The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

He was here to find partners for the Mchuchuma coal reserves . His intention, it seems, was to collect a good amount for himself from the Businessman here on the pretext of leasing out these coal reserves at a nominal cost.

This sounds like a case of utapeli... if it ever happened!
  1. If the author knew/suspected that "Karume's" intention was to collect money on the pretext of leasing the mines, as alluded in the letter, why didn't (s)he contact the Indian Police to have the person questionned?
  2. Why did the author choose Arushatimes as the place to report this incident?
  3. Why not contact Tanzania High Commision in India or the Tanzania Police to verify the identity of the person?
 
This sounds like a case of utapeli... if it ever happened!
  1. If the author knew/suspected that "Karume's" intention was to collect money on the pretext of leasing the mines, as alluded in the letter, why didn't (s)he contact the Indian Police to have the person questionned?
  2. Why did the author choose Arushatimes as the place to report this incident?
  3. Why not contact Tanzania High Commision in India or the Tanzania Police to verify the identity of the person?

Were you told this is the only forum s/he used? All I can tell is, it is the only one available here. And what makes you think this message is utterly confined here?
 
Were you told this is the only forum s/he used? All I can tell is, it is the only one available here. And what makes you think this message is utterly confined here?

I am responding to what is written on this forum. I cannot comment on something I have not seen/heard/read.

If you have extra information why not give it here!!
 
I am responding to what is written on this forum. I cannot comment on something I have not seen/heard/read.

If you have extra information why not give it here!!

But you are making a generalisation as if that is where it starts and ends. No room for benefit of doubt! Just re-read your questions, you will discover this loophole.
 
The Author of the e-mail is familiar with the internet version of Arusha Times. He may or may not be familiar with anything else in Tanzania. So, he reported it there in the hope that someone might shed some light on whether he was indeed dealing with the son of a president (former or otherwise).

Some years before that, someone else went to India and sold another business man there rights to process all uncut tanzanite from Tanzania. Who was that someone? He must have been another president's son, for it became more or less impossible for Mramba to reverse that arrangement later. You are probably aware of those details, Ndugu Demokrasia.

Why would the agent, presidents' son or otherwise, want to give away Mchuchuma for next to nothing? I fail to understand why anyone would be so corrupt as to not care about any benefits to Tanzania.

Who has the right sell our coal reserves at Mchuchuma? Should the people, through their parliament, have any say in the matter?

Augustine Moshi
 
Barrick kupasua jipu leo

Na Ramadhan Semtawa

SIKU chache baada ya kuibuka kwa mjadala wa utiaji saini mkataba wa madini wa Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi nchini Uingereza, uongozi wa Kampuni ya Barrick, umeamua kuvunja ukimya ambao leo unaweka hadharani mchakato mzima wa mkataba huo.

Mjadala wa mgodi wa Buzwagi uliibuliwa katika mkutano wa bunge uliomalizika na mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ambaye alihoji kwanini Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi aliamua kwenda kusaini mkataba nje ya nchi tena katika hoteli badala ya kutumia ofisi za ubalozi zilizopo Uingereza..

Baada ya kuibuliwa kwa sakata hilo, kumekuwa na joto kubwa la kisiasa nchini, hasa baada ya Kabwe kusimamishwa kuhudhuria mikutano ya bunge hadi Januari mwakani.

Kusimamishwa ubunge kwa Kabwe, kunaangaliwa na wachambuzi wa mambo kama kuliko ibua hasira na fikra zaidi za uzalendo kwa Watanzania, kuhusu kulinda na kutetea maslahi ya taifa lao ambayo ni pamoja na uchumi katika maliasili.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Meneja Uhusiano wa Barrick, Teweli Teweli, alisema uongozi umeamua kuweka bayana suala hilo ili kujenga imani kwa wananchi.

Teweli alisema siku zote kampuni yake imekuwa kimya kutokana na kwamba suala hilo, lilijadilwa bungeni.

Alisema tuhuma hizo zimepunguza hadhi ya Barrick, hivyo lengo ni kueleza wananchi ukweli wa mambo.

"Tumeamua kuzungumza ili kueleza wananchi mchakato ulivyokuwa na kurudisha imani yetu kwao," alithibitisha Teweli.

Sakata hilo ambalo limeongeza umaarufu wa Kabwe, sasa limekuwa ni kete kubwa ya kisiasa kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kujiimarisha Mikoani.

Kwa sasa viongozi wa ngazi za juu wa Chadema, akiwemo Kabwe, wako Mikaoni kujiimarisha na kueleza wananchi kuhusu jinsi maliasili za yao zinavyoporwa.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia amesema kwamba kwa sasa ni vema serikali ikaangalia upya sera za madini ili wananchi waweze kunufaika kuliko ilivyo sasa." Kwa sasa sera ya madini ina mapungufu hivyo ni bora sera hiyo ikaangaliwa kuliko kuanza kujadili watu. Napendekeza Watanzania wamiliki asilimia 40 na wageni ambao wanakuja na mtaji wapewe asilimia 60. Hali hii itafanya nchi na Watanzania waweze kufaidi rasilimali zao," alisema.

Maoni yangu ni kwamba pindi watakapoweka mambo hadharani basi ujue ndio CCM ipo katika hatua za mwisho katika uongozi wake ! Lets watch !
 
Controversial Buzwagi gold mine deal: Church leader gets a word in

SEBASTIAN MRINDOKO
Dar es Salaam

A LOCAL Christian church group has joined the fray in the growing national debate over the government’s handling of the country’s natural resources, particularly the vast mineral wealth apparently being monopolized and exploited by foreign mining conglomerates.

The director of the Undugu Association Tanzania & Family Chaplain Archdiocese of Dar es Salaam, Father Baptiste Mapunda, said yesterday that the ongoing debate on the controversial Buzwagi gold mine contract and irregularities in other mining contracts should be matters of grave concern to all Tanzanians.

’’It is high time that Christians and non-Christians in this country came out in public to reveal these evils in society, because they are not only against God's commandments but also breach our basic human rights,’’ said Fr. Mapunda in his sermon during Sunday prayers at the Sinza-based church.

He cited concerns raised by opposition Member of Parliament Zitto Kabwe (Kigoma North CHADEMA) over the manner in which the Buzwagi contract was signed by Energy and Minerals Minister Nazir Karamagi and Barrick Gold Corporation in London.

Fr Mapunda described Kabwe as a ’’prophet sent by God to proclaim the message of truth to all Tanzanians on how their resources are being snatched by a few unethical and corruptive political leaders.’’

He noted that most Tanzanians, including ordinary citizens and politicians, are too passive and appear afraid to speak out the truth.

’’I am a religious leader, not a politician. But as a Tanzanian priest and servant of God, I have a solemn duty to speak the truth at all times,’’ the leader of the church group told worshippers.

He said Kabwe had shown a true example of ’’courage and patriotism’’ worthy of emulation by all Tanzanians so that the majority of the people do not continue to live in abject poverty while a few greedy politicians throw away precious national resources.

According to Fr. Mapunda, corruption is not only a sin but it also denies people the right to a better life.

He joined a growing number of Tanzanians in condemning Kabwe’s suspension from the National Assembly for the rest of the year for calling for the formation of a parliamentary probe team to investigate the circumstances behind the Buzwagi deal.

’’A clean man and a man of God is always courageous to face the truth, and that’s why we all remain puzzled as to why parliament dismissed the call to form a Bunge committee to probe the Buzwagi gold mine contract,’’ he said.

Meanwhile, it has been learnt from reliable sources that Barrick Gold Corporation is planning to call a news conference this week to ’’clear the air on the Buzwagi gold mine contract.’’

Barrick Gold executives have already come out publicly in defence of Karamagi, claiming there was nothing wrong with the contract signed abroad and adding that the minister summoned them to London for the signing ceremony instead of the other way round.

The company’s executives made the remarks last week when President Kikwete visited the Buzwagi mining area during his tour of Shinyanga Region.

Kabwe has argued that the $800m contract was signed under dubious circumstances, based on outdated laws and regulations that are currently being reviewed by the government.

The opposition MP has maintained that the government itself declared in parliament last year that it had suspended the signing of any new major mining contracts until the ongoing review of existing contracts has been concluded.
 
Hoja ya Zitto yaigusa CCM
na Mwandishi Wetu

KWA mara ya kwanza, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimejitokeza na kutoa kauli kuhusiana na umaarufu anaoupata Mbunge wa Kigoma Kaskazini aliyesimamishwa, Kabwe Zubeir Zitto (CHADEMA).

Katika hatua ambayo haikutarajiwa na wengi, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Kapteni Jaka Mwambi, kwa mara ya kwanza ametoa kauli kuhusiana na suala hilo na kuwataka wanachama wa chama hicho kuwa makini na uzito wa suala lililoibuliwa na Zitto hadi kusababisha asimamishwe na Bunge.

Mwambi aliyasema hayo juzi Jumamosi, kabla ya kuanza kwa uchaguzi wa viongozi wa CCM ngazi ya Wilaya ya Kinondoni, uliofanyika ofisi mpya ya chama hicho iliyopo Kinondoni Mkwajuni.

“Zitto amekuwa Zitto, wapinzani sasa wamepata hoja, wametuzidi katika hoja, tunapaswa kuchagua viongozi walio bora ili (wapinzani) wasituzidi katika hoja.

“Inashangaza Zitto ambaye amepewa ‘red card’ bungeni kushabikiwa na idadi kubwa ya Watanzania wakiwemo wana CCM ambao walikwenda Jangwani kumlaki na kumsikiliza wakati akitokea Dodoma, ni lazima tukisafishe chama ili wapinzani wasije kutupiku,” alisema Mwambi.

Mwambi pia aliigeukia Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na kuituhumu kuwa sasa imekuwa tofauti na ya zamani.

Alidai kuwa jumuiya hiyo imekuwa chafu, hivyo inapaswa kujisafisha kwa kuchagua viongozi safi, watakaoifufua.

Huku akionekana kuwa makini na kauli zake, Mwambi alisema CCM sasa itakuwa makini na matajiri wanaowania uongozi ndani ya chama hicho kwa sababu wanaonekana chanzo cha tatizo la kuporomoka kwa maadili ndani ya chama.

Alisema yeye kama mwajiri wa viongozi wa chama hicho, hatasita kuwafukuza viongozi watakaobainika kuwa wanajihusisha na vitendo vya rushwa.

Aidha, Mwambi aliwashambulia waziwazi viongozi wa CCM wa Wilaya ya Kinondoni na kuwaeleza kuwa wanakitia aibu chama, na kutoa mfano wa kuvurugika kwa chaguzi kadhaa za chama wilayani humo kuwa ushahidi wa udhaifu wa viongozi hao.

Kadhalika, alisema kwamba endapo kutakuwa na wagombea watakaoshinda kwa kutumia hongo, wakigundulika nao watafukuzwa katika chama sambamba na kuvuliwa uongozi.

“Ole wao viongozi wanao panga safu ya watu kutaka chama kiwe na viongozi fulani kwa masilahi yao binafsi, nasema watashughulikiwa.

“Inashangaza kuona kiongozi anapanga safu yake, jambo hili haliwezekani, safu hupangwa na CCM na si kiongozi, hivyo tusiwaruhusu watu watupangie,” alisema Mwambi.

Mwambi aliendelea kusema kuwa ndani ya chama hicho kuna kinyamkela ambacho kinaweza kutoka kwa kuchagua viongozi madhubuti.

Katika uchaguzi huo, Aaron Yesaya Mwaikambo, alifanikiwa kutetea nafasi ya Mwenyekiti wa Wilaya ya Kinondoni.

Waliochaguliwa kuwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Kinondoni kupitia kundi la Wazazi ni Said Hemed Mkali na Alfred John Nchimbi.

Nafasi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa ilikwenda kwa Ahmed Mwilima, Asha Baraka, George Manyama, Clementina Mollel na Shy-Rose Bhanji.

Wengine waliochaguliwa kuwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa ni Janja Kibosa Janja na Azzan Ally Mangush. Nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu kundi la UWT, walichaguliwa Esther Mkandawire, Hafsa Mahinya Mtasiwa, Susan Alphonce Kolimba na Mary Enock Kalumuna.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya waliochaguliwa kupitia kundi la vijana ni Janeth John Sondoka, Furaha Kyesi, Vanessa Mugeta na Ashura Seng’ondo.

Wakati huo huo, Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Kiwanja cha Ndege mjini Dodoma, Padri Sospeter, amemfananisha Zitto na Yesu katika mahubiri yake ya jana Jumapili, na kusema kuwa mbunge huyo kijana anapaswa kuombewa ili Mungu amuongezee nguvu.

Muumini mmoja liyehudhuria ibada hiyo, aliliambia gazeti hili kuwa paroko huyo aliwataka waumini wa Kikristo nchini kote kumuombea Zitto ili apate ujasiri zaidi katika kutetea masilahi ya taifa.

Alisema kuwa anachokitetea Zitto ni haki, sawa na iliyotetewa na Yesu Kristo, ambaye alikufa akitetea haki kwa ajili ya kuwakomboa waumini wake.

Kutoka Kigoma, Mwandishi Wetu anaripoti kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, amemtahadharisha Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, kuachana na mtindo wa kununua wapinzani kwani unakipeleka pabaya chama hicho.

Dk. Slaa alitoa onyo hilo kwa nyakati tofauti jana wakati yeye, Zitto na viongozi wengine wa CHADEMA, walipokuwa wakifungua matawi 11 ya chama hicho mjini Kigoma, katika mwendelezo wa falsafa ya ‘CHADEMA ni Matawi.’

Dk. Slaa alibainisha kuwa kununua wapinzani si njia muafaka ya kuimarisha chama kwani kwa kutumia njia hiyo utawapata watu wengi ambao shida yao ni fedha.

Alisema kuwa watakaojiunga hawatakuwa na mapenzi ya dhati kwa chama kwani watavutiwa na fedha ambazo zinatumika kuwanunua na jambo hilo halitakiimarisha chama hicho.

Katika kampeni hiyo ya jana, ambayo kimsingi inalenga kukiimarisha chama hicho tangu ngazi ya chini, ilishuhudia ufunguzi wa matawi hayo 11, likiwemo tawi maarufu mjini Kigoma lijulikanalo kama Urusi.
 
Ziara ya Zitto yaamusha gumzo Mwanza

2007-08-27 08:43:17
Na Juma Ng`oko, PST Mwanza


Taarifa za kuwasili jijini Mwanza kwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Bw. Zitto Kabwe, zimeamsha gumzo la aina yake kwa maelfu ya wakazi wa Jiji la Mwanza� pamoja na Wilaya za jirani.

Wananchi wengi wakiwemo wanachama wa Chama Cha �Mapinduzi (CCM), wameonyesha shauku na hamu kubwa ya kumpokea mbunge huyo kijana.

Mbunge huyo alisimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge hadi Januari, mwakani kwa kosa la kusema uongo bungeni wakati akiwasilisha hoja binafsi kuhusu kusainiwa hotelini jijini London mkataba wa mgodi wa Buzwagi.

Baadhi ya wakazi wa jijini hapa waliiambia PST kuwa, wako�tayari kutoa� hata michango ya �hali na mali, zikiwemo fedha na hata magari� ili kuhakikisha Bw. Kabwe � na viongozi watakaofuatana� naye� wamefanikisha ziara hiyo.

Bw. Kabwe anatarajia kuwasili mkoani humu Septemba Mosi, mwaka huu.
�
` Mimi nasema�kwamba Septemba Mosi ni mbali� mno� kwa� Kabwe�kuwasili�mkoani hapa, labda tu ni kwa sababu yeye hawezi� kujua�kwamba ni kwa kiasi gani�hoja na msimamo� wake Bungeni� vimekonga �mioyo ya wapenda maendeleo wa Mwanza,`�alisema� Bw. Beka Juma, mkazi� wa Nyegezi jijini hapa.

` Kwa kifupi �mimi�ingawa� ni mwana-CCM, lakini �niko tayari kuchangia�kwa namna yoyote ili kufanikisha �ziara ya Zitto hata kama�atakuwa tayari�kufika kesho kutwa,` alisema Bw. Beka.

Alifafanua kuwa,�anatarajia kumwona Bw. Kabwe�ana kwa ana lakini pia�asikie hotuba yake na ikiwezekana amwuulize maswali�kuhusu mkataba� wa madini ambao� ulisainiwa nje ya nchi.

`Labda� Zitto anaweza kutupatia majibu� ya maswali yetu� ya muda mrefu, kwa sababu� viongozi wetu CCM na hata serikali yake,� imekaa� kimya� juu ya jambo hilo� muhimu ambalo� kimsingi ni kwa maslahi ya taifa,` alifafanua.

Kwa upande wake,� mmoja wa viongozi wa �serikali ya mtaa� wa�Uhuru�jijini (CCM ) (ambaye hakutaka jina lake litajwe), alisema�uamuzi uliotolewa bungeni dhidi ya� Bw. Kabwe, umeongeza umaarufu wa viongozi wa vyama vya upinzani hususan CHADEMA.

`Ni�vigumu��Bunge kuomba�radhi,�lakini matokeo yake� yatawagharimu�kwa sababu�wabunge wetu� walisahau kuwa ni wawakilishi wa wananchi. Na�pia wanadhani kuwa Watanzania� bado tumelala�kama ilivyokuwa enzi za chama kimoja,` alifafanua.

Alisema� ikiwezekana yeye atakuwa miongoni mwa watu watakaojitokeza� kwa ajili ya kumpokea�Bw. Kabwe mkoani hapa.

SOURCE: Nipashe
 
Ni furaha iliyoje kuona wapenda wenye nchi wakianza kuamka kudai haki zao. Ukweli wahenga walisema 'wakati ni ukuta'. Enzi za wanasiasa kuvuruga vichwa vya watu, na kutopanya mali zao bila idhini yao sasa zinaelekea ukingoni. CCM wanaweza kuhitimisha enzi hii katika nchi hii. Nawatakia mapokezi mema wana Mwanza ya kijana wao mwanamapinduzi wa kweli wa kizazi cha leo.
 
Hoja za Zitto (si hii ya Buzwagi tu), zimemfanya afahamike kitaifa. Kwenye mioyo ya Watanzania, Zitto ni kiongozi wa kitaifa. Anapendwa na kuaminika kwamba anatetea maslahi ya taifa. CCM imeshaanza kujenga hisia, kitaifa, kwamba haitetei tena maslahi ya wananchi.

Naomba Zitto, na CHADEMA kwa ujumla, wahoji vile vile Mkataba wa Kabanga Nickel Mine. Naona taarifa magazetini zinasema kwamba Barrick Gold wamekubaliana na kampuni ya Kichina iitwayo Xastra Nickel, kwamba Kabanga iwe 50% mali ya Barrick Gold, na 50% mali ya Xastra Nickel. Share yetu iko wapi?

Augustine Moshi
 
Hoja za Zitto (si hii ya Buzwagi tu), zimemfanya afahamike kitaifa. Kwenye mioyo ya Watanzania, Zitto ni kiongozi wa kitaifa. Anapendwa na kuaminika kwamba anatetea maslahi ya taifa. CCM imeshaanza kujenga hisia, kitaifa, kwamba haitetei tena maslahi ya wananchi.

Naomba Zitto, na CHADEMA kwa ujumla, wahoji vile vile Mkataba wa Kabanga Nickel Mine. Naona taarifa magazetini zinasema kwamba Barrick Gold wamekubaliana na kampuni ya Kichina iitwayo Xastra Nickel, kwamba Kabanga iwe 50% mali ya Barrick Gold, na 50% mali ya Xastra Nickel. Share yetu iko wapi?

Augustine Moshi

Kama alivyosema AM sie cha kwetu hapa ni nini?

The world's fourth largest nickel producer, Xstrata Nickel, and Barrick Gold joint venture Kabanga Nickel Mine in Tanzania's western region of Kagera is expected to become operational in 2011, the country's Commissioner of Minerals Dalaly Kafumu announced July 12.

A statement issued by Kafumu says construction of the mine is expected to begin in 2009 after the conclusion of feasibility studies currently being conducted by the diversified miner, Xstrata and Barrick Gold Tanzania - which has a number of ongoing projects in the country.

On February 15 this year, Xstrata announced that it was pumping in US$95 million in the 50:50 joint venture project, for the pre-feasibility study. In addition, media reports indicate that Xstrata had spent a further US$50 million to update the resource model of the Kabanga project as well as for preparation of an extensive scoping study.

The Kabanga nickel project, according to Xstrata, is among the world's most attractive undeveloped nickel sulphide deposits with a total estimated indicated resource of 9.7 million tonnes grading 2.37 percent nickel and a total estimated inferred resource of 36.3 million tonnes grading 2.8 percent nickel. This revised estimated is a notable increase from the project's previous estimate (inferred) of 26.4 million tonnes at 2.6 percent nickel.

A full feasibility study of the project is expected to be concluded in 2008. However recent tabloid reports in Tanzania indicated that Kabanga was among the many areas in the country which were heavily affected by illegal mining and that the country was losing millions due to the illegal mining.

But Minerals Commissioner Kafumu in his statement refuted the allegations saying what was taking place at the Kabanga mine was metallurgical testing which includes export of samples from the mine for testing. He said samples were being sent to the Lake Victoria mineral office in Mwanza town for inspection before an export permit was granted to the companies.

When fully operational, the Kabanga nickel project would provide employment to more than 2, 000 people.
 
Mwl

Share yetu ipo katika 50% ya Barrick........i.e. 3%
 
Sakata la Buzwagi, BoT lavuka mipaka ya nchi
*Mabalozi wa Jumuiya ya Ulaya wamwita Zitto, Slaa
*Walitaka maelezo ya kina kuhusiana na hoja zao

*Slaa asema taarifa ya hoja hizo zinasakwa kama lulu

*Zitto adai ufafanuzi wa Barrick wazidi kujichanganya

Kizitto Noya na Midraji Ibrahim
Kutoka Gazeti la Mwananchi

SAKATA la mkataba wa mgodi wa Buzwagi na madai ya ubadhirifu katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), umechukua sura mpya, baada ya mabalozi wa Jumuiya ya Nchi za Ulaya (EU) kuwaita faragha Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na yule wa Karatu, Dk Wilbroad Slaa kutaka kupata maelezo ya kina.

Habari ambazo Mwananchi imezipata zinasema kwamba Zitto na Slaa walikutana na mabalozi hao Ijumaa iliyopita majira ya saa nne katika ofisi za ubalozi wa Ubelgiji baada ya kuombwa kufika hapo kutoa maelezo ya kina kuhusiana na masuala hayo ambayo yamezua mjadala mkubwa nchini.

Kwa mujibu wa habari hizo zilizothibitishwa na maafisa kadhaa wa balozi hizo na kiongozi mmoja wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mabalozi hao walikutana na wabunge hao wa upinzani ambapo Balozi wa Ubelgiji, Peter Maddens, alikuwa mwenyekiti wa kikao kwa kuwa ndiye Rais wa mabalozi wa Jumuiya ya Ulaya nchini.

Katibu Mkuu wa Chadema, Wilbroad Slaa, alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, aliliambia Mwananchi jana kuwa mabalozi hao walimwita kuzungumzia mijadala tata kuhusu mkataba wa madini wa Buzwagi na suala la BoT iliyoibuka bungeni.

"Ni kweli mabalozi waliniita ili kuwapa taarifa za matukio ya Buzwagi na BoT, mtu yeyote ambaye anataka taarifa tutampa. Sasa vyombo mbalimbali duniani wanataka hizi taarifa kwa kina na sisi tukiombwa lazima tuwape kwa kuwa masuala haya yana maslahi kwa Watanzania wote," alisema Slaa.

Alipoulizwa kama katika kikao hicho walijadili nini, Slaa asliema asingependa kuingia kwa undani majumuisho ya mazungumzo yao na mabalozi kwani hapendi kuwagombanisha. "Ni vema wewe ukawauliza maana sisi tuliitwa ofisini kwao, wao ndio wanapaswa watoe taarifa, kama wangekuja kwetu basi sisi tungetoa taarifa," alisema.

Mmoja wa maafisa wa ubalozi wa Ubelgiji ambaye hakutaka jina lake litajwe, aliiambia Mwananchi juzi kuwa kikao hicho kilianza saa 4.00 asubuhi, baada ya Zitto kuwasili katika ofisi za ubalozi huo akiambatana na Dk Slaa.

“Kikao kilianza majira ya saa 4.00 asubuhi ambapo Zitto alikuja akiwa ameambatana na Mbunge wa Karatu, Dk Wilbroad Slaa,” alisema afisa huyo.

Jitihada za gazeti hili kumpata Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe jana kuzungumzia suala hilo, zilishindikana baada ya simu yake ya mkononi kuita bila majibu.

Mwananchi ilipowasiliana na Balozi wa Ubelgiji, Maddens hakukataa wala kukubali kuendesha kikao hicho siku ya Ijumaa, ingawa alikiri kuwa ni utaratibu wa kawaida kwa nchi za Jumuiya ya Ulaya kukutana na watu wa kada mbalimbali katika nchi wanazoziwakilisha kujadili masuala ya nchi husika.

“Mpango wa nchi za Jumuiya ya Ulaya ni kukutana na mtu mmoja mmoja au vikundi vinavyohusika na masuala ya siasa. Ni mpango wa kawaida kwa nchi zetu kokote duniani, mikutano hiyo hatuijadili hadharani,” alisema.

Kauli ya Balozi huyo iliungwa mkono na Afisa Habari na Siasa wa ubalozi wa Uingereza, John Bradshaw, aliyesema kuwa siyo kawaida kwa nchi hizo kujadili masuala ya siasa hadharani.

“Ni utaratibu wa kawaida kwa balozi za nchi za Ulaya kukutana na watu mbalimbali ikiwamo wanasiasa ila sina hakika kwamba wana tabia ya kujadili mikutano ya aina hiyo,” alisema Bradshaw.

Habari zingine zinasema baada ya mabalozi hao wa nchi za Ufaransa, Ubelgiji, Uingereza, Uswisi na Ujerumani kukutana na wabunge hao mwishoni mwa wiki, waliweka miadi kukutana na Spika wa Bunge, Samwel Sitta jana.

Sakata la mkataba wa mgodi wa Buzwagi na Benki Kuu limekuwa likiibua hisia za watu hasa baada ya Bunge kumsimamisha kazi Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kwa madai ya kulidanganya Bunge. Zitto atarejea bungeni mwezi Januari mwakani.

Wakati huo huo, Zitto amesema majibu yaliyotolewa na Kampuni ya Barrick yanachanganyana na yale ya serikali na kwamba, inazidi kudhihirisha kuwapo kwa mchezo mchafu katika kusainiwa kwa mkataba huo.

Zitto alidai, kilichomshtua zaidi ni ujumbe ambao aliunasa siku tatu kabla ya Barrick kufanya mkutano na waandishi wa habari, ukitoka kwa Meneja Mkuu Mtendaji wa Barrick, Kitengo cha Sheria, Deo Mwanyika kwenda kwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi ukimuomba kupitia taarifa yao ili isipishane na serikali. Soma makala nzima ya Zitto Kabwe ukurasa wa 8.
 
zittokatooni.jpg

hee heee zitto huyo kawezwa, watu wanajilia vyao, au kwa lugha ya sasa wanajinafasi
 
State freezes IPTL 2007 capacity charge payments
CHARLES KIZIGHA
Daily News; Thursday,August 30, 2007 @00:02

THE government has decided to stop paying electric generation capacity charges amounting to over 20bn/- to Independent Power Tanzania Limited (IPTL) until a tariff dispute is resolved.

The Minister for Energy and Minerals, Mr Nizar Karamagi, told the 'Daily News' recently that the government has decided not to pay IPTL for the charges since last January because of serious discrepancy in tariffs. “We have been advised by experts that the charges were not okay. We will hold back until the matter is sorted out. Capacity charges involve huge sums of money. We cannot just continue paying. It is taxpayers' money,” Mr Karamagi said.

Tanzania Electric Supply Company Limited (Tanesco) Managing Director, Dr Idris Rashid said his company owed IPTL about 20bn/- in capacity charges and about 10bn/- for the energy bill. He said Tanesco was ready to pay for energy consumed but not for the capacity charges because they were now disputed. However, he could not say when they would settle the energy bill.

IPTL General Manager, Mr C. Parthhiban, said Tanesco’s debt amounted to about 31bn/- out of which about 21bn/- was for capacity charges and the balance for actual energy consumed. He explained that Tanesco paid all invoices for 2002 to 2006 after they were certified by a consultant, Dr Martin Swales. He claimed that it was the same consultant who also verified the now disputed bills for 2007.

State owned Tanesco and IPTL have had an uneasy business relationship for almost ten years now. In 1998, the parties went to the London based International Centre for Dispute Settlement with the government winning in a 2001 ruling Shillings 1bn tariff reduction per month.

Mr Karamagi said the government was prepared for another round of arbitration while Mr Parthhiban threatened it would suffer severe loss in terms of lost man-hours and other “uncalled for services.”
 
Mr. Zero

Please take your time ku-scan vichwa vya habari kabla ya kuposti mada.........hiyo habari tayari Chifu alishaiweka
 
Mr. Zero

Please take your time ku-scan vichwa vya habari kabla ya kuposti mada.........hiyo habari tayari Chifu alishaiweka


Sorry mzee, Sikuiona!! Naomba Administrator aiondoe!
 
Back
Top Bottom