The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London


Leo Karamagi nami kanishangaza manake huwa hajui Kiswahili fasaha lakini leo kakomaa...na kum-reduce Zitto to almost nothing. Kachambua kipengele kimoja baada ya kingine, kwa data na kwa kujiamini. Kila mtu kaona kwamba Zitto alisema uongo ili kutaka umaarufu. Bado nadhani kumfungia sio jawabu, mimi nadhani ile aibu ya kwamba kadanganya, katoa data za uongo ingetosha (ingawa huyu bwana hana uso wa haya hata anapogundulika kasema uongo).

Kama alivyosema Maulida Komu, Mbunge mwenzake wa CHADEMA, anachohitaji Zitto ni kueleweshwa (ingawa shida yake ni kujifanya mjuaji).
 
"mimi nadhani ile aibu ya kwamba kadanganya, katoa data za uongo ingetosha (ingawa huyu bwana hana uso wa haya hata anapogundulika kasema uongo)."

this one sounds familiar.. labda na wewe tukuonee huruma tu kuwa huwezi kukiri kukosea isipokuwa ile "aibu" inatosha.
 
...anachohitaji Zitto ni kueleweshwa (ingawa shida yake ni kujifanya mjuaji).

1. Zito na Mugongo nani muongo?
2. Zito na Mugongo nani anajifanya mjuaji?
3. Zito na Mugongo nani mtetezi wa wabadhirifu?

Afande Sele yuko wapi atuimbie tungo hii?
 

Uwe unasoma kwanza kabla ya kupost. Hiyo habari imeshajadiliwa sana kwenye thread nyingine.
 
1. Zito na Mugongo nani muongo?
2. Zito na Mugongo nani anajifanya mjuaji?
3. Zito na Mugongo nani mtetezi wa wabadhirifu?

Afande Sele yuko wapi atuimbie tungo hii?

Kumbe niko ligi moja na Zitto? Mie nilijua Zitto Kabwe ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mugongo Mugongo is some anonymous lunatic in the net.
 
Zito amaeonyesha uwezo mkubwa wa kuwachallenge hawa watu ...
 
Masikini baba wa taifa...anatumiwa kuhalalisha mengi.....

Tanzanianjema
 
Wanamfungia Zitto kwa kosa gani? Tatizo letu ni sisi wananchi
ambao hatuwawajibishi wabunge wajinga na wanaotetea ujinga huko bungeni.

Hivi suala la madini, kweli Zitto ndio anatakiwa kufungiwa?
 
Hivi nani alisema yana mwisho haya.....hivi vicheko vilivyojaa bashasha na mikogo....

Mungu atupe uhai tuuone huo mwisho.....kwa salama


Tanzanianjema
 
Kumbe niko ligi moja na Zitto? Mie nilijua Zitto Kabwe ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mugongo Mugongo is some anonymous lunatic in the net.

Kuna mtu anamwamini Mugongo? Basi ataamini kile anachaondika. Je, yule asiyemwamini? Hataamini anachoandika. Mimi nawamini Mugongo.

Anajitambulisha kwetu kama Mugongo the lunatic. So, this is Mugongo. What a name! Au kuna mtu kamwandikia posting hii?
 
Muongomuongo,

Why hizo scripts while tunaona edited/live hapa?

Kwa kuwa unajua kuwa Karamagi ana timu ya watu kama ninyi kwa mamia na pamoja na umiliki wa huo mkataba unaongelewa hapa ambao anadai hauna hitilafu na wakati huohuo hayupo tayari kumpa Zitto ili kujenga kesi yake.

Tuhuma zinapanguliwa kwa majibu na sio vithibitisho ambavyo Mbunge amenyimwa lakini Waziri aliyenavyo hayupo tayar kuvitoa.

Kaka kama wewe upo hapa for Irresponsible endeavors tupo ambao tunatumia muda wetu hapa for responsible causes...

Hebu msikilize Field Marshall Chacha Wangwe hapo..

Tanzanianinjema
 

That is deep, philosophical, stuff right there.
 

..haya maswali yako hayana majibu sahihi!

..sababu hii issue ishakuwa siasa tayari!

..mwana si rizki tena huyu!
 
Hivi hawa watu ndio tunawalipa mamilioni ya pesa? SHAME ON THEM!
 
Wanamfungia Zitto kwa kosa gani? Tatizo letu ni sisi wananchi
ambao hatuwawajibishi wabunge wajinga na wanaotetea ujinga huko bungeni.

Hivi suala la madini, kweli Zitto ndio anatakiwa kufungiwa?

hii ndio ccm wanafanya as if wao pekee ndio wenye hati miliki ya nchi hii..hatutafika na hii nidhamu ya kichama wapinzani hata wakipeleka hoja muhimu kama hii wanafukuzwa na kupingwa tu kwa kuwa ni wapinzani...hatutafika!!! hatutafika!! hatutafika!!!.......wabunge wa ccm wako pale kutetea uzandiki tu.....tuongeze idadi ya wapinzani bungeni ..hata kama wewe ni mwana ccm makini itabidi ukubali haja ya upinzani wenye nguvu.....ameadhibiwa ili kukatisha juhudi za wapinzani kuleta hoja.....nafikiri ni bora wapinzani wote nao wakaungana na zitto ku walk out kwa hizo siku mbili ili na dunia ijue...........bunge limetekwa ..sio muhimili tena!!!!!!!!!!!!

nina hasira sana!!!!!!
 

Wewe, acha kutumia exclamation marks nyingi kiasi hicho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…