Insurgent
JF-Expert Member
- Jun 26, 2007
- 469
- 19
SPIKA:
Nitaita wachangiaji kadiri ambavyo mtakuwa mnaleta majina. Kwa hiyo sasa Mheshimiwa Zitto Kabwe.
wachangiaji waliokuwa wanamuunga Zitto walisemaje? Nasikia baada ya Karamagi kutoa HOJA wengine walikuwa wanatamani wasingekuwa wamepeleka majina yao mapema.
Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kunipatia fursa ya kuleta hoja hii hapa kwenye Bunge lako Tukufu kwa mujibu wa kanuni zetu za Bunge. Kuletwa kwa hoja hii, bila kujali maamuzi ya kuhusu hoja yenyewe, ni ishara tosha ya ukomavu wa demokrasia yetu ambayo inakuzwa na mijadala ya Bunge lako Tukufu. Nakupongeza kwa dhati kabisa kwa juhudi zako za kuliimarisha Bunge letu na kujenga muhimili imara wa ulinzi wa demokrasia ya vyama vingi nchini kwetu.
Hapa anakubali Spika na Bunge ana/lina demokrasia. BRAVO! Hii inaonyesha ukomavu kwa upande wake au ulikuwa unafiki akijua ameshafunga GOLI Kama unakubali Bunge lina demokrasia alishindwa nini kukubalia matokeo. Ngoja niendelee...
ninanukuu '…… naomba kutoa Taarifa Rasmi …… kwamba nakusudia kuleta hoja ya kuunda Kamati Teule kuchunguza mkataba mpya wa Madini ambao Waziri wa Nishati na Madini ameusaini bila kuzingatia maagizo ya Rais (wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) ya kupitia mikataba aliyoyatoa mbele ya Bunge lako tukufu tarehe 30 Desemba, 2005. Mwisho wa kunukuu.
Hii point imerudiwa kwenye kipengele namba 7 na ndio point ambayo aliitumia kama muhimili wa kujenga hoja, unfortunately katika kuongezea point aliongezea vipengele vingine vilivyokuwa very weak.
7. Mheshimiwa Spika, Kwanza kabisa napenda nilikumbushe Bunge lako Tukufu kuwa Rais alikwishapiga marufuku kusainiwa kwa mikataba mipya ya Madini mpaka hapo sheria za madini zitakarekebishwa. Akisoma hotuba ya Wizara ya Nishati na Madini mnamo tarehe 17/7/2006, Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Ibrahim Msabaha alilitaarifu Bunge kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amezuia kusainiwa kwa Mikataba mipya ya Madini. Nimeambatanisha Hansard ya siku hiyo kama uthibitisho wa kauli hiyo. Sasa inakuwaje Waziri wa Nishati na Madini kwenda kinyume na maagizo ya Rais? Tena nje ya Nchi
Point hii ndio ya muhimu lakini...
Kyoma (JF Senior Member) input:
Lakini tarehe 1 August 2007, Rais Kikwete akihojiwa na Bw. Shaka Ssali wa Voice of America's (VOA) Straight Talk Africa program,alisema kuwa suala la udurusu wa mikataba bado halijakamilika kwa makampuni ya uchimbaji wa madini nchini kwetu. Alisema Serikali ilifanikiwa kuishawishi kampuni moja tu ya Barrick Gold kufuta kipengere kinachotoa mwanya kwa makampuni ya uchimbaji madini nchini kulipa corporate tax kwa increment kwa jinsi makampuni yanavyopenda (Refer to http://www.voanews.com/english/Afric...TalkAfrica.cfm).
Obviously kampuni ya Barrick Gold ndio pekee ambayo imekubali vipengele vipya na ni ndio kampuni iliyosaini mkataba mpya!
Waziri Karamagi katika hoja yake anasema alisaini huo mkataba February 2007. Tafsiri yangu ya hoja ya Zitto ni kuwa wakati Waziri Karamagi anasaini huu mkataba February 2007, zoezi la kudurusu mikataba ya madini lilikuwa bado linaendelea. Akimjibu Zitto, Waziri Karamagi analiambia Bunge kuwa zoezi la kudurusu mikataba ya zamani ya madini limekamilika, ingawa hakuna maelezo yanayoonyesha tarehe ya kukamilika kwa zoezi lenyewe. Hata hivyo, Rais wa taifa ambalo maslahi yake yako mezani Mheshimiwa Kikwete ameiambia VOA siku 14 zilizopita kuwa zoezi la kudurusu mikataba halijakamilika. Katika suala la kudurusu mikataba ya madini, maelezo ya Zitto yanafanana na maelezo ya Rais Kikwete. Kama hivi ndivyo, nani anasema uongo?
Hapa Zitto amesahau Barrick PEKE YAO wameshakubali vipengele vipya na zoezi definitely haliwezi kurudiwa kwao bali litaendelea kwa kampuni nyingine!
HON. Minister Karamagi Response to This:
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Kabwe Zitto, anasisitiza kuwa zoezi la kudurusu mikataba bado linaendelea. Mtoa hoja labda anachanganya tena zoezi la kudurusu mikataba na zoezi linaloendelea na kudurusu Sheria ya Madini ya Mwaka 1998 na Sheria zinahusu mfumo wa kodi katika sekta ya madini kitu ambacho ni kipana zaidi na kinawahusu wadau wote yaani, wawekezaji wakubwa, wawekezaji wadogo na wote wanaojihusisha na utafiti katika sekta ya madini. Akielewa hili mtoa hoja atabaini kuwa maagizo ya Rais yalitekelezwa kikamilifu na matokeo yake yameishaanza kujitokeza kama faida nilizozieleza hapo juu.
----------------------------------------------------------------------------------
Point nyingine zimejibiwa vizuri sana na waziri, ukisoma ile doc tuliyoletewa hapa inatosheleza.