The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

k2kn5.jpg


Mambo yameanza. Karamagi at the press conference.


k1av0.jpg




Pictures: Credit Michuzi Blog
 
mie nadhani huu mkataba sasa upelekwe tena vijijini ili wakulima wauone,manaake mie nilikuwapo huku mwanza mwanzoni mwa mwezi huu katika kijiji kimoja nikawaeleza kuhusu mambo ya buzwagi..wananchi wakaniuliza "unataka kuchanganyikiwa"?.wanalalamika hawana barabara bora ila bado wanawasifia wasaniii,nikajua yatakuwa madhara ya Moshi wa Mwenge,na wenyewe upigwe marufuku manaake unatumika vibaya,pesa ya mwenge itumike kuhamasisha wakulima juu ya kilimo bora

...Bila Kuwaondoa Mafisadi nchi itayumba..
 
Mwafrika wa kike hapa naweza kupingana kidogo na wewe. Tanzania wanaopokea rushwa na wanaonunulika kirahisi ni mahakimu na sio majaji. Majaji waliowengi ni watu wenye msimamo wanajua wanachofanya. Lakini pia wakienda kinyume na serikali wanawekwa kando maamuzi yao huwa hayatekelezwi. Serikali yetu huwa inatunga sheria yenyewe kupitia wabunge wa CCM, na kuzitekeleza kupitia wabunge wa CCM na kuzivunja kupitia mawaziri wake. Kama utakumbuka hoja ya mgombea binafsi, pamoja na kuwa mahamaka kuu iliruhusu S. sitta wakati huo akiwa waziri wa sheria aliitolea nje.
tatizo ni kuwa mahakama Tanzania isipotendewa haki haina pa kwenda kushitaki, ndio maana serikali inafanya inavyotaka. Kama tungekuwa kwenye Privy coincil labda mahakama ingeheshimiwa kidogo.
Lakini hata hivyo still, naweza kusema sijui JK ameteua majaji wangapi na kama ni majaji wa mambo ya sheria au ni majaji wa siasa. Inawezekana kuwa wameshapiga mahesabau yao na sasa wanaanza utekelezaji wa kumsilence Slaa na upinzani.

Katika hili wewe uko right na wala sitapingana nawe hata kidogo..

the past experience ya maamuzi ya mahakama inanifanya niwe kinda of worried.... but yangu macho.... i hope and pray that you are right on this one
 
Nilitazama talk show hiyo aliyokuwa anahojiwa na Jenerali Ulimwengu. Lakini mabazazi wana tabia ya kutafuta maneno machache mtu aliyotamka na kuyatumgia kesi. Nilitazama na kusikiliza kwa wasiwasi pale Tundu alipotoa mfano wa wafalme wa Uingereza na Ufaransa waliokatwa vichwa na wananchi wao kwenye mapinduzi, basi Jenerali akawa anamng'ang'aniza "kwa hiyo unashawishi wananchi watende kinyume na katiba?".
 
.... i hope and pray that you are right on this one

I am hoping the same. Kwa sababu we have a system where de facto there is no separation of powers. Nadhani kuwa watakuwa wamekubaliana kitu ili kujaribu kuficha machafu yanayoendelea. Sina hakika kama kesi ya Nyari na Ditto zilifika kwa majaji, kama zilifika basi we should expect the same kwa Slaa. Nadhani Lissu atakuwa ameangalia legal implications za yote hayo kabla ya kusema hayo, kwa hiyo kutakuwa na defense nzuri.
 
kwanini waandishi hawakumponda na vitabu sababu ni mwizi kama walivyo wezi wengine,ndio maana jana TRA walienda katika gazeti la mwanahalisi..
kabla ya kuwashtaki hao wenye mdomo mkubwa(Mwanahalisi),kuna magazeti kibao yaliandika habazi za mafisadimbona hajayasema?aache chuki na gazeti la Mwanahalisi..
..Watu wameamka sasa,mie nina uhakika Muungwana amechoka kukaa na wasani wengi mabapo wengine wanamzidi ujanja,lazima akirudi atawatoa
 
HAKUNA CHA MAHAKAMANI WALA NINI.... Kwanza hata washauri makini walimwambia, "MZEE HILI NYAMAZA TU, HUNA CHA KUJIBU HAPA... HALAFU TIMING SI NZURI< LEO JAMAA WAMEMWAGA RADHI, THISDAY, KULIKONI NA TANZANIA DAIMA, UKIENDA WATAKUULIZA HAYO HAYO. HATA UKINYAMAZA WATAKULAZIMISHA HATA UTAKOHOA TU, NAO WATAANDIKA." lakini Karamagi akaenda na ikaelezwa kwamba alipata SHINIKIZO haya sasa. ANATIA HURUMA SANA
 
maindx9.jpg


SIGNATORIES: The minister, Nazir Karamagi (right), and Pangea Minerals Ltd representative Gareth Taylor, who is also executive general manager of Barrick Gold Tanzania Limited in-charge of operations

Chunga Mzigo wako!

Picture: Credit Thisday
 
Yote tisa, hilo la kufuta kipengele muhimu kwenye mkataba kwa mkono huko ugenini ndio funga kazi, nasubiri maelezo ya karamagi atakapofikisha kesi yake ya kashfa mahakamani...
 
Katika hili wewe uko right na wala sitapingana nawe hata kidogo..

the past experience ya maamuzi ya mahakama inanifanya niwe kinda of worried.... but yangu macho.... i hope and pray that you are right on this one

Uzoefu wa hivi karibuni unaonyesha wazi kuwa majaji wa tanzania hawana uhuru, ama wapewe shinikizo la kisiasa au la fedha, ni afadhali hakimu mla rushwa kuliko jaji mla rushwa..kwa hakimu kuna rufaa, sasa jaji akikunyima haki utaenda wapi...na kama wa rufa naye anapewa maagizo na EL utafanyaje, ...hali ni mbaya
 
haya ni maneno ya Mzee Mkapa
"Napenda tujikumbushe maana upo uwezekano wa wana-CCM kubweteka. Kwa vile tunajua chama chetu kina nguvu na mvuto, hatuweki mkazo mkubwa kwenye kujinoa binafsi. Badala yake tunapigana vikumbo kutafuta kuteuliwa, kwa kuamini ukishateuliwa ndio “umeula”. Na tukishaelekea huko, hakutakuwa na kingine kinachotusukuma ila ubinafsi—ubinafsi wa kusema mimi lazima niendelee, na anayenisogelea ni adui; au ubinafsi wa kusema wewe sasa imetosha, sasa ni zamu yangu."

hawa ndio wasaniii mabao mzee mkapa alikwishawaona nadhani utabiri umetimia,mambo ya Buzwagi ni matokeo ya "ukishateuliwa ndio “umeula”.

karamagi nenda ,ila Mzee Mkapa alitabiri mtakuwapo watu kama nyie,unasubiri nini Kusijiuzuru Uwaziri?

source:HOTUBA YA MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM), MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA, KWENYE MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA CCM, DODOMA, 25 AGOSTI 2004

Link:http://www.ccmtz.org/hotuba/040825nec.htm
 
haya ni maneno ya Mzee Mkapa
"Napenda tujikumbushe maana upo uwezekano wa wana-CCM kubweteka. Kwa vile tunajua chama chetu kina nguvu na mvuto, hatuweki mkazo mkubwa kwenye kujinoa binafsi. Badala yake tunapigana vikumbo kutafuta kuteuliwa, kwa kuamini ukishateuliwa ndio “umeula”. Na tukishaelekea huko, hakutakuwa na kingine kinachotusukuma ila ubinafsi—ubinafsi wa kusema mimi lazima niendelee, na anayenisogelea ni adui; au ubinafsi wa kusema wewe sasa imetosha, sasa ni zamu yangu."

hawa ndio wasaniii mabao mzee mkapa alikwishawaona nadhani utabiri umetimia,mambo ya Buzwagi ni matokeo ya "ukishateuliwa ndio “umeula”.

karamagi nenda ,ila Mzee Mkapa alitabiri mtakuwapo watu kama nyie,unasubiri nini Kusijiuzuru Uwaziri?

source:HOTUBA YA MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM), MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA, KWENYE MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA CCM, DODOMA, 25 AGOSTI 2004

Link:http://www.ccmtz.org/hotuba/040825nec.htm

mkapa naye mwizi tu .....
 
Hivi hao jamaa apo kwenye picha-nadhani 'wasaidizi' wa waziri...ndo wamemshauri aitishe mkutano na waandishi? Maana mi naona kama hili linaweza kuwa na athari mbaya zaidi kwake kuliko ilivokuwa kabla?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anakula viapo vitatu:



· Kiapo cha kwanza ni cha utii, ambapo anaapa kuwa atakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuitumikia kwa moyo wake wote, na kwamba ataihifadhi, kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;



· Kiapo cha pili ni cha Rais, ambapo anaapa kwamba atatenda kazi zake za Urais kwa uaminifu na kutimiza wajibu wa kazi hizo kwa bidii na moyo mkunjufu, na kwamba atawatendea haki watu wote kwa mujibu wa Sheria, mila na desturi za Tanzania bila woga, upendeleo, huba wala chuki; na,



· Kiapo cha tatu ni cha kudumisha Muungano, ambapo anaapa kwamba ataitetea na kudumisha umoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Hivi hao jamaa apo kwenye picha-nadhani 'wasaidizi' wa waziri...ndo wamemshauri aitishe mkutano na waandishi? Maana mi naona kama hili linaweza kuwa na athari mbaya zaidi kwake kuliko ilivokuwa kabla?

Halafu angalia body language ya wa kulia kabisa na kushoto kabisa.. as if they r saying "this really stupidity but I have to b here kulinda mkate wangu..."
 
If my memory serves me right, siku ile Mzee Mwanakijiji alipokuwa akimhoji Dr.Slaa, alipoulizwa kwanini hawawapeleki mahakamani hawa wanaodhaniwani mafisadi, alijibu kuwa mahakama zetu zina-stretch sana mambo, na hata wakipeleka madai haya mahakamani, itachukia miaka kadhaa kupata judgement. Hii ni kweli to the best of my knowledge.

Hivyo basi, Huyu Karamagi analeta tisha toto, maana anajua hata kama yuko guilty kwenda kwake mahakamani, itachukua muda kupata ufumbuzi. Na it won't be long, tutakuwa tunazungumzia maswala na ishu nyingine. Mifano tunayo hapa, kesi nyingi sana ziko pending na zinapigwa tarehe tuu. In other words, in the eyes on many, Karamagi ataonekana mshindi, na kama amesingiziwa vile.
Mimi nadhani kwa mtindo huu, kina Dr.Slaa, wangepeleka tu hayo madai yao mahakami, kabla hawa/huyu jamaa hajafikiria kufanya hivyo, regardless of how long the process may take...
 
Huu mchezo mtamu kweli kweli.

Ushauri kwa Karamangi, watawala wengi wameanguka kabisa wakijaribu kujisafisha. Ni rahisi kusingiziwa mitaani kwamba ni fisadi kuliko mahakama iki confirm kwamba ni fisadi.

Nilivyomwona Karamangi nafikiri anataka kujisafisha kwa cost yoyote, bahati mbaya hayo maji ya kujisafishia yanaweza kuwa aghali kuliko fedheha ya kuitwa fisadi.
 
Wana JF wanademokrasia wa kizazi kipya, wacha tumuone huyu jamaa akienda mahakamani. Hii inanikumbusha kesi ya minofu ya samaki; ni nani aliyemwona Masilingi siku alipotoa ushahidi mahakamani? na wengine wengi kutoka serikali ingawa mahakama ni ya kwao lakini viti vilikuwa vya moto.

Tunachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kuunga mkono hawa waliojaribu kutetea maslahi ya nchi kwa nguvu zetu zote kwa hali na mali.

Tukumbuke tunapambana na mafisadi yasiyo na haya wala huruma. Wakati umefika wa kalamu na matendo kwenda pamoja. Kwa sababu Karamg na wezi wenzake watatumia kodi zetu kuendeshea kesi "kama ipo" inabidi nasi tutoe suport ya kutosha kwa waliahoi wenzetu.

Naomba Mungu usiku na mchana Karamag aende mahakamani.
 
Back
Top Bottom