Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Posted Date::9/26/2007
Alisema kwa kuwa ana heshima ya kulinda jina lake na kulisafisha, anaamini kuwa yeye ni mwadilifu, hivyo ameamua kwenda mahakamani kutafuta haki yake dhidi ya wale wote walioshiriki na wanaoendelea kumpaka matope.
mimi napenda tu kujua kuwa vipi gaezti la "Uhuru" linaripoti vipi matukio haya?pili I'm just trying to speculate what'll be habari ya kuuzia RAI kesho taking into account kwamba na wao walijaribu kumjibu Zitto kwa kujaribu kutafsiri maliciously mahojiano yao na Bw.Mtei,hasa na kwa vile Jenerali Ulimwengu alivyomwalika Tundu Lissu na kuuchambua mkataba,vipi makamarade wa kuimba nyimbo za sifa kwa mafisadi kina Dr.Shoo,Muhingo,et al...mbona wako kimya kwenye huu muziki,au "wameshaupima" unapiga kwa decibels ngapi?
![]()
SIGNATORIES: The minister, Nazir Karamagi (right), and Pangea Minerals Ltd representative Gareth Taylor, who is also executive general manager of Barrick Gold Tanzania Limited in-charge of operations
Picture: Credit Thisday
Kweli waziri amepewa mamlaka makubwa ya kusaini mikataba n.k. Vipi uhalali wa huu mkataba ambao kwanza umefutwafutwa vipengele vyake tena kwa mikono? Je ni nani hasa hapa anahusika, Karamagi inavyoonekana hayuko peke yake katika hili. Je ni mikataba mingapi ambayo imeingiwa kwa kufutwafutwa namna hii? Hivi ni kweli rais wa nchi yuko hapo Hotelini na kuna mkataba wa millioni zaidi ya 400 na rais haambiwi kwamba kuna Sungura hapa tumenasa? Maana yake huu ni mtego mdogo wa kunasa Sungura tu kama anavyosema waziri mkuu. Kama rais wa nchi kweli alikuwa halifahamu hili kwa nini bado hajamchukulia hatua kali waziri Karamagi? Gareth Taylor naye anafahamu nani alikuwepo wakati wanaweka huo mkataba na nani aliamrisha ku-ufutafuta kama vile sisi walipa kodi hamnazo.
Sasa sisi WTZ tunasema ama zao au zetu, huu mkataba uvunjwe kama ni kweli ulisainiwa bila mashahidi na kufutwafutwa bila ridhaa ya stake holders wa Tanzania na kama hilo haliwezi kutokea basi tutafahamu ni nani hasa muhusika katika deal yote hii. Hao wawekezaji itakuwa vigumu kwao kuendelea kukomba mali TZ bila kulipa fedha halali ya ardhi kwani hii ni ya babu zetu sio babu zao. Yale yanayotokea Nigeria Delta kwa mtutu wa bunduki hatuwezi tukakubali yatokee Tanzania na rais ambaye ndiye mlinzi wa katiba ya Jamhuri ya Muungano lazima sasa aamue, waswahili walisema ukiyavulia maji nguo..............................................Vinginevyo harufu hii inanukia hadi manzese uzuri.
![]()
![]()
Credit: Mjengwa blog
Mkuu heshima zako mkuu,
Vipi mazuri ya serikali yameisha tayari? au!
sam nimekupata vizuri,
ni hatari ukiangalia vipengele, na bado wabunge wanapinga kura ya kumnyamazisha zitto. tunashangaa mawaziri wake kusaini mikataba ya ajabu. sasa kuna nini la ziada. tupige kura ya kukosa imani na hawa watu.