The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

Revealed: Details of the Buzwagi contract

SIGNATORIES: The minister, Nazir Karamagi (left), and Pangea Minerals Ltd representative Gareth Taylor, who is also executive general manager of Barrick Gold Tanzania Limited in-charge of operations
-Final draft prepared by experts was further 'amended' before signing in London

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

A KEY provision in the Buzwagi gold contract was deleted by hand at the controversial signing of the deal in London early this year, effectively exempting the Barrick Gold subsidiary handling the project from paying all taxes falling under the East African Customs Management Act of 2004.

According to the leaked contract seen by THISDAY, a sentence in Article 4.2 of the agreement � obliging the investor to pay the government any tax, duty, fee or other fiscal obligation under the EA customs union - was struck out of the final contract draft before signing.

The agreement for the development of a gold mine at the Buzwagi area in Kahama District, Shinyanga Region was signed by the Minister for Energy and Minerals, Nazir Karamagi, representing the Tanzanian Government on one hand, and Gareth Taylor of Pangea Minerals Limited - a subsidiary of Barrick Gold Corporation � on the other. Taylor is also the executive general manager of Barrick Gold Tanzania Limited in-charge of operations.

No witnesses on either side of the pact, signed in the UK capital on February 17 this year, were listed.

Under the terms of the agreement, the government is to grant a special 25-year mining licence to Pangea Minerals Ltd ''as soon as possible and in any event not later than 60 days'' after the Barrick Gold subsidiary lodges an application for such a licence.

The Buzwagi contract was signed at a time when the government was in the process of reviewing the various gold mining policies, laws and contracts in the country, with a view towards creating what has been officially termed a 'win-win' situation.

However, at least two independent sources familiar with the deal have told THISDAY that the signatories to the agreement - Karamagi and Taylor - amended the final draft by hand during the signing function in London.

It is now understood that the original contract, drafted by a team of experts from the Ministry of Energy and Minerals in Dar es Salaam, took into account the fact that the East African Customs Management Act of 2004 was in force and should be duly incorporated in the agreement.

But in what now appears to have been a surprise move, the key sentence was penned out with Karamagi's approval just before the signing.

''All other major mining contracts in Tanzania were signed before 2004 - that's why they don't fall under the East African customs union. But the Buzwagi contract is different because it was signed after the customs union came into force, and should therefore have fallen under the East African Customs Management Act,'' said one well-placed insider on the deal.

Under other fiscal terms of the agreement on the same Article 4 provision, Pangea Minerals Ltd would be required to pay the (Tanzanian) government ''a royalty at the rate of 3% on the Net Back Value of all minerals produced from the Contract Area, other than diamonds, in respect of which the royalty shall equal 5% of the Net Back Value.''

The company is also legally bound to pay the government ''stamp duty under the Stamp Duty Act No.20 of 1972, as in effect on the Fiscal Stabilization Date,'' and $125,000 by December 31 of every year of production as a contribution to the state's Empowerment Fund.

On payments to local government, the agreement stipulates that the rates and taxes should not exceed those generally applicable in Tanzania; should not be based on profit, turnover, sales or output from mining operations; and should not be based on the value of land used for the mine, mining infrastructure or installations.

This, however, is provided that the aggregate of such rates does not exceed $200,000 in any one calendar year.

The signing of the Buzwagi contract in London has raised a lot of controversy with opposition Member of Parliament Zitto Kabwe (Kigoma North-CHADEMA) demanding a parliamentary probe into the deal.

For all his insistence, the MP ended up being suspended from parliamentary duties. But this somewhat bizarre turn of events only served to gift the political opposition camp with a popular platform to further advance their convictions on the subject of mismanagement of the country's natural resources.

Minister Karamagi has endeavoured to defend himself on the Buzwagi affair, claiming that there were no irregularities involved and maintaining that the agreement signing was fast-tracked to meet strict funding and production schedules.

Barrick Gold Tanzania Limited has also sought to clear the air over the deal, asserting that there was no wrongdoing involved as suggested by opposition politicians.

The company's executive general manager (corporate and legal affairs), Deo Mwanyika, told a news conference in Dar es Salaam recently that the agreement was pre-approved by relevant government authorities in the country after 'thorough negotiations' spanning a period of about eight months.

''(During the negotiations) we were asked to give very detailed presentations to the government's advisory committee on minerals, which has the legal obligation of advising the minister of energy and minerals on matters related to minerals development and mines,'' said Mwanyika.

It is further noted that although Barrick Gold officials have claimed the agreement was signed in the presence of Tanzania's High Commissioner to the United Kingdom, Ms Mwanaidi Maajar, her signature does not appear anywhere in the document, as a witness or otherwise.

This is despite the fact that Ms Maajar herself is also a well-known lawyer.

The Buzwagi area has proven and probable gold reserves of around 2.64 million ounces, where Barrick Gold has announced plans to invest up to $400m (approx. 520bn/-) for mine development purposes.
 
I guess in june i post a forum concern this non sense contracts that Tanzania leaders are puting the country in to. Now we will see what is the reaction from Karamangi and JK after the leakage of the contract? He need to answer why they subsize this Gold company? why they even gave them tax brake? Can someone ask this Nazis about where they take us to?

While Mr JK is enjoying NY environment, the result of smart monetery system, intelligent fiscal policy, and modernized private properties rules, and good utilizing of tax payer money, does he ask him self where is Tanzania going, and where it have been? Or he just order nice break fast, lunch and dinner and tend to forget what he promise to mum and pap in Tanzania?
 
Na kabla ya hata kuona mkataba wenyewe ni budi kujua kwamba huu ndio ukoloni mamboleo ambapo viongozi wachache wa Tanzania na Afrika kwa ujumla, wanatumika kuvuja mali za bara letu tukufu la Afrika kwa kusaidiana na matajiri (capitalists) ambao huja na makampuni yao makubwa "corporates" na "multinational companies" kwa lengo la kuchota na kupeleka kwao kwa ajili ya ku-process na kuuza kwa bei ya juu hivyo kupata faida kubwa mno.

Juzijuzi niliangalia duka la kwenye TV linaitwa QVC na kushangaa bei ya Tanzanite ile "Premier" ni si chini ya £200 stelling na sijui sisi tunakata vipi kodi.

Nenda link hii ya chini na uone jinsi madini haya yanavosifiwa:

http://www.qvcuk.com/ukqic/qvcapp.a...7Cukhtml|U119_about,html/walk.yah.UKJE~7EU119

Ni mpaka pale wale wote wanaoongoza kwa kuchukua 10% watakapofikishwa mahakamani kwa ufisadi ndio tutajua Tanzaia iko safi.

Mimi naiheshimu sana kauli ya Aung San Suu Kyi inayosema:

"It is not power that corrupts but fear. Fear of losing power corrupts those who wield it and fear of the scourge of power corrupts those who are subject to it."

Aung San Suu Kyi ni mwanamke mwanaharakati wa usawa kule Burma,kwa sasa yuko kizuizini tokea mwaka 2003.

Lakini sasa wananchi wa Burma wamechoka na mpaka sasa nipo mitamboni idadi yao wanaoandamana imevuka 100,000 kwa ajili ya kudai haki sawa na maisha bora.

Burma ni nchi iliopata uhuru mwaka 1948! Hadi leo hii wanachi wake wanavaa mashuka wakiabudu "Budhiism" ingawa bado najiuliza maana halisi ya dini hii.

Burma ina utajiri wa kuanzia ardhi yenye rutuba,mafuta,mpira,mbao iitwayo "Teak" ambayo hutumika kutengeneza mbao za urembo iwe katika sakafu au milango.

Pia Burma ikiwa chini ya utawala wa Kiingereza ilikua ikiongoza kwa kusafirisha mchele duniani!,gesi asilia,madini,chuma na malighafi za ujenzi.

Lakini hadi leo nchi hii ni moja ya nchi maskini duniani kwa sababu tu ya watu wachache ambao ndio wanafaidi.

Maliasili ya nchi yoyote ile ndio chachu ya watu wake kuwa na akili,maisha bora, mahala pazuri pa kulala na uhakika wa kusomesha watoto.

Pia maliasili ni utajiri wa wananchi wote na suala lolote lile kuhusu maliasili hio hasa kwa wananchi waishio pahala penye maliasili hio ni lazima washirikishwe.
 
Siri ya Buzwagi
Wapinzani kuuanika kesho

na Mwandishi Wetu


MKATABA wa uchimbaji wa madini wa Buzwagi uliozusha mabishano makali wakati wa kikao kilichopita cha Bunge hata kusababisha kusimamishwa kwa uwakilishi wa Kabwe Zitto, kwa miezi mitano, umevuja.

Kuvuja kwa mkataba huo uliosainiwa Februari 17 mwaka huu, hatimaye kumeweza kufichuka kwa siri ya kile ambacho kilishindwa kubainika kabla na baada ya Zitto kuwasilisha hoja binafsi bungeni ya kumtuhumu Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, kwa kulidanganya Bunge, hatua ambayo iligeuka na kumtia matatizoni mbunge huyo mdogo kuliko wote wa kuchaguliwa.

Habari za uhakika kutoka ndani ya kambi ya upinzani ambayo imeushikia bango mkataba huo zinaeleza kuwa, kuvuja kwa mkataba huo kumewawezesha kubaini mapungufu makubwa yaliyomo ndani ya mkataba huo ambayo kiongozi mmoja wa juu wa upinzani ameyaeleza kuwa hatua muhimu katika kuthibitisha mkweli kati yao na serikali.

Kwa mujibu wa habari hizo, tayari kamati maalumu ya kambi ya upinzani inayohusisha watu wenye taaluma mbalimbali wakiwamo, wachumi na wanasheria, wameishaupitia mkataba huo mzima wenye kurasa 24, uliosainiwa na Waziri Karamagi kwa upande wa serikali na Gareth Taylor wa Pangea Minerals Ltd, ambayo ni kampuni tanzu ya Barrick Gold Corporation ya Canada.

Katika kufanikisha malengo yao, wapinzani kupitia katika kamati yao hiyo mahususi, imeainisha maeneo kadhaa yenye mapungufu makubwa yaliyo katika maeneo sita, ambayo yanaonyesha namna mkataba huo unavyoliumiza taifa zaidi ya kulinufaisha.

Moja ya mapungufu ya haraka haraka yanayoonekana ni ukweli kwamba, wawekezaji hao katika kipindi chote cha mkataba hawatalazimika kulipa kodi kwa halmashauri na serikali kuu, ambazo zinazidi viwango vya sehemu nyingine nchini na ambazo zimetokana na faida, mauzo au uzalishaji unaotokana na uchimbaji madini.

Pamoja na ukweli kwamba wawekezaji hao watalipa dola za Marekani zisizozidi 200,000 kwa mwaka kwa halmashauri, na serikali kuu hawatalipa kodi zinazotokana na thamani ya ardhi inayotumika kama mgodi, kwa miundombinu ya uchimbaji madini au mitambo.

Miongoni mwa maeneo yaliyoainishwa kuwa yenye mapungufu yasiyozingatia masilahi ya taifa na ambayo yanaonekana kuwa na athari kubwa kwa uchumi wa taifa ni eneo la kodi ambalo linaonekana kuwa pungufu kuliko ilivyobainishwa na Waziri Karamagi bungeni.

Aidha, eneo jingine lililobainishwa na kamati hiyo mahususi, imebainisha kuwapo kwa upungufu mkubwa katika mkataba huo unaoonyesha kuwa, kiwango cha kodi kimekadiriwa kuwa kitakuwa kisicho na mabadiliko makubwa katika kipindi chote cha mkataba.

Kwa mujibu wa mkataba huo, ambao gazeti hili limefanikiwa kuuona, mafao mengi ambayo Karamagi aliyataja kuwa nchi itajipatia katika maelezo yake bungeni hayaonekani, hali ambayo inatarajiwa kuwa ajenda kuu ya kuishambulia serikali katika mkutano wao kesho.

Wapinzani katika uchambuzi wao huo wamebaini kuwa, vifungu vya mkataba huo vinaonyesha kwamba nje ya malipo ya mrahaba na kodi ya zuio, Serikali ya Tanzania, ikiwa ni pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Kahama unakojengwa mgodi huo, itakuwa inalipwa jumla ya dola za Marekani 583,980 kwa mwaka.

Kwa mujibu wa mkataba huo, baadhi ya kodi zitakazolipwa na Pangea Minerals, ni pamoja na asilimia tatu ya thamani ya madini baada ya kuondoa gharama za uzalishaji kama mrahaba kwa madini yote yatakayochimbwa eneo la Buzwagi isipokuwa almasi, ambayo mrahaba wake utakuwa asilimia tano.

Aidha, kampuni italipa ushuru wa stempu kama ulivyoainishwa na Sheria ya Ushuru wa Stempu Na. 20 ya Mwaka 1972 kuanzia tarehe ya kuanza kwa mkataba wa Buzwagi.

Hata hivyo, kuna uwezekano wa Pangea Minerals kutolipa hata senti moja kama ushuru wa stempu, kwani kifungu cha 5(1) cha Sheria ya Ushuru wa Stempu kimetoa angalizo kwamba "hakuna ushuru wowote utakaolipwa kutokana na waraka wowote uliosainiwa na, au kwa niaba au kwa taarifa ya Serikali." Ambapo kama kifungu hiki kisingekuwapo, basi Serikali ingekuwa na wajibu wa kulipa ushuru huo kuhusiana na waraka huo.

Pangea italipa pia dola za Marekani 125,000 kwa ajili ya Mfuko wa Uwezeshwaji zitakazolipwa kila tarehe 31 Desemba ya kila mwaka kuanzia mwaka wa uzalishaji.

Kwa mujibu wa mkataba huo, ‘Mwaka wa Uzalishaji' umetafsiriwa kuwa ni kipindi ambapo uzalishaji wa dhahabu safi au isiyosafishwa utafikia kiasi cha wakia 20,000, hivyo Pangea Minerals haiwajibiki kulipa kodi ya Mfuko wa Uwezeshwaji iwapo uzalishaji wa dhahabu hautafikia wakia 20,000 kwa mwaka.

Kwa ujumla, vipengele vya mkataba huo vinaonyesha kuwa kiwango cha jumla ya kodi zote ambazo Pangea Minerals italipa kwa halmashauri za wilaya au serikali za mitaa kwa ujumla hakitazidi dola za Marekani 200,000 kwa mwaka, tofauti na ilivyoelezwa na Karamagi bungeni.

Aidha, kampuni haitalipa kodi za halmashauri na/au serikali za mitaa ambazo zinazidi viwango vya sehemu nyingine za Tanzania na ambazo zimetokana na faida, mauzo au uzalishaji unaotokana na uchimbaji madini au ambazo zimetokana na thamani ya ardhi inayotumika kama mgodi, kwa miundombinu ya uchimbaji madini au mitambo.

Kwa mujibu wa mkataba huo, kampuni hiyo haitawajibika kulipa ushuru, ada au mchango wowote wa lazima zaidi ya vile ilivyoelezwa katika aya ya (iv) ya mkataba huo, isipokuwa kwa kodi, ushuru, ada au michango midogo midogo ambayo kwa pamoja haitazidi dola za Marekani 10,000 kwa mwaka.

Kampuni hiyo pia haitalipa malipo yatozwayo chini ya Sheria ya Madini au kanuni zake yanayozidi dola za Marekani 2,000 kwa kilometa ya mraba kwa mwaka.

Wapinzani wamebaini pia kwamba, Pangea haitalipa kodi ya matumizi ya barabara iliyowekwa na Sheria ya Kodi za Mafuta na Barabara ya mwaka 1985 itakayozidi dola za Marekani 200,000 kwa mwaka na kodi yoyote ya mauzo, matumizi au ongezeko la thamani, isipokuwa kama ilivyowekwa chini ya Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 1997.

Kama hiyo haitoshi, imebainika pia kwamba, Pangea Minerals italipa kodi ya zuio (withholding tax) kutokana na malipo kwa watu wengine kama inavyotakiwa na sheria husika, isipokuwa kampuni haitawajibika kushikilia kodi kwa kiwango chochote kutokana na malipo ya mkopo au deni la riba inayotakiwa kulipwa kwa fedha za kigeni kwa ajili ya mikopo, ikiwa ni pamoja na mikopo ya washirika wake, iliyokopwa nje ya Tanzania kwa ajili ya shughuli za uchimbaji madini.

Pia mkataba unaonyesha kuwa Pangea Minerals itaruhusiwa kukata asilimia 80 ya mtaji uliotumika kwa mwaka huo, na baada ya hapo itakata asilimia 50 kwa mwaka, isipokuwa tu kwamba Serikali ya Tanzania itatakiwa kufanya marekebisho ya sheria ili kuyafanya makato haya yakubalike chini ya sheria za Tanzania.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa mambo ya sheria, kifungu hiki cha mkataba kina maana kwamba endapo serikali haitafanya marekebisho ya sheria husika, basi Pangea Minerals itaendelea kukata asilimia mia moja ya mtaji uliotumika kwa mwaka wa kwanza.

Kwamba, mradi huo unaweza kuipatia Tanzania mamilioni hayo ya fedha, inatia shaka, kwa sababu kwa mujibu wa maelezo ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, Serikali ya Tanzania imepokea dola za Marekani milioni 78 tu kama mrahaba na kodi nyingine kutoka kwa migodi yote sita ya dhahabu ambayo inafanya kazi hadi sasa.

Kwa kiwango hicho, Buzwagi ambao Waziri Karamagi mwenyewe aliuita kama ‘Marginal Mine', yaani ‘Mgodi Mdogo' ni wazi kwamba matarajio ya serikali kuhusu manufaa ya Mgodi wa Buzwagi hayana msingi wowote katika hali halisi.

Aidha, mkataba huo una kipengele ambacho kinamlazimisha Waziri Karamagi kutoa leseni Maalumu ya Uchimbaji kwa Pangea Minerals ya muda wa kuanzia, wa miaka ishirini na mitano (25).

Mkataba unataka leseni hiyo kutolewa haraka iwezekanavyo na kwa vyovyote vile ndani ya muda usiozidi siku sitini (60) tangu Pangea Minerals kuwasilisha maombi yao ya Leseni Maalumu ya Uchimbaji.

Aidha, mkataba unaipa uhuru Pangea Minerals kuongeza muda wa leseni hiyo kwa masharti hayo hayo kwa miaka mingine ishirini na mitano (25).

Mkataba huo unairuhusu pia kampuni hiyo kuhamisha rasilimali ya taifa kwenda nje ya nchi (capital flight) kwa muda wote wa uhai wa mkataba.

Kuhusu manunuzi ya bidhaa na huduma, tofauti na alivyosema Karamagi, kifungu cha 7 cha mkataba kinasema: "Kampuni itatoa upendeleo wa kununua bidhaa na huduma zilizoko Tanzania, ilimradi bidhaa na huduma hizo zina ubora wa kimataifa, zinapatikana kwa wakati na idadi inayotakiwa na zinauzwa kwa bei ya ushindani zinapofikishwa Tanzania."

Vile vile kampuni kwa kushauriana na waziri itaweka utaratibu wa zabuni utakaowawezesha makandarasi kushindania zabuni hizo kwa kuangalia mazingira ya Tanzania, hakuna chochote katika kifungu hiki cha mkataba kinachoelezea kiasi cha fedha kitakachotumika katika kununua bidhaa na huduma ndani ya nchi na kama bidhaa au huduma zenyewe zitazalishwa Tanzania au zimenunuliwa nje kwa matumizi ya ndani.

Kwa upande mwingine, mkataba huo unaibana serikali kuhakikisha kwamba vifungu vya sheria vinavyohusu manufaa, haki na wajibu wa Kampuni na/au wanahisa wa kampuni hiyo, hazibadilishwi wakati wowote wa uhai wa mkataba.

Mkataba unairuhusu Pangea Minerals kuingiza Tanzania wafanyakazi wa nje, mashine, mitambo, magari ya usafirishaji na vifaa vingine muhimu kwa ajili ya ujenzi wa mgodi na uendeshaji wa shughuli za uchimbaji madini.

Kuhusu sheria itakayotumika, mkataba huo pamoja na kutambua sherisa za Tanzania, una kipengele kinachoongeza; "na taratibu za sheria za kimataifa zinazohusika."

Jambo hili limetiliwa nguvu zaidi na kifungu cha 13 cha mkataba kinachoamrisha kwamba mgogoro wowote "utatatuliwa kwa upatanishi kufuatana na Kanuni za Upatanishi za Tume ya Umoja wa Mataifa ya Sheria za Kimataifa za Biashara (UNCITRAL)."

Pili, mahakama za Tanzania hazina mamlaka ya kusikiliza na/au kutatua migogoro chini ya mkataba huu, kwani jukumu hilo imepewa "Mahakama ya Upatanishi ya Kimataifa ya London, kufuatana na kanuni za upatanishi za UNCITRAL, zitakazokuwa zinatumika wakati wa kusaini mkataba huu."

Tanzania Daima 25-09-2007
 
Inasikitisha! Unatamani mtu uangushe kilio. Viongozi wanasimama mbele ya majukwaa na kusema kwamba siku zote watatetea maslahi ya Tanzania kisha wanasaini mkataba kama vile ni mahayawani wasiojua mkataba huo hauna maslahi kwa nchi yao. Na wananchi wanapoomba kuiona mikataba hiyo wanakataa kata kata kwamba ni siri! Inakuwaje mali ya Watanzania iwe siri kwa wenye mali! Hawa wote ni wahujumu wa uchumi na hawastahili kuongoza Tanzania.
 
Having seen this, sasa napenda sana kujua kama kweli Kingunge ataendelea na maneno yake kuwa wapinzani wanaipaka matope serikali, au atafuta kauli hiyo.
 
Hivi jamani nisaidieni,
Mkataba umesainiwa ndiyo, lakini bado hawajaanza kuwekeza yaani kutumia hizo pesa zao, Hivi haiwezekani kuutolea nje kwa sasa na tusilipishwe fidia kwa vile haujaanza bado?

nasema hivi kwasababu, bado sioni tutafaidika nini hata huyo Karamagi akiwajibishwa, cha msingi hapa ni kubatilisha mkataba ili kabla mkenge haujafika mbali ama ndo haiwezekani tena??

Rwabugiri, ni vyema kama hawatawekeza, maana ninahisia kubwa kuwa wameanza kupata tetesi kuwa Watanzania hawakubaliani na huo mkataba wao waliojitungia na kumpatia peremende limbukeni mmojawapo ili au saini kwa nia ya Watanzania wote.

Wakijifanya wabishi na kuendelea kuwekeza watayaona yale yanayowakuta kule NIGER DELTA, Nigeria kwenye visima vya mafuta. Maana kila leo hii unasikia raia kutoka nchi fulani katekwa na shinikizo la kulipa juu mbele ili aachiliwe huru. Pamoja na kuwa katika Tanzania hili linaweza kuonekana far-fetched, lakini miaka 25 ni mingi, wataalam watapatika wakusuka mission za sabotage... wewe acha waendelee kuwekeza bila kusahihisha makosa yao katika mkataba. Ndipo utakapo jua kuwa Tanzania imebadilika na ina wataalam!!

SteveD.
 
Nimewawekea mahojiano yote yaliyofanyika jana ya Tundu Lissu na Jenerali.. tembelea KLH News International
 
Shukrani kwa watu wote wenye mapenzi mema na wananchi wa nchi hii. Natumaini huu hautakuwa mwisho wa kufunua uovu na maovu ambayo viongozi kwa nyazifa zao wanaamua kutulazimisha umasikini ambao sio staili yetu na kutufundisha kuwa nistaili yetu.

Hii inanifanya nikumbuke hadithi moja ya mtu masikini ambae kitu alichokuwa nacho kama mali yake ni bakuli la kuombea sarafu, ndio urithi wake kutoka kwa baba yake na babu yake.

Aliendelea kuomba kwa muda mrefu, pia kwa kutumia bakuli hilo hilo alioga na kulia chakula.

Siku moja akapita kwa sonara ili aombe, sonara akatupia sarafu kwenye bakuli aliposikia mlio akaomba aone bakuli.

Alipoliangalia na kulikwangua akamwambia yule masikini "Unaomba hali wewe sio masikini bakuli lako ni dhahabu safi una haja ya kuomba"

Tidu Lisu ametuonyesha bakuli letu ni dhahabu na jinsi gani viongozi kwa makusudi mazima wanataka bakuli letu wapewe wageni hali sisi tukiendelea kuomba.

Kuomba sio stahili yetu, hawa wanatulazimisha tuombe kwa nini?
 
Nafikiri kwenye hii mikataba kuna na kipengere kinachoikataza serikali kuiweka hadharani--yaani hata kama unaona umenyongwa shingo lakini jikaze baba. Sasa kama kuna hicho kipengere kumbe BARRICK ndo watakuwa wa kwanza kuipeleka mahakamani lakini si mahakama za Tanzania kwani hazina uwezo wa kisheria.

Ndo mambo ambayo JK alienda scandnavia akaishiwa cha kuomba ikabidi aaombe wataalamu wa kutusaidia kusaini mikataba. Nafikiri na wenyewe walimwona CHIZI NO.1
 
Habari ambazo zimenifikia sasa hivi ni kuwa Waziri wa Nishati na Madini Bw. Nazir Karamagi amekusudia kumfikisha Mahakamani Dr. Slaa, gazeti la Mwanahalisi na Printec wachapishaji wa gazeti hilo. Stay tuned.. hata hivyo watu wanaona kama amejiumbua.. hasa kufuatia maelezo ya Tundu Lissu
 
Namtakia kheri huko Mahakamani. Kama mambo yenyewe ndiyo haya......
 
Review ya JK ilikuwa danganya toto na ukweli ndio huo JK hawezi kufanya chochote hadi pale atakapojua kwamba WTZ wamechoka, hivi sasa inaonekana ni kelele tu za mlango. Swala hili la ardhi tuliliuliza hapa:
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=1747&page=13

Swala la wageni kutokulipa kodi tuliliuliza katika mada tofauti hapa:
”While the majority of huge consulting deals are taken by foreign firms, they usually deploy less than 10 per cent of foreign personnel to execute the job; while 90 per cent of personnel are locally sourced,” Prof. Katima said.

He said: ”Simple translation is that local experts do more jobs than foreigners, but foreign firms take away 90 per cent of the revenue. How can we fight poverty at this juncture?”

Hadi pale Wabongo watakapoamua na kusema tumechoka kuonewa na kudhulumiwa kile kidogo ambacho ni chetu. Kwa nini chetu kiwe chao na chao kiwe chao pekee? Rais amepewa madaraka makubwa sana na WTZ na ana uwezo hivi sasa wa kufuta mikataba yote na kuanza alifu. Kwa nini tuwapigie magoti watu wa kuja?
 
Wana JF wote Salut! Maana nadhnai ni jambo la heshima kuwasabahi magwiji niliwakuta hapa na kuwapa heko kwa michango yenu mizito na moto moto.

Nije kweje hoja, mimi binafsi naona kama akienda mahakamani, sijajua atakwenda kusema nini lakini kama ni suala la mkataba, itakuwa amefika mbali kuwapeleka wananchi waliomchagua mahakamani kwa kuhoji uadilifu wa utendaji kazi!

Inapofikia mahali unampeleka mwajiri wako mahakamani kwa kuhoji kiwango chako cha utendaji, hapo ninaona kuna mawili, mwajiri aondoke au wewe uondolewe kwenye ajira

Sasa hapo mnaweza kujua nani ameshika mpini na nani ameshikilia makali!
 
Patamu hapo! Tunasubiri kwa hamu. Lakini wasiwasi wangu ni kwamba inaweza kugeuzwa igizo kama lile la Jambazi Justin Nyari wa Arusha.
 
Habari ambazo zimenifikia sasa hivi ni kuwa Waziri wa Nishati na Madini Bw. Nazir Karamagi amekusudia kumfikisha Mahakamani Dr. Slaa, gazeti la Mwanahalisi na Printec wachapishaji wa gazeti hilo. Stay tuned.. hata hivyo watu wanaona kama amejiumbua.. hasa kufuatia maelezo ya Tundu Lissu

Duu.. tena akimbie haraka sana!

Ama kesi ikiwa mahakamani tutazibwa mdomo tusiiongelee tena? I mean itakataza vyombo vya habari visiandike tena juu ya hilo? isije ikawa jamaa anatafuta jinsi ya kutuliza huu moto wa kuwa kwenye front page ya kila news!
 
http://issamichuzi.blogspot.com/

BREKING NYUUUUUZZZZZZZZZ

waziri wa madini na nishati mh. nizar karamagi ametangaza sasa hivi hapa dar kwamba atamfikisha mahakamani mbunge wa karatu (chadema), mh. dk. wilbroad slaa kwa madai ya kumkashifu na kumchafulia jina lake baada ya kumtuhumu kwa ufisadi katika mkutano uliofanyika septemba 15, 2007 katika viwanja vya mwembeyanga temeke.


mh. karamagi, ambaye amewasomea waandishi taarifa hiyo hapo juu ofisini mwake, amesisitiza kwamba yeye ni muadilifu na ameamua kwend mahakamani ili kutafuta haki yake dhidi ya wale wote ambao amesema wameshiriki na wanaoendelea kushiriki katika vitendo vya kumpaka matope.


amesema ameshawaelekeza mawakili wake kufungua kesi mahakamani mara moja dhidi ya mh. dk. slaa, gazeti la mwanahalisi na kwianda cha printech ambacho anadai kilichapa matokeo ya gazeti hilo lililobeb kashfa hiyo.
 
Good move huu ubabaishaji wake utakwisha.
 
hata aibu hana,kama wenzake kina Mkono na Chenge wanaosadikiwa kuwa wanasheria mahiri wameiogopa mahakama yeye anafikiri atapata kitu gani huko?fine acha aende perhaps atafungua njia for more drama to unfold...now the political situation in bongo is taking a dramatic u-turn...kumbe kuleta mabadiliko huhitaji majeshi,na kundi la mafisadi nyuma yako,all you need is a little bit of Zitto Kabwe you add up with some Dr.Slaa and mix up with strong Tundu Lissu...the result everybody will be fighting for more of that democratic soup...
 
Back
Top Bottom