The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

hapo sasa hapo, haya leteni maneno, shujaa wetu huyo.

inanikumbusha kule Zanzibar salim Msabah alipohama CUF na kujiunga CCM kukawa kuna kasheshe oooh katekwa nyara, Salim Msabah shujaa na maneno kibao, kumbe hana lolote ni unafiki wake tu. katoka kwa hiyari yake.

halafu kinachonikera kuwafuli wananchi, hawa wapinzani wanadai ooh CCM inawafuli wananchi kumbe na wao wako mbele hivyo hivyo nyote jahazi moja.

wananchi wanaambiwa waingie barabarani shujaa, semeni ukweli jamaa hajajipanga kakurupuka kaliwa basi.

kukaa ni kujipanga na mkitaka kumkomalia nyani msimtazame usoni, pangeni mashambulizi yenye maana. kwa hili nendeni mahakamani tuone nn kitatokea msije hapa mkasema kuwa mahakama ni CCM.

mwaka huu ni mwaka mgumu kwa wapinzani
 
Mimi naona hapa kuna maswali mengi sana ya kujibu kabla ya kukimbilia kusema waziri alikuwa right :

Waziri anaonekana ya kuwa alikuwa na wasi wasi kuwa thamani ya gold inaweza kupungua siku za usoni , je ni vigezo gani alivyotumia kufukia huo uamuzi ? Pili kama kuna mtu yoyote anayejua ukuaji wa thamani ya gold in relation to american dollar katika kipindi cha miaka mitano atupatie ili tuone kama kuna uwiano wowote na yale yaliyosemwa na waziri.

...tunazotakiwa tuzijadili. si nani kamshinda nani,kwani ni upuuzi mtupu,wakati wazungu wanapeleka dhahabu kwao na kutuachia mahandaki na vilima vya mchanga wenye sumu!

...rufiji,unafikiri kama thamani ingekuwa inashuka hao jamaa wangeendelea kuwekeza heavily?

...kama thamani ingekuwa inashuka wangeendelea na strategy za ku-monopolize gold mining in tz?

...na maswali mengine,wengine wachangie!
 
kama kuna jambo ambalo nnahisi lilikuwa lifikiriwe mara mbili ni adhabu aliopewa kuwa ni kubwa na si zaidi.

maana hoja zake zilikuwa za kitoto mno
 
Mimi nilivyoona ni kuwa majibu ya Karamagi kweli yalikuwa yamenyooka kiasi kuwa hoja za Zitto zilionekana kuwa hazikufanyiwa maandalizi ya kutosha. Inaelekea aliyaandaa majibu yale kwa muda wa kutosha. Hata hivyo ninapoyapitia kwa makini majibu yale dhidi ya hoja Zitto na kuchambua facts, nashindwa kukubaliana na majibu hayo kwa kiasi kikubwa. Ukiachia sehemu chache ambazo inaelekea Zitto hakujua facts, sehemu kubwa ya majibu hayo yalikwepa hoja za msingi na kuzijibu kwa kutumia taarifa zisizohusika nadhani ili kuweka mtiririko nzuri.

Kilichonishangaza ni kuwa wabunge wamesikiliza majibu yale wakafurahishwa na mtiririko ule wakasahahu kuchambua facts. Nimekuwa naona Maseneta wa marekani wanapoletewa majibu na kiongozi wa serikali huchukua kama siku mbili kuyatafakari kabla hawajayajadili. Ilikuwaje wabunge wetu hawakujipa hata nusu siku ya kuyatafakakari majibu yale.

Kwa sasa sipendi kuweka uchambuzi wangu kwa vile sijapata sheria za madini na sheria za fedha ambazo zimezungumziwa katika hoja na katika majibu, nikishazipata na kukamilisha uchambuzi wangu nitauweka hapa kuonyesha nguvu na upungufu katika majibu ya Waziri.
 
Kilichonishangaza ni kuwa wabunge wamesikiliza majibu yale wakafurahishwa na mtiririko ule wakasahahu kuchambua facts. Nimekuwa naona Maseneta wa marekani wanapoletewa majibu na kiongozi wa serikali huchukua kama siku mbili kuyatafakari kabla hawajayajadili. Ilikuwaje wabunge wetu hawakujipa hata nusu siku ya kuyatafakakari majibu yale.

..ile kwao ilikuwa kama mashindano ya ngonjera hivi!ambayo huhitaji kutafakari wakati huo,realy!
 
Niwaulize wenye kujua uchumi. Endapo ujenzi wa jengo unagharimu dola milioni 500, na baadaye ujenzi kama huo baada ya miaka kumi tunaambiwa ungeweza kugharimu dola milioni 1000. Je, ni nini kinaweza kusababisha jambo hilo ukizingatia kushuka thamani kwa dola na vigezo vinginevyo? Kwa ufupi, je kweli inawezekana in terms of dollars jengo kugharimu maradufu ndani ya miaka kumi?
 
Niwaulize wenye kujua uchumi. Endapo ujenzi wa jengo unagharimu dola milioni 500, na baadaye ujenzi kama huo baada ya miaka kumi tunaambiwa ungeweza kugharimu dola milioni 1000. Je, ni nini kinaweza kusababisha jambo hilo ukizingatia kushuka thamani kwa dola na vigezo vinginevyo? Kwa ufupi, je kweli inawezekana in terms of dollars jengo kugharimu maradufu ndani ya miaka kumi?

..unaongelea nini?

..minara mapacha?
 
WanaJF,

Habari za siku nyingi. Ninawaletea mjadala wote ulivyokuwa. Hii ni Hansard (kumbukumbu rasmi za Bunge).

Angalia hoja yangu, majibu ya Karamagi, na majibu yangu ya kuhitimisha hoja. Pia michango ya wabunge wengine. Msome vizuri Kabuye, Hamad Rashid na Mudhihir!

Kila la kheri

ZZK
 

Attachments

WanaJF,

Habari za siku nyingi. Ninawaletea mjadala wote ulivyokuwa. Hii ni Hansard (kumbukumbu rasmi za Bunge).

Angalia hoja yangu, majibu ya Karamagi, na majibu yangu ya kuhitimisha hoja. Pia michango ya wabunge wengine. Msome vizuri Kabuye, Hamad Rashid na Mudhihir!

Kila la kheri

ZZK


Kwa niaba ya wengine nasema asante tutasoma
 
Ibrah,

That is what I have been suspecting all along.That is what seems the obvious reason for their collective action; behaving like a bunch of frigtened animals fighting for survival.
 
Mugongo ni kichekesho kikubwa na wale waswahili waliopitwa na wakati kimawazo. Msimamo wako ni upi, Je unasema nini kuhusu hili swala? badala ya kukaa na kutuwekea vijimaneno vya kiswahili ni bora uelezee hoja ya msingi na tukosoane badaya ya uswahili na vijimaneno. Wengi wetu tunatumia hizi website kwasababu tuko nje lakini Watanzania wengi kwa sasa wamechoshwa na rushwa na unavyosema zitto akatafute ushahidi au mambo ya rushwa yanayofanya ni maneno tu basi wewe uko dunia ya pekee. Mfano imebainika kuwa ndege ya rais ilikuwa na rushwa, rada, richmod je ni nani ka athibiwa, Mugogo kuanzia Kikwete aingie madarakani ni nani kastahafishwa kwa rushwa, au watu wote ni safi na haya mambo ya rushwa ni maneno tu!?. Kitu chochote kinachokosoa serikali ni kibaya hata hakielimu ni mbaya kwa CCM je ni kitu gani ambacho si cha CCM ni kizuri?. Mbona huku marekani watu wanapeleza hoja walizosoma kwenye magazeti ya New York Times, je ni lini Mwakilishi wa Marekani kafungiwa kutokana na hoja aliyopeleka?. Tatizo kubwa la Watanzania kama wewe ni unafiki unajua ukweli lakini huwezi kuandika mnabaki kubeza kitoto kitoto . Je si wakati sasa wa kuonyesha ukweli, kupinga rushwa, kukuza uhuru, na kuonyesha mapenzi ya nchi na si ya chama wala tumbo. Tanzania ni nchi yetu sisi tulioko nje tungeweza kukaa huku na elimu zetu na kuishi vizuri tu lakini tunaipenda nchi yetu sana na ndiyo maana tutasema hatakama mawakala hampendi. Mika 20 ijayo wengi wa hao wazee watakuwa wameondoka hivyo ni kwa faida yao kuhakikisha wanaacha nchi mahali pema kwani hizo mali walizojilimbikizia kwa rushwa hakuna uhakika kama zitakuwepo lakini wakiacha nchi pazuri watakuwa na uhakika wa wajukuu zao kwenda shule, kutibiwa, na kuywa maji safi.Sisi watoto wetu wanazaliwa nje lakini bado tunajali nchi. Hivyo ningeshauri ushabiki wa siasa uishe na tuendeleze nchi yetu kama Watanzania kwa ujumla. Mugongo nyie mawakala hamtaweka kutusimamisha watanzania wenye mapenzi, mtafungia magazeti, website lakini hamtaweza kufungia nafsi inayo jali ukweli, inayopinga rushwa, na inayopenda haki za binadamu na democrasia.
 
MAREKEBISHO KICHWA CHA HABARI

Hoja ya Zitto yatupwa; asimamishwa KUHUDHURIA VIKAO VYA BUNGE

TUWE WAZALENDO KIDOGO TUSIANDIKE NA KUCHANGIA HOJA KWA ITIKADI TANZANIA YOTE NI YETU NA ZITTO TUNAOMBA UNAPOJIBU HOJA USITUMIE MICHANGO YA MITANDAO KAMA FORUMS AU CHATROOMS FANYIA TAFITI MAJIBU YAKO AU ULIZA KABDA HUJAKURUPUKA

AHSANTE
 
shy... amesimamishwa shughuli za Bunge...ndio maana hawajamkata posho ya vikao tu wamekata mshahara wake kwa miezi mitano ijayo. Kwa kifupi, Zitto hawezi kufanya shughuli zake kama Mbunge.
 
ZITTO TUNAOMBA UNAPOJIBU HOJA USITUMIE MICHANGO YA MITANDAO KAMA FORUMS AU CHATROOMS FANYIA TAFITI MAJIBU YAKO AU ULIZA KABDA HUJAKURUPUKA

AHSANTE

Kama unafahamu ni chartroom gani amedesa hiyo hoja naomba utupe reference na sisi tusome kabla hatujahukumu kati yako na wewe...na kama ni hapa JF, link?
 
Mimi naona hapa kuna maswali mengi sana ya kujibu kabla ya kukimbilia kusema waziri alikuwa right :

Waziri anaonekana ya kuwa alikuwa na wasi wasi kuwa thamani ya gold inaweza kupungua siku za usoni , je ni vigezo gani alivyotumia kufukia huo uamuzi ? Pili kama kuna mtu yoyote anayejua ukuaji wa thamani ya gold in relation to american dollar katika kipindi cha miaka mitano atupatie ili tuone kama kuna uwiano wowote na yale yaliyosemwa na waziri.

Barrick has made a windfall profit and its share value has gone up in multiples because of the profits they have made in Tanzania. Gold value has more than doubled in the last 10 years. But because of the useless contracts that the goverment has etended into with these mining companies there has been no upward adjustments to the goverment earnings from our gold. This is the main reason for them refusing to make public these contracts.
 
Mheshimiwa Zitto afanyiwa bonge la pati

2007-08-16 19:18:08
Na Ramadhan Mbwaduke, Dodoma


Ingwa mbunge wa Kigoma Kaskazini Mheshimiwa Zitto Kabwe amefanyiwa kitu mbaya kwa kusimamishwa kazi kwa muda, lakini amini usiamini, usiku wa kuamkia leo, alibebwa juu juu kama shujaa katika bonge la pati aliloandaliwa kupongezwa kwa ushujaa alioonyesha katika kutetea maslahi ya taifa.

Sherehe hiyo ya `kufa mtu` imefanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Dodoma Hoteli, mjini hapa na kuhudhuriwa na vigogo kibao wa kambi ya upinzani na wengine `wanaojiita wana harakati`.

Waliohudhuria sherehe hiyo wanasema walikula, kunywa na kusaza.

Wakiongea kwenye sherehe hiyo, baadhi ya wabunge wa kambi ya upinzani walisema wamefikia uamuzi wa pamoja wa kumlipa
Mhe. Kabwe mapesa yote atakayoyakosa katika kipindi chote alichosimamishwa.

Wakasema kwa kuanzia, watamdakisha Sh. Milioni 1.5 kila mwezi, kwa lengo la kuziba pengo la kipato alichopoteza kutokana na kuadhibiwa kwake.

`Kama ulikuwa unakula mchemsho, sasa utaanza kula rost (nyama ya kukaangwa), kwani kambi ya upinzani iko pamoja na wewe,` alimwambia mheshimiwa mmoja.

Mbali na sherehe hiyo, chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, ambacho Mhe. Zitto anakiwakilisha Bungeni, kimeandaa mapokezi makubwa punde atakapotia timu Jijini Dar es Salaam.

Pia wapinzani watajimwaga katika viwanja vya Jangwani kutema cheche zao na kueleza kile kilichotokea hadi mheshimiwa Kabwe akakumbwa na kibano hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini, Mkurugenzi wa Vijana wa CHADEMA, Bw. John Mnyika alisema Mhe. Kabwe anastahili mapokezi kwa vile ni shujaa na ni watu wachache wenye ujasiri kama wake.

Mheshimiwa Kabwe alisimamishwa jana kujihusisha na shughuli za Bunge hadi mwezi Januari mwakani, kwa madai kuwa alisema uongo Bungeni.

Mbunge huyo machachari alipewa adhabu hiyo kwa kupigiwa kura na wabunge, baada ya kuwasilisha hoja binafsi bungeni, akimtuhumu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Nazir Karamagi kwa kusaini mkataba wa madini na kampuni ya Barrick Gold akiwa huko majuu.

Katika madai yake Mhe. Kabwe aliliambia Bunge kuwa Waziri Karamagi alisaini mkataba huo nchini Uingereza, kinyume na taratibu, na kutaka tume huru iundwe na Bunge kuchunguza mazingira ya kusainiwa kwa mkataba huo.

SOURCE: Alasiri
 
Kama unafahamu ni chartroom gani amedesa hiyo hoja naomba utupe reference na sisi tusome kabla hatujahukumu kati yako na wewe...na kama ni hapa JF, link?

..we acha!

..mitazamo ya watu wengine ni kama ya wale wabunge!

..we mbunge anaweza pata issues kwenye chatrooms? hicho ni kichekesho!

..hawezi toa refs!
 
..kwahiyo tupige makofi kama wale wabunge? kwani alikuwa anatoa ngonjera? usanii mtupu!

..hoja hapa haiko kwenye kupangua au kujibu!

..hoja iko kwenye wizi wa mchana wa maliasili yetu,ilhali hali zetu taaban!

..hili si suala la partisanship bali national interests!

Vichekesho...
So asingejibu? Then ingekuwa HOJA?
 
Hiyo consesus umefikia wewe mwenyewe au imefikiwa na kikao cha halmashauri ya chama....?

Watu hawafanyi uchambuzi kwa mwonekano bali kwa facts... maneno na styles nyingi kisha unatumia lugha ya mwonekano....

Huo mwonekano ni wako na wala Zito hana chuki na uelewa mdogo kama unavyotaka kudai hapa....

Grrrrrr...... jipange zaidi

Bibie...kila mtu ana mtizamo wake. Hujakatazwa kuleta views zako. Wewe ndio unahitaji kujipanga badala ya kusaga meno.
Whether you like it or don't like it, he was defeated on the FACTS. Vitu viko wazi, hakuna siri.
 
Bibie...kila mtu ana mtizamo wake. Hujakatazwa kuleta views zako. Wewe ndio unahitaji kujipanga badala ya kusaga meno.
Whether you like it or don't like it, he was defeated on the FACTS. Vitu viko wazi, hakuna siri.

Sijui definition yako ya neno defeat lakini unahitaji kusoma zaidi matumizi na maana ya neno hilo kisha ukalihusisha na kesi ya zito hapa.....
 
Back
Top Bottom