PreGE2025 The Chanzo yaondoa Maudhui ya Askofu Gwajima YouTube Kufuatia wito wa TCRA

PreGE2025 The Chanzo yaondoa Maudhui ya Askofu Gwajima YouTube Kufuatia wito wa TCRA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Leo Mei 27, 2025, The Chanzo imepokea wito kutoka kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kuhusu maudhui ya video tuliyochapisha katika chaneli yetu ya Youtube, ambayo ni mkutano na waandishi wa habari mazungumzo aliyoyafanya Askofu Josephat Gwajima, Mbunge wa Kawe (Chama cha Mapinduzi - CCM), mnamo Mei 24, 2025.

Kutokana na mazungumzo hayo kuendelea kufuatiliwa, ili kuboresha uwazi, na imani ya wafuatiliaji wetu, The Chanzo inapenda kuwajulisha wasomaji na wadau wake wengine kuwa imetubidi kuyaondoa maudhui hayo kutokana na wito huo.

Sehemu ya taarifa tuliyopokea kutoka TCRA inaeleza:

"Maudhui hayo yaliyopakiwa na Chanzo Online TV yalikuwa ni maelezo ya mtu aliyejitambulisha kwa jina la Josephat Gwajima, hayakufuata Sheria, Kanuni, Maadili wala Misingi ya Uandishi na Utangazaji wa Habari kutokana na kukosa mizania/kuwa na taarifa za upande mmoja tu bila ya kuwapa nafasi upande wa Serikali au Mamlaka husika kutolea ufafanuzi shutuma au taarifa kuhusu idadi ya watu waliodaiwa kutekwa kama ilivyodaiwa katika taarifa husika. Kitendo cha Chanzo Online TV kupakia taarifa zenye kuegemea upande mmoja kinaweza kuhamasisha au kuchochea chuki dhidi ya Serikali kutoka kwa wananchi wake."

Wakati ni nadra wito wa namna hii kutokea, kutokana na wito huu kutoka TCRA, leseni ya maudhui inatutaka kuyaondoa maudhui hayo; jambo ambalo tumelifanya leo Mei 27, 2025, 10:09 asubuhi.

View attachment 3347334
Nani mmiliki wa chanzo?
 
Poleni sana
Hiyo tcra imejaa vilaza mikund wasiojitambua , sasa Serikali ingekuwa imejibu hizo tuhuma halafu nyie mngekuwa hamjazirusha hapo ndipo ingeonekana mnamakosa.
Sasa kama serikali haijajibu hizo tuhuma sasa utabalance vipi hiyo story?
Huko ni kiminya uhuru wa kupata habari
 
Kwani the chanzo ni kina nani jamani,wenye habari hiyo ni wao tu??, Naomba kujua kwa mwenye kujua please
 
Back
Top Bottom