The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

Nimejaribu kuweka dakika tano za kwanza za haya mahojiano.

Nitajitahidi kuweka kadri muda unavyokwenda..
 
jamani naombeni mnisaidie mie jinsi ya kupata hiyo channel ten manake nikifungua nasikia miziki tuu na inaonyesha ni ya kulipia, asanteni
 
jamani naombeni mnisaidie mie jinsi ya kupata hiyo channel ten manake nikifungua nasikia miziki tuu na inaonyesha ni ya kulipia, asanteni

Kijakazi inategemea uko wapi, sehemu zingine inagoma, hata mie nilipo siipati!
 
poa basi shukrani kwa hilo, yaani mfumo wa nchi yetu ungekua unafanya kazi kwa mpangilio na haraka kama hii jf basi tungekua mbali sana, yani unafuta kitu unakipata mara moja! lkn tutafika...
 
Namshukuru sana MH Lissu kwa kazi nzuri na ya ujasiri mkubwa ya kwenda mbele ya chombo cha habari na kufafanua sehemu tu ya mkataba wa Buzwagi kwa lugha nyepesi ambayo kila mtanzania anaielewa.
Namshukuru pia J Ulimwengu kwa kuendesha kipindi hicho.

Mimi huku Ughaibuni,UESIEI,nimekipata kipindi hiki kama vile nami naishi Vingunguti Dampo Neck of the wooods ya dar.

Pia nemefurahishwa kwa namna Lissu alivyo lijibu swali la msikilizaji mmoja kwamba namna ya kulitatua tatizo hili la mikataba ya ovyo ya serikali ni wananchi kusema basi na kukiri kwamba si lazima kusubiri siku ya kupiga kura kuna njia nyingine za kuiondoa serikali.
Hapo ni Patamu sana.

Penye Uchungu wa kukata maini ni hapa:

Migodi 6 ya Dhahabu kwa miaka 10 imezarisha $2,614,000,000,000.00

Serikali ya Tanzania imepata $ 78,000,000.00

Mapato haya ya Serikali kutokana na dhahabu ni 2.9%
Sidhani hata tukijumrisha fedha yote waliyo pokea RUSHWA mawaziri,wanasheria, watu wengine muhimu ndani ya serikali pamoja na Rais Jakaya Mrisho Kikwete mwenye itafika 5% ya Hizo Billioni 2.614.

Bank ya Dunia, Serikali ya Marekani hata Umoja wa mataifa wamsifiapo Rais JK wanaangalia Taarifa kama hizo.
Ukweli ni kwamba anayefaidi utajiri wa asili wa Tanzania ni Wezi wetu wale wale wa siku zote ambao leo hii katika ziara yake hapa nchini Marekani wanamvisha kilemba cha Manyasi(UKOKA) kwa misifa ya kukuza uchumi.

Ni kweli kwamba Sura yake na Suti vinamfanya aonekane ni Handsome boy wa nguvu lakini uchumi wetu hauko Handsome hata kidogo.

Najua kabisa serikali hii imewekwa na wajomba,shangazi, baba,mama,kaka na dada zangu walio sambaa kila kona ya nchi ambao wanaendelea kuipa nafasi SISIEMU kuiongoza nchi.
Wajomba zangu hawa wameshindwa kabisa kutambua kwamba hali zao duni za maisha zimetokana na maamuzi ya viongozi wa serikali waliyo iweka wenyewe.
Mpira umerudishwa kwao wenyewe waiondoe kama walivyoiweka.
 
Still waiting for MP3 files,

Namheshimu Lissu sana, lakini sina imani kwamba uchumi umezama kichwani kwake kwa hiyo nitakuwa mnafiki kama sitasema ninamwamini kwenye uchambuzi wa sheria kama contract/agreement, zaidi ya uchambuzi wa kwamba nchi imepata nini? in terms of ROI?, kwa kuwa hii haihitaji simple algebra kama wengi wetu wanavyoamini... ni complex kiasi fulani...and sometimes it is easy kumpleka mtu mahali mchambuzi yeyote anapotaka!!!
 
Still waiting for MP3 files,

Namheshimu Lissu sana, lakini sina imani kwamba uchumi umezama kichwani kwake kwa hiyo nitakuwa mnafiki kama sitasema ninamwamini kwenye uchambuzi wa sheria kama contract/agreement, zaidi ya uchambuzi wa kwamba nchi imepata nini? in terms of ROI?, kwa kuwa hii haihitaji simple algebra kama wengi wetu wanavyoamini... ni complex kiasi fulani...and sometimes it is easy kumpleka mtu mahali mchambuzi yeyote anapotaka!!!


Mzee kilitime, hapa ni data tu!

We shuka ROI zako hapa zinazo tuonyesha tunavo faidika na hayo madini yetu! hapendwi mtu hapa ni facts tu mkuu!
 
Hey JF Members.

Am just trying to breakdown everything. ili iwe rahisi kwangu kuupload.

Bellow are the next 10 minites.
 
Poor Jenerali he was craping in his pants.he is soo scared they might lock him up.But Tundu ni dume haswa.If only there were another Ten Tundu Liso we would make headway in liberating this country from the hands of hawa Mafisadi
 
Jambo la kuongeza urefu wa mkataba, halina issue yoyote asipende kutufanya kwamba watu wapumbavu kwani baada ya miaka 25 Karamagi atakuwepo?
 
Uchambuzi huu umemfanya hata J Ulimwengu kushindwa kuuliza maswali kwani alifika mahali yeye mwenyewe akawa haamini anachosoma ndani ya mkataba.

Kuna mahali aliisoma sentensi kwa zaidi ya mara mbili na kuitafsiri kiswahili lakini bado maana iliendelea kuwa ile ile aliyo isema Lissu.

Kutokana na Uchambuzi wa MH Lissu sidhani kama maneno ya Rais Jakaya mrisho Kikwete ni ya kweli kwamba wanasheria wetu hawajui namna ya kuingia mikataba.

Maelezo ya Lissu yandhihirisha wazi kwamba mapungufu mengi katika mikataba yameongezewa au kupunguzwa kwa makusudi kabisa.
Mtu,au kundi la watu ndani ya serikali haliwezi kukubali kuikosesha mapato serikali kwa kwenda kinyume na katiba na kanuni za nchi bila kupata faida binafsi.

Watendaji wa serikali ya SISIEMU wameingia mikataba hii mibovu si kwa kushindwa kuelewa kilichomo ndani ya mikataba, ila ni kwa kuandika makusudi mikata inayo wapa Uhuru wawekezaji kuiba mali asili ya nchi leo, kesho na siku zote wakati vilembwe wao watakapo kuwa viongozi wa nchi.

Watendaji wa serikali wameweza kuingia mikataba mibovu kwa kuneemeka wao binfsi.

Tusichokijua mimi na wewe ni kiasi cha fedha au thamani ya mali waliyopewa na wawekezaji ili waiuze nchi yao.

Hata watemi walioingia mikataba na Karl Peters wengi walifanya hivyo kwa kipengere cha Rushwa kilichosema, Mfalme wa ujerumani atakupa ulinzi dhidi ya maadui zako(Makabila allokuwa akipigana nayo vita), jambo ambalo baada ya muda mfupi watemi hao hao walibaini si kweli.

Leo hii Karne ya 21 Mawaziri wasomi wanao jua fika maana ya Ukoloni Mambo Leo wanaingia mikataba ya Kichawi na mkuu wa nchi Jakaya Mrisho Kikwete,Mchumi,anawatetea kwamba hawajui kuandika mikataba?

Kikwete anasema Uongo Chama chake SISIEMU kinasema Uongo serikali yake inasema uongo.

KIKWETE and his Government Must Go
Uongo utawaangamiza wao binafsi na serikali yao.
 
labda sijui, lakini anayoclaim mengine hayana msingi wowote! sorry to say, tunaomba mkataba kama uko wazi uletwe hapa tuchambue, pamoja na kwamba sisi mambumbu! do you think ungekuwa investor ungewaachia serikali wabadilishe kanunu za mkataba kila kwenye bunge la budget au kila mwezi!

Issue ya kwamba ati baada ya miaka 25, Waziri anaweza kuongeza miaka zaidi ya 25 tofauti na sheria,,, pia... hiyo mimi siiamini kwa sababu moja kuu, mikataba yote inakuwa na kipengele kwamba sheria za nchi husika zisivunjwe ikiwa pamoja na sheria hiyo ya madini,,, kwa maana waziri hatakuwa na mamlaka ya kuongeza miaka zaidi ya 25... destination ya Lissu at the end of the day will be politics, tusubiri!!!
 
naona pointi kubwa ni ile ya manufaa ya mgoni, kama migodi sita kwa miaka 10 imetuingia milioni 78, je mgodi mmoja (ambao ni marginal kwa maneno ya mzee wa Siagi) kwa miaka kumi na mbili utaweza vipi kutuingia milioni 100 na zaidi?
 
mikataba yote inakuwa na kipengele kwamba sheria za nchi husika zisivunjwe ikiwa pamoja na sheria hiyo ya madini,,, kwa maana waziri hatakuwa na mamlaka ya kuongeza miaka zaidi ya 25... destination ya Lissu at the end of the day will be politics, tusubiri!!!

What a crap....

mikataba inatenguliwa hapa duniani all the time.. hata ile ya kibiashara na yenye vipengere kama hivyo...

Hapa USA kuna mikataba imetenguliwa baada ya congress kuingilia kati... wewe unaishi dunia ya wapi?
 
naona pointi kubwa ni ile ya manufaa ya mgoni, kama migodi sita kwa miaka 10 imetuingia milioni 78, je mgodi mmoja (ambao ni marginal kwa maneno ya mzee wa Siagi) kwa miaka kumi na mbili utaweza vipi kutuingia milioni 100 na zaidi?

Kweli hii ni hoja muhimu ya kuverify claims,,, nisingependa kuamini kirahisi mpaka nipate upande wa pili, especially from economics and not from a laywer, i could listen if it was from a mathematician at least!
 
Sasa kwa nini mkataba usiandikwe kwa kufuata sheria ya nchi kuhusu madini neno kwa neno?

Kulikuwa na haja gani ya Kuongeza kipengele kinacho toa fursa ya kukiuka kipindi cha miaka 50 ambacho kampuni inaweza ingia mkataba wa kuchimba madini nchini Tanzania?
 
Kweli hii ni hoja muhimu ya kuverify claims,,, nisingependa kuamini kirahisi mpaka nipate upande wa pili, especially from economics and not from a laywer, i could listen if it was from a mathematician at least!

kwani nani amekuambia kuwa Lusu amejiita economist .... mbona kuanzia upasi class ya Math 102 na ile ya econ 0095 unatangaza sana .....

huo upande wa pili ni kazi yako kuuleta na kuuchambua.. damn it
 
Back
Top Bottom