The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

Hivi ukitoa hoja ya kuundwa kamati teule ya uchunguzi ya Bunge, unaruhusiwa kuwa mjumbe au kuongoza hiyo tume kwa kuwa mwenyekiti? Ni nani anapendekeza mwenyekiti wa tume? Maana najua ukishatoa hoja tayari unakuwa na interest kwenye swala linalochunguzwa na hivyo huwezi kupewa uenyekiti au ujumbe kwa ajili ya kuepuka mgongano wa maslahi. Mwenye ufahamu na haya mambo naomba ufafanuzi tafadhali.
 
Alisema mbunge anapoanzisha hoja ikifanikiwa kuundiwa tume yeye anakuwa ndiye Mwenyekiti, hivyo mgogoro wa Buzwagi lengo lake lilikuwa kutafuta fedha za Tume hiyo ambayo ingefanya uchunguzi hadi Uingereza ulikofungiwa mkataba.

Hii itakuwa kanuni mpya ya Bunge!
 
Nina mashaka huko Kahama hao jamaa wamepata mapokezi hafifu sana na ndiyo maana wamejikuta wanaongelea habari ya mapokezi ya kishujaa aliyopewa Mh. Zitto!

Nimesoma hiyo habari zaidi ya mara 4 lakini sijaona hata hoja moja wala point waliyoongea. Sana sana wanazidi kuaibika na hasa baada ya mkataba wenyewe kuvuja na kuonekana kwamba ni mkataba bomu sana. Sijui watajitetea nini tena baada ya mkataba wenyewe kuonekana wazi?

Eti tume ingetumia hela zaidi ya milioni 100, sasa utalinganisha uchunguzi wa ule uzushi wa Mh. Malima na uchunguzi wa swala muhimu ambalo linagusa mapato ya nchi na tena kwa maslahi ya wananchi?
 
The only thing I can see ni wao kukubali makosa na mapungufu yao katika matumizi ya fedha za wananchi katika shughuli zisizo na uzito wa aina yoyote ile hakuna hoja hata moja iliyosemekana hapa.

Kitu kinachonishangaza sana kuhusu hawa wapinzani wanaohamahama, how can you be fighting for one great course and the next minute you are doing the exact opposite?

hata kama ni pesa, which is tax payers' money, hauwezi kusema vitu kama hivi halafu asubuhi ukaamka ukaendelea na shughuli zako like nothing happened?

kitu kinachowafanya hata hawa kushinda kwa kishindo pamoja na kuiba kura ni kwamba wengi wetu tunaongea tu lakini ikifika wakati kutenda matendo yetu sijui kitu gani kinaatuingilia tunarudia makosa mabayo tumeyafanya over and over again.
 
hivi mmejaribu kuongea na wabunge wa majimbo yenu hata kwa simu kuwauliza kuhusu hili swala na kutaka maelezo yao au ni blah blah za hapa tuu
 
"Alidai yeye akiwa CHADEMA walipanga mbinu za kutengeneza uongo ili wapate umaarufu" Hivi Akwilombe anadhani anaongea na watoto wa chekechea? kwa hiyo anajaribu kutuambia kuwa sasa hivi pia wametengeneza uongo na kina Makamba ili kupotosha ukweli wa hoja za zitto sababu hiyo ndio tabia anayotuonyesha.

Naye Hiza anasema "lengo kuu la Bw. Zitto kuzusha hoja hiyo bungeni ni kutaka iundwe tume ya kuchunguza utiwaji saini mkataba huo ili yeye awe Mwenyekiti wa Tume hiyo ili ajipatie posho wakati wa uchunguzi". Jamani Kweli CCM imeishiwa Hoja kiasi hiki!!!!. Chama Ambacho kinajisifu kuwa na hazina ya viongozi makini ndio hawa kweli?
Mimi nafikiri wakati umefika sasa wa watanzania kuamka na kuhoji kile wanachoambiwa na hawa wanaojiita "watawala". Tusikubali kufanywa wajinga hadi wa fikra. Ukisoma Hiyo taarifa utaona jinsi ilivyojaa maneneno ya "kisanii" kama vile waliokuwa wanaelezwa ni watoto wadogo. Ama kweli kama kuna mwaka wa shetani, basi kwa kina makamba nako pia huu ni "mwaka wa shetani"
 
hivi mmejaribu kuongea na wabunge wa majimbo yenu hata kwa simu kuwauliza kuhusu hili swala na kutaka maelezo yao au ni blah blah za hapa tuu
Mbunge wangu anatoka chama cha mafisadi. Nimemuuliza juu ya hili suala akanijibu kuwa huo mkataba ni siri. Nikamkumbusha kuwa siri huwa ni ya mtu mmoja tu ikishazidi hapo huwa siyo siri tena, aliishia kuguna tu.Sasa kwa kuwa umevuja kama zile paper za NECTA nimeamua kuukomalia mpaka kieleweke.
 
Mkaguzi ... jina lako limenikumbusha mtu mmoja alikuwa maarufu sana hapa JF alikuwa akiitwa Mchambuzi a.k.a mpambe wa EL!

Twende kwenye hoja sasa: Hiza alishaishia tangu alipogalagazwa kwenye uchaguzi wa ngazi ya wilaya kule Temeke. Alidhani kwamba akirudi CCM basi mambo yangemnyookea kwa kupewa ulaji. Lakini naona ulaji uko mikononi mwa Makamba. Sina hakika kama kuna kiongozi makini ndani ya CCM anaweza kumpa uongozi Bwana Hiza. Hata hiyo post aliyopewa na Makamba ni basi tu ameamua kumpa kwa kuwa alivutwa kwa ahadi na sasa ataishia kusema longolongo kwenye majukwaa na kuonekana mtu asiye na msimamo na hana jipya mbele ya watanzania!
 
Yaani mazungumzo yao yote ni propaganda za zamani za akina Kingunge kwani hakuna point hata moja. Wananchi walikosea wangeliwachapa mawe kama alivyofanywa mkuu wa wilaya KInondoni
 
Buzwagi: Was the govt taken for a ride?

-The burning questions continue to pile up

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

NEW discoveries in the controversial Buzwagi gold mining agreement signed between the government and Barrick Gold Corporation subsidiary company Pangea Minerals Limited suggest even less value in terms of state revenue and national economic benefits from the planned $400m (approx. 520bn/-) investment.

While royalty on exports has been set at the industry standard of 3 per cent (for gold) and 5 per cent (diamonds), there are specific caps set on exactly what the investor company will pay to both the central government and local government authorities in Kahama District, Shinyanga Region where the mine will be located.

The agreement, signed in London last February by Energy and Minerals Minister Nazir Karamagi on behalf of the government and Barrick Gold Tanzania Limited’s executive general manager (operations) Gareth Taylor representing Pangea Minerals Ltd, specifies a set limit of $200,000 (approx. 260m/-) in maximum amount that Pangea Minerals Limited would be legally obliged to pay each year in local government tax.

A similar ceiling is also cited for road toll taxes that the project shall be required to pay every year under the Fuel and Road Tolls Act of 1985.

Furthermore, the project implementing company may not pay more than $10,000 (approx. 13m/-) in any one year for ’’any duty, levy, charge, fee or compulsory contribution’’ that has not been specified in the agreement.

With regard to the land at Buzwagi where the mine is to be set up - an area covering about 24.49 square kilometres � Pangea Minerals Ltd is not required to pay any taxes on the property in excess of $2,000 (approx. 2.6m/-) per square kilometre per annum.

Legal experts have confirmed to THISDAY that this means regardless of any developments made on the land or any future increases in the property value, the investor may pay a maximum of just $48,980 (approx. 63m/-) per year in taxes on the land throughout the lifespan of the mine.

Another interesting clause in the agreement is Article 4.1.3, which specifies that Pangea Minerals Ltd will make a fixed contribution of $125,000 (approx. 162.5m/-) by December 31 of each calendar �year of production� to the state-run national economic empowerment fund.

But as legal experts point out, there is a catch here too. For the document defines a ’’Year of Production’ as a time when production from the mine reaches a ’minimum of 20,000 ounces of gold contained in ore or concentrate, as the case may be, during the applicable calendar year.’’ In other words, for each year that the gold mine management declares production to be less than the stated 20,000 ounces, the government will get no contribution for its empowerment fund.

’’So, minus the 3 per cent royalty which is itself negligible, Tanzania as a country will earn a mere $583,980 (approx. 760m/-) from the Buzwagi gold mine each year,’’ Dar es Salaam-based lawyer Tundu Lissu told a local television talk show earlier this week.

Lissu, who works with the Lawyers Environment Action Team (LEAT) and is noted for his extensive researches into the country’s mining industry, described the Buzwagi deal as ’scandalous’ and asserted that the planned investment would be of little benefit to the national economy.

He cited government figures presented in parliament recently suggesting that out of $2.614bn (approx. 3.4tr/-) in total gold exports over the past ten years, Tanzania earned just $78m (approx. 100bn/-) in royalty.

According to the government’s 2006/07 figures, minerals (almost entirely dominated by gold) accounted for around 63 per cent of the country’s total export revenues. But paradoxically, the minerals sector (particularly gold) contributes a paltry 2.7 per cent to Tanzania’s gross domestic product (GDP), or total economic output.

Meanwhile, minister Karamagi has this week steadfastly avoided making any comment on the Buzwagi deal or his own role in it, especially with regard to the circumstances of its signing in a London hotel on February 17 this year.

Among other things, the agreement legally binds the government to maintain the same taxes and fiscal laws applicable to Pangea Minerals Ltd today for the entire duration of the mine, which is a minimum of the next 25 years and a maximum that by the terms of the pact is more or less indefinite.

The minister responsible for mining is given extraordinary discretionary powers to extend the company’s special mining licence as he or she sees fit, without any limits on duration.

An earlier report by THISDAY revealed that at least one key provision in the original final draft of the agreement, approved by the government’s advisory committee on minerals, was deleted by hand just before the signing, effectively exempting Pangea Minerals Ltd from paying any taxes falling under the East African Customs Management Act of 2004.

And going by the document itself and signatures therein, it appears there were no witnesses to the signing for either of the two parties involved.

At the time the Buzwagi deal was signed, the fourth phase government under President Kikwete had announced the start of a formal review of the various existing gold mining policies, laws and contracts, and the suspension of any new major mining contract signings until the review process was completed.
 
Hiza, Akwilombe watumika kummaliza Zitto

Na Patrick Mabula, Kahama


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewatumia wanasiasa waliojiunga kutoka Upinzani kuzima hoja za mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe, kuhusu mgodi wa Buzwagi wilayani hapa, kuhusu mkataba wa madini kusainiwa Uingereza.

Wakihutubia mkutano wa hadhara juzi wanasiasa hao Bw. Tambwe Hiza aliyetoka CUF na Bw. Shaibu Akwilombe aliyetoka CHADEMA, walisema Bw.Zitto alitunga uongo na anatafuta umaarufu wa kisiasa.

Awali, Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusufu Makamba, aliyeanza kuhutubia, aliwaeleza wananchi wa hapa kuwa madai ya Bw. Zitto ni ya uongo yenye lengo la kukwamisha uwekezaji na maendeleo ya wananchi wilayani hapa.

Alisema wananchi wanapaswa kumpuuza, kwani ana lengo la kukwamisha ajira ya vijana wapatao 600 watakaoajiriwa na mwekezaji wa Kampuni ya Barrick wakati mgodi wa Buzwagi utakapoanza kazi.

Bw. Makamba alisema anashangazwa na baadhi ya wananchi wa Kanda ya Ziwa kumpokea Bw. Zitto kama shujaa wakati hoja zake zilikuwa si za kweli na kuwataka watu wa hapa, atakapokuja wasimpokee kwa namna hiyo wakati wa ziara yake.

Bw. Akwilombe alisema yeye anamfahamu vizuri Bw. Zitto kuliko watu wa hapa, na kwamba hoja zake zilikuwa za kutunga ili kutafuta umaarufu, kwa kuwa hakuna sheria yoyote inayozuia mkataba kusainiwa nje ya nchi.

Alidai yeye akiwa CHADEMA walipanga mbinu za kutengeneza uongo ili wapate umaarufu na kuongeza kuwa hata mkataba wa Reli yaTAZARA ulisainiwa China, lakini reli ilijengwa nchini, hivyo akawataka wananchi wampuuze Bw. Zitto.

Bw. Akwilombe alisema akija kuhutubia masuala ya mgodi wa Buzwagi, kama anavyohutubia sehemu zingine za Kanda ya Ziwa na kupokewa kishujaa wampuuze.

Naye Bw. Hiza alisema CHADEMA wanatumia kigezo cha mgogoro wa mkataba wa Buzwagi kuzunguka nchi nzima kutafuta umaarufu na kujipatia wanachama.

Alisema lengo kuu la Bw. Zitto kuzusha hoja hiyo bungeni ni kutaka iundwe tume ya kuchunguza utiwaji saini mkataba huo ili yeye awe Mwenyekiti wa Tume hiyo ili ajipatie posho wakati wa uchunguzi.

Alisema mbunge anapoanzisha hoja ikifanikiwa kuundiwa tume yeye anakuwa ndiye Mwenyekiti, hivyo mgogoro wa Buzwagi lengo lake lilikuwa kutafuta fedha za Tume hiyo ambayo ingefanya uchunguzi hadi Uingereza ulikofungiwa mkataba.

Bw. Hiza alisema kama Tume ya Malima ilitumia sh. milioni 100 uchunguzi wa uwekaji mkataba wa Buzwagi ungegharimu zaidi ya kiasi cha pesa, kutokana na uchunguzi wake kufika Uingereza.

Alisema mkataba uliowekwa ni halali na taratibu zote zilifuata sheria za nchi na kuwataka wananchi wasiyumbishwe na hoja za wapinzani ambao alidai yeye anawafahamu.

Nini chanzo cha habari hii? Yaani naulizia imechapishwa gazeti gani?

Wakati mwingine ni vyema ukajua habari inatokea wapi, kwani kujua chanzo cha habari chaweza kukupa uelewa zaidi wa habari yenyewe.

Mbona sioni makadirio ya watu walio hutubiwa? waliupokeaje huu ujumbe? mbona sioni akishangiliwa/wakiguna/ wakizomewa???

Wanaweza kusema lolote kwani ni uhuru wao, issue ni jinsi huo ujumbe ulivo pokelewa!
 
"Alidai yeye akiwa CHADEMA walipanga mbinu za kutengeneza uongo ili wapate umaarufu"

Yaani huyu bwana Akwilombe anawatangazia rasmi Watanzania kuwa yeye ni muongo halafu wakati huo huo anawataka Watanzania wamuamini kwa kauli zake kuhusu wapinzani wakati ameshakiri kwamba yeye ni Muongo.

Haya ni maajabu kabisa,Mimi ninadhani huyu bwana amepoteza credibility kubwa,
Alipoingia CCM nadhani angefanya jambo la busara sana kama angerudi matawi ya chini na kucheki upepo unavuma kuelekea wapi,

Lakini yeye bila kutambua CCM wamemgeuza Mgambo kwakumtanguliza msitari wa mbele, huku CCM wakijua wazi kuwa wale wa Msitari wa mbele ndo hufa wa kwanza kwanza katika vita,Majemedari wenyewe kina Mramba, Meghji,JK wametulia tu kwanza ili hawa mgambo wafe ndo wao waingie kwenye mapambano.

Akwilombe hakulijua hilo matokeo yake sasa hilo alilolifanya litakuwa ni mzigo Mkubwa kweli kwake kisiasa.
 
Haya ni mapambano ya kifikra, tatizo ni kuwa CCM bado hawajajua ni jinsi gani wapambane. Bado wana mawazo ya kujifikiria kuwa chochote watakachosema kwa vile kimesemwa na CCM basi watu watakubali. Wajiandae kwa umati mkubwa zaidi sehemu nyingine. Mapinduzi ya kifikra yameanza, na hakuna kurudi nyuma.
 
saying the govt "was taken for a ride" would tantamout to saying the Minister and for that matter the govt did not know what is meant by signing a contract (just like with Mangungo and Karl Peters)........but with Buzwagi the big NO, Karamagi knew exactly what he was up to,I hear he is a "qualified" engineer and more over he is advised by a team of legal and (definitely) economic experts, the key question here is: why was there so much hurry into signing, why was the contract kept a secret?why did karamagi not disclose it even to his cabinet pals? why were some clauses deleted by hand at signing?

No, there can in no way be taking for a ride!!!This is simply embezzlement of public resources,ufisadi,ubadhirirfu,call-whatever-names-you-like...!!!!
 
*Wagawanywa kwa waandishi na vyama vya upinzani

*Wapinzani waahidi kuupeleka kila mkoa, wilaya


Na Muhibu Said


VYAMA vya upinzani vilivyoko katika ushirikiano wa kisiasa, vimegawa kama njugu nakala za mkataba wa uchimbaji wa madini wa mradi wa Buzwagi, wilayani Kahama ambao hoja yake ilimfanya Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe kufungiwa kuhudhuria vikao vya Bunge hadi Januari mwakani.


Umoja huo unaoundwa na vyama vya Chadema, CUF, TLP na NCCR-Mageuzi, ulianza kusambaza nakala za mkataba huo kwa kuwagawia waandishi wa habari katika mkutano ulioitishwa na vyama hivyo, makao makuu ya Chadema, jijini Dar es Salaam jana.


Katika tamko lao lililosomwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Victor Kimesera kwa niaba ya viongozi wenzake, vyama hivyo vimeeleza kuwa vimefikia uamuzi huo ili kutoa fursa kwa umma kuufahamu mkataba huo, kuujadili na kuujua mchakato uliosababisha usainiwe haraka.


Tamko la vyama hivyo, lilisainiwa na Katibu Mkuu wa TLP Taifa, John Komba, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Taifa, Juma Duni Haji, Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Sam Ruhuza na Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Kimesera.


Viongozi hao walikutana na waandishi wa habari kuzungumzia majibu ya serikali kuhusu tuhuma kwa vigogo kumi na moja, wakiwamo mawaziri wa serikali ya awamu ya nne waliotuhumiwa na Mbunge wa Karatu ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kuwa ni mafisadi waliohusika na ubadhirifu wa mabilioni ya fedha za umma.


Mkataba huo ulisainiwa na Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi kwa niaba ya serikali na kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick, jijini London, Uingereza.


"Tunachukua fursa hii kuanika wazi kwa umma, kupitia vyombo vya habari, mkataba wa uchimbaji wa madini Buzwagi ambao ni sehemu ya msingi wa tuhuma za ufisadi dhidi ya Karamagi. Katika hatua ya sasa tungependa kutoa nafasi kwa umma kujadili kuhusu yaliyomo pamoja na mchakato uliopelekea mkataba huo," alisema Kimesera.


Akisoma tamko hilo, Kimesera alisema watasambaza orodha hiyo inayoitwa ya "mafisadi" kwa viongozi wa vyama hivyo wa mikoa, wilaya na kwa wananchi kwa ujumla.


Mbali na hilo, Kimesera alisema pia kuwa watafanya ziara nzima ili kuwaelimisha wananchi juu ya kile walichokiita "uporaji" au "utapanyaji" wa mali zao wanaodai kufanywa na baadhi ya vigogo wa serikali.


"Sisi kama viongozi wa vyama vilivyoko kwenye ushirikiano tutaisambaza orodha ya mafisadi nchi nzima kwa viongozi wa vyama vyetu mikoani, wilayani na kwa wananchi kwa ujumla pamoja na kufanya ziara ya kuwaelimisha wananchi wa Tanzania juu ya uporaji au utapanyaji wa mali zao," alisema Kimesera.


Kimesera alisema wamefikia uamuzi huo baada ya baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu serikalini kuzungumzia orodha ya vigogo hao bila kutoa majibu yanayoridhisha.


Viongozi hao walizungumzia orodha hiyo kwa nyakati tofauti siku chache baada ya Dk Slaa na mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu, kuitoa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mwembeyanga, jijini Dar es Salaam, Septemba 15, mwaka huu.


Hadi kufikia jana, viongozi wa serikali waliokwishajitokeza na kuzungumzia tuhuma hizo ni watano ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Philip Marmo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Siasa na Mahusiano ya Jamii), Kingunge Ngombale-Mwiru, Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja. Mwingine ni Mbunge wa Musoma Vijijini ambaye pia ni wakili wa kujitegemea, Nimrod Mkono.


Tamko hilo limetolewa na vyama hivyo vilivyoko kwenye ushirikiano wa kisiasa, siku moja baada ya Waziri Karamagi kutangaza azma ya kufungua kesi mahakamani dhidi ya Dk Slaa, Gazeti la Mwana Halisi, kiwanda kilichochapisha gazeti hilo pamoja na wengine wote walioshiriki na wanaoendelea kushiriki katika kumdhalilisha.


"Hatutaogopa au kusita kutimiza wajibu wetu kwa wananchi wa Tanzania kwa sababu ya vitisho vya mashtaka dhidi ya viongozi wetu au dhidi ya vyama vyetu, tutaendelea na mchakato wa kuuanika wazi ufisadi na mafisadi," alisema Kimesera.


Kimesera alisema pamoja na viongozi hao wa serikali kuzungumzia orodha hiyo, taarifa walizozitoa zinatofautiana.


"Kwa mfano Marmo amesema kwamba ushahidi wa ufisadi upelekwe kwenye vyombo vya dola, Kingunge amesema madai hayo ni uzushi mtupu na Chenge amekubali kuwa yeye ni mkurugenzi katika kampuni ya kigeni ya Tangold. Wakati huo huo Karamagi hajakanusha tuhuma juu yake, lakini amesema anakwenda mahakamani na amekwepa kuzungumzia mkataba wa Buzwagi ambao ni sehemu ya msingi ya tuhuma za rushwa dhidi yake," alisema Kimesera.


Alisema mbali na hivyo, viongozi wengine wa serikali waliotajwa kwenye orodha hiyo, wamekaa kimya kwa wiki mbili tangu tuhuma hizo zitolewe dhidi yao. Kwa sababu za kisheria, kwa sasa hatuwezi kutaja majina ya viongozi hao.


Kimesera alisema kutokana na majibu yaliyotolewa na viongozi waliotajwa kutofautiana, imekuwa vigumu kwa wananchi kuelewa ni ipi kati ya taarifa zilizotolewa inawasilisha msimamo wa serikali na pia wanashindwa kuelewa iwapo misimamo hiyo tofauti ni mawazo binafsi ya hao mawaziri watano.


Pia kutokana na ukimya wa viongozi na watendaji wengine wa serikali waliotajwa, wananchi wanashindwa kuelewa iwapo kimya hicho maana yake ni kukubaliana na tuhuma za ufisadi zilizotolewa hadharani dhidi yao.


Alisema ukosefu wa msimamo wa serikali unaoeleweka, unatia wasiwasi mkubwa kwa wananchi kwa sababu tuhuma zilizotolewa ni nzito, zinahusu wizi au ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma, matumizi mabaya ya madaraka ambayo yameliletea taifa hasara kubwa kiuchumi na pia yanawahusu viongozi wa ngazi za juu wa kiserikali.


Kimesera alisema pia tuhuma zilizotolewa zinahusu matukio mahsusi yaliyofanyika kwa vipindi vilivyotajwa na zinataja kiasi cha fedha zilizoibwa au vitendo vinavyoashiria matumizi mabaya ya madaraka na madhara yake kwa taifa.


"Hivyo tulitarajia serikali itoe majibu mahsusi hatua kwa hatua kuhusu tuhuma hizo badala ya kutoa majibu ya jumla," alisema Kimesera.


Kutokana na kukosekana majibu ya mambo hayo, aliwaomba wananchi, vyombo vya habari na taasisi za kiraia kuendelea kuishinikiza serikali kutangaza msimamo wao kuhusiana na tuhuma hizo, pia vyombo vyenye mamlaka kisheria kuchukua hatua za kuchunguza matukio hayo ya ufisadi na kuwachukulia hatua wahusika.


"Hoja kwamba vyama vyetu vipeleke tuhuma hizo kwenye vyombo husika ni hoja potofu kwa sababu nyaraka zote zilizotajwa kuhusiana na ufisadi huu zimetoka serikalini," alisema Kimesera.


Hata hivyo, Kimesera alisema mambo yaliyoelezwa na viongozi wa ngazi ya juu wa vyama hivyo katika mkutano wao na waandishi wa habari jana, ni madogo na kusema kuwa: "Mzinga wenyewe utapasuliwa kesho kutwa Ijumaa (kesho)".


Akitetea uhalali wa kugawa nakala ya mkataba huo, kinyume cha Sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1976 inayozuia mtu wa kawaida kuwa na waraka wa serikali, Lissu alisema sheria hiyo ni miongoni mwa sheria zilizopendekezwa na ripoti ya Tume ya Jaji Nyalali kufutwa, lakini hadi sasa bado ipo.


Hata hivyo, alisema sheria hiyo imevunjwa na Katiba ya nchi Ibara ya 18 ambayo inatoa haki kwa kila raia kutoa na kupewa habari hivyo wana haki ya kugawa nakala ya mkataba huo kwa wananchi wa kawaida.


Akizungumzia kauli ya Kingunge iliyoziita tuhuma za Dk Slaa dhidi ya vigogo hao kuwa ni uchochezi, Lissu alisema sheria ya uchochezi, ilitungwa na wakoloni mwaka 1955 kwa lengo la kuwadhibiti wapigania uhuru wa Tanganyika mwaka mmoja baada ya harakati za kudai uhuru kuanzishwa na kwamba, mtu wa kwanza anayepaswa kutuhumiwa kwa suala hilo, ni hayati Mwalimu Julius Nyerere kutokana na hatua yake ya kuongoza harakati hizo.

SOURCE:MWANANCHI
 
Historia zao zinafanana. Hiza alihamia CCM akitokea CUF baada ya kushindwa ubunge wa Temeke mara tatu mfululizo. Baada ya uchaguzi wa 2005, mwenyekiti wa CUF akafanya mabadiliko ya uongozi na yeye akaachishwa ukurugenzi wa Uenezi na Sera mara moja akarejea CCM. Wenye kumbukumbu mtakumbuka kwamba wakati akihamia CCM toka CUF, Hiza alisema anafanya hivyo kwa sababu zake binafsi. Hiyo inatosha kutuambia kwamba ni njaa ndiyo ilimrudisha baada ya kukosa hata ukurugenzi uliokuwa unampa kula.

Akwilombe alihamia CCM baada ya kushindwa vibaya katika uchaguzi wa ubunge wa Tunduru. Wakati anafanya hivyo hakueleza ubaya wa upinzani na alihama kimya kimya mpaka kaja kuripotiwa na magazeti baadaye. Kama angesimama wakati huo na kusema, "Jamani mimi siasa za upinzani zimenishinda maana sasa tumekaa kwenye vikao wenzangu wanalazimisha kwamba tutunge uongo dhidi ya chama tawala na serikali yake ili tupate umaarufu. Kwa kuwa mimi ni mwanasiasa safi na siwezi kushiriki, nimeamua kujitenga nao" Leo tungemwelewa. Lakini katoka kimya wala hakuwahi kusema ubaya wa CHADEMA, leo Makamba anataka kumtumia ndo anaamua kutunga huo uongo ili tu ajikombe kwa Makamba atafutiwe cheo.Na huyo Hiza anafikiri watanzania bado ni wale wa mwaka 1947 ambao unawaambia tu sheria inasema hivi wanakubali hata kama umenukuu hewani? Hizo kanuni za Bunge kazitengeneza za kwake? Mbona Mrema aliporusha mabomu kwa Mbirinyi mwenyekiti wa kamati aliteuliwa Idd simba? Mara ngapi Mzindakaya kaleta hoja Bungeni na hakuwahi kuwa mwenyekiti? Ni sheri za Propaganda za CCM hizo? Kwamba mlalamikaji ndiye awe mwenyekiti wa jopo la majaji kwenye kesi ambayo yeye ni mlalamikaji? Asituokote.

Hawa ni wa kuhurumia tu na wananchi hawawezi hata kuwasikiliza. Walidhani kila atakayejisalimisha atapigiwa upatu mpaka apewe ubunge wa Afrika Mashariki kama mwenzao Amani Kaburu. Wamenoa, vyeo vimeisha na Makamba atabaki kuwabunia vyeo visivyo rasmi wala visivyo na maslahi kama hicho cha Propaganda ambacho huenda hata kamati kuu ya CCM haikijui, ni cha Makamba tu.
 
Vipi wanndugu....mbona hamuuweki?????????????????????
Au mmekosa scanner. Uleteni hbasi hapa kijiweni kwangu K/koo? Watu tunakosa usingizi...Uko wapi mkataba "full version"??????????????
 
Ngoja waipatepate kwanza; Hakuna dhambi kubwa kama usaliti hasa wakati wa mapambano ya kudai haki. Hawa jamaa ( Hiza na Akwilombe)walidhani wangefunikwa dhambi yao hii na ccm, bila kuathirika zaidi, bahati mbaya wakati umebadilika na sasa wataonekana vituko majukwaani!
 
Back
Top Bottom