya madini.

Shirika hilo lilishauri kuwa kwa vile Rais katika hotuba yake ya Desemba 2005 alipozindua Bunge alitangaza kuwa mikataba ya madini itapitiwa upya, ni vyema taarifa ya kamati iliyoteuliwa kuchunguza mikataba ikawekwa hadharani ili wananchi wajue kilichoibuliwa katika kupitia nyaraka hizo.

`Agizo la Rais Jakaya Kikwete juu ya kupitia upya mikataba ya madini litekelezwe na taarifa ya kamati iliyoteuliwa kuidurusu itoe ilichoona kwa umma ili wananchi wajue nini kimejiri na kujadili,` alisema Mchungaji Mbuga.

Tamko hilo lilisema kwamba kazi ya kurekebisha sheria ya madini kutokana na mapungufu yaliyobainishwa na kamati ya Rais iwashirikishe wadau wote.

Kwa upande wa mradi wa madini wa Buzwagi mkoani Mwanza uliozua gumzo na mashaka, TCDD ilimtaka Rais kuunda kamati huru kwa ajili ya kuchunguza suala zima la mradi huo.

`Ili kurahisisha uchunguzi, kamati huru itakapoundwa na Rais, basi Waziri wa Nishati na Madini , Bw. Nazir Karamagi ajiuzulu au asimame kazi mpaka uchunguzi huru utakapokamilika.

TCDD imesema kuwa mkutano wao mkuu ulitafakari na kugundua kwamba maendeleo ya demokrasia nchini, hususan mgawanyo wa madaraka baina ya mihimili ya uongozi, watawala, Bunge na Mahakama bado umezorota.

* SOURCE: Nipashe

Jamani mimi nadhani tukipata wa akina zito 10 wajitoe sadaka kwa mambo makubwa kumi ilikuibua mijadala ya kitaifa tunaweza tukapiga hatua na kuondoa ukiritimba wa watu wachache kufanya maamuzi makubwa kwa faida binafsi bila kushirikisha wananchi ambao wisho wa siku ndio wanaotaabika kutokana na maamuzi haya. MEMBERS MNASEMAJE?
 
kama huitumii elimu yako inachujuka na kukosa maana. Haya ndiyo ambayo yanamkuta dr shoo kwani elimu yake haifai hata kwa wauza vitumbua, anajikomba ili apate madaraka, sasa wakiongezeka kina shoo kumi ndani ya ccm kazi tunayo.
Dr shoo ushauri wa bure tumia elimu yako kuelimisha jamii bila woga, kwani umri ulionao hunaulichobakiza. Umaskini wa akili usiuonyeshe adharani. Heri ukae kimya kuliko kujiumbua.
Angalia wana zuoni waliotukuka na makala zao: kama shivji, baregu, mvungi, mabere. hawa na wengine wengi sio kwamba hawana maswahiba ndani ya system bali wameona system haibebeki, wewe utaweza kuibeba? Ungelikuwa na akili ungejua umaskini wako ambao unapelekea kujikomba kwa vihiyo wa ccm na kudhalilisha elimu yako ni maamuzi mabovu ya viongozi unaowatetea. baada ya kununuliwa na rostoma rai imekosa dira.

BILA JASHO LA DAMU, MAENDELEO TANZANIA NI NDOTO.
 
Hapana, mi nadhani humu JF inabidi tuargue beyond petty politics za kuganga njaa! Jamani, mimi simhukumu Zitto wala KARAMAGI, ILA NAOMBA KUULIZA, JEE, BUNGE LILITUMIA VIGEZO GANI KUAMUA KWAMBA ZITTO NI MUONGO NA KARAMAGI YUKO SAHIHI? Kwanini Zitto aonekane muongo wakati hajahukumiwa? si ndilo bunge hilo hilo linalotunga sheria kwamba kila mtu ana haki ya kusikilizwa kabla ya kuhukumiwa? Mbona Bunge lilitoa maamuzi kwa kuangalia upande mumoja? wa waziri? maana hakuna impartial kamati iliyoundwa kubaini ukweli. Kwa hiyo kama waungwana wengine wanavyosema, Dr, Shoo ni wale wale tuliowazoea wasomi walio tayari ku-compromise taaluma na ujuzi wao kwa ajili ya kulinda maslahi yao ya mda mfupi.


Mzee Masanja, kwa sababu siwezi kumjibu "Dr" Shoo, basi nikuuunge mkono tu, maana huyu doktar, ndio kina Dokta Mzindakaya hawa!

Keep it up mkuu!
 
Huyu Hosea mbona hakusema wanashughulikia madai ya Dr Slaa? hii taasisi naona inataka kufanya watu hawana akili, basi si bora wangeingia kimya kimya wakaja kutoa hayo majibu baadaye.
 
mbona hata hawahitaji kujitosa. Uchunguzi wao utaonesha hivi:

a. baadhi ya taratibu za kuingiwa mkataba huu hazikuwa wazi sana na hivyo kuacha taswira ya rushwa au ufisadi
b. Kuna baadhi ya mambo ambayo yangeweza kufanywa tofauti na hilo lingechangia kuweka uwazi na ukweli mbele ya wananchi
c. Taratibu ambazo zipo zilifuatwa na Waziri, Mwanasheria mkuu n.k wote walifuata taratibu hizo.

Hivyo basi, PCB wamefikia hitimisho kuwa rushwa haikuhusika.

My take:

Hivi ni wapi Zitto alisema kuna rushwa?
NAOMBA UTABIRI HUU UTUNZWE VIZURI MAANA KAMA PCB WAKICHUNGUZA MAJIBU YATAKUWA NI HAYO AU MENGINE YA KUSAFISHA UCHAFU WA WAHUSIKA. PCB ni ka laundy/au bafu la kuoshea rushwa. haiwezi kudhubutu. tusubiri unabii wa mkjj utimie.
 
Mwanakijiji,
Hivi ni wapi Zitto alisema kuna rushwa?

Nakwambia watazua kila aina ya uongo kujaribu kupindisha ukweli...labda wao wenyewe wameisha gundua kuwa kuna kiharufu cha rushwa! unajua tena guilty conscious!
 
Hosea hana credibility tena na watu wenye akili zao timamu hivyo ameamua na yeye kama chichiemu kujikita kwa wajinga ambao ndiyo wengi. unapoamua kufanya kitu cha kipumbavu hadharani moja kwa moja inaonesha kuwa umeshafanya tathmini na kugundua kuwa wengi wa watakao pata hiyo taarifa ni wajinga
 
Nadhani Dr.Shoo ametoa maelezo yake akiwa chooni uchi wa nyama, yaani kesha vua hizo digree zake zote.
Nimesoma maelezo yake hayakwenda shule kabisa, anaongea sawa na mtu wa mtaani ambaye anatumia dhana na hadithi za simulizi. Ebu amtazame prof Shivji alivyovunja vitu hapo kwa kunukuu vipande na sheria zake.. Hii ndio elimu sio kuja na habari ambazo hata mimi hapa Mkandara nilosema chini ya mwembe siwezi andika.
Mawazo yake na ya yule Mudhihir hayana tofauti kabisa kwani wanachoona wao ni Mungu Karamagi ametukanwa!.. huyu ni binadamu na kweli amefanya makosa mengi makubwa ambayo sasa yanadhihirika wazi zaidi ya hoja za Zitto bungeni. Ushahidi gani unaotakiwa ikiwa maiti kunayo na Kisu kipo mezani hii sii kazi yenu wataalam wengine kuchunguza!.. maneno mengi kortini sio ushahidi hata kidogo na hakuna hoja inayoweza tolewa kwa kubembelezana.
Rais hakujulishwa, Wabunge hawakujulishwa, Wananchi wote Tanzania hatukufahamu, mbunge wa Kahama na wakazi wa Buzwagi walikuwa kizani...kuna ushahidi gani zaidi hali mkataba ulisainiwa hotelini tena akiondoka na mihuli (seal) ya nchi yetu mfukoni.

Ushahidi gani tena mnauhitaji wajinga nyie... huu udaktari mlopata ni ule wa visiwa vya Virgin Island ama?
 
kukurupuka
kukurukukuru
kupurukuta
kupukutika
kukurukakara

Kutumia maneno mahali pasipo takiwa kunaleta unyafuzi wa lugha
 
(Makala hii ilichapwa na RAI jana alhamisi)
Zitto hakuwatendea wananchi haki
na dkt gideon shoo
”Naomba kutoa
taarifa rasmi kwamba nakusudia kuleta hoja ya kuunda kamati teule kuchunguza
mkataba mpya wa madini ambao Waziri wa Nishati na Madini ameusaini
bila kuzingatia maagizo ya Rais (wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) ya
kupitia mikataba ya madini aliyoyatoa mbele ya Bunge lako tukufu tarehe
30 Disemba, 2005.Õ Ð Zitto Zubeir Kabwe- Mbunge wa Kigoma Kaskazini,
Julai 16, 2007- Dodoma.
Bila ya kujiuma uma wala kujikwaa kijana huyo
alihakikisha kwamba takriban mwezi mmoja baadaye anaibuka tena katika
hadhara hiyo hiyo ya Bunge huko Dodoma na hoja yake kwapani.Kazi kubwa ambayo
ingemsibu ilikuwa ni kuthibitisha kwamba Waziri muhusika alikiuka
utaratibu na kufanya kinyume na maagizo ya mkuu wake wa kazi au tunaweza
hata kusema maagizo ya aliyempendekeza kuajiriwa na kuwa na wadhifa huo
mkubwa.Ni wazi kwamba anapotokea mwanasiasa, tena mwenye shahada ya chuo
kikuu, kuamua kuleta hoja mbele ya wenzake ambao bila shaka nao si
wazungu wa reli, bila shaka hiyo itakuwa hoja iliyokamilika.Lakini katika
hili la Zitto hoja iliyokuwa ikisubiriwa si ile ambayo ilikuja kuibuka
katika kipindi cha kuelekea mwisho wa kikao cha 9 cha Bunge la
Muungano. Kwa lugha ya mitaani ni kwamba kibao kiligeuzwa na mtuhumu akageuka
mtuhumiwa.Katika kuisukuma hoja tena nzito kama ya Zitto iliyokuwa
ikilenga kuonyesha udhaifu wa baadhi ya watendaji katika Serikali utafiti wa
kina ni muhimu sana. Lakini hata kabla ya utafiti wa kina ni muhimu
kujiridhisha kwamba hoja za msingi unazoziibua ni za msingi kweli kwa
maana ya kuongeza thamani katika kile unachokilenga. Bila shaka Zitto yote
hayo alikuwa amejiandaa nayo na naamini isingelimjia kichwani hata kwa
mbali sana kujaribu kuibua hoja ambayo haina mantiki na wala haina
ushahidi wa kutosha.Zitto alikuwa na ajenda ambayo bila shaka inafanana na
kazi mahsusi ambayo wametumwa kwenda kuifanya Dodoma. Ajenda ya kuibua
mambo ambayo yatasaidia katika kuongeza thamani katika maisha ya
Mtanzania.Kazi ya mbunge anayetambua wajibu wake ni kuingia katika uchambuzi
na uhojaji wa masuala ya msingi na bila shaka Zitto anastahili
kuingizwa katika kundi la wale ambao wanahangaika kutafuta kila chembe ya
nafasi ili kuwathibitishia waliowapigia kura kwamba si bure wakatumwa
kwenda kwenye jumba hilo lenye hadhi ya kipekee. Wana nia na uwezo wa
kuhakikisha kwamba mabadiliko ya kweli yanatokea kwa kumpatia Mtanzania
maisha bora zaidi.Mbunge anapokuwa bungeni anao wajibu kwa wapiga kura wake.
Kwa sababu kama wapiga kura wakigundua kwamba mbunge wao hawatetei
huko Dodoma, sasa ni kwa nini wamchague tena kwenye uchaguzi
unaofuata?Lakini jambo moja ni wazi katika hili la Zitto na wabunge wenzake nalo ni
lile la kutafuta mchawi. Ule usemi kwamba mchawi mkubwa wa mtu ni mtu
mwenyewe umejidhihirisha pale tulipotumbukizwa katika tamthilia ya
kuangalia jinsi hoja ilivyowasilishwa au ilivyokuwa imewasilishwa awali.
Inawezekana kabisa kwamba Zitto alikuwa na hoja na bila shaka bado kuna
hoja na wengi wanaamini kwamba ipo hoja. Katika kukubali ukweli huo ni
muhimu mambo kadhaa yakazingatiwa. La kwanza ni kwamba uzito wa hoja
hauwezi kuongezeka kwa kubandika tuhuma nyingine juu ambazo zina muonekano
wa kulenga mtu au kikundi cha watu fulani.Pili ni wazi kwamba katika
kujenga hoja yenye maslahi kwa umma ni vyema na busara zaidi kuiweka
katika mazingira ya kuilinda hoja yenyewe na tusikubali kuipaka sifa ambayo
inaweza kwa urahisi kabisa kutumika katika kuiua hoja yenyewe ya
msingi. Ikumbukwe kwamba kwa kila hoja kuna mpinga hoja na mpinga hoja
atatafuta kila udhaifu kuhakikisha kwamba anamalizana na hoja tajwa. Kwa
nini isiwe hivyo kama kuna kanuni na taratibu zilizowekwa kwa ajili ya
utoaji wa hoja zenyewe? Kanuni ambazo zinapovunjwa adhabu zake huwa ni
pamoja na kumtupa mtoa hoja nje ya ulingo yaani kumsimamisha kuhudhuria
vikao kwa muda fulani?Zitto alijaribu kujenga hoja lakini alisahau kwamba
tayari alikwisha kutumia lugha ambayo kama ilivyo ada kwa kila
aliyejiandaa kupangua hoja au hata kuiteteresha lakini ikafanikiwa,
ingelitumika kwa ajili ya kuitupilia mbali hata kama ni kwa muda
mfupi.Kilichomwangusha Zitto pengine ni ujana kwa sababu kuna taarifa kwamba aliaswa
kuepukana na lugha ya tuhuma za moja kwa moja dhidi ya mbunge mwenzake
hata kama huyo mbunge ni waziri.Inawezekana kuhoji, na ni halali kabisa,
kwamba hivi msamiati unawezaje kuua hoja nzito? Unaweza! Hasa
ikizingatiwa kwamba msamiati huo haukuwa wa jumla bali ni mahsusi uliomlenga mtu
maalumu. Hapo ndipo penye shughuli pevu.Kwa upande mmoja kuna Zitto
ambaye anaamini kabisa kwamba kuna hoja nzito katika mkataba wa mgodi wa
Buzwagi. Lakini Zitto huyo huyo akatanguliza dibaji iliyomuhusu
Waziri aliyelengwa katika tuhuma hizo. Ni dibaji hiyo iliyosisitiza kwamba
Waziri kasema uongo au Waziri kaliongopea Bunge.Zitto alitaka kutumia
ushawishi kwa wabunge wenzake bila ya kujali itikadi za kichama kuonyesha
kwamba kuna utata na maslahi ya umma yapo hatarini. Hiyo ni
hoja-tuhuma na ilikuwa haijafikia tamati.Katika Bunge kuna kanuni ambazo
zimekubalika miongoni mwa wabunge. Kanuni hizo zinatoa maelekezo kuhusu jinsi
ya kuwasilisha hoja na pia lugha inayokubalika wakati wa kufanya
hivyo.Katika kuwasilisha hoja uteuzi wa msamiati ni muhimu kwa sababu jambo
linalotangulizwa mbele ni kwamba muulizaji hutaka kutanabahishwa na ndiyo
sababu swali hupitia kwa Spika na kamwe hoja haiwezi kutolewa kama
hukumu kwa mantiki hiyo basi lugha ya kuhukumu haikubaliki. Ndivyo
walivyokubaliana hao wakubwa. Lugha inayotumika katika bunge huwa ni ya
kistaarabu na inayolenga katika dhana kwamba wabunge wote ni sawa na ni
wawakilishi wa wananchi kwa namna moja au nyingine.Kwa mantiki inayotokana
na nafasi yao katika jamii haikubaliki katika bunge kutumia lugha ya
kuhukumu bila ya kuwa na ushahidi wa kutosha.Ushahidi mzuri kuhusiana na
tuhuma dhidi ya Waziri ye yote ule unatosha si tu kumfukuza muhusika
kutoka katika kiti cha ubunge na kumnyangÕanya uwaziri bali pia unatakiwa
ili kuona ni namna gani muhusika anaweza kushitakiwa katika mahakama
ya kawaida kwa makosa ya kuhujumu uchumi au kudidimiza maslahi ya nchi
au kwenda na kinyume na maadiuli na miiko ya uongozi.Hakuna bunge
linaloweza kuwa na amani kama wajumbe wake wataachiwa kutumia lugha za
kuhukumu tena zinazofisha kwa kiasi kikubwa sifa za mbunge mwingine.Bunge
linaloruhusu lugha za hukumu kama vile kudai kwamba mtu ni mwongo au
fisadi n.k. hali kadhalika kuruhusiwa kwa lugha za kejeli, matusi na hukumu
zisizokuwa na mahakama lazima litaishia kudharaulika kwa sababu ngumi
na makonde ya kila aina vitakuwa ni mambo ya kawaida.Hata hivyo,
inapotokea kwamba mtoa hoja anasimama kidete na kumnyooshea mwenzake kidole
kuhusu tuhuma za tabia za kishenzi, kwamba tuhuma aliyoitoa kuhusu tabia
ya kishenzi, kwa sababu wizi, uongo n.k. ni katika kundi la tabia za
kishenzi, ndivyo hivyo na hakuna simile, basi ili tuhuma hiyo
isichukuliwe kuwa ni matusi ya rejareja ni lazima atoe ushahidi hadharani
kuyathibitisha hayo. Anapodiriki mtu kujitosa na kumtuhumu mwingine hadharani
ni lazima kuwepo na ushahidi wa kutosha kuthibitisha hayo.Ushahidi huo
ni muhimu ili aliyemwingiza muongo huyo kwenye chombo adhimu kama bunge
atambue kwamba hana mtetezi na aliyechaguliwa atambue kwamba
amegundulika udhaifu wake huo usio wa kistaarabu. Hivyo ndivyo inavyotakiwa kuwa
na si vinginevyo.Katika hali hiyo basi Zitto alitakiwa, kabla ya
lolote lile kutoa ushahidi wa uongo wa Waziri ili kutoonekana kamba
kamtukana tu bila ya sababu yoyote. Au ili kutenda haki kwa wananchi basi
angeliondoa tuhuma zake hizo walau kwa muda ili kutoa nafasi kwa hoja ya
msingi kuweza kusikilizwa na kusonga mbele kwani kilichomvurugia mambo ni
msamiati ambao angeliweza tu kuuchomoa kama mbinu ya kivita.Pengine
katika kuisaidia demokrasia ya nchi yetu Zitto angelikuja na hoja yake ya
kuhoji uhalali wa mkataba wa Buzwagi na kuwaachia wabunge wenzake
waamue kama kweli hakuna matatizo na kama matatizo hayo yanaweza kuingizwa
katika kundi la uongo. Zitto alishiriki katika kuvuruga mjadala mzuri
ambao pengine ungelitusaidia sisi na wananchi wa Jimbo la Waziri
kujithibitishia kama anafaa au hafai.Kwa mujibu wa kanuni zilizokuwapo hadi
Bunge linamaliza muda wake wa kikao Agosti 17 ilikuwa ni kazi ya Zitto
kuthibitisha hadharani uongo wa Waziri Karamagi. Hakufanya hivyo na badala
yake akashupalia hoja yake na matokeo yake ikawa rahisi sana
kushughulika naye kwa wale ambao walilenga kutafuta njia ya kumpiga dafurau. Na
katika kupigwa dafurau Zitto aliirahisisha mno kazi hiyo kiasi kwamba
wahusika walibaki kumnyooshea kidole na kumwonyesha ni kwa kiasi gani
hajui michezo ya kisiasa.Ni wazi kwa kutosimama na kutaka kufanya mbinu
tofauti katika suala hili Zitto hakuwatendea haki Watanzania ambao
alionekana kama kutaka kuwasaidia pamoja na mambo mengine kutaka kujua jinsi
serikali yao inavyoendeshwa. Pengine jambo kubwa ambalo Zitto
ametusaidia katika kipindi hiki ni kuonyesha kwamba huwezi kupambana na CCM kwa
kupayuka tu. Ili kuweza kuiweka mahali pa kufanya kazi zake kwa
uadilifu zaidi ni lazima akina Zitto wajipange upya na kutambua kwamba siasa
za umaarufu wa reja reja zina hasara zake. Tafakuri ya kina ndio siri
ya mafanikio si ndani ya Bunge bali mahali popote pale kwenye maisha. Kwa makala zaidi, maoni na picha, tembelea; http://mjengwa.blogspot.com

TOOO BIG, AINT GONNA READ ALL THIS DAWG
2004_07_08_powell_africaspeech_600.jpg
 
Mwandishi wetu, Fadhili Abdallah, anaripoti kutoka Kigoma kuwa mapokezi makubwa yanamsubiri Zitto ambaye anatarajiwa kufanya ziara ya siku mbiili wilayani Kigoma kuzungumzia yale yaliyojiri bungeni.

Katika ziara hiyo, Zitto ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, anatarajiwa kuongozana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilbroad Slaa na Kiongozi wa Upinzani bungeni Hamad Rashid Mohammed na Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa chama chao, Tundu Lissu.

Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Kigoma, Msafiri Wamalwa alisema jana kuwa sambamba na viongozi hao, wengine katika msafara huo ni wabunge wawili wa Viti Maalumu wa chama hicho, Muhonga Ruhwanya na Grace Kihwelu, na Kaimu Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Sam Ruhuza.

Akieleza ratiba ya mbunge huyo, Wamalwa alisema baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kigoma asubuhi, Zitto na msafara wake, watakwenda Ofisi ya Mkoa ya CHADEMA ambako watapata taarifa ya utekelezaji ya chama hicho.

Alisema baada ya hapo, msafara huo utakwenda eneo la Urusi Mwanga ambako sehemu kubwa ya ngome ya chama hicho ilimeguka na kujiunga na CCM. Atasimama kwa muda na kuwasalimia viongozi na wanachama wa ngome hiyo.

Baadaye ataondoka eneo hilo kwa kutembea kwa miguu kwenda kwenye Uwanja wa Michezo wa Mwandiga katika jimbo lake la Kigoma Kaskazini ambako kutafanyika mkutano wa hadhara. Kutoka mjini hadi njiapanda ya Mwandiga ni umbali wa kilomita saba na hadi mkutanoni ni kilomita tisa.

Wamalwa alisema kesho Zitto na viongozi wengine wa chama hicho watakuwa na ratiba ya kufungua matawi mbalimbali wakati wa asubuhi katika Wilaya ya Kigoma Mjini.

Baada ya hapo, atakuwa na kikao cha ndani cha viongozi na baadhi ya wanachama wao mkoani na atahitimisha ratiba ya siku hiyo kwa kuwa na mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Mwanga Community Centre mjini Kigoma.

Keshokutwa wataendelea na kazi ya kufungua matawi ya wanachama wapya na wale wa kutoka CCM katika Wilaya ya Kigoma Vijijini wakati wa asubuhi, na wanategemea kufungua matawi 15. Wataondoka mchana kurejea Dar es Salaam.

Source: HabariLEO Agosti 25, 2007
 
Gideon Shoo ni mwandishi wa siku nyingi sana. Nadhani safari hii aliombwa na "RAI" aandike "riwaya ya kufikirika inayoonyesha kuwa Zitto alikosea."
 
JApo Scotland Yard walikuja na kufanya uchunguzi juu ya moto wa Shule ya ShauriTanga.
MH Malecela alitoa taarifa ya utafiti kwa niaba ya Scotland Yard na kusema ulikuwa ni Mshumaa.

Jamani Mshumaa???

Hizi nyumba za Marekani na mshumaa sawa! Lakini zile nyumba zetu Bongo hapana mshumaa utaunguzaje ghafla.
Malecela alipika majibu ya SY.

Kwa hiyo hata nani afanye uchunguzi CCM watayakorofisha hayo majibu au watakaa na Taarifa mpka ujuo wa Yesu.
 
Hili bomu jingine kama kweli lisha sainiwa basi tumewaibua kabla mapemaaa!
Maneno ama maombi ya Adam Malima kwa waziri Mh. Karamagi yamedhihirisha wazi kuwa tunaibiwa.
Adam Malima kwa kujisifu kamuomba waziri Karamagi kutafuta mwekeshaji ktk jimbo lake kuwekesha bila kujua kama Mwekeshaji tayari kisha patikana na mgawanyo umesha fanyika. Hivyo dhahiri hata yeye mwenyewe mbunge wa Nkuranga alikuwa kizani wakati akitoa hoja yake Bungeni.
Kwa kumtaarifu tu - Karamagi sio mtaalam, hivyo asitumie wataalam kusaini mikataba kuwa ndio somo hapa. Uganda kwa taarifa yake walipeleka vijana wao nje kusomea Utaalam wa mikataba ktk sectors za energy na mineral (wizara) na walisimamisha kabisa mikataba yote hadi hapo vijana wao watakapo kuwa tayari. Na ktk hiyo list ya wataalam M 7 wala Bibie ( Ms.) Syda Bbumba sii mmmoja wao. Wamevumbua tayari mafuta na wameisha anza kujikusanya kesho Uganda itakuwa moja ya nchi zinazotoa mafuta! vijana wameisha anza kazi zao, M7 anacheka tu.
Ndugu Adam inabidi afahamu kuwa Waziri sio Mtaalam wala mtendakazi hatupo jeshini hapa.
 
Back
Top Bottom