Sina tatizo sana na mheshimiwa Karamagi kufungua kesi dhidi ya Dr. Slaa. Ila nina tatizo sana na kesi dhidi ya gazeti lililoripoti tangazo la Dr. Slaa na kampuni inayochapisha gazeti hilo. Makosa yao ni nini, anataka wasitoe taarifa za matukio mbali mbali kama yanavyotokea? Je kazi ya gazeti ni nini? Litafanya kazi kwa kuripoti maneno ya serikali na CCM tu lakini lisiripoti maneno ya vyama vya upinzani?
Kichuguu,
Hizo ndizo sheria ambazo baadhi yetu tunazipinga kila siku. Tunasema zifutwe. Kimsingi, hata kuandika tunayoandika ni kwamba tumeamua kuziasi. Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 ndiyo inampa mlalamikaji nguvu ya kushitaki wote hao - wakiwamo wahariri na waandishi wa habari husika. Ipo. Ni miongoni mwa sheria dhalimu 40 ambazo Tume ya Jaji Mkuu Nyalali ilipendekeza zifutwe tangu miaka ya 90. Wamekataa, kwa sababu wanazitumia kutisha vyombo vya habari.
Tulidhani huyu bwana Kasi mpya angeingie na jipya, na walau kusaidia kuzifuta sheria hizi dhalimu. Naona serikali yake inatunga nyingine mpya, hata tusizohitaji.
Kila mara miswada inapelekewa Bungeni. Sheria dhalimu hazifikiriwi. Walipofikiria kuhusu vyombo vya habari, wakaunda muswada mchafu zaidi ya sheria zilizopo - tukaukataa.
Ndiyo maana baadhi yetu tunaamini kwamba Tanzania bado iko utumwani. Tunahitaji kuasi na kujikomboa. Tuliowaweka pale hawaoni haja hiyo, wanatafuta fursa nono kwa ajili yao navizazi vyao.
Jambo ambalo hatujafanikiwa kulifanya ni kupandikiza uasi huu hata kwa vyombo vya habari. Ndiyo maana, kwa kuogpa sheria hiyo na nyingine, na ndani ya kivuli cha 'maadili' vilichapisha stori ya mafisadi bila kuwataja majina. Hiki ndicho walichoogopa.
Mhariri wa MwanaHALISI namjua. Ni mkongwe. Ni kichwa. Ni muasi kwelikweli. Anaendelea kuwanoa vijana wadogo wadogo kama huyo mmiliki mwenyewe wa gazeti kujifunza kwamba uasi kwa ajili ya jamii ni jambo takatifu.
Kumbukeni, mahakamani haipatikani haki, bali mshindi. Ni wazi, kitaaluma na kitaratibu mahakamani ndiko tunakopaswa kupata haki. Lakini katikamisingi hiyo hiyo, tunajua kuwa hata asiye na haki aweza kushinda kesi. Suala la Ditto ni mojawapo ya mambo mapya yanayosisitiza hoja yangu hii. Kwa hiyo, tusishangae kina Ditto wako huru, huku wezi wa kuku wako ndani wanasota.