The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

SPIKA:

Nitaita wachangiaji kadiri ambavyo mtakuwa mnaleta majina. Kwa hiyo sasa Mheshimiwa Zitto Kabwe.

wachangiaji waliokuwa wanamuunga Zitto walisemaje? Nasikia baada ya Karamagi kutoa HOJA wengine walikuwa wanatamani wasingekuwa wamepeleka majina yao mapema.

Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kunipatia fursa ya kuleta hoja hii hapa kwenye Bunge lako Tukufu kwa mujibu wa kanuni zetu za Bunge. Kuletwa kwa hoja hii, bila kujali maamuzi ya kuhusu hoja yenyewe, ni ishara tosha ya ukomavu wa demokrasia yetu ambayo inakuzwa na mijadala ya Bunge lako Tukufu. Nakupongeza kwa dhati kabisa kwa juhudi zako za kuliimarisha Bunge letu na kujenga muhimili imara wa ulinzi wa demokrasia ya vyama vingi nchini kwetu.

Hapa anakubali Spika na Bunge ana/lina demokrasia. BRAVO! Hii inaonyesha ukomavu kwa upande wake au ulikuwa unafiki akijua ameshafunga GOLI Kama unakubali Bunge lina demokrasia alishindwa nini kukubalia matokeo. Ngoja niendelee...

ninanukuu '…… naomba kutoa Taarifa Rasmi …… kwamba nakusudia kuleta hoja ya kuunda Kamati Teule kuchunguza mkataba mpya wa Madini ambao Waziri wa Nishati na Madini ameusaini bila kuzingatia maagizo ya Rais (wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) ya kupitia mikataba aliyoyatoa mbele ya Bunge lako tukufu tarehe 30 Desemba, 2005. Mwisho wa kunukuu.

Hii point imerudiwa kwenye kipengele namba 7 na ndio point ambayo aliitumia kama muhimili wa kujenga hoja, unfortunately katika kuongezea point aliongezea vipengele vingine vilivyokuwa very weak.

7. Mheshimiwa Spika, Kwanza kabisa napenda nilikumbushe Bunge lako Tukufu kuwa Rais alikwishapiga marufuku kusainiwa kwa mikataba mipya ya Madini mpaka hapo sheria za madini zitakarekebishwa. Akisoma hotuba ya Wizara ya Nishati na Madini mnamo tarehe 17/7/2006, Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Ibrahim Msabaha alilitaarifu Bunge kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amezuia kusainiwa kwa Mikataba mipya ya Madini. Nimeambatanisha Hansard ya siku hiyo kama uthibitisho wa kauli hiyo. Sasa inakuwaje Waziri wa Nishati na Madini kwenda kinyume na maagizo ya Rais? Tena nje ya Nchi

Point hii ndio ya muhimu lakini...

Kyoma (JF Senior Member) input:

Lakini tarehe 1 August 2007, Rais Kikwete akihojiwa na Bw. Shaka Ssali wa Voice of America's (VOA) Straight Talk Africa program,alisema kuwa suala la udurusu wa mikataba bado halijakamilika kwa makampuni ya uchimbaji wa madini nchini kwetu. Alisema Serikali ilifanikiwa kuishawishi kampuni moja tu ya Barrick Gold kufuta kipengere kinachotoa mwanya kwa makampuni ya uchimbaji madini nchini kulipa corporate tax kwa increment kwa jinsi makampuni yanavyopenda (Refer to http://www.voanews.com/english/Afric...TalkAfrica.cfm).

Obviously kampuni ya Barrick Gold ndio pekee ambayo imekubali vipengele vipya na ni ndio kampuni iliyosaini mkataba mpya!

Waziri Karamagi katika hoja yake anasema alisaini huo mkataba February 2007. Tafsiri yangu ya hoja ya Zitto ni kuwa wakati Waziri Karamagi anasaini huu mkataba February 2007, zoezi la kudurusu mikataba ya madini lilikuwa bado linaendelea. Akimjibu Zitto, Waziri Karamagi analiambia Bunge kuwa zoezi la kudurusu mikataba ya zamani ya madini limekamilika, ingawa hakuna maelezo yanayoonyesha tarehe ya kukamilika kwa zoezi lenyewe. Hata hivyo, Rais wa taifa ambalo maslahi yake yako mezani Mheshimiwa Kikwete ameiambia VOA siku 14 zilizopita kuwa zoezi la kudurusu mikataba halijakamilika. Katika suala la kudurusu mikataba ya madini, maelezo ya Zitto yanafanana na maelezo ya Rais Kikwete. Kama hivi ndivyo, nani anasema uongo?

Hapa Zitto amesahau Barrick PEKE YAO wameshakubali vipengele vipya na zoezi definitely haliwezi kurudiwa kwao bali litaendelea kwa kampuni nyingine!

HON. Minister Karamagi Response to This:

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Kabwe Zitto, anasisitiza kuwa zoezi la kudurusu mikataba bado linaendelea. Mtoa hoja labda anachanganya tena zoezi la kudurusu mikataba na zoezi linaloendelea na kudurusu Sheria ya Madini ya Mwaka 1998 na Sheria zinahusu mfumo wa kodi katika sekta ya madini kitu ambacho ni kipana zaidi na kinawahusu wadau wote yaani, wawekezaji wakubwa, wawekezaji wadogo na wote wanaojihusisha na utafiti katika sekta ya madini. Akielewa hili mtoa hoja atabaini kuwa maagizo ya Rais yalitekelezwa kikamilifu na matokeo yake yameishaanza kujitokeza kama faida nilizozieleza hapo juu.
----------------------------------------------------------------------------------

Point nyingine zimejibiwa vizuri sana na waziri, ukisoma ile doc tuliyoletewa hapa inatosheleza.
 
Point nyingine zimejibiwa vizuri sana na waziri, ukisoma ile doc tuliyoletewa hapa inatosheleza.

Observation yako kuhusu zoezi la kudurusu mikataba ni nzuri lakini sijakubaliana na conclusion yako kuwa point zote zinazotosheleza kwa vile bado kuna utata katika majibu ya Karamagi kuhusu vifungu vya sheria alivyotumia.
 
Msilolijua ni kama usiku wa giza.. what do Karamagi, Kikwete, Barrick, and Sinclair have in common?
 
Kichuguu.. naona unachanga sheria mbili. Sheria ya Fedha ni ya 2004. Unayotaka ni sheria ya Public Finance ya 2001. Sivyo?

Naona unanichanganya kidogo hapa; Zitto na Karamagi walikuwa wakitumia Finance Act No 14 ya mwaka 2001, hiyo ndiyo ninayotaka kusoma.
 
Katika majibu ya Kramagi tarehe 16/7 kwa Zitto alisema mgodi wa Buzwagi ni mdogo sana,

Katika majibu yake anaonyesha huo mgodi ulikuwa wa mhimu sana, utaongeza pesa lukuki na ajira zaidi ya 600!

Huu ndio mgodi mdogo? na kama huu ndo mdogo mikubwa ni ipi na imezalisha ajira na kuingizia Taifa pesa kiasi gani?

Mbona majibu yake haya mawili yana gongana? kuna nini hapo kati kati?
 
Msilolijua ni kama usiku wa giza.. what do Karamagi, Kikwete, Barrick, and Sinclair have in common?

Mwanakijiji,

Swali zuri sana. Mimi sina jibu wala sijui wanahusiana vipi, zaidi ya Sinclair kusema mara kadhaa kwenye barua zake kuwa JK ni Rafiki yake!!!

FD
 
Yaani Wbunge wetu wamepoteza opportunity ya ajabu- Kuunda tume kuchunguza nani muongo katia ya Waziri Karamagi na Mhe. Zitto.

Kumbe hawa Wabunge wa CCM wanaunga mkono hizi siri za mikataba ya madini. Nimekunguwazwa sana, kama wangekuwa wakweli na wanaitakia nchi hii mustakabali mwema hiyo ilikuwa ni good opportunity ya kuungalia huo mkataba vizuri, kumbe wanapiga kelel bure kutudanganya Watanzania. Wamelishwa yamini, wako tayari ku-support uozo kwa kulishwa carrot na Serikali.

Kwang mimi kama tume ingeundwa, whatever the judgement after matokeo ya uchunguzi wa tume ya Bunge ningefurahi sana; lakini kwa kukwepa kuunda tume basi kuna jambo linafichwa na linajulikana. Bado naamini Zitto amesema ukweli vinginevyo tume ingeundwa na matoke ya uchunguzi wa Tume hiyo nadhani yangebadili mustakablai mzima wa nchi hii, kitu ambacho Wakubwa wetu wanakijua na ndiyo maana wamembania Zitto!

Wana JF, serikali imeshituka ndiyo maana wameizima hoja ya Zitto, tungeona mengi na pengine mwisho wa Walanchi hawa ungefika.
 
Mwanakijiji,

Swali zuri sana. Mimi sina jibu wala sijui wanahusiana vipi, zaidi ya Sinclair kusema mara kadhaa kwenye barua zake kuwa JK ni Rafiki yake!!!

FD

FD... sit and wait.. the truth will finally come to light. Ndio maana mtaelewa ni kwanini Karamagi alienda London kutia sahihi mkataba huo akifuatana na Kikwete..na kwa haraka hivyo. Hamjajiuliza ni kwanini utiaji sahini mkataba huu haukusemwa kwenye Bunge la Februari au kwenye hotuba ya bajeti ya mwaka huu?
 
Katika majibu ya Kramagi tarehe 16/7 kwa Zitto alisema mgodi wa Buzwagi ni mdogo sana,

Katika majibu yake anaonyesha huo mgodi ulikuwa wa mhimu sana, utaongeza pesa lukuki na ajira zaidi ya 600!

Huu ndio mgodi mdogo? na kama huu ndo mdogo mikubwa ni ipi na imezalisha ajira na kuingizia Taifa pesa kiasi gani?

Mbona majibu yake haya mawili yana gongana? kuna nini hapo kati kati?

..maneno hayo ndo yanayozua maswali mengi,majibu yanakosekana!

..simply,kuna uongo fulani kwenye the whole issue!
 
Hivi ni kweli kuwa Waziri Karamagi alishtukizwa na kikao cha Barrick kule London na hakutaka kulazia damu ikabidi achangamkie tenda?
 
Hivi ni kweli kuwa Waziri Karamagi alishtukizwa na kikao cha Barrick kule London na hakutaka kulazia damu ikabidi achangamkie tenda?

..ukisikia usanii ndo huo!

..kulazia damu tenda ipi? kwani nani anayefaidika zaidi?

..au unamaamisha hakutaka kulazia damu "tenda"!
 
...yah, Bunge limejikosesha nafasi ya kushirika ktk mchakato wa kuboresha sheria yetu ya uwekezaji ktk sekta ya madini na nishati.
 
Post yangu ya mwisho niliiandika bado nikipitia maswali na majibu ya Zitto na Karamaji. Kama nilivyoainisha. Mhimili wa argument umeshaondoka, hebu twende ndani sasa...

Alianza Zitto kupiga penalti lakini kipa yule (Karamagi) alikuwa makini! Kweli naamini mtu akiamua kupotosha, kurekebisha inahitaji utulivu. Huwezi kushindwa kukubali kama kwenye "war of facts", Karamagi alifanya kweli. Karamagi yuko makini kuliko nilivyofikiri au niseme Serikali iko makini.

Maelezo yalitakiwa katika mambo mawili makuu:-

(i) Kusainiwa kwa Mkataba mpya wa wa Madini wa mgodi (mradi) wa Buzwagi kati ya Serikali na Kampuni ya Barrick na sababu za mkataba huo kusainiwa nje ya nchi, London Uingereza na vilevile kwa nini mkataba huo umesainiwa wakati bado serikali inafanya durusu (review) ya mikataba kufuatana na maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete.

(ii) Kuondolewa kwa kipengele katika Sheria ya Kodi ya mapato ya mwaka 1973 kuhusiana na asilimia 15% ya 'capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure' bila ya kibali cha Bunge lako Tukufu.

Point (i) ilikuwa na mhimili wa HOJA(soma post yangu ya mwanzo) na suala lingine, "sababu ya mkataba huo kusainiwa nje ya nchi."

Zito aliyakinisha kwamba Waziri akijibu swala la kusainiwa nje kwa kutumia kipengele cha marginal mine na kwamba kulikuwa na umuhimu wa kufinalize haraka ili kutokupoteza nafasi hiyo.

Zitto alimnukuuu Karamagi: "Mheshimiwa Spika, katika tathmini ya Migodi, Mgodi wa Buzwagi ni Marginal Mine ambao uhai wake si wa muda mrefu. Bila ya kutumia fursa ya bei ya Dhahabu uwekezaji wake usingeweza kuwa wa faida. Hata hivyo, Mkataba wa Buzwagi hauna mapungufu yaliyokuwamo kwenye mikataba ya zamani". Mwisho wa kunukuu.

Karamagi:

Mheshimiwa Spika, mgodi wa Buzwadi kuwa ni Marginal mine. Nilisema kwamba katika tathimini ya migodi, Mgodi wa Buzwagi ni Marginal Mine ambao uhai wake si wa muda mrefu na kwamba bila ya kutumia hela fursa iliyokuwepo hususan bei kubwa ya dhahabu uwekezaji wake usingekuwa wa faida. Wizara ya Nishati na Madini ilifanya uchambuzi wa taarifa ya uwekezaji katika Mgodi wa Buzwagi na kuonekana kuwa mgodi huo ni marginal project na ukianza kuendelezwa wakati huu ambapo bei ya dhahabu ni kubwa wastani wa zaidi ya dola za Marekani 600 kwa wakia, ndiyo utatoa marginal profit na kuwezesha mwekezaji kuendeleza mradi wa Buzwagi hadi kufikia hadhi ya kuwa mgodi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Kabwe anasema kuwa mgodi wa Buzwagi hauwezi kuitwa marginal mine kwa kigezo utashika nafasi ya pili kwa migodi inayomilikiwa na kampuni ya Barrick kwa kulinganisha moja kwa moja gharama za uwekezaji kati ya Mgodi wa Bulyanhulu uliofanyika miaka ya tisini na mgodi wa Buzwagi unaotarajiwa kujengwa mwaka ujao 2008.

Mheshimiwa Spika, mtoa hoja inaelekea anazungumzia suala la utaalamu wa fedha ambalo inaonyesha wazi hana ujuzi nalo. Hata hivyo mtu hahitaji kuwa mtaalamu ili kuelewa kuwa kama mwekezaji alitumia thamani ya dola za Kimarekani milioni 600 kujenga mgodi wa Bulyanhulu miaka kumi iliyopita, akitaka kujenga mgodi kama huo kwa sasa thamani yake itakuwa kubwa maradufu. Labda kwa manufaa ya Bunge lako tukufu, naomba nito ufafanuzi wa ziada ili kuonyesha kuwa gharama za uwekezaji siyo kigezo pekee cha kupima ubora wa mgodi. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, vigezo vingine vinavyotumika kujua ubora wa mgodi ni pamoja na mashapo yaliyopo na kiwango cha upatikanaji wa dhahabu kwa tani ya miamba (ore grade per tonne). Kiwango cha upatikanaji wa dhahabu katika mgodi wa Bulyanhulu ni wastani wa gramu 11 za dhahabu kwa tani ikilinganishwa na Buzwagi ambapo ni gramu 1.8 za dhahabu kwa tani. Mashapo yaliyopo Bulyanhulu ni kiasi cha wakia milioni 12 inayoweza kuchimbwa kwa miaka karibu 25 wakati Buzwagi ni wakia milioni 2.2 inayoweza kuchimbwa kwa miaka 10. Kutathiminiwa Mgodi wa Buzwagi kama Marginal mine ni suala la kitaalamu lenye takwimu za wazi ambalo halipingiki wala halipindishwi. (Makofi)

Hapa anaonyesha wazi Utafiti wa Zitto ulikuwa weak na alijenga HOJA ama kwa CHUKI au UELEWA MDOGO.

Suala la kusaini wapi ndio lilinifurahisha, alionyesha wazi muhimu sio wapi umesainiwa bali sheria za Nchi gani zitatumika kwa mkataba huo.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Kabwe Zitto anauliza kwenye mkataba huo, Je, kipengele kimekuwa signed in London ama signed in Dar es salaam?

Mheshimiwa Spika, hali ya maendeleo tuliyoyafikia dunia ya kileo, si muhuimu tena kwenye mikataba kuweka kipengele cha kubainisha mkataba kuweka kipengele cha kubainisha mkataba umewekwa saini eneo gani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Format ya mkataba wa Madini wa Buzwagi hauna kipengele anachokiuliza Mheshimiwa Kabwe Zitto. Hiki si kitu cha ajabu kwa mikataba ya siku hizi ambapo mkataba unaweza kusainiwa na pande zaidi ya mbili zikiwa nchi tofauti. Mkataba unaweza ukasainiwa upande mmoja na ukatumwa kusainiwa na upande mwingine nchi nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kitu muhimu katika mkataba ni kuonyesha kwenye mkataba ni sheria ya nchi gani itaongoza mkataba. Mkataba wa Mgodi wa Buzwagi unataja kuwa sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo itaongoza mkataba huo. (Makofi)

Hebu naomba hata wale waliokuwa biased wamsifu walau kidogo Waziri huyu alivyoweza kujibu HOJA kwa HOJA. Mimi siweki siri, niliamini maneno ya Zitto mwanzo na nilihisi mazingira ya rushwa, lakini lazima nikiri Waziri Karamagi alijibu vizuri akitumia FACTS.

Kipengele na (ii) cha sheria bado natafuta hizo sheria nizipitie vizuri.
 
..kwahiyo tupige makofi kama wale wabunge? kwani alikuwa anatoa ngonjera? usanii mtupu!

..hoja hapa haiko kwenye kupangua au kujibu!

..hoja iko kwenye wizi wa mchana wa maliasili yetu,ilhali hali zetu taaban!

..hili si suala la partisanship bali national interests!
 
Hapa anaonyesha wazi Utafiti wa Zitto ulikuwa weak na alijenga HOJA ama kwa CHUKI au UELEWA MDOGO.

Hiyo consesus umefikia wewe mwenyewe au imefikiwa na kikao cha halmashauri ya chama....?

Watu hawafanyi uchambuzi kwa mwonekano bali kwa facts... maneno na styles nyingi kisha unatumia lugha ya mwonekano....

Huo mwonekano ni wako na wala Zito hana chuki na uelewa mdogo kama unavyotaka kudai hapa....

Grrrrrr...... jipange zaidi
 
Mimi naona hapa kuna maswali mengi sana ya kujibu kabla ya kukimbilia kusema waziri alikuwa right :

Waziri anaonekana ya kuwa alikuwa na wasi wasi kuwa thamani ya gold inaweza kupungua siku za usoni , je ni vigezo gani alivyotumia kufukia huo uamuzi ? Pili kama kuna mtu yoyote anayejua ukuaji wa thamani ya gold in relation to american dollar katika kipindi cha miaka mitano atupatie ili tuone kama kuna uwiano wowote na yale yaliyosemwa na waziri.
 
..kwahiyo tupige makofi kama wale wabunge? kwani alikuwa anatoa ngonjera? usanii mtupu!

..hoja hapa haiko kwenye kupangua au kujibu!

..hoja iko kwenye wizi wa mchana wa maliasili yetu,ilhali hali zetu taaban!

..hili si suala la partisanship bali national interests!

kwi kwei kwi.

Asante Dar si Lamu....
 
Post yangu ya mwisho niliiandika bado nikipitia maswali na majibu ya Zitto na Karamaji. Kama nilivyoainisha. Mhimili wa argument umeshaondoka, hebu twende ndani sasa...

Alianza Zitto kupiga penalti lakini kipa yule (Karamagi) alikuwa makini! Kweli naamini mtu akiamua kupotosha, kurekebisha inahitaji utulivu. Huwezi kushindwa kukubali kama kwenye "war of facts", Karamagi alifanya kweli. Karamagi yuko makini kuliko nilivyofikiri au niseme Serikali iko makini.

Maelezo yalitakiwa katika mambo mawili makuu:-

(i) Kusainiwa kwa Mkataba mpya wa wa Madini wa mgodi (mradi) wa Buzwagi kati ya Serikali na Kampuni ya Barrick na sababu za mkataba huo kusainiwa nje ya nchi, London Uingereza na vilevile kwa nini mkataba huo umesainiwa wakati bado serikali inafanya durusu (review) ya mikataba kufuatana na maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete.

(ii) Kuondolewa kwa kipengele katika Sheria ya Kodi ya mapato ya mwaka 1973 kuhusiana na asilimia 15% ya ‘capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure’ bila ya kibali cha Bunge lako Tukufu.

Point (i) ilikuwa na mhimili wa HOJA(soma post yangu ya mwanzo) na suala lingine, "sababu ya mkataba huo kusainiwa nje ya nchi."

Zito aliyakinisha kwamba Waziri akijibu swala la kusainiwa nje kwa kutumia kipengele cha marginal mine na kwamba kulikuwa na umuhimu wa kufinalize haraka ili kutokupoteza nafasi hiyo.

Zitto alimnukuuu Karamagi: “Mheshimiwa Spika, katika tathmini ya Migodi, Mgodi wa Buzwagi ni Marginal Mine ambao uhai wake si wa muda mrefu. Bila ya kutumia fursa ya bei ya Dhahabu uwekezaji wake usingeweza kuwa wa faida. Hata hivyo, Mkataba wa Buzwagi hauna mapungufu yaliyokuwamo kwenye mikataba ya zamani”. Mwisho wa kunukuu.

Karamagi:

Mheshimiwa Spika, mgodi wa Buzwadi kuwa ni Marginal mine. Nilisema kwamba katika tathimini ya migodi, Mgodi wa Buzwagi ni Marginal Mine ambao uhai wake si wa muda mrefu na kwamba bila ya kutumia hela fursa iliyokuwepo hususan bei kubwa ya dhahabu uwekezaji wake usingekuwa wa faida. Wizara ya Nishati na Madini ilifanya uchambuzi wa taarifa ya uwekezaji katika Mgodi wa Buzwagi na kuonekana kuwa mgodi huo ni marginal project na ukianza kuendelezwa wakati huu ambapo bei ya dhahabu ni kubwa wastani wa zaidi ya dola za Marekani 600 kwa wakia, ndiyo utatoa marginal profit na kuwezesha mwekezaji kuendeleza mradi wa Buzwagi hadi kufikia hadhi ya kuwa mgodi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Kabwe anasema kuwa mgodi wa Buzwagi hauwezi kuitwa marginal mine kwa kigezo utashika nafasi ya pili kwa migodi inayomilikiwa na kampuni ya Barrick kwa kulinganisha moja kwa moja gharama za uwekezaji kati ya Mgodi wa Bulyanhulu uliofanyika miaka ya tisini na mgodi wa Buzwagi unaotarajiwa kujengwa mwaka ujao 2008.

Mheshimiwa Spika, mtoa hoja inaelekea anazungumzia suala la utaalamu wa fedha ambalo inaonyesha wazi hana ujuzi nalo. Hata hivyo mtu hahitaji kuwa mtaalamu ili kuelewa kuwa kama mwekezaji alitumia thamani ya dola za Kimarekani milioni 600 kujenga mgodi wa Bulyanhulu miaka kumi iliyopita, akitaka kujenga mgodi kama huo kwa sasa thamani yake itakuwa kubwa maradufu. Labda kwa manufaa ya Bunge lako tukufu, naomba nito ufafanuzi wa ziada ili kuonyesha kuwa gharama za uwekezaji siyo kigezo pekee cha kupima ubora wa mgodi. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, vigezo vingine vinavyotumika kujua ubora wa mgodi ni pamoja na mashapo yaliyopo na kiwango cha upatikanaji wa dhahabu kwa tani ya miamba (ore grade per tonne). Kiwango cha upatikanaji wa dhahabu katika mgodi wa Bulyanhulu ni wastani wa gramu 11 za dhahabu kwa tani ikilinganishwa na Buzwagi ambapo ni gramu 1.8 za dhahabu kwa tani. Mashapo yaliyopo Bulyanhulu ni kiasi cha wakia milioni 12 inayoweza kuchimbwa kwa miaka karibu 25 wakati Buzwagi ni wakia milioni 2.2 inayoweza kuchimbwa kwa miaka 10. Kutathiminiwa Mgodi wa Buzwagi kama Marginal mine ni suala la kitaalamu lenye takwimu za wazi ambalo halipingiki wala halipindishwi. (Makofi)

Hapa anaonyesha wazi Utafiti wa Zitto ulikuwa weak na alijenga HOJA ama kwa CHUKI au UELEWA MDOGO.

Suala la kusaini wapi ndio lilinifurahisha, alionyesha wazi muhimu sio wapi umesainiwa bali sheria za Nchi gani zitatumika kwa mkataba huo.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Kabwe Zitto anauliza kwenye mkataba huo, Je, kipengele kimekuwa signed in London ama signed in Dar es salaam?

Mheshimiwa Spika, hali ya maendeleo tuliyoyafikia dunia ya kileo, si muhuimu tena kwenye mikataba kuweka kipengele cha kubainisha mkataba kuweka kipengele cha kubainisha mkataba umewekwa saini eneo gani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Format ya mkataba wa Madini wa Buzwagi hauna kipengele anachokiuliza Mheshimiwa Kabwe Zitto. Hiki si kitu cha ajabu kwa mikataba ya siku hizi ambapo mkataba unaweza kusainiwa na pande zaidi ya mbili zikiwa nchi tofauti. Mkataba unaweza ukasainiwa upande mmoja na ukatumwa kusainiwa na upande mwingine nchi nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kitu muhimu katika mkataba ni kuonyesha kwenye mkataba ni sheria ya nchi gani itaongoza mkataba. Mkataba wa Mgodi wa Buzwagi unataja kuwa sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo itaongoza mkataba huo. (Makofi)

Hebu naomba hata wale waliokuwa biased wamsifu walau kidogo Waziri huyu alivyoweza kujibu HOJA kwa HOJA. Mimi siweki siri, niliamini maneno ya Zitto mwanzo na nilihisi mazingira ya rushwa, lakini lazima nikiri Waziri Karamagi alijibu vizuri akitumia FACTS.

Kipengele na (ii) cha sheria bado natafuta hizo sheria nizipitie vizuri.

Lazima tukubali kwamba katika rhetoric, Karamagi alimzidi Zitto. Kwa wanaotazama rhetoric wanaishia kwenye utetezi mzuri wa Karamagi kusema Zitto ni mwongo.

Ukweli hapa ni kwamba hoja za Karamagi zimesimama kwa sababu serikali ilipata muda wa kuziweka sawa kwa kutumia document za Zitto. Hata mimie ningeweza kumshushua Zitto kama ningekuwa upande mwingine na akanipa hoja zake mapema.

Zitto mwenyewe alipoomba apewe mkataba wenyewe auone na baadhi ya documents alinyimwa. Hapa ndipo alipopigwa bao. Hivyo, ilitarajiwa kwamba serikali ingejibu mapigo kwani ilishajiandaa. Lakini kujibu mapigo siyo kusema ukweli.

Zitto, kwa kujua hili, ndiyo maana aliomba iundwe kamati ichunguze hata majibu haya ya Karamagi. Ingekuwa fursa pia ya kujua uchafu ulio katika mkataba huu na mingine ambayo serikali imekuwa inawanyima wabunge.

Kinachompa ushujaa Zitto ni unpopularity ya serikali kwa sababu sasa wananchi wameshajua kwamba ni corrupt government by corrupt leaders! Hata hivyo, bila KAMATI majibu ya Karamagi yanabaki kuwa rhetoric tu.
 
Back
Top Bottom