The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

burmayv0.jpg




Nguvu ya Umma Burma

Credit Mjengwa blog
 
2.justification; this is used to indicate that what is said is true. according to Dr. everything is likely to be obvious.

3. fair comments. what Dr. did was just a fair coment on the contract, and its content, done for the public interest.

therefore Karamagi has a long way to go before is made to resign.
 
Akiongea na Nipashe kwa njia ya simu juu ya hatua hiyo ya Bw. Karamagi, Dk. Slaa alimtaka afanye haraka kufungua kesi hiyo.

Alisema ana mawakili wengi ambao wamejitolea kumtetea mahamakani bure.

`Mimi nina uhakika na nilichokisema, tena afanye haraka kwenda mahakamani,` alisisitiza Dk. Slaa na kuongeza kwamba huko mahakamani ndiko mengi zaidi yataibuliwa.

`Mtu mwizi ni mwizi tu na sina jina lingine la kumuita bali kumuita hivyo,` alisisitiza Dk. Slaa.

Alisema vyama vyote vya upinzani vitashirikiana kujibu madai yao watakapofikishwa mbele ya mahakama ili hatimaye umma wa Watanzania upate kujua nani mkweli na nani mzushi.

Aliongeza kuwa Bw. Karamagi anakabiliwa na tuhuma nyingine za rushwa kupitia kampuni ya kutoa na kupakia makontena bandarini (TICTS) ambayo ana hisa nyingi.

Dk. Slaa alisema, maovu mengine ya Bw. Karamagi atayatoa leo atakapokutana na waandishi wa habari makao makuu ya CHADEMA ili kuendelea kumuanika hadharani.

Hapa hatoki mtu. Hakuna kulala mpaka kieleweke. Kwa msisitizo "Mtu Mwizi ni mwizi tu, hana jina jingine ila mwizi tu"
 
As Karamagi refuses comment on shadowy deal

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

Energy and Minerals Minister Nazir Karamagi (pictured above) yesterday declined to comment on the latest reports of alleged irregularities in the $400m (approx. 520bn/-) Buzwagi gold mining contract.

Addressing a news conference in Dar es Salaam that he himself convened to express his intention to sue opposition Member of Parliament Dr Wilbrod Slaa (Karatu-CHADEMA) and a tabloid newspaper for alleged defamation, the minister chose to dodge a barrage of questions from journalists specifically on the Buzwagi deal.

’’I have called you here in my personal capacity as Nazir Karamagi - not as a cabinet minister of this government,’’ he declared, although the news conference was conducted at the headquarters of the Ministry of Energy and Minerals in the city.

Asked directly to comment to the media reports outlining details of the controversial Buzwagi pact and his own role in it, an evasive Karamagi responded with the refrain: ’’Please don’t ask me anything about the Buzwagi contract today�I am here to speak about my defamation in person and not in my capacity as a minister.’’

Instead, he concentrated on announcing that he had instructed his lawyers to immediately begin civil litigation proceedings against Dr Slaa, the Kiswahili weekly tabloid MwanaHalisi, and the private newspaper printing firm Printech.

Karamagi said the pending lawsuit against Dr Slaa is in response to the inclusion of his name in a list of top government and public leaders alleged to have been involved in various shady monetary deals in recent years, unveiled by the legislator at a public rally in Dar es Salaam.

Asked if he also planned to sue another CHADEMA MP, Zitto Kabwe (Kigoma North), for first raising the Buzwagi contract issue both in and out of parliament, Karamagi said his lawsuit will zero in on Dr Slaa.

’’I didn’t hear Zitto making any serious allegations against me at the Mwembeyanga public rally (in Temeke District, Dar es Salaam). So, he won’t be in my lawsuit,’’ said the beleaguered minister.

According to Karamagi, Dr Slaa made the alleged defamatory remarks at the public rally on September 15 this year, which is also where he produced his now-famous ’List of Shame’.

Still, most journalists at the media conference appeared more interested in the Buzwagi contract and less in the planned lawsuit, and continued to try to pin down the minister on the matter.

Asked by one journalist to explain why the agreement had to be signed in London, he remarked: ’’It seems you don’t realize that I didn�t travel to London to sign the (Buzwagi) contract.’’

More questions were thrown at him as he left the conference room on the fifth floor of the ministry’s headquarters building, including whether or not he would step down over the allegations. But he remained tight-lipped.
 
Ni kweli mwizi ni mwizi kwani anaweza kupewa jina lingine?

Hapa i patamu sana kwani inaonyesha kuwa DR. SLAA anakiamini kile ambacho anakisema na yupo tayari kukionyesha hadharani.
 
Posted Date::9/26/2007
Karamagi: Sijiuzulu ng'o

* Asema JK anamjua ni safi

* Atampeleka Dk Slaa mahakamani

* Agoma kuzungumzia mkataba wa Buzwagi

* Waandishi wamzuia mpaka ajibu maswali


Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi

MMOJA wa vigogo wanaotuhumiwa kwa ufisadi, Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, amesema hatajiuzulu kwa tuhuma hizo badala yake ataitumia mahakama ili itoe uamuzi kama yeye ni fisadi au siyo.

Karamagi alitoa msimamo huo jana baada ya kuulizwa kama atakuwa tayari kujiuzulu kufuatia tuhuma hizo katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa wizara hiyo katika barabara ya Samora jijini Dar es Salaam jana ili kupisha uchunguzi.

Waziri Karamagi alisema Rais (Jakaya Kikwete), alimteua yeye akijua kuwa ni mtu mwadilifu, hivyo tuhuma anazopewa haziwezi kuwa za kweli hadi zithibitishwe na mahakama.

"Mimi nimeteuliwa na Rais na yeye ndiye anajua uadilifu wangu ndiyo maana kaniteua, sasa hizi ni tuhuma...! Hivi wewe mtu akikutuhumu tu unaweza kuamini ni kweli?" alihoji Karamagi.

Akizungumzia tuhuma hizo kwa undani, Karamagi alisema si kwamba zimemchafua tu bali zimemfanya aonekane mtu asiyefaa kukabidhiwa madaraka yoyote yale katika jamii.

Karamagi alisema kutokana na uzito wa tuhuma hizo ambazo Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Mbunge wa Karatu, Dk Wilbroad Slaa na wenzake wamezitangaza hadharani, haitakuwa busara kwake kukaa kimya badala yake atachukua kuchukua hatua zinazokubalika kisheria ili kuweka kila kitu hadharani na kuacha sheria ichukue mkondo wake.

Waziri huyo alisema ameona ni busara zaidi na ustarabu wa utawala bora na demokrasia ya kweli kufuata mkondo wa sheria ili kubaini ukweli wa mambo na hatimaye haki itendeke.

Alisema kwa kuwa ana heshima ya kulinda jina lake na kulisafisha, anaamini kuwa yeye ni mwadilifu, hivyo ameamua kwenda mahakamani kutafuta haki yake dhidi ya wale wote walioshiriki na wanaoendelea kumpaka matope.

"Nimewaelekeza mawakili wangu, kufungua kesi mahakamani mara moja dhidi ya Dk Slaa, gazeti la Mwanahalisi na kiwanda kilichochapisha gazeti hilo, pamoja na wengine wote walioshiriki na wanaoendelea kushiriki katika kunidhalilisha," alisema.

Hata hivyo, mkutano huo wa Karamagi ulitawaliwa na purukushani za hapa na pale ambazo zilitokana na uamuzi wa waziri huyo kutaka kukimbia maswali ya waandishi wa habari, ambapo mara baada ya kusoma taarifa yake alisema: "asanteni, nimemaliza", kisha alinyanyuka na kuanza kuondoka, lakini waandishi walisimama na kumzuia ili ajibu maswali yao.

"Hapana, tuna maswali yetu, tunaomba ujibu maswali," walisema waandishi wakiwa wamesimama kumzuia asitoke.

Baada ya kuona shinikizo linazidi kuwa kubwa, Karamagi alitaka kujibu maswali akiwa amesimama, lakini waandishi wakambana tena wakisema: "Rudi kakae kwenye kiti, rudi kakae tuulize maswali"!

Hali hiyo, ilimfanya Karamagi kurudi kwenye kiti na kusema: "Lakini nitajibu maswali matatu tu," alisema, na waandishi wakagoma tena.

Alipokaa, waandishi walionyesha utulivu, lakini walimuuliza maswali zaidi ya 20 kwa utaratibu ambao aliyajibu.

Miongoni mwa maswali aliyoulizwa ni pamoja na kutakiwa kueleza tuhuma za ufisadi katika mkataba wa Buzwagi.

Akijibu, alisema hakufika katika mkutano huo kueleza tuhuma za mkataba wa Buzwagi, bali mambo mawili tu ambayo ni kuchafuliwa kwa kuitwa mfisadi na mbadhirifu.

Karamagi amekuwa kigogo wa pili kueleza msimamo wake mbele ya waandishi wa habari kuhusiana na tuhuma hizo, ikiwa ni wiki moja baada ya Dk Slaa kuibua tuhuma za ufisadi wa viongozi wa juu wa serikali Septemba 15., mwaka huu. Mwingine aliyekwisha jitokeza kuelezea msimamo wake ni Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono ambaye alisema hatampeleka mahakamani Dk Slaa.

Hata hivyo, wiki iliyopita Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, aliliambia gazeti hili kuwa anasubiri kupata nakala ya tuhuma hizo kwa Dk Slaa ili aweze kuamua hatua za kuchukua
 
Karamagi agoma kujiuzulu
Aahidi kupasua jipu Jumamosi

na Irene Mark
Tanzania Daima

HOMA ya hoja ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa ya kuwatuhumu viongozi 11 wa serikali na wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa vitendo vya ufisadi, inaendelea kuchukua sura mpya kila kukicha.
Jana, mtuhumiwa wa tatu, Waziri wa Madini na Nishati, Nazir Karamagi, aliibuka na kutangaza azima yake ya kuchukua hatua za kisheria kufanya kile alichokiita kutafuta haki na kusafisha jina lake dhidi ya tuhuma hizo alizozikanusha.

Karamagi alitangaza uamuzi wake huo wa kumshitaki Dk. Slaa, gazeti la MwanaHalisi na Kampuni ya uchapishaji ya Printech, huku akiweka kiporo masuala mengine hadi Jumamosi wiki hii, mbele ya waandishi wa habari, ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Uamuzi wa Karamagi kuitisha mkutano huo wa waandishi wa habari umekuja wakati kukiwa na taarifa kwamba, Rais Jakaya Kikwete ambaye yuko nje ya nchi kikazi, amewaagiza viongozi wote wa serikali na CCM waliotajwa katika tuhuma hizo kujitokeza na kujibu tuhuma zao zote, kila mmoja kwa wakati na kwa namna yake.

Aidha, uamuzi huo wa Karamagi unakuja wakati kukiwa na taarifa nyingine zinazoeleza kuwa, waziri huyo alikuwa akitarajiwa kutoa tamko zito kuhusu hatima yake Jumamosi wiki hii.

Hata hivyo Karamagi hakuwa tayari kuweka bayana iwapo katika mkutano wake wa Jumamosi hii, atafikia uamuzi wa ama kujiuzulu uwaziri, au kukanusha taarifa mpya zinazohusisha kuvuja kwa mkataba wa uchimbaji wa madini wa Buzwagi, ambao aliusaini Februari mwaka huu katika mazingira yanayoliacha taifa likiwa katika mvutano mkubwa kimtazamo.

"Naenda mahakamani kwa kuwa mimi siyo mbadhirifu… Nimeteuliwa na rais. Hivi rais anaweza kumteua waziri mbadhirifu? Unayesema nijiuzulu, kwani ni nani anayemteua waziri?" alisema Karamagi nje ya chumba cha mikutano wakati akijibu swali la mwandishi mmoja wa habari aliyetaka kujua iwapo alikuwa akifikiria kujiuzulu baada ya sakata hilo.

Kujitokeza kwa Karamagi kujibu tuhuma hizo, mbele ya wanahabari na kuweka bayana msimamo wake, kunamfanya awe mtuhumiwa wa pili kufanya hivyo baada ya hivi karibuni Mbunge wa Musoma Vijijini na wakili maarufu nchini, Nimrod Mkono, naye kukana kufuja fedha za BoT kupitia kampuni yake ya uwakili ya Mkono Company and Advocates.

Nje ya utaratibu huo wa kuzungumza na wanahabari, mtu mwingine pekee aliyekanusha tuhuma dhidi yake ni Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, aliyekaririwa na gazeti moja akikiri kuwa na hisa katika Kampuni ya Tangold inayohusishwa na tuhuma za upatikanaji na fedha isivyo halali kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na akakana kufanya jambo lolote lenye harufu ya ufisadi.

Akizungumza jana, Karamagi alisema ameamua kwenda mahakamani kusafisha jina lake lililochafuliwa na Dk. Slaa katika mkutano wa hadhara, Mwembe Yanga, akiamini kuwa yeye ni mtu safi.

"Kwa sababu ninayo heshima ya kulinda jina na kulisafisha, na nina amini kuwa mimi ni muadilifu, nimeamua kwenda mahakamani ili kutafuta haki yangu dhidi ya wote walioshiriki na wanaoendelea kushiriki katika vitendo vya kunipaka matope na kunihukumu kwa ufisadi.

"Nimewaagiza mawakili wangu kufungua kesi mahakamani mara moja dhidi ya Dk Slaa, gazeti la MwanaHalisi na Kiwanda cha Printech kinachochapisha gazeti la MwanaHalisi," alisema Karamagi.

Alisema tuhuma zilizotolewa na Dk. Slaa zililenga kuchafua jina lake na kuonyesha kwamba yeye (Karamagi) ni fisadi na mtu asiyestahili kukabidhiwa madaraka yoyote katika jamii.

Waziri Karamagi alisema Dk. Slaa na wenzake (ambao hakuwataja kwa majina) wamezitangaza kwamba si tuhuma bali ni ukweli, hivyo hawakuona sababu ya kufuata mkondo wa sheria.

Katika hilo, Waziri Karamagi alisema amechukua hatua hiyo bila kujali wadhifa wake kwa taifa akiwa na ushahidi wa kutosha wa kuwafikisha mahakamani wote wanaomtuhumu kwa ufisadi.

"Nitawashitaki kama Nazir Karamagi na siyo Waziri wa Nishati na Madini… ninao ushahidi wa tape (kanda) ya video na nakala ya gazeti la MwanaHalisi," alisema waziri huyo.

Mara tu baada ya kusoma tamko lake hilo, Waziri Karamagi alisimama na kuanza kuondoka kutoka ndani ya chumba cha mikutano, kabla ya kujibu maswali yaliyoanza kuelekezwa kwake na waandishi wa habari.

Hatua hiyo ilipingwa na waandishi wa habari waliotaka arejee kujibu maswali yao, wakisema walikuwa hawajaridhishwa na maelezo yake, na akakubali kurejea akitaka aulizwe maswali matatu tu, huku akiahidi kuzungumza kwa ufasaha Jumamosi wiki hii wakati atakapozungumzia kuhusu mkataba wa madini wa Buzwagi.

"Sihitaji maswali jamani, mnatakiwa mfahamu kwamba nitafungua kesi, basi, hayo maswali nitayajibu Jumamosi… mpo wengi sana, nitaruhusu maswali matatu tu.

"…Mnielewe… hapa sitazungumza issue (suala la) ya Buzwagi, mkiyataka hayo tutakutana Jumamosi, na yule aliyeniuliza kama nilikwenda London kusaini mkataba si kweli," alisema mara baada ya kurejea katika kiti chake.
 
Posted Date::9/26/2007

Alisema kwa kuwa ana heshima ya kulinda jina lake na kulisafisha, anaamini kuwa yeye ni mwadilifu, hivyo ameamua kwenda mahakamani kutafuta haki yake dhidi ya wale wote walioshiriki na wanaoendelea kumpaka matope.


Mimi nilidhani ni jambo la UADILIFU pia kwa yeye kujiuzulu kwanza halafu uchunguzi ufanyike, ikibainika kuwa hajashiriki arudishwe kwenye ofisi yake na 'waliomchafua' wawajibishe.....au kwa vile yeye anaamini ni 'muwadilifu' inatosha kukmfanya aendelee kubaki ofisini?
 
mimi napenda tu kujua kuwa vipi gaezti la "Uhuru" linaripoti vipi matukio haya?pili I'm just trying to speculate what'll be habari ya kuuzia RAI kesho taking into account kwamba na wao walijaribu kumjibu Zitto kwa kujaribu kutafsiri maliciously mahojiano yao na Bw.Mtei,hasa na kwa vile Jenerali Ulimwengu alivyomwalika Tundu Lissu na kuuchambua mkataba,vipi makamarade wa kuimba nyimbo za sifa kwa mafisadi kina Dr.Shoo,Muhingo,et al...mbona wako kimya kwenye huu muziki,au "wameshaupima" unapiga kwa decibels ngapi?
 
mimi napenda tu kujua kuwa vipi gaezti la "Uhuru" linaripoti vipi matukio haya?pili I'm just trying to speculate what'll be habari ya kuuzia RAI kesho taking into account kwamba na wao walijaribu kumjibu Zitto kwa kujaribu kutafsiri maliciously mahojiano yao na Bw.Mtei,hasa na kwa vile Jenerali Ulimwengu alivyomwalika Tundu Lissu na kuuchambua mkataba,vipi makamarade wa kuimba nyimbo za sifa kwa mafisadi kina Dr.Shoo,Muhingo,et al...mbona wako kimya kwenye huu muziki,au "wameshaupima" unapiga kwa decibels ngapi?

Kusema kweli nilikuwa 'mfuasi mwadilifu' wa Rai karibu miaka 8 hivi, lakini tangu 'walipolibinafsisha' limekuwa halina tena yale meno yake,,,kwa hiyo wala sijutii kulikosa..hivi na wao ni lini watakwenda online?

utashangaa hapo kesho usikute hata artcle moja inayohusiana na hii ishu
 
sasa kama hutaki kuondoka walau kwa tuhuma kidogo basi ngoja rungu jingine linakuja utaondolewa na kutupiliwa segerea. maana nasikia hata hiyo kampuni yako ya makontena yenye hisa kibao pale bandarini inanuka kwa rushwa. bora ondoka kabla rungu hilo nalo halijaja
 
maindx9.jpg


SIGNATORIES: The minister, Nazir Karamagi (right), and Pangea Minerals Ltd representative Gareth Taylor, who is also executive general manager of Barrick Gold Tanzania Limited in-charge of operations

Picture: Credit Thisday

Kweli waziri amepewa mamlaka makubwa ya kusaini mikataba n.k. Vipi uhalali wa huu mkataba ambao kwanza umefutwafutwa vipengele vyake tena kwa mikono? Je ni nani hasa hapa anahusika, Karamagi inavyoonekana hayuko peke yake katika hili. Je ni mikataba mingapi ambayo imeingiwa kwa kufutwafutwa namna hii? Hivi ni kweli rais wa nchi yuko hapo Hotelini na kuna mkataba wa millioni zaidi ya 400 na rais haambiwi kwamba kuna Sungura hapa tumenasa? Maana yake huu ni mtego mdogo wa kunasa Sungura tu kama anavyosema waziri mkuu. Kama rais wa nchi kweli alikuwa halifahamu hili kwa nini bado hajamchukulia hatua kali waziri Karamagi? Gareth Taylor naye anafahamu nani alikuwepo wakati wanaweka huo mkataba na nani aliamrisha ku-ufutafuta kama vile sisi walipa kodi hamnazo.

Sasa sisi WTZ tunasema ama zao au zetu, huu mkataba uvunjwe kama ni kweli ulisainiwa bila mashahidi na kufutwafutwa bila ridhaa ya stake holders wa Tanzania na kama hilo haliwezi kutokea basi tutafahamu ni nani hasa muhusika katika deal yote hii. Hao wawekezaji itakuwa vigumu kwao kuendelea kukomba mali TZ bila kulipa fedha halali ya ardhi kwani hii ni ya babu zetu sio babu zao. Yale yanayotokea Nigeria Delta kwa mtutu wa bunduki hatuwezi tukakubali yatokee Tanzania na rais ambaye ndiye mlinzi wa katiba ya Jamhuri ya Muungano lazima sasa aamue, waswahili walisema ukiyavulia maji nguo..............................................Vinginevyo harufu hii inanukia hadi manzese uzuri.

Kara.... alikuwa anatumia experience yake ya Utape... maana sio ya kibiashara, katika kufanikisha Utapel.....
So now i know him as not a real Busine... person bali TP wakimataifa. kwa Ufupi Msanii.
 
karamagi zimemruka naona,yeye aje kwetu wananji akiri kosa na tujue tumfanye nini kama ni bakola 100 kwenye makalio matupu tumchape,tena hadharani kwenye viwanja vya jangwani.
 
Anatafuta jinsi walau ya kusema japo hakuna mantiki, Waswahili husema kuwa mbwa akitaka kufa huwa anaziba pua zake mwenyewe, huyu naye anaziba pua mwenyewe ?
 
sam nimekupata vizuri,

ni hatari ukiangalia vipengele, na bado wabunge wanapinga kura ya kumnyamazisha zitto. tunashangaa mawaziri wake kusaini mikataba ya ajabu. sasa kuna nini la ziada. tupige kura ya kukosa imani na hawa watu.

....Mmemwelewa Mushobozi??? Je kama serikali ikikosa imani kwa wananchi na bunge likashindwa kuiwajibisha, nini kinafuata?? je tupige kura ya kutokuwa na imani na wawakilishi wetu au tuitishe uchaguzi mkuu tena??

nadhani Mushobozi amenena jambo la kujadili hapa
 
Back
Top Bottom